Kwa muktadha huu: Dr Slaa ikulu hapamfai!

Mwanzia Thread an mtindio wa ubongo. Miaka 10 nyuma Mwai Kibaki alikuwa na Umri gani na Je? unajua amefanya nini Kenya? Thread yako haina mshiko unaonyesha jinsi CCm ilivyokunyonya ubongo na kukuacha mtupu. Lowasa kwa sasa ni mkubwa kwa miaka miwili na Sitta vivyo hivyo na wote wanataka Urais. Kama hujafanya uchunguzi huna haki ya kutoa habari

Mkuu nimefungua bila kusoma mwanzisha mada kumbe ni nepi! Tumsamehe anapigania buku saba! Lakini ukweli anaujua na angalia maelezo yake yalivyo,povu tupu!
 
Uzee ni dhana inayojidhihisha kwa namna mbalimbali, moja ni matendo, namna ya kufikiri na maamuzi. Kwa kigezo hiki naona CCM wote ni vizee vihunihuni, mf Gulunet, Kazi, 6, Harambee, Tusi kubwa, Mbwa na Nyepes wa CDM
 
WanaJF!

Pamoja na mapenzi makubwa ambayo wengi wenu mmekuwa nayo kwa Dr Slaa na mngependa kuona siku moja Dr Slaa akiapishwa na kuwa rais wa Tanzania, ila nasikitika kusema hilo haliwezekani kwa kuwa Dr Slaa Ikulu hapamfai.

Ni muhimu kwa mashabiki na wanachama wote wa CHADEMA wenye hamu ya kuona Dr Slaa anakuwa rais kufahamu jambo hilo ni gumu na hatuna budi kulikubali, ugumu wenyewe kwa Dr Slaa kuwa rais upo kwenye maeneo yafuatayo;

Umri wa Dr Slaa sio sahihi kutumikia umma.

Dr Slaa ambae imeandikwa kuwa amezaliwa October 29, 1948, kwa sasa kama angekuwa mtumishi kwenye ofisi za umma basi angekuwa ni mstaafu miaka 5 iliyopita.

Ieleweke mpaka ifikapo mwaka 2015 Dr Slaa atakuwa na miaka 67, umri ambao hawezi kumudu changamoto za nchi kwani ni mkubwa mno na madaktari uwa wanashauri mtu mwenye umri huo inapaswa apumzike.

Mahusiano ya Dr Slaa na vyombo vya ulinzi na usalama.

CHADEMA na viongozi wake wakubwa (Mbowe na Dr Slaa) wamekuwa wakitangaza hadharani kuwa hawana maelewano mazuri na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Viongozi hawa wa CHADEMA wamekuwa wakilalamika kuwa chama chao kimekuwa kinakandamizwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kupokea maagizo toka serikalini.

Jambo ambalo limekuwa likipingwa na vyombo hivyo na imeshuhudiwa kwa askari kadhaa kusema wanasiasa wa upinzani hawapendi kuona hali ya nchi hii ikiwa kwenye amani na utulivu. katika hali hii, unatarajia askari watakuwa tayari kufanya kazi na CHADEMA endapo wakitwaa dola?

Utaratibu wa mahusiano ya ndoa na familia.

Kama itakumbukwa kauli ya hayati mwl Nyerere iliyosema, "ikulu ni mahali patakatifu" ingawa aliitumia kueleza rushwa, ila neno takatifu lina maana pana na kwa upande wa mahusiano ya familia ni sawa kusema rais anae tarajiwa kuingia Ikulu ni lazima awe na mke/mume wa ndoa pia na familia inayo kubalika kisheria.

Tuhuma za ubadhilifu ndani ya chama chake.

