Kwa muktadha huu: Dr Slaa ikulu hapamfai!

Kwa muktadha huu: Dr Slaa ikulu hapamfai!

HAMY-D,

Wewe ni mpenda amani sina budi kukupongeza kwa uchambuzi wako murua uliojaa maneno ya ujenzi, tunashakuru kwa kuweka wazi hizi bayana za Dr Slaa.

Mpenda AMANI? uwezo wa vijana wa Lumumba ni mdogo sana, jifunzeni, jisomeeni, karne ya 21 unaandika utumbo kisa buku7?
 
Mkuu Ritz,

Nashukuru sana kwa pongezi, unajua hili suala la amani ni jambo letu sote, sio serikali wala sio vyama vya upinzani. Hatuna budi wapenda amani wote tushirikiane kuilinda tunu hii ambayo haina bei.

Somi zima umeingia kwenye mkumbo wa hao ma mburula, ukija na ID yako nyingine unajifanya muelewa, na hapo PPRA soon watajitambua, tutakuona...
 
Kumbe kuna vijana wa kitz wameshanyongwa china kwa kukamatwa na dawa za kulevya, na wengine wamefungwa lkn serikali iko kimyaaa!!
Nani alaumiwe zaidi ya serikali inayowafuga wauza unga??
 
Hizi ni propaganda za ccm kwani kingunge mlimlea kwenye uwaziri mpaka akiwa na umri gani? Vyombo vya usalama kuelezwa ukweli ndo taabu, kwani wao ndo wanaoamua anaetakiwa kwenda ikulu? Mbona ccm wanawapigia promo mafisadi pamoja na wazee ambao mnaowaona wakiwa upinzani hawezi kutumikia uma?
 
Dr Slaa ni tishio kwa ccm...watayasema mengi lakini ukweli utabaki tu kuwa ndiye rais wa tz kuanzia 2015,Hamy-D anatumia katiba ya wapi? Tunatumia written constitution and not unwritten constitution,sio mtu Hamy-D anakurupuka tu kutoka ambako hakueleweki,ni katiba gani inayoonesha ukomo wa umri katika kugombea urais? Akili ndogo haiwezi kuongoza akili kubwa,rais sio mtendaji kama unavyofikiria gamba wewe,au ndio buku saba project from Lumumba,tumia kichwa kufikiri na sio utumwa wa tumbo lako.
 
Kwenye katekisimu yetu kuna swali hili
'Mungu yupo wapi?'

tumesoma hivi 'Mungu yupo mahali pote'

sasa wewe mburula katekisimu yako inasemaje?mungu yupo ccm au?

mungu wa unzinzi na tindikalit yupo chadema
 
HAMY-D,

Wewe ni mpenda amani sina budi kukupongeza kwa uchambuzi wako murua uliojaa maneno ya ujenzi, tunashakuru kwa kuweka wazi hizi bayana za Dr Slaa.
\


Wale wauza unga wa cCm ndio wapenda amani pia!!!
 
WanaJF!

Pamoja na mapenzi makubwa ambayo wengi wenu mmekuwa nayo kwa Dr Slaa na mngependa kuona siku moja Dr Slaa akiapishwa na kuwa rais wa Tanzania, ila nasikitika kusema hilo haliwezekani kwa kuwa Dr Slaa Ikulu hapamfai.

Ni muhimu kwa mashabiki na wanachama wote wa CHADEMA wenye hamu ya kuona Dr Slaa anakuwa rais kufahamu jambo hilo ni gumu na hatuna budi kulikubali, ugumu wenyewe kwa Dr Slaa kuwa rais upo kwenye maeneo yafuatayo;

Umri wa Dr Slaa sio sahihi kutumikia umma.

Dr Slaa ambae imeandikwa kuwa amezaliwa October 29, 1948, kwa sasa kama angekuwa mtumishi kwenye ofisi za umma basi angekuwa ni mstaafu miaka 5 iliyopita.

Ieleweke mpaka ifikapo mwaka 2015 Dr Slaa atakuwa na miaka 67, umri ambao hawezi kumudu changamoto za nchi kwani ni mkubwa mno na madaktari uwa wanashauri mtu mwenye umri huo inapaswa apumzike.

Mahusiano ya Dr Slaa na vyombo vya ulinzi na usalama.

