Mwali,nimekupata sawia.
Napenda niseme kwamba,ni ukweli umeidhinisha kuwa, maybe udhaifu wa JK wa kutoyapatia ufumbuzi ama kuyashughulikia matatizo ya wananchi kumetafsiriwa na mimi mleta hoja kwamba ni udini.
Kimantiki,nakubaliana na wewe kwasababu inamake sense kwa jinsi tunavyouona utendaji wake wa kazi.Lakini pia,mada hii ni pana sana na nimejaribu kucover hizo "weaker sides" of my main point kwa kadri ya uwezo wangu.
Kwanza nilifanya hivyo kwa kuhusisha hoja ya JK na watu wake kwamba ameruhusu uhuru wa habari.Na nikasema kuwa,hiyo si kweli,nikatolea mfano wa vyombo vya habari vyenye kueneza chuki za kidini ambavyo vinaachwa vifanye hivyo bila wasiwasi.Na wakati kwa upande mwingine,nilitolea mfano wa gazeti la mwanahalisi kufungiwa kwa kuandika yale yasiyompendeza.Hata mtandao huu walishajaribu kuufanyia kipindi cha nyuma kama sikosei.Hivyo yale anayoyaacha,naweza kuconclude kwamba yanamfurahisha(siyo yote).
Na kwahiyo licha ya kwamba inaonyesha mnaomtetea mnaya attribute haya kwenye udhaifu wa kiutendaji,bado kuna mambo ambayo hajaonyesha udhaifu hata kidogo.Mambo ambayo watu wake wanayafanya yenye kuonyesha ubabe kabisa na ukiukwaji wa haki za kimsingi kabisa za watanzania.
Sasa tunapopima yanayofanyika kwenye taifa letu,na kuona matokeo yake,basi tunajuwa kuwa something is deadly wrong,nchi haiwezi kuwa kwenye chuki za kidini kuliko wakati wowote ule kwenye historia yetu,halafu eti lawama tupeleke kwa mtu alyetawala zaidi ya miaka takriban 30 iliyopita.
Mimi sizungumzi nani analalamika kuhusu udini,nazungumzia chuki za kidini.Kama kuna waliokuwa wakilalamika udini chini ya mwalimu,basi hiyo ni topic nyingine.
Na kwakukusaidia tu,ni kwamba kama Nyerere alikuwa mdini,basi uweke sababu ie kulikuwepo na udini etc.Hilo tutapingana sana tu,kwasababu chini ya utawala wake tulikuwa na mshikamano.Ila maybe unaweza kuitetea pointi yako kwa kuingiza hoja ya mfumo kristo.Hilo lina thread yake limejadiliwa na bado linaendelea kujadiliwa.
Sasa ninapojiuliza ni kwanini hili ama lile,kwa mfano kukiwa na machafuko kwenye taifa,ama uchumi ukiwa mbaya nk,credits kama nilivyosema hapo awali,zinamwendea mkuu wa nchi.
Na kusema ukweli hiyo mifano uliyoitoa,kwamba JK hajasema hiki ama kile against dini nyingine,ukweli ni kwamba hathubutu kusema hayo kwani asingekuwepo madarakani kwa maneno kama hayo.Ila rais anapimwa kwa matokeo.We look at the results.Nchi ikiwa na mshikamano,atapewa credit,and the opposite is also true.
Sasa ngoja nimalizie kwa kusema haya tena kwa mara nyingine.Nilisema kuwa,JK serikali yake ina kashfa za ufisadi,lakini toka hizi hoja za udini zilipoanza,basi huwezi kushangazwa na watu kumtetea fisadi kwenye issue wazi kabisa ya ufisadi bila kusikia wengine wakisema kiongozi huyo anaonewa kwasababu ya dini yake endapo ni muislam.
Yani issue iliyowaunganisha watanzania ya ufisadi,inaangaliwa kwanza kwa basis ama jicho la udini.Na hata JK mwenyewe akishutumiwa kwa hili ama lile,utasikia ni kwasababu ni muislam.Sasa hapo unategemea niseme nani ni mdini endapo watu wake ndo wameanzisha hayo?
Inasemekana kwenye uchaguzi uliopita,alitumia issue hiyohiyo kuwagawa wananchi.Hili ni tatizo kubwa.Kama alikuwa na uwezo wa kulifungia mwanahalisi,anashindwa vipi kukemea vyombo vya habari vyenye mienendo hiyo?
Naomba niseme kwamba,kama huu udini usingemnufaisha yeye,basi nisingemuhusisha nao hata kidogo.Mimi napenda sana kuwa fair,napenda usawa,sipendi ukandamizaji wala uonevu hata kidogo,hiyo siyo character yangu.
Kama anajuwa kuupinga udini kutawaunganisha watanzania dhidi ya mafisadi,basi naamini yeye anafurahia hali hiyo,so siwezi kumwona tofauti na kwamba ni mdini.Regardless of the reason on how it happens.Nimeconnect dots nikafikia kwenye conclusion hii.However nakubaliana kwa kiasi kikubwa na baadhi ya points zako.