Kwa mtu mwenye HIV, Ni dalili gani za kwanza humpata, na huonekana baada ya muda gani?

Nahitaji kujua hili wakuu!

Nazani itakuwa msaada kwa wengi , maana ni swala linalotuzunguka sote!

Maambukizo ya VVU na ugonjwa wa UKIMWI

VVU huathiri sehemu nyingi za mwili wa mtu. Vinaweza kufanya hivyo kwa
njia mbili. Njia ya kwanza ni kwa kushambulia moja kwa moja viungo mbali

mbali, njia nyingine ni kwa kudhoofisha mfumo wa kinga na kuruhusu viini
au vimelea vinavyosababisha magonjwa mengine kuingia mwilini. Katika sura

hii, tutaelezea uharibifu wa aina ya kwanza ambao VVU husababisha, katika
nyongeza tutajadili aina ya pili ya uharibifu unaofanywa na VVU.

VVU hushambulia seli za ubongo wa mtu. Hii inaathiri uwezo wa mtu
kufikiri (kwa sababu ya uharibifu uliopo kwenye ubongo). Husababisha maumivu
na ganzi katika mikono na miguu (kwa sababu ya uharibifu wa mishipa

ya fahamu (neva). Husababisha kuharisha (uharibifu ulio tumboni) husababisha
upungufu wa damu na kuvuja kwa damu (husababishwa na uharibifu

unaotokea kwenye damu). Ingawaje VVU, vinasababisha mtu augue, tunafahamu
sio kila mtu, mwenye VVU ni mgonjwa. Ndiyo sababu kuna hatua, za

mtu alieambukizwa anapitia, kuanzia mtu anapoambukizwa na VVU, kipindi
ambacho aliyeambukizwa haonyeshi dalili zozote, hufikia hatua ya alieambukizwa
huanza kuonyesha dalili za mwanzo, na hatimaye UKIMWI.


N i n i d a l i l i z a a l i y e a m b u k i z w a n a V V U ?


Hatua nne za maambukizo ya VVU


1. Wiki chache baada ya kuambukizwa, watu huwa na dalili kama homa ya mafua.

2. Kipindi cha utulivu, wakati kuna dalili chache za UKIMWI.

3. Dalili za awali za UKIMWI.

4. UKIMWI, mwathirika huwa mahututi sana.
Huchukua muda toka kipindi kimoja hadi kingine.


Wiki za mwanzo baada ya maambukizo

Baada ya kuambukizwa VVU, kwa kawaida watu hawawezi kutambua
kwamba wameshaambukizwa VVU; hawawezi kujua kwamba wana VVU
mpaka baadae wanapokwenda kupima au wanapokuwa wagonjwa. Hata

hivyo watu wachache, huanza kuona dalili kuanzia wiki 1-4 baada ya maambukizo
ya virusi. Dalili zinazofanana
na mafua, maumivu ya
koo, homa, maumivu ya kichwa,

maumivu ya tumbo, kuharisha
na kujisikia kuchoka. Baada ya
wiki, vipele vinaweza kutokea

kwenye kifua, uso na shingo. Watu
wanaweza wakatokwa na jasho
usiku, maumivu ya misuli na

viungo, uvimbe wa tezi, kichefu
chefu na kutapika. Dalili hizi
kwa kawaida hudumu kwa muda
mfupi, sio zaidi ya wiki mbili.

Ni nadra kwa hatua ya kwanza
baada ya maambukizo ya VVU
kuwa mbaya sana na kuharibu
mfumo wa neva wa mtu. Mtu

aliyeambukizwa anaweza akawa
na uvimbe kwenye ubongo na
ngozi inayoufunika. Hii inaweza

kusababisha maumivu ya kichwa,
kugangamaa kwa shingo, homa,
kuchanganyikiwa, matatizo ya
mfumo wa neva na kupoteza

fahamu. Mtu anaweza kuwa na
matatizo ya neva kwenye mikono
na miguu na matatizo ya neva za

usoni. Hii inaweza kusababisha
maumivu ya ngozi na shida ya
kutembea, tezi wakati mwingine
huvimba na hubakia zimevimba
kwa miezi au miaka.

