Kwa muktadha huu: Dr Slaa ikulu hapamfai!

Kwa muktadha huu: Dr Slaa ikulu hapamfai!

Ham mada si usitaafu siasa kama mwenzako Christina Lucas aka Chris lucos make naona siku hizi umekosa habari ya kupost zaidi ya Dr Slaa, naona anakunyima usingizi.
 
slaa hakuna anapofaa si msikitini wala kanisani hatuwezi kuwa na rais muhuni sisi hili siyo taifa la wahuni uhuni wao wabaki nao chadema hukohuko.

Pima uhuni wako kabla haujanyooshea kidole mwenzako. Inawezekana kabisa wewe ukawa muhuni uliyekithiri.
 
Aweda, kumbe na wewe ni dj zero? Hivi huo upumbavu alioandika Nswima hawe unauita ni shule. Kama ndo hivyo basi chadema ni majanga. Hamna uwezo wa kushirikisha akili zenu hat kidogo

Hivi kumtukana mwenzako -------- kwako ndio SHULE.Ustaarab ni kitu cha bure jifunze kujadiliana na wapinzani wako bila kuingiza lugha zilikosa staha au ndivyo mnavyofundishwa huko CCM?
 
Sasa wewe mbona unaenda kwenye mambo binafsi? Hayo tuyaweke pembeni.
Tukiingia huko itakuja swali la JK ana wake wangapi na watoto wangapi? Siku ya kuapishwa tuliambiwa ana mke mmoja na watoto kadhaa. Hata kama ni watoto 30 si tungeambiwa? Unajua kilichokuwa kinafichwa?
Je, JK kuwaomba wezi wa EPA warudishe pesa ni uvunjifu wa KATIBA?
Je, unajua JK amehusishwa kwenye Richmond na Lowasa na mpaka sasa hakuna majibu?
Hizo tuhuma za kutunga za DHIDI ya chadema haziwezi kufuta.
Mnakumbuka kauli ya Tundu Lissu mwaka 2010 kuhusu nani anayebadilisha damu kila baada ya miezi 6? Unajua kauli ya Dr Slaa alipomwuliza Mzee Makamba kwa nini ulifukuzwa kazi ya ualimu mkuu? Tangu hapo makamba hajawahi kusema hayo unayoyasema wewe hadharani tena!
Tuache mambo binafsi tujadili hoja zenye tija ufisadi.
Hapo kwenye red ukumbuke JK ni muislamu na anaruhusiwa kuwa na wake wanne na watoto hata 1000

sasa Dr slaa si aliapa kiapo cha kutumikia upadre vipi leo hii anaukimbia upadre au watoto wanazidi kung'ara?
 
Endeleeni kumjadili Dr Slaa wakati CCM yenyewe mpaka sasa haijitambui ni nani atagombea uraisi 2015. Wanashindwa ku dili na makundi yaliyopo sasa kuelekea uchaguzi wa 2015 maana wengine Wameanza kampeni kwenye nyumba za ibada
 
Nilishasema mwaka juzi kwenye arusi ya dadangu na narudia kusema leo ili kila mtu asikie: ''Slaa ni mtu anayeugua ugonjwa wa akili unaotokana na laana ya kuacha kazi ya Mungu na kugeukia mambo ya kidunia''

Kichaa ni wewe unaetaka ukuu wa wilaya kwa kugawa nyuchi zako wa viongozi wa magamba.
 
Miaka 67 atakuwa babu sana aachie na wenzake


Bora mwenye miaka 67 mwenye nguvu, akiri na Afya tele kuliko mwenye umri mdogo wakati akiwa na Afya na akili dhaifu huku akianguka majukwaani bila kuteleza wala kusukumwa.
 
Kumbe Dr Slaa ndio kiboko ya magamba wote mnamugopa mnaomba asigombee vyura magamba nyie na 2015 Slaa atagombea na atakuwa Rais wenu nawabakiza viporo.
 
Hoja yako ni nyepesi sana Mkuu ya kwanini Dr Slaa hastahili Ikulu.Hivi ni kweli Mungu wa Upendo analaani?Nani kakudanganya kuwa Mungu ana hisia?
Kuhusu Tsvangirai na Besegye nakushauri uwe unafuatilia siasa za nje pia.

slaa kajilaani mwenyewe kwa kuchukua wake za watu tena zaidi ya wawili wala hahitaji kulaaniwa ni yeye mwenye anamikosi na nuksi za kutosha atachafua taifa letu bule.
 