Dr Slaa alipata tuhuma kuwa amekwapua pesa kwa namna ya kujikopesha na kilikuwa kiasi cha milioni 140 pesa za kitanzania, tuhuma hizi hapo awali alipinga kuwa si za kweli, ila baada ya kuhojiwa mara kadhaa Dr Slaa alikiri kuwa ni kweli alichukua pesa hizo na tayari amezirejesha.

kwa mtu ambae tayari ameonyesha udhaifu mkubwa katika kupigana na nafsi yake kwa matamanio mbalimbali ya kidunia, hasa masuala yanayo husu fedha, hii ni hatari kwa HAZINA (mfuko mkuu wa serikali) yetu ya taifa kama Dr Slaa akipata urais.

HITIMISHO,

Kwa mujibu wa hoja mbalimbali kama nilivyo eleza, ni ukweli usio pingika kuwa Dr Slaa Ikulu si mahali pake na ni kheli afuate ushauri wa madaktari wa kupumzika na kuachana na mambo ya utumishi wa umma kama anavyo panga.

kuhusu mashabiki ni vyema sasa tukaacha ushabiki wa kisiasa ambao umekuwa hauna faida yoyote zaidi ya kurudisha nyuma maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla badala yake tujikite kwenye uzalendo na kuchagua viongozi wanaofaa kwa mustakabali mwema wa taifa letu.

Tukishika dola tunahalalisha haramu, pombe bangi, uzinzi nk
 
kimuonekano tu hafai licha ya kuja kwa matendo na hoja, ndio kabisa
 
Mwanzia Thread an mtindio wa ubongo. Miaka 10 nyuma Mwai Kibaki alikuwa na Umri gani na Je? unajua amefanya nini Kenya? Thread yako haina mshiko unaonyesha jinsi CCm ilivyokunyonya ubongo na kukuacha mtupu. Lowasa kwa sasa ni mkubwa kwa miaka miwili na Sitta vivyo hivyo na wote wanataka Urais. Kama hujafanya uchunguzi huna haki ya kutoa habari

Wote wazee, hatutaki mtu ambae suruali itaanguka akiwa kwenye jukwaa...!
 
WanaJF!

Pamoja na mapenzi makubwa ambayo wengi wenu mmekuwa nayo kwa Dr Slaa na mngependa kuona siku moja Dr Slaa akiapishwa na kuwa rais wa Tanzania, ila nasikitika kusema hilo haliwezekani kwa kuwa Dr Slaa Ikulu hapamfai.

Ni muhimu kwa mashabiki na wanachama wote wa CHADEMA wenye hamu ya kuona Dr Slaa anakuwa rais kufahamu jambo hilo ni gumu na hatuna budi kulikubali, ugumu wenyewe kwa Dr Slaa kuwa rais upo kwenye maeneo yafuatayo;

Umri wa Dr Slaa sio sahihi kutumikia umma.

Dr Slaa ambae imeandikwa kuwa amezaliwa October 29, 1948, kwa sasa kama angekuwa mtumishi kwenye ofisi za umma basi angekuwa ni mstaafu miaka 5 iliyopita.

Ieleweke mpaka ifikapo mwaka 2015 Dr Slaa atakuwa na miaka 67, umri ambao hawezi kumudu changamoto za nchi kwani ni mkubwa mno na madaktari uwa wanashauri mtu mwenye umri huo inapaswa apumzike.

Mahusiano ya Dr Slaa na vyombo vya ulinzi na usalama.

CHADEMA na viongozi wake wakubwa (Mbowe na Dr Slaa) wamekuwa wakitangaza hadharani kuwa hawana maelewano mazuri na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Viongozi hawa wa CHADEMA wamekuwa wakilalamika kuwa chama chao kimekuwa kinakandamizwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kupokea maagizo toka serikalini.

Jambo ambalo limekuwa likipingwa na vyombo hivyo na imeshuhudiwa kwa askari kadhaa kusema wanasiasa wa upinzani hawapendi kuona hali ya nchi hii ikiwa kwenye amani na utulivu. katika hali hii, unatarajia askari watakuwa tayari kufanya kazi na CHADEMA endapo wakitwaa dola?