Kwa vile dalili hizi huonekana pia kwenye maradhi mengine mbali na
VVU, hatuwezi kusema kuwa kila mwenye dalili zinazofanana na hizi nchini
kwamba ana VVU. Ili mtu afahamu ana maambukizo ya VVU anahitaji

Mitoki
Mitoki mara nyingi huitwa “tezi”,
ni kiini cha mfumo wa kinga ya
mtuo. Huwa zina vimba na kuuma
zinapo kabiliana kuondoa viini vya

maradhi. Mfano, mitoki ya shingoni
huvimba mtu anapopata maambukizo
katika koo. VVU husababisha
kuvimba kwa tezi, wakati mwingine
mwili mzima, wakati mwingine kwa
muda wa miaka.


kupima damu. Hata hivyo, kipimo cha kuchunguza VVU, wiki chache baada
ya maambukizo hakiwezi kutoa matokeo ya uhakika. Sababu ni kwamba
kipimo, huangalia kama mtu ana askari dhidi ya VVU (antibodi). Kama ndio

mwanzo tu wa maambukizo ya VVU na mwili wako bado haujatengeneza
askari dhidi ya VVU, kipimo hakiwezi kuonyesha kama mtu ameambukizwa
au la. Watu wengi miili yao huanza kuonyesha kama ina askari dhidi ya

VVU wiki nne baada ya maambukizo. Mtu yo yote anayedhani kwamba
inawezekana ameshaambukizwa na VVU anaweza kupima kwanza na kurudia
baadaye (soma zaidi juu ya kipimo cha VVU sura ya 7 na 8).
Kipindi cha ukimya baada ya maambukizo ya VVU

Siku chache baada ya dalili za
mwanzo zinazoambatana na
maambukizo ya VVU hutoweka na

mgonjwa hujisikia nafuu. Kwa miaka
kadhaa baadaye hujisikia vizuri,
huonekana mwenye afya na kuendela

na maisha ya kila siku. Mfumo wa
kinga unauwezo wa kukabiliana na

virusi kipindi hicho chote na huitwa
kipindi cha ukimya. Ni kipindi
kuanzia maambukizo hadi dalili


za mwanzo za ugonjwa wa UKIMWI. Kwa watu wazima, kipindi hiki huwa
miaka 10 kwa wastani. Kwa sasa watu wengi wenye VVU wako katika kipindi
hiki (cha ukimya). Hawasikii dalili yeyote na wengi hawajui kama wameshaambukizwa
na virusi na wanaweza kuambukiza.


Ugonjwa wa UKIMWI unavyoanza

Baada ya kipindi cha maambukizo, watu wenye VVU huanza kuugua, VVU

hudhoofisha mifumo yao ya kinga, kiasi ambacho uwezo wao ambao kwa
kawaida mfumo wa kinga unaokabiliana na viini hutoweka na kuruhusu
magonjwa mengine, magonjwa hayo huitwa "magonjwa nyemelezi"- na baadhi

ya kansa, ni dalili ya moja kwa moja ya UKIMWI. Tutajadili tiba zake
katika nyongeza. Wakati mfumo wa kinga unadhoofika, watu wenye VVU


Kundi la lishe bora

Protini – Husaidia mwili kukua na kuponya. Vyakula vyenye protini vingi, , ni
samaki na aina nyingine ya vyakula toka baharini, Nyama, mfano, ya ngombe, ya
kondoo na mbuzi. Nyama za kuku, bata, bata mzinga, mayai, maziwa, jibini, jamii
ya kunde, mchele, mbaazi, mchicha mweusi, nafaka, jamii ya karanga, tofu na vitu
vitokanavyo na soya, njegere.

