Kuhusu matokeo ya kidato cha sita mwaka huu 2023

Nyamboboy

JF-Expert Member
Jun 22, 2017
361
451
Habari ndugu zangu,

Nianze kwa kuwapongeza wale wote waliofanya vizuri mitihani yao ya kidato cha sita. Niwapongeze pia walimu na wazazi bila kuwasahau walezi wa wanafunzi wetu hao. Niende moja kwa moja kwenye kiini cha mada hii. Kama taifa hatuna budi kujadili kuhusu mwenendo wa elimu yetu, Tumekuwa tukiona matokeo yanazidi kupanda kila mwaka na kuwa na Division One nyingi(za kumwaga) kila mwaka tofauti na miaka ya nyuma.

Wanachojiuliza wadau wa elimu(wa zamani) ni kwamba siku hizi Physics imekuwa rahisi au Chemistry imekuwa rahisi tofauti na ile ya zamani? Jibu ni hapana, Kitu gani kinafanya ufaulu uwe wa kufulu kama ilivyokuwa mwaka huu?

Wadau tulio wengi hatuna tatizo na ufaulu mkubwa kama ilivyokuwa mwaka huu,tunatamani tupate wataalamu wazuri watusaidie kama nchi huko mbeleni. Tatizo ni je,Hivi kweli matokeo haya yanaaksi uhalisia wa wanafunzi wetu kiakili na kiulewa?

Nilikuwa naongea na baadhi ya watahini(wasahihishaji) wa mitihani hii ya kidato cha sita mwaka huu wanasema wamebaki kinywa wazi baada ya matokeo haya kutangazwa maana ni tofauti na kile walichokuwa wanakiona kipindi wanasahihisha,Mathalani mmoja aliyetahini somo la Advanced Chemistry two (02) anasema wanafunzi walifanya vibaya kinyume na matokeo yaliyotoka.

Mifano iko mingi,ila itoshe kusema kuna walakini katika mchakato wa utoaji matokeo.Wengine wanasema wanatumia Continous Assessment zinafanya ufaulu kuwa juu,Bado tunajiuliza kwani NECTA zamani walikuwa hawatumii hizo Continous Assessment? Mbona matokeo hayakuwa kama hivi sasa?

Kuna mdau alifika mbali hadi akasema labda serikali ina mpango(ambao hauko wazi) kuwa kila anayeenda kidato cha tano na sita afike chuo kikuu kwa namna yeyote ile.Itoshe kusema Elimu yetu inafikirisha sana tunapoelekea kuliko tulipotoka!

Akhsanteni.
 
kwahiyo unataka watoto wafeli??.... ili elimu isikufikirishe?

Watanzania bhana.
 
Mimi kama mmoja wapo ya wanafunzi niliemaliza mwaka huu(pcb), ipo hivi...elimu haijawa rahisi lakini serikali imeongeza waalimu wenye ujuzi, pia ukiangalia zamani kaka zetu mlitumia vitabu vigumu sana, tuchukulie mfano kwenye chemistry kuna hiki kitabu Cha Ngaiza, kwa wewe hapo unaweza ukakiona chepesi, ndio, lakini serikali kupitia taasisi ya elimu Tanzania (tet), wameleta vitabu vyepesi saana kusoma na vinaelewesha vizuri kuliko hioo Ngaiza....pia necta wanatoa maswali yaliokwenye vitabu vya tie, ukiangalia necta yetu na mwaka jana kuna maswali ni mifano ya vitabu vya tie inatoka necta, kwanini tusifaulu?? Na form 6 tuliowaacha wanampango wa kuvunja record yetu, ni mwendo wa kuweka record na kuvunjiwa.....ufaulu unapanda kila mwaka....
 
Back
Top Bottom