Ipo haja hizi dawa ARV kutolewa kwa masharti eg sheria kali,kuwalazimisha wajitambulishe kwa jamii na nk.
Dah inasikitisha!..kazi ipo...sasa kwa wale wasiomjua ni wangapi wameshapata maambukizi mpya...tuko kwenye kampeni ya kuzuia maambuzi lakin wale waliokwisha pata hawatoi ushirikiano zaidi ya kuendeleza chain. mungu amsamehe na ampe moyo wa huruma awahurumie wengine na kuwalinda
Hapana DA umekosea! Umeileta hii topic kwa sababu aliyekutongoza ana HIV. Bila kuwa na HIV huyo bwana usingeleta hii thread wala usingemshangaa. Je, huu si unyanyapaaa?? Achilia mbali kwamba umemsaidia sana. Lakini deep down wewe una unyanyapaa na hao unaowahudumia. Unahitaji kubadili mind set yako.Ungepata nafasi ya kuzungumza naye angekwambia jinsi navyomsaidia na kumuheshimu na wala sitaweza kumwambia maneno kama hayo.
Anyway ni maoni yako asante
Mbona mnamsemea hayo maneno kua haweki status yake hadharini? yaani ki uhalisia kabisa jamaa anaonekana yupo opened ndo maana kamtoke mtu ambaye anajua kabisa hali yake ilivyo! kama ingekua mtu mwingine asingeweza, angeenda kwa hao ambao hawamjui.!
Yaani nimejikuta nahurumia kila mdada naye muona no matter what!!! Maana nafikiria kama anaweza kunambia mimi ambaye I know him very well wasiomjua??? Nimekosa raha kabisa kwa siku ya leo mpaka mkoloni ananiuliza kulikoni namwambia Kichwa kinaniuma tu kumbe mawazo yaani sina nguvu kabisa dah!!!!
Hapa mkuu inadepend na huyo mke wa mtu anavyo behave, Wangapi humu wameshatongoza wake au waume wa watu?Ukitafakari kwa undani utajua huyo jamaa ni player, kwa sababu kama nia yake ni kupata mtu wa kuishi nae si angetafuta ambaye hayuko comitted aongee nae na wakikubaliana maisha yaendelee. Kumtongoza mke wa mtu kunaonyesha hajali wala hana mapenzi ya kweli.
Well said, mi nashangaa watu wanashindwa kuelewa point ipo wapi hapa.Haya ni mambo ya kawaida kwenye jamii yetu,sioni cha kushangaza hapa ni nini!watu kama hao wapo na wataendelea kuwepo hoja ya kuwa amekutaka naye bado ana hisia haijalishi kuwa ni muathirika au vipi na wewe kuwa umeolewa kwa hiyo usitongozwe tena sidhani kama inawezekana na sitaki kuamini kuwa huyo unayemwita muathirika ndiye wa kwanza kukutongoza toka umeolewa!mbona hujasema wengine waliokutongoza ilhali una mume?kifupi nauchukulia huu uzi kama umemnyanyapaa jamaa na si vinginevyo.
Mwita Maranya, Tuweke ushemeji pembeni hebu niambie concern ya mwanzisha thread hapa ni ipi?Poa shem.
Huyo jamaa alikuwa anakupimia, si unajua siku zote tunafanya trials.
Ingawa kuna watu naona hawataki kuelewa concern yako. Lakini ndo watanzania hawa wavumilie tutafika tu.
Very low my friend.Hapa hakuna unyanyapaa wala nini ila ukweli wa mambo ulioelezwa na DA!
utamtongozaje mke wa mtu na kumwambia una mapenzi ya dhati juu yake? Tena ajuae hiv status yako? Hata tukiweka suala la kuwa DA ni mke wa mtu pembeni,ni nani humu ndani awezae date hiv+ person while you are hiv-?
Je hao dada zetu sekondari,vyuo,mtaani,makazini etc wanaambiwa ukweli na huyu jamaa kuhusu hiv status yake? Umefanya jambo jema DA na nashauri ungemripoti kwenye vyombo vya dola ili achunguzwe kwani anaweza kuwa anasambaza ukimwi makusudi kitu ambacho ni kosa kisheria.
Tuache ulimbukeni wa ku label kila kitu unyanyapaa wakati he behaves recklessly!
<br />Very low my friend. <br />
Nani hapa amesema amelazimishwa ku date na mtu mwenye HIV?
Hebu kua mkweli, we hii thread umeielewaje?Kwani neno kulazimishwa limetumika wapi hapo?
Kila mtu ana haki ya kudate japo kwa watakiwa ona barrier kati yako na mtu alie kwenye ndoa wether positive or negative!