Wanga – ni vyakula vya kutia nguvu mwili. Wanga upo kweye nafaka, mchele,
ngano, mtama, ulezi, uwele, viazi na muhogo.

Vyakula vya kutia joto na nguvu mwilini - husaidia mwili kuweka akiba ya
chakula cha kuupa mwili nguvu. Kuna nguvu mara mbili zaidi kama ilivyo kwenye
protini na vyakula vya kuupa mwili nguvu. Hii ina maana, ulaji wa mafuta husababisha
ongezeko la uzito kwa watu. Ladha nzuri, shida au tatizo la mafuta husabibisha

ugonjwa wa moyo kwa watu na ongezeko la uzito. Kwa watu walio athirika na

VVU hili siyo tatizo lao kwa kawaida kwa sababu, wao wanajitahidi waongezeke
uzito. Vyakula vyenye mafuta ya mgando na ya maji maji ni– siagi, karanga ufuta,
soya, nazi, (embe mafuta) parachichi, krimu, maziwa, nyama nyekundu kama ya
ngombe, nguruwe na kondoo.

Vyakula vya kulinda mwili – ni muhimu sana, mwili huhitaji kiasi kidogo kwa
afya ya mtu, hupatikana kwenye vyakula vya aina nyingi tofauti, ndio maana
vyakula tofauti katika mlo ni muhimu kwa afya ya binadamu, hutoa aina tofauti
(mbali mbali) ya vitamini na madini.


VVU, kupungua uzito na utapiamlo

Watu wengi huishi katika jumuia ambazo zina upungufu wa chakula na tatizo

la utapia mlo. Watu hawahitaji chakula cha kutosha tu, bali pia wanahitaji
aina mbalimbali ya vyakula, mfano, anayetumia muhogo kama chakula na
habadilishi, atadhoofika. Kama mtu anaweza kuwa mgonjwa kwa kutokula

chakula cha kutosha na sahihi, ana ugonjwa wa utapiamlo. Utapiamlo
unaweza kusababisha magonjwa na kupungua uzito. Njia mojawapo ya kudumisha
afya mzuri ni kula chakula bora. Huu ni ukweli hasa kwa wenye VVU

na UKIMWI. Wana uwezekanao wa kuwa na utapiamlo kutokana na kuugua
mfulululizo, kuharisha kunakosababisha mwili usipate lishe iliyopo kwenye

chakula, kupoteza hamu ya kula na vidonda mdomoni husababisha kula kwa
shida. Kupungua uzito ni kawaida kwa wenye VVU, kiasi kwamba baadhi ya
sehemu ya Bara la Afrika ugonjwa wa UKIMWI huitwa "slim".


Kama mtu yeyote ana shida wakati wa kula


Walioathirika na VVU wanaweza kuwa
na kichefu chefu na kutapika. Chai

au dawa yaweza kusaidia. Mwenye
vidonda mdomoni vyakula baridi na
visivyo na viungo hufanya maumivu
kupungua wakati wa kula. Watu wenye

kumeza kwa shida, kusogeza kichwa
mbele, na kula vyakula laini, husaidia
kumeza kwa urahisi. Uangalifu uzingatiwe

wakati wa kunywa ili kuepuka
kupaliwa. Utumiaji mrija wakati wa
kunywa kunaweza kukasaidia wakati
mwingine. Shida ya kula au kunywa

huenda ikawa ni kwa sababu ya ugonjwa ambao waweza kutibika, mfano ukungu
mdomoni; katika hali hii waeleze watu wakamuone mhudumu wa afya.


Kula vyakula bora vya aina mbali mbali; husaidia wenye VVU kuwa na
nguvu na afya. Chakula bora ni mlo mmoja wenye mchanganyiko wa vyakula
vyenye lishe mbali mbali muhimu. Lishe muhimu ni protini, wanga, mafuta
yaliyoganda na ya maji, vitamini na madini.