CHADEMA na viongozi wake wakubwa (Mbowe na Dr Slaa) wamekuwa wakitangaza hadharani kuwa hawana maelewano mazuri na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Viongozi hawa wa CHADEMA wamekuwa wakilalamika kuwa chama chao kimekuwa kinakandamizwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kupokea maagizo toka serikalini.

Jambo ambalo limekuwa likipingwa na vyombo hivyo na imeshuhudiwa kwa askari kadhaa kusema wanasiasa wa upinzani hawapendi kuona hali ya nchi hii ikiwa kwenye amani na utulivu. katika hali hii, unatarajia askari watakuwa tayari kufanya kazi na CHADEMA endapo wakitwaa dola?

Utaratibu wa mahusiano ya ndoa na familia.

Kama itakumbukwa kauli ya hayati mwl Nyerere iliyosema, "ikulu ni mahali patakatifu" ingawa aliitumia kueleza rushwa, ila neno takatifu lina maana pana na kwa upande wa mahusiano ya familia ni sawa kusema rais anae tarajiwa kuingia Ikulu ni lazima awe na mke/mume wa ndoa pia na familia inayo kubalika kisheria.

Tuhuma za ubadhilifu ndani ya chama chake.

Dr Slaa alipata tuhuma kuwa amekwapua pesa kwa namna ya kujikopesha na kilikuwa kiasi cha milioni 140 pesa za kitanzania, tuhuma hizi hapo awali alipinga kuwa si za kweli, ila baada ya kuhojiwa mara kadhaa Dr Slaa alikiri kuwa ni kweli alichukua pesa hizo na tayari amezirejesha.

kwa mtu ambae tayari ameonyesha udhaifu mkubwa katika kupigana na nafsi yake kwa matamanio mbalimbali ya kidunia, hasa masuala yanayo husu fedha, hii ni hatari kwa HAZINA (mfuko mkuu wa serikali) yetu ya taifa kama Dr Slaa akipata urais.

HITIMISHO,

Kwa mujibu wa hoja mbalimbali kama nilivyo eleza, ni ukweli usio pingika kuwa Dr Slaa Ikulu si mahali pake na ni kheli afuate ushauri wa madaktari wa kupumzika na kuachana na mambo ya utumishi wa umma kama anavyo panga.

kuhusu mashabiki ni vyema sasa tukaacha ushabiki wa kisiasa ambao umekuwa hauna faida yoyote zaidi ya kurudisha nyuma maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla badala yake tujikite kwenye uzalendo na kuchagua viongozi wanaofaa kwa mustakabali mwema wa taifa letu.


Ndugu HAMY D,

Kwanza unamkosea adabu Mzee Slaa kwani kama ulivyosema ni kweli kabisa ni mtu mzima sana. Nakushauri umuombe radhi.

Pili, nadhani siyo vizuri hasa kijamii, kumshambulia Mzee Slaa binafsi. Ni dalili chuki binafsi kwake na ni ukosefu wa heshima kwa mtu anayeweza kuwa sawa na baba yako au basi kaka yako mkubwa, sijui amekufanyaje binafsi. Na pia hayo aliyo kufanya kama yapo sikuingilieni. Yamalizeni wenyewe! Lakini nitafurahi kama utamu-address Katibu Mkuu wa CHADEMA na kumpa tuhuma za kupwaya kwenye chama chake, of which wanachama wake hawajaona kupwaya huko na bado wana imani naye. Hivyo unachofanya ni kuwachochea tu.....na sijui kwa nini! Hawa wanachama wana haki zao kikatiba, haki ambazo wewe unaanza kuziingilia! siyo vizuri hivyo.

Tukiongelea umri....mi nadhani bado unakosea. Kinachoongoza huwa siyo miaka, ni akili na busara za mtu pamoja na uzoefu katika kukabiliana na yanayomkabili. Katika historia ya nchi hii nimeona watu wengi sana wanaofikia umri wa kustaafu na wanaombwa kuendelea na "kazi" ili kuokoa taifa. Sioni ni kwa nini imekuwa dhambi sana kwa Mzee Slaa kutakiwa kuendelea na nafasi yake ya uongozi.