Nimesoma makala yako nimegundua sio mtu unayependa kuafua habari na ukweli wote, ndio maana story yako haiko balanced, nakushauri kajipange upya kwani baadhi ya hoja unazoibua hapa zilishajibiwa kwa uwazi kabisa. umri sio kigezo si unamuona Mugabe ana zaidi ya miaka 80 mbona anaongoza vizuri na nchi inaenda? kibaki wa kenya amestaafu ana miaka mingapi, je alishindwa kuiongoza kenya? kajipange upya kisha uje na hoja banuai
 
slaa hakuna anapofaa si msikitini wala kanisani hatuwezi kuwa na rais muhuni sisi hili siyo taifa la wahuni uhuni wao wabaki nao chadema hukohuko.


Mbona huyo Rais wako aliyekaa miaka 7 ana watoto wa4 nje ya ndoa(hao wanaofahamika) Wawili kawapatia kwenye matokeo yake ya kupenda disco.

Sasa mkuu hapo kati ya Silaha na Jei Kei nani muhuni maana kama watoto nje ya ndoa jamaa kazidi na bado alikuwa mpenda disco.
 
Wake halali?
Hapo kwenye red ukumbuke JK ni muislamu na anaruhusiwa kuwa na wake wanne na watoto hata 1000

sasa Dr slaa si aliapa kiapo cha kutumikia upadre vipi leo hii anaukimbia upadre au watoto wanazidi kung'ara?
 
Hoja yako ni nyepesi sana Mkuu ya kwanini Dr Slaa hastahili Ikulu.Hivi ni kweli Mungu wa Upendo analaani?Nani kakudanganya kuwa Mungu ana hisia?
Kuhusu Tsvangirai na Besegye nakushauri uwe unafuatilia siasa za nje pia.

Mkuu, nilichoongea ndicho nilichokimaanisha. Nambie kama hao akina Tsvangirai na Besigye wamefanikiwa kuingia Ikulu. Nimesema kuwa Besigye amelazimika kustaafu siasa baada ya kuona kuwa uwezekano wa yeye kwenda Ikulu ni mdogo kutokana na ujinga wake mwenyewe wa kutukana vyombo vya dola. Tsvangirai hata iweje hawezi kutangazwa kuwa Rais wa Zimbabwe. Subiri huu uchaguzi ujao ndipo utakapothibitisha kauli yangu.

kuhusu Uzinzi wa dr slaa, ni wehu pekee watakaomtetea. Kila kitu kipo wazi kabisa
 
Acha uwongo wa mchana kweupe, CHADEMA hawewezi kuwa na mahusiano mabaya na vyombo vyote vya ulinzi. Unadhani hao wanaotoa nyaraka za ufisadi za ccm kutoka ndani ya serikali ni Usalama wa Taifa wa KENYA au Tanzania? Tuna matatizo na hao wachache wanaoharibu sifa ya vyombo hivyo, na mara nyingi na wale wenye madaraka makubwa.
Je, unajua kwamba Chadema ilishinda kwa kura nyingi kituo cha Lugalo? JK aliachwa Mbali sana. Je, unajua kuwa Ukonga magereza na field force Chadema ili shinda kwa kishindo? Wwe unazungumzia vyombo gani mkuu?

Pili, vipi pendekezo lako la moyoni anaendeleaje kisiasa? Unadhani anasafishika? Vipi tukilinganisha uchafu wake na tuhuma zako hizo za uwongo dhidi ya Dr Slaa?

Mikael P Aweda,

Ni kweli kwamba Dr Slaa alikuwa na mahusiano mazuri na baadhi wa maafisa wa serikali, ikiwemo na vitengo vya usalama, na kama utakumbuka hili ndilo lilimsaidia kujizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa watanzania kwa kuibua mambo ya ufisadi. lakini kwanini haujiulizi kwamba umaarufu wa Dr Slaa bado ni ule ule?, kwanini sasa hapati taarifa yoyote ya ufisadi?, ni kwamba ufisadi umekwisha serikalini? jibu ni hapana, ila kwa sasa Dr SLAA hana tena mahusiano mazuri na maafisa wa serikali. Hili ni tatizo kubwa sana hasa kwa mtu ambae anatarajia kuwania nafasi ya urais.
 
Last edited by a moderator:
Ni vyema kwa CHADEMA wakajitathmini na kuibua mtu mwingine badala ya kutegemea mtu mmoja kuwa nguzo ya chama ilhali nguzo yenyewe imeanza kuchoka.