Wanawake na watoto wanahitaji lishe bora. Kwa sababu wanawake
hupoteza lishe nyingi wakiwa kwenye hedhi, ujauzito na wakati wa kunyonyesha.

Watoto huhitaji chakula cha ziada kwa sababu wanakua haraka. Watoto
wenye VVU huhitaji chakula zaidi ili wawe na afya nzuri, VVU huongeza
mahitaji ya chakula mwilini mwao.
 
Homa kali, mafua vidonda kwenye koo,matezi(tonsils) na mengineyo. Ukitumia dawa hautapona wala kupata nafuu, bali utapona pale tuu kinga zako zitakapoweza kufight maambikuzi mapya yaliyoingia mwilini. Hivi dalili utaanza kuziona wiki ya pili hadi ya nane baada ya maambukizi na pia uwezekano wa kutoziona hizi dalili upo na ukawa umepata maambukizi


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Hapana chezeya Ukwimi aka Ngoma, Moto, Mawaya. Kuna jamaa yangu nilikutana naye baada ya kitambo kidogo. Ile rangi yake nyeupe na ngavu imebadilika kama mtu aliye unguzwa na radi

Umenikumbusha kitu. Miaka ya 90 kuna mzee mmoja mtaani kwetu wenzake wakamwambia kama ulifanya.... .. na mama fulani basi umeshaambukizwa. Yule mzee akabisha na kwa kupaniki akaondoka na baiskeli kwenda angaza ili atuonyeshe kuwa hana maambukizi. Amini usiamini baada ya muda mfupi tulishuhudia mzee anarudishwa na tax baiskeli imepakizwa nyuma, masikini mzee wa watu hakufikisha mwaka akafariki. Hapana chezeya ukimwi.
 
Homa kali, mafua vidonda kwenye koo,matezi(tonsils) na mengineyo. Ukitumia dawa hautapona wala kupata nafuu, bali utapona pale tuu kinga zako zitakapoweza kufight maambikuzi mapya yaliyoingia mwilini. Hivi dalili utaanza kuziona wiki ya pili hadi ya nane baada ya maambukizi na pia uwezekano wa kutoziona hizi dalili upo na ukawa umepata maambukizi


Sent from my iPad using JamiiForums

oooh! Ahsante sana mkuu! Kiukweli mimi hakuna hata moja ya dalili nilizoziona kati ya hizo ulizoorodhesha, pia nafurahi kukwambia kuwa mpaka sasa nina wiki nne toka nijishtukie
ila hapo uliposema si lazima kuonesha hizo dalili na ukawa bado ni muathirika...umeniondoa ktk mood mkuu
ila nashukuru kwa maelezo yako!
 
oooh! Ahsante sana mkuu! Kiukweli mimi hakuna hata moja ya dalili nilizoziona kati ya hizo ulizoorodhesha, pia nafurahi kukwambia kuwa mpaka sasa nina wiki nne toka nijishtukie
ila hapo uliposema si lazima kuonesha hizo dalili na ukawa bado ni muathirika...umeniondoa ktk mood mkuu
ila nashukuru kwa maelezo yako!

Utakufa na kihoro Majigo nakuambia!
Ivi kupima unaona shida gani?
 
wadau kuna ukweli juu ya hili kua kipimo cha full blood picture(culture) kama lymphocytes(LYM) ikiwa chini ya level inayotakiwa uhakika wa kua na VVU ni mkubwa?
 
wazeya leo mdau wanu nimekwenda kupata vipimo vya HIV, sasa naipenda MMU
nitahama kwa mda hili jukwaa, narud MMU
kwa herin madokta wangu
ahsanten sana
 
Kile kitendo cha kuanza kujihofia kuwa unao, n hatari maana utaanza kukonda, kuumwa hakutakuisha, raha utakosa, na kuanza kufuatilia uliekuwa unatembea nae je anakonda asa hv au ananenepa. ombea awe ananenepa km kaanza kupungua bas hapo mawazo n kuwa tayar unao. Malaria hazitakuisha wew, vichwa
kuumwa ovyo, kumbe mawazo, mara hik mara kile.. acha kbsa, epuka kuwaza kuwa umeupakua utaisha bila kupima. Heri ukapime haraka.. uchelew kujiua mwenyew
 
Nahitaji kujua hili wakuu!