Mahusiano na vyombo vya ulinzi na usalama?... Nafikiri ni kweli mahusiano yao siyo mazuri. Uchunguzi binafsi niliofanya ni kuwa mahusiano ya Watanzania wengi hasa maskini, na wapenda haki siyo mazuri na vyombo hivyo hasa polisi. Hii ni kwa sababu vyombo hivyo vimeacha kuwa na uadilifu. Kwa sasa ni kawaida kumkamata mtu barabarani na kumbambika kesi ya kuteka nyara au kuua. Kwa sasa ni sawa kwa polisi kumpiga raiya mpaka anakufa na kumpeleka morgue "Mwanyamala hospitali" kabla hata ya kufikishwa mahakamani akahukumiwe! Kwa sasa ukimpeleka mhalifu polisi umepeleka dili. Utahonga ili ashughulikiwe na atahonga ili aachiwe! Kama haitoshi Kwa sasa ni kawaida kwa Polisi kuingilia mikutano ya siasa hasa ya wapinzani na kuanzisha fujo! Polisi kuanzisha fujo!.... Unapaswa kuona aibu mwenyewe kwa kuhoji hilo. Ulitaka mahusiano yawe mazuri katika hali hiyo?......."kuhusu askari hao kufanya kazi na CHADEMA" ... nadhani siyo muhimu sana. Polisi wanatakiwa wajue kuwa wanapaswa kufanya kazi za Watanzania siyo CHADEMA wala CCM, wala chama cha siasa! Mbona hata sasa wanakataa kufanya kazi walizotumwa na wananchi na bado we are surviving? au unafikiri polisi kutakiwa kutoa ulinzi kwenye mikutano ya Vyama vya siasa ni kazi za vyama hivyo? hiyo ndiyo kazi waliyoitiwa...usalama wa raiya na mali zao. Pamoja na CHADEMA au CUF ambao ni raiya halali wa nchi hii! Lakini ni mara ngapi raiya na mali zao wamekuwa wahanga wa matukio ya uvunjifu wa amani na mauaji ya polisi?...Wasipofanya kazi na CHADEMA we will do just fine and is what we actually want. Wangelijua hilo mapema we wouldn't have been here at first place.
Na napenda nikutoe hofu kuhusu hilo kwani polisi na vyombo vingine vya usalama wana tabia ya ajabu kidogo ya "Kuimba Wimbo wa Bosi" Hata akija shetani leo watafanya naye kazi vizuri tu kama walivyofanya na malaika jana! Nawafahamu vizuri hawa watu, usijali kabisa juu ya hilo.

Utaratibu wa mahusiano ya ndoa na familia? Haya ni mambo binafsi sana. Nadhani hata wewe binafsi una mambo yako ambayo usingependa kusikia yanajadiliwa na watu wengine. Na kuna mengine hutapenda hata kushauriwa na mtu. Kuwa mwanasiasa hakumfanyi yeye kuwa siyo binadamu wa kawaida. Bado ni vizuri ikakumbukwa ni binadamu na ana haki zake, ambazo zinapaswa kuheshimiwa. Na kama kutokuwa na mke wa ndoa ni tatizo sana ni viongozi wangapi wana "wake wa ndoa" na ni mafuska wanaotisha? kuna haja gani ya kuwa na ndoa hiyo? Bado labda ni kwa kuwa hujajua. Hiyo ikulu yako... "ni mahali patakatifu" imeshuhudia kukaliwa na rais ambaye hiyo ndoa ilishamshinda na akaamua kuachana na mwenzie kienyeji. Ila kwa sababu ya upotofu huo wakamshauri arudiane na "mwenziwe" ili tu waonekane kwa picha nzuri. Unajua ni adha gani mliwasababishia kwa kuwaweka pamoja? mi huwa nashawishika kuwa hata yale matibabu aliyokwenda kufanya ulaya ni matokeo wa ugomvi wa ndani! Otherwise ni kwa nini hajawahi kuumia kabla na baada ya pale? ( Siyo nia yangu kuongelea maisha yake, nataka uone how you are wrong). Bado hiyo "ndoa concept na mahali patakatifu" ikasababisha ikulu ikapata rais fuska ambaye wengi wanajua uchafu wake hata baada ya kuoa! Na bado kuna watoto kibao ambao wamezaliwa mtaani kwa sababu hizo huku mkiambiwa ana mke mmoja na watoto wangapi sijui. Na wala hukumbuki yule kiongozi mashuhuri wa chama na serikali ambaye aliwahi kuwa Mwalimu mkuu shule moja na akampa mimba mwanafunzi na ameendelea kuwa mtakatifu mbele yenu mpaka leo.(Hizi ni tabia binafsi tu, hata wewe una zako!) Hizo busara za aina hiyo huwa hazilengi kutatua matatizo ila zinakimbilia kuyafunika na kutafuta "sura nzuri". Na ni kwa sababu ya busara za aina hiyo ndiyo maana tumeishia kuwa na "Muungano Hoi" na nchi yenye manunguniko kila kukicha.
Kama ni ndoa tumwache Mzee Slaa aamue anafunga lini na na nani. Yeye ni mtu mzima na amekuwa kiongozi wa muda mrefu. Naamini anajua ni lipi anapaswa kufanya juu ya hili na ni wakati gani ni muafaka kwake. Ni suala binafsi zaidi. Otherwise kama una uelewa wa sheria japo kidogo , mpaka hapo walipo yule ni mkewe kwa tafsiri ya sheria ya ndoa ya Tanzania, ambayo kama unaona ina mapungufu unapaswa kumwambia mbunge wako apeleke hoja bungeni sheria irekebishwe.

