Mkomamanga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2011
- 815
- 190
Katika uchambuzi wako weka na Jedwali la sifa za kujiunga Ualimu, Kilimo na Afya.
[TABLE="width: 500"]
[TR]
[TD]Ualimu[/TD]
[TD]Div IV[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kilimo[/TD]
[TD]Div I-III[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Afya[/TD]
[TD]Div I-III[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Baada ya hapo tafakari jibu utalipata kirahisi sana ndugu yangu.
Si kweli kwamba kilimo wanakuwa katika kiwango cha daraja la kwanza hadi la tatu...cheti katika kilimo kwa sasa unatakiwa kuwa na D mbili za masomo ya Sayansi, na ni kigezo hichohicho kwa mwalimu wa cheti kwa upande wa sayansi.
Na mbona mwalimu mwenye digree analipwa kidogo wakati hakwenda na daraja la nne mahali popote? Kwa vigezo vya kujiunga hana tofauti na aliyejiunga kusoma degree ya sanaa ya jamii (BA Sociology) na huyu akienda kazini anaanza na mshahara mkubwa? Ni sera mbovu tu katika nchi yetu na si vinginevyo.
Mwisho ni kipi kianze, watu wanye madaraja ya kwanza kuanza kujiunga na ualimu ili wakitarajia mishahara yao kuwa mizuri au mishahara kuwa mizuri kwanza halafu ndiyo wenye madaraja ya kwanza wakajiunga na mafunzo kwa ualimu? Nahisi kipindi maslahi yatakapokuwa mazuri na waliofaulu watajiunga na profession hiyo iliyotelekezwa na serikali yetu tunayoipenda.