WanaJF!
Pamoja na mapenzi makubwa ambayo wengi wenu mmekuwa nayo kwa Dr Slaa na mngependa kuona siku moja Dr Slaa akiapishwa na kuwa rais wa Tanzania, ila nasikitika kusema hilo haliwezekani kwa kuwa Dr Slaa Ikulu hapamfai.
Ni muhimu kwa mashabiki na wanachama wote wa CHADEMA wenye hamu ya kuona Dr Slaa anakuwa rais kufahamu jambo hilo ni gumu na hatuna budi kulikubali, ugumu wenyewe kwa Dr Slaa kuwa rais upo kwenye maeneo yafuatayo;
Umri wa Dr Slaa sio sahihi kutumikia umma.
Dr Slaa ambae imeandikwa kuwa amezaliwa October 29, 1948, kwa sasa kama angekuwa mtumishi kwenye ofisi za umma basi angekuwa ni mstaafu miaka 5 iliyopita.
Ieleweke mpaka ifikapo mwaka 2015 Dr Slaa atakuwa na miaka 67, umri ambao hawezi kumudu changamoto za nchi kwani ni mkubwa mno na madaktari uwa wanashauri mtu mwenye umri huo inapaswa apumzike.
Mahusiano ya Dr Slaa na vyombo vya ulinzi na usalama.
CHADEMA na viongozi wake wakubwa (Mbowe na Dr Slaa) wamekuwa wakitangaza hadharani kuwa hawana maelewano mazuri na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Viongozi hawa wa CHADEMA wamekuwa wakilalamika kuwa chama chao kimekuwa kinakandamizwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kupokea maagizo toka serikalini.
Jambo ambalo limekuwa likipingwa na vyombo hivyo na imeshuhudiwa kwa askari kadhaa kusema wanasiasa wa upinzani hawapendi kuona hali ya nchi hii ikiwa kwenye amani na utulivu. katika hali hii, unatarajia askari watakuwa tayari kufanya kazi na CHADEMA endapo wakitwaa dola?
Utaratibu wa mahusiano ya ndoa na familia.
Kama itakumbukwa kauli ya hayati mwl Nyerere iliyosema, "ikulu ni mahali patakatifu" ingawa aliitumia kueleza rushwa, ila neno takatifu lina maana pana na kwa upande wa mahusiano ya familia ni sawa kusema rais anae tarajiwa kuingia Ikulu ni lazima awe na mke/mume wa ndoa pia na familia inayo kubalika kisheria.
Tuhuma za ubadhilifu ndani ya chama chake.
Dr Slaa alipata tuhuma kuwa amekwapua pesa kwa namna ya kujikopesha na kilikuwa kiasi cha milioni 140 pesa za kitanzania, tuhuma hizi hapo awali alipinga kuwa si za kweli, ila baada ya kuhojiwa mara kadhaa Dr Slaa alikiri kuwa ni kweli alichukua pesa hizo na tayari amezirejesha.
kwa mtu ambae tayari ameonyesha udhaifu mkubwa katika kupigana na nafsi yake kwa matamanio mbalimbali ya kidunia, hasa masuala yanayo husu fedha, hii ni hatari kwa HAZINA (mfuko mkuu wa serikali) yetu ya taifa kama Dr Slaa akipata urais.
HITIMISHO,
Kwa mujibu wa hoja mbalimbali kama nilivyo eleza, ni ukweli usio pingika kuwa Dr Slaa Ikulu si mahali pake na ni kheli afuate ushauri wa madaktari wa kupumzika na kuachana na mambo ya utumishi wa umma kama anavyo panga.
kuhusu mashabiki ni vyema sasa tukaacha ushabiki wa kisiasa ambao umekuwa hauna faida yoyote zaidi ya kurudisha nyuma maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla badala yake tujikite kwenye uzalendo na kuchagua viongozi wanaofaa kwa mustakabali mwema wa taifa letu.