Tuhuma za ubadhilifu ndani ya chama chake? Ungewahi kuwa kiongozi ungeelewa kuwa kuna wakati matatizo yanatatuliwa kwa busara zaidi ya sheria. Kuna wakati sheria hutakiwa kupinduliwa kwa ubinadamu. Hata polisi ukipelekwa huwa huambiwi "sasa umekamatwa una kwenda ndani" Labda wawe na visa na wewe! nimeona wengi tu wanashauriwa kuzingatia ujirani....."karudishe tu simu ya watu tuyamalize" "magereza siyo nzuri kijana" "Kazungumzeni nyumbani, talaka siyo nzuri mna watoto" Sheria haitoshi kuendesha maisha ya binadamu aliyestaarabika! Nikirudi kwa Mzee Slaa, sijawahi hata kuuliza ni kweli au uwongo kuwa alitumia fedha hizo, na sijajua aliwahi kutumia kwa lipi. Kama nilivyosema awali unaweza kufanya "kosa" ambalo busara na ubinadamu ukaamua ilikuwa muhimu ufanye hivyo na ukaachwa tu. Nikupe mfano: Kuna siku niliwahi kuchukua gari la bosi nikamkibiza mfanyakazi mwenzangu hospitali baada ya kuuanguka ghafla. Sikuomba gari wala ruhusa kazini. Na kwa taarifa yako bosi alikuwa na kikao na Waziri na alichelewa appointment! Unafikiri walinifanyaje? hata wangetaka kunipa warning wangeshindwa kueleweka na jumuiya!..........Nashauri: kwa kuwa hatukuwepo wakati anachukuwa, na kwa kuwa hatujui alikwenda kufanyia nini na kwa kuwa hatukuwepo anapohojiwa na chama, na kwa kuwa hatujui kama chama waliona nini....ni vizuri tukawaachia WanaCHADEMA hilo. Otherwise lingekuwa worse angeshasimamishwa uanachama na chama chake......by the way what is the point of kujidai tuna uchungu na milioni 140 wakati kuna billions zinatumika ovyo kila siku na serikali iliyo madarakani? Ni nani haoni kuwa nchi imekuwa incapacitated mpaka haijiwezi tena ili hali viongozi wakijilimbikizia mali na fedha kwenye account nje ya nchi? Huu ndiyo uzalendo gani kwanza kushindwa kuona boriti na kushobokea vibanzi. Au wale wa EPA waliokwiba na wakarudisha ni malaika? ( Kwa taarifa yako hawakurudisha wala rais hakuwa na nia ya dhati juu ya hilo) vinginevyo it is point less kumpeleka mtu mahakamani kwa tuhuma za ufisadi na kumpigia kampeni kuwa ni mtu safi, kabla hata mahakama haijatoa hukumu. Na wala sikusikia mtu akiweka pingamizi la kuingiliwa kesi iliyo mahakamani kwa kuhukumu hana hatia, ni kiongozi safi wakati mahakama haijamaliza kazi( of which inaeleweka ataachiwa huru!) na baada ya kukosa ubunge unampa ubalozi! anawakilisha nini? ufisadi?.....Hilo hukuliona?.....Uzalendo!??.... hili somo ni gumu sana..tuliache. Otherwise tuache unafiki.

