Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,891
Wanasema lugha ambayo Mungu alitumia kuumba ulimwengu ni hesabu. Hata wanapoangalia na kulinganisha performance ya elimu kwa nchi mbalimbali, huangalia Hesabu na sayansi.
Sasa basi, ufaulu wa Hesabu mwaka huu ni asilimia 20. Au ni 30? Hii inamaanisha asilimia 80 ya watahiniwa wote wamepata F ya hesabu. Nafikiri F inaanzia 20 kushuka. Sasa maana yake asilimia 80 wamepata chini ya ishirini. Kulikuwa na watahiniwa karibu laki nne na nusu. Maana yake karibu watoto 360,000 wameshindwa kupata 20 kati ya 100 kwenye hesabu.
Physics ufaulu ni kama 55%. Lakini hii si kila mtu anafanya, ni kama nusu tu, (na pengine chini yake) ya wanafunzi ndiyo wanafanya physics. Sasa katika hii cream ya wanafunzi wenye uwezo, 45 kati ya mia wameshindwa kupata 21!!.
Hesabu ni muhimu sana. Huwezi kufahamu Physics na Chemistry kama hufahamu hesabu. Huwezi kuwa Daktari, mfamasia, mwanasheria, au kufanya kazi yoyote vizuri bila kujua hesabu. Hata mwanasiasa kusoma research na takwimu unahitaji hesabu.
Tutizo ni nini? Je hatuna waalimu wazuri wa hesabu? Hatujalipa somo mkazo? Au ni nini?
Nini kifanyike? Ni wastani gani wa ufaulu tuufikie ili tuseme sasa watanzania wanajua hesabu?