Kwa maneno haya ya Kocha Minziro wa Prisons FC na mwana Yanga SC lia lia nitamshangaa Mtu aliyechukia kwanini Simba SC imeshinda leo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,647
109,036
"Kiukweli Wachezaji wangu hawako Smart Kichwani ( akimaanisha ni Wapumbavu ) kwani kila Siku katika Uwanja wa Mazoezi nawapa Maelekezo yale yale lakini tukija katika Mechi wanayarudia. Niliwaambia Simba SC ina Wachezaji wengi wenye Vipaji vikubwa na Binafsi hivyo tusipokuwa makini Watatufunga na kweli Wametufunga.

Inakera mno" amesema Kocha Mkuu wa Prisons FC Fred Felix Minziro Kataraiya Majeshi ( ambaye hata Malaika wa Mbinguni wanamjua kuwa ni mwana Yanga SC kindakindaki ) alipokuwa akizungumza na Mtangazaji wa Azam Tv Patrick Mnyembera.

Sasa kama tayari Kocha wao keshasema Timu yake ya Prisons FC Wachezaji hawana Akili Vichwani ( yaani ni Fools ) Mimi GENTAMYCINE ni nani nimkatalie na nipoteze muda wangu Kumbishia?

Kudadadeki tumeshawaacha tayari kwa Alama ( Points ) Tatu ( 3 ) hivyo hii ndiyo nitolee kwa Kukaa Kileleni hadi Ubingwa.
 
Back
Top Bottom