Naunga mkono hoja ya Watanzania kuacha ushabiki wa kisiasa, waangalie maslahi ya Taifa na waache kutumiwa, ila ni kwa mtizamo tofauti na wako. Napenda kuona Tanzania huru, ambapo haki za wote, hata mzee Slaa na wanaokamatwa kila siku (mahabusu na wafungwa) zinaheshimiwa. Tanzania huru ambapo matatizo yanashughulikiwa kwa dhati kwa kutafuta chanzo badala ya kufunika na ku save faces. Tanzania huru ambapo vijana wanathaminiwa na kupewa nafasi yao katika kuongoza vita dhidi ya umaskini, magonjwa na maradhi na siyo kutafutwa wakati wa kampeni tu. Tanzania huru ambapo watanzania watajua kumchagua kiongozi siyo kwa sababu ni mwenzetu, wa chama chetu , wa dini yetu au wa kabila letu, ila kwa kuwa ni muwajibikaji, mchapa kazi na mwaminifu.....Naaam Tanzania huru ambapo hata mhalifu anapewa hukumu stahili badala ya kubambikwa kesi za uwongo na za kutunga kama ilivyo sasa!

Sijui nisemeje...nashawishika kuwa ndugu yangu Hamy D kuna kitu unachojaribu kufanya. Ila sijajua ni kipi, kwani hoja zote unazotoa kama unavyoona mwenyewe hazijitoshelezi wala hazibebi maana ya dhati.

Niwie radhi kama nitakuwa nimekuudhi kwa mtizamo wangu.
 
  • Thanks
Reactions: Pai
Mkuu, Nswima, unajaribu sana kumtetea dr slaa wakati amelaaniwa na Mungu. Kumbuka zinaa aliayokataza Mungu haiweI kuhalalishwa na sheria yoyote ya kdunia. Kumbka, hakuna aliye mkuu zaidi ya Mungu na mamlaka zote ulimwenguni zinatoka kwake. Zinaa ni zinaa na haiwezi iutakaswa na post zetu humu mitandaoni. Pia hiyo zinaa imepelekea kuzaliwa kwa watoto 3 wa nje ya ndoa. Hilo doa halitakasiki.

kuhusu hiyo mifano ya akina Kiza Besigye na Morgan Tsvangirai uliyotoa, nadhani jibu unalo mwenyewe. Hao watu kutokana na ujinga wao, walidhani kuwa kutukana vyombo vya dola ni ufahari. Ndo maana mpaka sasa ndoto zao za kwenda ikulu zimeyeyuka. Besigye tayari amestaafu siasa bila ya kuingia ikulu. Tsvangirai naye muda si mrefu atapata aibu katika huu uchaguzi wa zimbabwe.

Mungu alipokuwa ana mlaani Slaa na wewe ulikuwepo?.
 
hivi Slaa alipoanguka chooni kule mwanza madaktar wake walisema anaumwa nn, kama ana kifafa semeni watu wa ufipa mapema
 
Ni vyema kwa CHADEMA wakajitathmini na kuibua mtu mwingine badala ya kutegemea mtu mmoja kuwa nguzo ya chama ilhali nguzo yenyewe imeanza kuchoka.

Kwa hali ilivyo sasa, anguko la Dr Slaa ni anguko la CHADEMA.
Ama kweli,akili ni mali!! Unaacha nyumba yako(CCM) inateketea kimaadili,kama huoni vile unakwenda kwa jirani (CDM) eti kuwashauri ili nyumba yao iwe imara kimaadili!!
Siku zote uzalendo huanzia nyumbani,naomba utushauri na sisi (CCM)chama chetu tusimsimamishe nani tumuweke nani kwa ushindi wa kishindo
?
 
Kweli Dr. Slaa kawashika pabaya magamba hamlali bila kumtaja? Mungu mbariki Dr. Slaa, Mungu ibariki CDM Mungu ibariki Tanzania.
 
Hivi bado kuna watu hadi leo hii wanaota slaa atakuwa rais wa inji hiii?????? mnahitaji maombi
 
Mikael P Aweda,

Ni kweli kwamba Dr Slaa alikuwa na mahusiano mazuri na baadhi wa maafisa wa serikali, ikiwemo na vitengo vya usalama, na kama utakumbuka hili ndilo lilimsaidia kujizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa watanzania kwa kuibua mambo ya ufisadi. lakini kwanini haujiulizi kwamba umaarufu wa Dr Slaa bado ni ule ule?, kwanini sasa hapati taarifa yoyote ya ufisadi?, ni kwamba ufisadi umekwisha serikalini? jibu ni hapana, ila kwa sasa Dr SLAA hana tena mahusiano mazuri na maafisa wa serikali. Hili ni tatizo kubwa sana hasa kwa mtu ambae anatarajia kuwania nafasi ya urais.