Kwa hali ilivyo sasa, anguko la Dr Slaa ni anguko la CHADEMA.

mnapozungumzia umri kwani Slaa ataibeba Tanzania mgongoni mseme itamlemea? Akili na michango ya Slaa ni imara na ina mashiko, tunacho hitaji ni busara zake na sio umri

Issue ya ndoa yake huo ni upungwani kuzungumzia maisha binagsi ya mtu, hivi unajua Mh Ben alikaa bila mke kwa muda gani na walipatanishwa lini na akawa rais wa nchi kwa tiketi ya ccm?

Sidhani kama umekuwa consultant wa Cdm hadi uwashauri kutafuta mgombea mwingine wa urais, ni kikao gani cha Cdm kilicho kaa na kutangaza Dr Slaa ndie mgombea urais wa Cdm 2015? Ushauri wa bure kwenu watu wa buku saba ni kwamba bora mtatue mipasuko ndani ya chama chenu badala ya kuiota Cdm mkiwa hamjalala
 
Mikael P Aweda,

Ni kweli kwamba Dr Slaa alikuwa na mahusiano mazuri na baadhi wa maafisa wa serikali, ikiwemo na vitengo vya usalama, na kama utakumbuka hili ndilo lilimsaidia kujizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa watanzania kwa kuibua mambo ya ufisadi. lakini kwanini haujiulizi kwamba umaarufu wa Dr Slaa bado ni ule ule?, kwanini sasa hapati taarifa yoyote ya ufisadi?, ni kwamba ufisadi umekwisha serikalini? jibu ni hapana, ila kwa sasa Dr SLAA hana tena mahusiano mazuri na maafisa wa serikali. Hili ni tatizo kubwa sana hasa kwa mtu ambae anatarajia kuwania nafasi ya urais.

Naona unajisifu kuwa siku hizi siri za ufisadi hazimfikii Dr. Umejipambanua pia kuwa ufisadi bado upo palepale kwenye serikali yenu ila unajipa hongera kwa kufanikiwa kudhibiti uvujaji wa siri za ufisadi huo ambazo according to you ndizo zilimpaisha Dr. Hivi unafikiria vizuri unapaandika humu?
By the way, Hivi unajua umri wa viongozi waliopo madarakani au ni kigezo kwa Dr. SLAA pekee!
 
Last edited by a moderator:
HAMY-D,
Wewe ni mpenda amani sina budi kukupongeza kwa uchambuzi wako murua uliojaa maneno ya ujenzi, tunashakuru kwa kuweka wazi hizi bayana za Dr Slaa.
 
Jifunze kuwa na roho ya utu wewe, mimi nimeeleza hisia zangu kuhusu Dr Slaa hasa kwenye uhalali wake wa kugombea urais, mambo ya ajali yanatoka wapi ndugu?

Kuhusu suala la mahusiano ya Dr Slaa na vyombo vya ulinzi hilo halina ubishi, mahusiano ni mabovu, askari kwa wanajeshi wamekiri hili mara kadhaa.

Acha kubaka demokurasia, ama siku hizi vyombo vya ulinzi ndio wanapiga kura??
na tunampenda mtu jasili asiye na uwogo na si mtu wa kujipendekeza...
Mlipo muuwa kamamanda Mwangosi, alimtumia msg IGP Said mwema kamuulizie...

Dr.tunamhitaji hana uoga na kujipendekeza.

Jifunze kuishi wewe kama wewe siyo kukaa unajipendekeza kama ambayo unayoendesha maisha yako.

that why tunaomba Mungu upate tena ajali ya pikipiki ili na huo mkono mwingine ukatike... ila usife ili 2015 ujionee mambo!
 
HAMY-D,

Wewe ni mpenda amani sina budi kukupongeza kwa uchambuzi wako murua uliojaa maneno ya ujenzi, tunashakuru kwa kuweka wazi hizi bayana za Dr Slaa.

Mkuu Ritz,

Nashukuru sana kwa pongezi, unajua hili suala la amani ni jambo letu sote, sio serikali wala sio vyama vya upinzani. Hatuna budi wapenda amani wote tushirikiane kuilinda tunu hii ambayo haina bei.
 
Last edited by a moderator:
Lowasa mume wako nini??? Badala yakuongelea maendeleo wewe unaongelea watu!!!!!!! ama kweli bado wewe ni mbumbumbu kabisaaa . . . Jipange mtuwangu
 
Back
Top Bottom