Shinto
JF-Expert Member
- Dec 6, 2010
- 1,781
- 96
Nimefuatilia midahalo mitatu baina ya vyama vyetu vikubwa vya upinzani wakiwemo na CCM muda mwingine, kilichowazi ni kuwa kwa wachambuzi huru wanaona CUF hufanya vizuri kuliko CMD kwenye midahalo yote iliyowahi kufanyika..
Anza na ile wa HR vs Mbowe, HR alionyesha umahiri na ukomavu wa kisiasa, wakati Mbowe akidhihirisha uchanga na jazba za kishabiki zisizo na maana.
Ukaja mdahalo wa Jusa v Nape v Marando..
Same story Jussa aliweza kueleza vizuri falsafa za chama chake, akimuacha mkongwe Marando akishindwa kujieleza vema.. Hata magazeti yanayoelemea CHADEMA yalimpa Ushindi mkubwa Jussa dhidi ya Marando..
Juzi madahalo wa wagombea Ubunge Igunga, Mahona wa CUF, Kashindye wa CDM na Kafumu wa CCM hali ilikuwa kama hivyo. Magazeti yanampa ushindi mgombea wa CUF..
Swali ni kuwa, ikiwa CHADEMA kinachojiita chama makini, cha wasomi tena vijana, mbona hugaragazwa na wale tunaowakejeli kuwa hawakwenda shule na sio makini?
Pili mbona CDM husimamisha watu wazee waliochoka tofauti na image wanayotaka kuijenga juu ya chama chao?