Ujumbe kwa Jeshi la Polisi Tanzania kitengo cha Usalama Barabarani

Bususwa

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
429
1,011
Naandika uzi huu kwa huzuni kubwa sana.

Jana mnamo saa nne usiku,nilipigiwa simu na rafiki yangu, kwanza nilishituka, hii simu ya usiku hivi kwa yule jamaa, lazima kuna shida maana muda wa saa nne, yeye na familia yake hua wameshalala sio mtu wakukesha kuangalia mpira au kunywa pombe kama kina sisi!

Baada yakupokea ile simu,nilisikia sauti ya mke wake ikiwa yenye majonzi, kwikwi na huzuni, shemeji, ndugu yako amepata ajali, alikua anatoka hospital kumuangalia mfanyakazi mwenzake, baada yakutoka hospital alipita kwa dada yake kumusalimia pia nakumpa hongera kwa kupata mtoto!

Akili yangu iligonga haraka sana kwamba kaumia sana kiasi cha kwamba atapoteza baadhi ya viungo vyake? Au kafariki? Nikauliza yuko wapi? Mke wake akajibu tupo hospital hapa ila kavunjika mguu wakulia mara mbili, nikaenda pale hospital kutoa sapoti ya hapa na pale kuweza ndugu yetu apate matibabu! Hadi naandika hivi ni kwamba ndugu yetu, kafanyia upasuaji na kawekewa chuma kwenye paja.

Story iko hivi!

Sasa hivi kuna mtindo wa hovyo sana umejitokeza kwa vijana kuchinja pikipiki nakuzi pimp, kama wasemavyo wenyewe, pia wanatoa zile taa orginal za pikipiki nakuweka vile vitochi, sasa ndugu yangu alikua na usafiri wake wa pikipiki mida ya saa tatu anarudi kwake, akakutana na boda boda mwenye pikipiki amefunga kitochi, jamaa yangu alishituka tu yuko chini, hawezi hata nyanyua mguu, hii nikutokana nakugongwa na yule boda mwenye taa yakitochi.

Sasa basi jeshi la polisi usalama wa barabarani, mnasubiri nini kuzipiga marufuki hizi pikipiki? Kwanza wanaziiba huko wanakuja kuzichinja,na pikipiki inakua na muundo tofauti kabisa na chapa yake halisi, mfano TVS au Boxer inakua imebadilika kabisa!

Mbili hawa vijana wa boda boda, watakufa wengi sana, watauwa watu wengi sana,wataacha watu na vilema vyakudumu!

Ombi langu, wadau wenzangu hasa watumiaji wa hizi boda boda, ogopa sana mtu mwenye pikipiki yakitochi au kaichinja, hawa vijana watatumaliza tusipokua makini, they have nothing to loose, wengi hawana hata familia!

Tupaze sauti
 
Hapa mkuu umeongea fact,maana piki piki inapokuja na vitu vyake vile kuna maana.Mfano,taa orijino yake huweza kuwasha full light na ule mwanga mfupi ambapo huwezi kumpoteza mtumia barabara mwingine
 
Nahisi nitakuwa nimewapa vilema au wamekufa... Ktk nyakati tofaut usiku mara tatu nimewah kukutana na bodaboda walioweka hizo tochi, kiukweli zinakuumiza macho na usipokuwa makini unapoteza muelekeo...
Huwa ninacho fanya nikiwa naendesha gari na mimi nawasha Full nahama upande wangu na kumfuata upande wake, in any means lazima akimbilie pemben (kushoto kwake) ambapo atakutana na mtaro au korongo au chochote kitakacho msababishia ajali ya kupata maheraha ulemavu au umauti...
Bodaboda wengi ni wapumbavu, ukikutana na bodaboda mshenz mfanyie unyama...
 
Bodaboda ni chawa wa CCM hawezi kuzuiwa labda tu wapunguziwe tena faini ili wasiwe na stresi za kutafuta hela.
 
Nahisi nitakuwa nimewapa vilema au wamekufa... Ktk nyakati tofaut usiku mara tatu nimewah kukutana na bodaboda walioweka hizo tochi, kiukweli zinakuumiza macho na usipokuwa makini unapoteza muelekeo...
Huwa ninacho fanya nikiwa naendesha gari na mimi nawasha Full nahama upande wangu na kumfuata upande wake, in any means lazima akimbilie pemben (kushoto kwake) ambapo atakutana na mtaro au korongo au chochote kitakacho msababishia ajali ya kupata maheraha ulemavu au umauti...
Bodaboda wengi ni wapumbavu, ukikutana na bodaboda mshenz mfanyie unyama...
Hiki unachofanya ni unyama.
Ni kweli hii ni changamoto lakini haitatuliwi kwa namna hii.
 
Kuna kama wawili nimeshawaona hata taa hawana na wanaendesha usiku.. af kuna mijitu mijinga kwel inapanda na kupanda kabisa huku linaona taa hakuna likianguka litasema et mapenz ya MUNGU..
 
Nahisi nitakuwa nimewapa vilema au wamekufa... Ktk nyakati tofaut usiku mara tatu nimewah kukutana na bodaboda walioweka hizo tochi, kiukweli zinakuumiza macho na usipokuwa makini unapoteza muelekeo...
Huwa ninacho fanya nikiwa naendesha gari na mimi nawasha Full nahama upande wangu na kumfuata upande wake, in any means lazima akimbilie pemben (kushoto kwake) ambapo atakutana na mtaro au korongo au chochote kitakacho msababishia ajali ya kupata maheraha ulemavu au umauti...
Bodaboda wengi ni wapumbavu, ukikutana na bodaboda mshenz mfanyie unyama...
Usifanye hivi wanafamilia zinawategemea na maisha Yao pia tunaweza kurekebisha pasi na kuumiza
NB
Binafsi sipendi mabadiliko hayo ya taa yana athari sana nyakati za usiku na wale wa kuweka kelele za exhaust
 
Bodaboda na bajaji wengi wako juu ya Sheria. Serikali hawajaona sababu ya kuweka kampeni maalum ya kuwaelimisha na kuwadhibiliti na vitendo hatarishi wanavyofanya wakiwa barabarani.