Mwanalumumba HAMY-D mimi ninakupongeza kwa dhati kwa kuendelea kuing'arisha CHADEMA na viongozi wake wakuu hasa Dkt Slaa na Kamanda Mbowe hapa JF.

Kila ukigusa keybord lazima uitaje CHADEMA, Dkt Slaa ama Mbowe, hiyo ni dalili ya wazi kuwa mapenzi yako kwa Chadema ni makubwa sana ingawa umelzamika kuitumikia lumumba project ili watoto wako(kama unao lakini) waende cmsalani.

Siku hizi afisa habari wa chama chetu Tumaini Makene hapati shida ya kuwafahamisha Watanzania na dunia nzima juu ya kile kinachoendelea kufanywa na CHADEMA kwakuwa afisa habari wa kujitolea kutoka lumumba yupo.

Nikuhakikishie tu kwamba watumishi waaminifu na wazalendo wa nchi hii wanaofanya kazi ndani ya serikali ya ccm na wengine kwenye vyombo vya dola bado wana imani kubwa sana na Dkt Slaa pamoja na uongozi mzima wa CHADEMA. Kama unadhani kuwa taarifa za ufisadi wenu hazivuji basi nikupe pole kwakuwa umeamua tu kujitia upofu wakati macho yako yanaona.

Unaweza kujiuliza ilikuwa kuwaje CHADEMA ikawatambua maafisa usalama wa Taifa waliokuwa wanatumiwa na mwigulu kujaribu kutengeneza kesi feki za ugaidi dhidi ya wanachama wetu na viongozi wetu? maafisa hao walitajwa kwa majina yao na Mabere Marando, kama kweli siku hizi siri zenu hazivuji unaweza kutuambia hii habari ya maafisa usalama kutumika na ccm hata kutaka kuwarubuni na kuwahonga vijana wetu wa ulinzi na usalama ili wakaotoe ushahidi wa uongo dhidi ya viongozi wetu zilipatikanaje?

Wakati unaendelea kujikusanyia buku saba zako toka hapo Lumumba nakusisitizia kwamba nimeipenda sana kazi yako ya kuinadi CHADEMA na hasa kwa kazi yako kubwa sana ya kumnadi Dkt Slaa hapa JF.
 
Nilishasema mwaka juzi kwenye arusi ya dadangu na narudia kusema leo ili kila mtu asikie: ''Slaa ni mtu anayeugua ugonjwa wa akili unaotokana na laana ya kuacha kazi ya Mungu na kugeukia mambo ya kidunia''

Kwanini Dr Slaa pekee kila siku humu jamvini? Sasa mnatuchagulia nani awe Rais ajaye? Na nani kasema Dr Slaa atagombea Urais? Naomba tujenge Taifa letu sio kila siku Dr Slaa, Mbowe,Zitto au LISSU. Kuna mambo mengi sana yenye tija katika mstakabari wa hili Taifa.
 
we umeendika kwato kisa housgerl wa slaa
Hata kuandika vizuri huwezi, (punctuation) wala sishangai haya ni matokeo ya serikali dhaifu ya maCCM, inaharibu vijana, uwezo wa kufikiri unakuwa mdogo, Yes, kwani ukiwa ni haouse girl wa Dr.Slaa inakuwa ni taabu? ok vipi wale jamaa wa TISS? walifanikuwa kukula mzigo?
 
Kwanini Dr Slaa pekee kila siku humu jamvini? Sasa mnatuchagulia nani awe Rais ajaye? Na nani kasema Dr Slaa atagombea Urais? Naomba tujenge Taifa letu sio kila siku Dr Slaa, Mbowe,Zitto au LISSU. Kuna mambo mengi sana yenye tija katika mstakabari wa hili Taifa.
 
HAMY-D una wivu mtoto wa kike weee!!!!!!!!!!! na unazikamata kweli buku tatu tatu!!
 
Back
Top Bottom