Kwa mtu mwenye HIV, Ni dalili gani za kwanza humpata, na huonekana baada ya muda gani?

wakuu ahsanteni sana kwa kunipa matumaini, sasa nimepata nguvu na kujijua kuwa niko fresh kabisa..pia nina hakika huu uzi utawasaidia wengi walio na mashaka juu ya afya zao kabla hawajaamua kupima
nikipata nafasi itabidi niende kupima
 
eti wadau kwa hapa dar, ni wapi wanatoa huduma nzuri ya upimaji ukimwi?(mpimaji awe wa kiume)
ahsanteni madokta!
 
Homa za mara kwa mara zisizoeleweka, dizzy, ujauzito kupotea after few month, kuchoka bila kufanya kazi, kijasho chembamba kinavuja, vichomi kila kona, hofu nyingi, mawazo yasiyokwisha, kupenda kuangalia mada nyingi hasa zinazohusu ukimwi, kufuatilia kwa karibu nani kakuambukiza, kuwa na wasiwasi, woga, kukata tamaa.
Aisee dalili ni nyingi sana ila ukishaanza kuharisha tu kwisha habari yako.

Hapo kwenye kupenda kuangalia mada umeongea vice versa.Mtu mwenye HIV hapendi kabisa kusikiliza habari hizo kwani nyingi zinamuongezea hofu
 
Vituo vya Angaza.Tafuta kilichojirani nawe.Vipo katika Hospital za serikali.Kuna Hospital nyingine za binafsi wanapima ila inabidi ulipie.
 
Achana na dalili kaka nenda kapime tu......afu siku hizi ukimwi watu wanapima kama mimba tu....kanunue HIV test....unajitoboa kimtindo kidoleni baada ya dk kama saba hivi utajielewa.
 
Homa za mara kwa mara zisizoeleweka, dizzy, ujauzito kupotea after few month, kuchoka bila kufanya kazi, kijasho chembamba kinavuja, vichomi kila kona, hofu nyingi, mawazo yasiyokwisha, kupenda kuangalia mada nyingi hasa zinazohusu ukimwi, kufuatilia kwa karibu nani kakuambukiza, kuwa na wasiwasi, woga, kukata tamaa.
Aisee dalili ni nyingi sana ila ukishaanza kuharisha tu kwisha habari yako.
Duh! ebwana eeh
 
Achana na dalili kaka nenda kapime tu......afu siku hizi ukimwi watu wanapima kama mimba tu....kanunue HIV test....unajitoboa kimtindo kidoleni baada ya dk kama saba hivi utajielewa.

mkuu hii njia naitaduta sana hata mimi , nitafanya mpango naitafuta hiyo test!
 
Hapo kwenye kupenda kuangalia mada umeongea vice versa.Mtu mwenye HIV hapendi kabisa kusikiliza habari hizo kwani nyingi zinamuongezea hofu
Kabla hujapima unahofu tu huenda umeambukizwa!! hapo ndipoo unapopenda kuchungulia hizo mada za UKIMWI huku ukichukua taswira yako na kucheki upepo kama kweli unao au lah.....sasa ukishapima ukajikuta muathirika ndo maneno yako yanapotimia hapo, kwamba hizo mada wanazikimbia coz zinawaongezea hofu, na hata mtu akifa hawaendi kuzika mpaka ajikubali na ile hali.
 
Hahaaaa hauna utando mweupe kwenye ulimi? Vp asubuhi ukiamuaka hauna tongotongo kubwa machoni? Mafua ama kikohozi cha haja kimepotea?

mkuu Sizinga mimi niko kamili kama mwamba wenye madini ya almasi huko mwadui!
 
Last edited by a moderator:
wakuu ahsanteni sana kwa kunipa matumaini, sasa nimepata nguvu na kujijua kuwa niko fresh kabisa..pia nina hakika huu uzi utawasaidia wengi walio na mashaka juu ya afya zao kabla hawajaamua kupima
nikipata nafasi itabidi niende kupima

kwenye bluu na red unatuchanganya
 
Back
Top Bottom