Juzi hapa tulimzika ndugu yeti wakili. Aligongwa kwanza na bodaboda; wakati anajivuta kutoka barabarani akakanyagwa tena na bajaji iliyokuwa nyuma. Wote hawakusimama. Ilikuwa muda wa saa moja usiku na inasemekana bodaboda ilikuwa haina taa!
 
Nahisi nitakuwa nimewapa vilema au wamekufa... Ktk nyakati tofaut usiku mara tatu nimewah kukutana na bodaboda walioweka hizo tochi, kiukweli zinakuumiza macho na usipokuwa makini unapoteza muelekeo...
Huwa ninacho fanya nikiwa naendesha gari na mimi nawasha Full nahama upande wangu na kumfuata upande wake, in any means lazima akimbilie pemben (kushoto kwake) ambapo atakutana na mtaro au korongo au chochote kitakacho msababishia ajali ya kupata maheraha ulemavu au umauti...
Bodaboda wengi ni wapumbavu, ukikutana na bodaboda mshenz mfanyie unyama...
Ukiongea hivyo unakosea mkuu.Mimi siyo boda boda ila nina pikipiki yangu binafsi huwa naendesha kistaarabu sana ila nimekoswa koswa na gari.Wenye magari huwaona wenye pikpik wote ni bodaboda kwa hyo kumchomekea hawaoni shida.Tubadilike jamani hiyo ni level tu ya maisha ambayo kila mtu anaweza kufika.
 
Hamna akili nyie boda
 
Mada njema na pole mno mtoa mada hii, tuangalie tulipo jikwaa sio kuangukia, tatizo kila taasisi imekua politicized, sheria zinapindwa kwa makusudi na wengi wanajua they can get away with murder, chombo cha moto kinapokua kwenye public roads LAZIMA kifuate sheria za traffic, na huwezi kubadili muundo wa chombo bila permit ya wahusika, na ukibadili tayari kinakua unroadworthy na huwezi kukitumia kwenye public roads, kaendeshe kwenye private entrance yako. Angalia haya mabus yetu, malori yetu yamewekewa spot lights ambazo haziko kisheria na usiku hawa madereva wako very stupid, hawajui jinsi ya kuzitumia wao ni full lights kama ITs drivers, dawa wakiwasha full lights nawe unahamia upande wake na kuwasha/kuzima taa zako, hii inamfanya naye achanganyikiwe
 
Usifanye hivi wanafamilia zinawategemea na maisha Yao pia tunaweza kurekebisha pasi na kuumiza
NB
Binafsi sipendi mabadiliko hayo ya taa yana athari sana nyakati za usiku na wale wa kuweka kelele za exhaust
Huyo aliyevunjika mguu kwasabab ya upumbav wa bodaboda hana familia..? Kwa taarifa yenu sikuhiz wahusika hawahangaik na bodaboda kuwakamata, wameambiwa waachane na bodaboda ni wasumbufu kwanza wakifa hawana msaada ktk jamii...
 
Ukiongea hivyo unakosea mkuu.Mimi siyo boda boda ila nina pikipiki yangu binafsi huwa naendesha kistaarabu sana ila nimekoswa koswa na gari.Wenye magari huwaona wenye pikpik wote ni bodaboda kwa hyo kumchomekea hawaoni shida.Tubadilike jamani hiyo ni level tu ya maisha ambayo kila mtu anaweza kufika.
Kuna watu wanaendesha bodaboda miaka zaidi ya 10 hawajawah hata kugonga kuku au kupata ajali...
Bodaboda ukiwa mstarabu barababarani kilamtu atakuheshimu, ajali zipo ila zisiwe za kizembe...
Waendesha bodaboda kuna wakat wanasahau kufuata Sheria mwenye gari akikukosakosa unamlaumu...
 
Nadhani kuna haja ya kukirudisha tena kile kitengo cha polisi walokuwa wakitembea na pikipiki barabarani angalau miezi sita waendeshe oparesheni maalumu kudhibiti hawa watu wapambane na wote ambao wanaoleta vurugu barabarani
Wawe na vipimo maalumu vya ulevi,wakague walobadili milio ya pikipiki, walobadili taa,wanaoenda spidi na wakague leseni,hiki kitengo kirudishwe tena naamini mambo yatabadalika
 
Nahisi nitakuwa nimewapa vilema au wamekufa... Ktk nyakati tofaut usiku mara tatu nimewah kukutana na bodaboda walioweka hizo tochi, kiukweli zinakuumiza macho na usipokuwa makini unapoteza muelekeo...
Huwa ninacho fanya nikiwa naendesha gari na mimi nawasha Full nahama upande wangu na kumfuata upande wake, in any means lazima akimbilie pemben (kushoto kwake) ambapo atakutana na mtaro au korongo au chochote kitakacho msababishia ajali ya kupata maheraha ulemavu au umauti...
Bodaboda wengi ni wapumbavu, ukikutana na bodaboda mshenz mfanyie unyama...
Unaounguza tatizo au unaongeza?
 
Back
Top Bottom