Utaratibu wa mahusiano ya ndoa na familia.

Kama itakumbukwa kauli ya hayati mwl Nyerere iliyosema, "ikulu ni mahali patakatifu" ingawa aliitumia kueleza rushwa, ila neno takatifu lina maana pana na kwa upande wa mahusiano ya familia ni sawa kusema rais anae tarajiwa kuingia Ikulu ni lazima awe na mke/mume wa ndoa pia na familia inayo kubalika kisheria.

Tuhuma za ubadhilifu ndani ya chama chake.

Dr Slaa alipata tuhuma kuwa amekwapua pesa kwa namna ya kujikopesha na kilikuwa kiasi cha milioni 140 pesa za kitanzania, tuhuma hizi hapo awali alipinga kuwa si za kweli, ila baada ya kuhojiwa mara kadhaa Dr Slaa alikiri kuwa ni kweli alichukua pesa hizo na tayari amezirejesha.

kwa mtu ambae tayari ameonyesha udhaifu mkubwa katika kupigana na nafsi yake kwa matamanio mbalimbali ya kidunia, hasa masuala yanayo husu fedha, hii ni hatari kwa HAZINA (mfuko mkuu wa serikali) yetu ya taifa kama Dr Slaa akipata urais.

HITIMISHO,

Kwa mujibu wa hoja mbalimbali kama nilivyo eleza, ni ukweli usio pingika kuwa Dr Slaa Ikulu si mahali pake na ni kheli afuate ushauri wa madaktari wa kupumzika na kuachana na mambo ya utumishi wa umma kama anavyo panga.

kuhusu mashabiki ni vyema sasa tukaacha ushabiki wa kisiasa ambao umekuwa hauna faida yoyote zaidi ya kurudisha nyuma maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla badala yake tujikite kwenye uzalendo na kuchagua viongozi wanaofaa kwa mustakabali mwema wa taifa letu.

huyu jamaa akwende mirembe akalambe cpz
 
kwan mbona humzungumzii Lowasa kwa hivyo vigezo hasa umri na ubadhirifu wa pesa za nchi ambae ata hayati Nyererealiagiza asipewe uongozi. najua akili yako imestack ndo maana unatumika na kufikiriwa.
 
Ibada zipi? Katika ibada za Kikristo anayetajwa zaidi ni Yesu Kristo mwokozi wa dunia. Hebu tujuze ni ibada za akina nani hao ambapo Ibilisi hutajwa zaidi?

Nina wasiwasi na ukristo wako,mi kila nikenda kanisan majina haya ndo yanatajwa sana
1.Shetani(mwovu,mtenda dhambi)
2.Mungu(muumbaji wa yesu na Shetani)
3.Yesu(mwokozi,njia ya wokovu)
 
Mambo mengine uamriwa na mazingira tu sio mpaka katiba iseme, sasa suala kama la kikomo cha umri sio mpaka katiba iliseme, ni busara tu itumike kuwa Dr Slaa umri umemtupa mkono na awapishe wengine.

Jambo la kusema eti tuna hofu ya kushtakiwa kuhusu hilo mtatoka patupu, kwa serikali hii ya kikwete hakuna kiongozi mwenye ajenda ya siri na hili taifa.

acha unafiki wewe, lipumba ana miaka mingapi? pinda ana umri gani? lowasa ana miaka mingapi? wasira naye ana miaka mingapi? shimon perez wa israel ana miaka mingapi?, rais wa italia ana umri gani, michael sata je? mgabe je?, urusi je? ujerumani je? ujana si kigezo cha kuongoza na km ndivyo basi hakuna haja ya baraza la wazee ccm lifutwe. wakati huohuo nipe age ya viongozi wa kamati kuu ya ccm tuone km wanapaswa kukalia hivyo viti.
 
Hata kama angekua na miaka 95 kama mandela tunampa urais dr slaa maana anatufaa watanzania kutuongoza
 
Back
Top Bottom