Nazani itakuwa msaada kwa wengi , maana ni swala linalotuzunguka sote!

Baada ya kambukizwa VVU unaweza kukaa ata miaka kumi bila ya kuonyesha dalili yoyote uku kinga yako ikizidi kushuka taratibu.
Cha msingi ni kufanya maamuzi magumu ukapime afya yako ili kama umeathirika uanze tiba mapema.
 
Nahitaji kujua hili wakuu!

Nazani itakuwa msaada kwa wengi , maana ni swala linalotuzunguka sote!

kirus kikiingia tu mwili unareact na askari i mean cd4 zinajiandaa na mapambano ya kulinda mwili mwezi mmoja tu utaona dalili kama homa pamoja na uchovu
 
Kutojitambua kuwa ni mjinga ndio tatizo kubwa zaidi ya ujinga wenyewe.Bado siamini kama watu hawajui kuwa HIV/AIDS ni ugonjwa feki na kinachoua si HIV bali ni dawa za ARVs.Pengine ni kwa sababu sayansi na siasa iliyotumika kutudanganya kuhusu ugonjwa huu feki ni ya kiwango cha juu sana kuliko upeo wa jamii kubwa ya watu hasa nchi masikini kama Tanzania.HIV hasababishi AIDS kama watu wengi wanavyoamini zaidi ya miaka 30 iliyopita.Badala yake nafasi ya HIV inachezwa na ARVs,sina uhakika kama wengi watanielewa hapa.Tanzania bila Ukimwi ilishawezekana zamani sana kwa watu kama mimi,ila kwa wajinga msemo huu bado unaendelea mpaka mwisho wa dunia maana hutakaa usikie dawa ya HIV imepatikana.
Jambo hili ni pana sana,linahitaji mtu kujituma kusoma mambo mengi.Mimi nimewasaidia ndugu zangu ili niwaokoe kwenye ujinga huu ambao siku fulani unaweza kukusababishia kifo chako au watu wako wa karibu.Kinachosumbua wengi ni kasumba,hata kama ataona mke na mume wanaishi pamoja na wamezaa watoto mmoja ana huyu HIV feki lakini mwingine hana lakini bado atang'ang'ani kwamba HIV anaambukizwa kwa njia ya ngono bila kinga bila hata kujiuliza swali lolote.Tumepewa ubongo ili tuutumie kudadisi na sio kushabikia mambo tuliyoambiwa na wengine bila kujiuliza.Albert Einstein alisema "The important thing is to never stop questioning".
Kwa kuwasaidia zaidi ili mjue nina maana gani,hebu nendeni kwenye uzi huo hapo chini na mfuatilie post zangu zote;

Korea Kaskazini yatoa ushahidi kuwa Marekani ndiye mwanzilishi wa Ebola


"OFFICIAL LIES ARE ALWAYS THE GREATEST LIES OF ALL"
 
eti eeh!.......basi mi nitakuwa sina tatizo mkuu!

mkuu mi sina tatizo, hujasoma maelezo ya mumak?

mkuu Sizinga mi sina tatizo lolote, yaani niko fiti kama mashine ya kusaga vyuma vya pua!

dah! Hizo dalili zako kidogo zinatuletea utata ila mimi sina mafua na huo utando, pia nimeshajua sina tatizo lolote... bali ni kauchovu ka kawaida tu!

ahsante mkuu!
Haina shida, nimegundua mi sina tatizo lolote!

Huna tatizo lolote.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom