Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Status
Not open for further replies.
Hilo halina ubishi kuhusu udini alionao Jk. Haiwezekani dini yake iwe kila kukicha inatoa matamko yenye mrengo wa kidini halafu yeye yu kimya . Nchi inaendeshwa utafikiri haina serikali sababu ya ubinafsi na udini aliona kiongozi mkuu wa nchi.
Tatizo ni kuwa hamtaki kuukabili ukweli badala yake mnakimbilia katika kivuli cha kumlaumu JK!
Kama kusingekuwana na dhulma dhidi ya Waislamu huyo JK angewaingilia Waislamu kwa gear gani?!
 
Mahakama ya nchi itasimamia haki hizo kama mmeshindwa kukubaliana kwenye mahakama ya kadhi. Na je ikimpata mkristo atasimamiwa na mahakama gani? Nnachotaka kukuambia mambo ya kidini ni ya hiari si ya lazima. Huwezi kutaka nguvu ya serikali ili kulazimisha mambo ya kidini. Kama hamkukubaliana kwa kutowepo uhiari kuna mahakama ya nchi itakayolazimisha upande unaotakiwa kuchukua hatua kufanya hivo nk.

Jibu swali wewe....nimekuambia unitajie jambo moja la waislamu linaloendeshwa na serikali!!!
 
Jibu swali wewe....nimekuambia unitajie jambo moja la waislamu linaloendeshwa na serikali!!!

Mmepewa chuo Morogoro, mmepewa na majengo na serikali kwa ajili ya mahakama zenu ili mkate watu mikono:croc:
 
Mmepewa chuo Morogoro, mmepewa na majengo na serikali kwa ajili ya mahakama zenu ili mkate watu mikono:croc:

Ni nani alikuambia Mahakama ya Kadhi inakata watu mikono?! Zanzibar ipo, umeshawahi kusikia mtu amekatwa mkono kule? Kenya ipo, umeshawahi kusikia mtu amekatwa mkono kule?! Acha kurukia mambo usiyoyajua, na chuki zenu za kipuuzi zitawaua hizo!
 
mkuu tatizo ni huwa unalazimishia badala ya kumwelewesha mtu,badala ya kukurupuka kumwita mpuuzi,basi umweleweshe inavyofanya kazi bila kuingiliana na sheria husika za nchi,wala bila kuvunja katiba ya nchi mkuu.
 
Wote nyinyi mnafahamu kwamba hakuna mahakama ya kadhi inayokata mikono watu huku lakini ili kukashfu wenzenu ili waonekane ni dhalimu hayo ndo madai yenu kila siku so it's wastage of time kumwelewesha mtu ambae hana nia ya kutaka kuelewesha otherwise angekuwa muungwana ktk kuuliza kuliko ku-conclude kitu ambacho hakifahamu. Angekuwa honesty kama unavyotaka kunidhanisha basi asingesema kwamba waislamu wanataka mahakama ya kadhi ili wakate watu mikono!
 
UDINI? Nyerere ndo aliuanzisha baada ya kuaminiwa na wazee wa pwani (waislam) kwa kupewa uraisi kisha akaanza kuwatenga kielimu, kuvunja east Africa muslim association, akawafili mali pesa taslimu na raslimali zisizo hamishika through issues za uhujumu uchumi na mengine mengi. Haya yote yalilenga kuwadhoofisha waislam ambao walikuwa juu kiuchumi na elimu. Haya aliyafanya muda wote wa uongozi wake na alitengenza system ambayo mpaka leo ina-operate the same way. Mbaya zaidi mafundisho haya ya ukandamizaji na ubaguzi hutolewa huko makanisani hadi leo. So suala la udini limeanza mbali. sasa hivi watu wanasema kuna-udini kwa kuwa watu wameamka wanada haki zao kama elimu, na fair representation ktk secta mbalimbali za kiuchumi na jamii. Mambo yaliyo necta ni product ya system waliyotengeneza akina-Nyerere et al. sasa hivi elimu imeshuka sana simply because Necta sio waadilifu.... wanahakachua matokeo ya watoto.... na victims wengi wamekuwa ni wa dini ya waislam.....the story is just long!. kwa hiyo udini ulikuwepo tangu mwanzo....wanyonyaji (kanisa) hawakuwa wanasema just because wanaonyonywa walikuwa wavumilivu.....sasa people are fighting back their rights!
 
Hii sasa ni jazba, mnahangaika na chuo kikuu kimoja? Kanisa linavyuo vikuu vingi...na majengo walipewa mengi. ni kwamba tu you guys dont feel happy wenzenu wakiendelea. We need this country to keep moving! Si sahihi kuwabeza wenzenu....hii inaonyesha imaturity!
 
Si sahihi pia kumwita President ni janga la taifa. yaani unamfananisha na ukimwi? na majanga mengine? This you are doing great mistake. Kwa wachambuzi wa siasa tunasema kwa maneno haya ya kashfa wewe ndio mdini. Alipokuwa Nyerere au mkapa hukusema ni janga la taifa. Mkapa alikuwa fisadi na ameuza mashirika ya umma mengi....then huyu yeye mnamfagilia. This is hypocrisy na ndio udini wenyewe.
 
Umeyaona ya shekh PONDA tu, ya maasikofu hujayaona kweli wewe huiwezi siasa!!Waislam wanahaki ya kudai kipengele cha dini ktk sensa.kwanini wadai tembelea web hizi upate reference
1) www.wikipedia.com/tanzania
2) www.arc.com/tanzania

web zote hzo zinatoa idadi ya watanzania kwa mujibu wa dini yao wakati tangu 1967 watanzania hatuja hesabiwa kwa mjibu,wa dini zetu.swali hawa WA RC Takwim hz wanazitoa wapi????
Sipendi sana kuchangia mijadala ya dini lakini naona hapa unatakiwa uwe mwelewa kidogo hizi web ulizo weka hapa sidhani kama zinamilikiwa na MASKOFU. Ili uweze kusema jambo unatakiwa ufanye utafiti kidogo. mfano hii wikipedia ni moja moja ya sources ambazo siyo reliable kila mtu hata asiye na taaluma yeyote anaweza kuchangia chochote. Kama waislam ni wengi kuliko wakristo au wakristo ni wengi kuliko waislam hiyo siyo hoja. Hoja ni kwamba kila mtu apate haki kama raia halali wa tz. bse kuna makundi yenye watu wachache mathalan watu wasio na didi yeyote kati ya hiz mbili kama tutakuwa tunaangalia wing it means tutawaumiza. Tatizo ni kwamba
naona tanzania sasa hivi watu wanatafsiri mambo kwa perspective za dini kitu ambacho nikibaya sana. mtu akifanya jambo baya haukumiwi yeye kama yeye utsikia watu wakilalamikia dini yake. KILA MTU ANASHABIKIA UDINI HADI VIONGOZI WA JUU WASERIKALI YETU. Nasikitika sana kuona kwamba badala ya kuendelea tunrudi nyuma kwenye makabila na dini zetu.
 
Hivi kwanini JKN alimkataa JMK kuwa prezidaa? Huenda alijua haya yote ce tukajifanya kichwa ngumu tkamchagua sasa kila kitu ukigusa ni moto tuuu
 
Wote nyinyi mnafahamu kwamba hakuna mahakama ya kadhi inayokata mikono watu huku lakini ili kukashfu wenzenu ili waonekane ni dhalimu hayo ndo madai yenu kila siku so it's wastage of time kumwelewesha mtu ambae hana nia ya kutaka kuelewesha otherwise angekuwa muungwana ktk kuuliza kuliko ku-conclude kitu ambacho hakifahamu. Angekuwa honesty kama unavyotaka kunidhanisha basi asingesema kwamba waislamu wanataka mahakama ya kadhi ili wakate watu mikono!
Usi assume watu wanafahamu kila kitu mkuu,ingekuwa hivyo,basi kusingekuwa na haja ya kuelimishana.

Hakuna mtu atakayekubali kitu asichokifahamu,wewe unaposema "nyie mnafahamu",basi unakosea,si kila mtu anafahamu mambo ya dini za wengine.Pia ni muhimu kuzingatia utanzania kabla ya lolote lile.
 
Nchi ilipofikia,credits huwa anapewa rais na serikali yake,kwahili la udini,hakuna ubishi umeshaota mizizi.Na sijawahi kusikia kauli ama vitendo kutoka kwa JK vya kukemea haya mambo ya udini.

Kinachonifanya niamini ni JK,ni kwasababu hao wanaopinga kasi ya upinzani,wanapoijibia serikali ya ccm,basi wanaoonyesha chuki za wazi kabisa za kidini.Ule udugu tuliokuwa nao wakitanzania haupo tena,na sijui utarudi kwa njia gani.

Kuna habari kuwa hata mtu na mke wake wanataka kutoana roho kwasbabu hizo hizo.Sheick Ponda alipotoa kauli kinyume na yakwake kuhusu sensa,kaliachia na gazeti lenye kusambaza sumu hizo huku akilifungia lenye kusema ukweli(mwanahalisi)

Ninamini kabisa kuwa tulipofikia,uwezekano wa kuingia kwenye vurugu na mapigano ya kidini ni mkubwa kuliko wakati wowote ule kwenye historia ya Tz toka tupate uhuru.

Kama JK ni mdini,tufanyeje?Ni wazi anapenda haya yaendelee kuwepo kwasababu ni kama anauwa ndege wawili kwa jiwe moja,yani kwasababu yeye ni fisadi na mdini,basi issue za ufisadi wake anazifukia kwa kupenyeza sentiments za kidini kwasababu anajuwa the issue is extremely sensitive.

Je kama taifa tutapona dhidi ya udini huu wa JK?je kukitokea mapigano,nani atakuwa responsible?Je nini kifanyike kukomesha udin8I hu?ama tumeridhika?!....

You R very RIGHT... Nina Rafiki yangu MUISLAMU kaishi NJE ya NCHI tumekuwa nae toka tukiwa WATOTO; Nimeongea nae

kuhusu SENSA akaniambia Kwanini SENSA; akaniambia haijui inafanya NINI Maishani kwake... Nikazidi kutaka kujua zaidi

akabadilisha story; na hakutaka kuongelea ila kaniambia HAKUHESABIWA. Huyu ni kijana ambaye tulipokuwa wadogo Wazazi wetu

walikuwa pia Marafiki; Mfungo wa RAMADHANI Mama yangu alikuwa anamsindikiza Mama yake wakati wa kufunga na SISI

TULIKUWA TUNAFUNGA na yeye wote tulikuwa VIKOBE... lakini tulikuwa tunafuturu @ SUNSET

Sasa hivi hata kuongea inaonyesha kuwa tu wageni hatujuani; Amejaa HOJA na SERA tofauti na Ameishi NCHI ZA NJE

RAIS wetu ametupa KIDONDA NDUGU; SIJUI KAMA kitapona; Sasa Akimaliza Muda wake ataishi Nchi GANI? Yeye Mwenyewe

hapendi ARABUNI Sasa kama ameacha Machafuko NCHINI WAWEKEZAJI wataipenda sababu GAS iko BAHARINI wataichota na

kuondoka na Madini Mengine Wataweka Majeshi yao kuyachunga na sisi tunapigana kuuana na UDINI wetu
 
lugha za kejeli umeanzisha wewe.Sasa mkuu unataka kusema kwamba serikali hii anayoiendesha JK inafuata mfumo wa kikatoliki?ama sijakuelewa?Kilitokea kitu gani hapo wakati wa JK kuapishwa?

Kwa kuwa hapa tunaelimishana,na wewe umekisoma kitabu hicho,je unaweza kusummerize dondoo zake ili nipate kukuelewa vyema?

Na pia utofauti kwenye madhehebu ya wakristo ni sawa tu na ulioko kwenye uislam ambako kuna wale "sufi",shiite na sunni.Hao wanatofauti pia,so wawe treated the same?they don't even get along na wanauwana utadhani si wote si waislam.Nasubiri kuelemishwa,ila dini yenye amani haitakiwi kuendeleza haya mkuu.Nasubiri elimu.

Ahali yangu acha kabisa uvivu wa kufikiri. Kitabu kipo huko huko wewe nenda tu pale mtaa wa mansfield Cathedraw bookshop , Posta kwenye kanisa la st Joseph kinunue ukisome kwa wasaa.

Suala langu lilikuwa dogo tu kwako. Wakatoliki wanamwamini Yesu. Madhehebu mengine ya kikiristu wanamwamini Yesu. hawa wote kijumla wao tunawaita wakristo. sasa iweje kanisa katoliki litambulike kipekee na makanisa mengine. Na kama utaangalia uapishwaji wa Rais wenu utaona kuna mwakilishi wa kanisa katoliki na mwakilishi wa makanisa mengine ya kikristo huko Tanzania.

hapo ndio chimbuko la suala langu kwako. Je unajuwa kwanini?

Uvivu wa kufikiri?kweli?na suffi mwakilishi wao awe sunni na sunni mwakilishi wao awe shiite?nijibu kwanza kama wote hao wako sawa na wanahitaji wawakilishi sawa.Wote si waislam?sasa unashangaa kitu gani kama kuna wakristo walioko tofauti?

Kuhusu hicho kitabu,nimekwambia weka elezea kwa ufupi,unaniambia niende pahala ambapo hata sipajui.Halafu toka juzi leo ndo unakurupuka kujibu,unadhani sijui kwamba ulikuwa unajibu posts nyingine?we unadhani umenipatia jibu ama unadhani nitakuwa nimesahau?naomba unipatie majibu kabla ya kukurupuka na kuja na pumba mpya mkuu.
 
Yale yale ya kungoja kutafuniwa kila kitu na kudevelop uvivu wa kujisomea. Lakin makini sana wa kulalama.
kalaga baho.

Yale yale ya kungoja kutafuniwa kila kitu na kudevelop uvivu wa kujisomea. Lakin makini sana wa kulalama.
kalaga baho.

mkuu usilete dharau halafu ukidharauliwa unali lia ka mtoto wa kike.Tuachane na kitabu chako cha ki ****,kwasababu hakina mantiki kwenye mjadala huu,mbona hujibu maswali niliyokuuliza kuhusu utofauti ulioko miongoni mwa waislam?Jibu,sunni ni sawa na suffi na shiite ni sawa na sunni na suffi?

Kama huna point siyo lazima uchangie.Safari njema uendako.
 
Usi assume watu wanafahamu kila kitu mkuu,ingekuwa hivyo,basi kusingekuwa na haja ya kuelimishana.

Hakuna mtu atakayekubali kitu asichokifahamu,wewe unaposema "nyie mnafahamu",basi unakosea,si kila mtu anafahamu mambo ya dini za wengine.Pia ni muhimu kuzingatia utanzania kabla ya lolote lile.

Narudia, anafahamu na kama hafahamu basi hana haja ya kufahamu vinginevyo angeanza kwa kuuliza!! All in all, uwepo wa mahakama ya kadhi hauondoi wala kuhatarisha u Tanzania wa yeyote.Ni mara ngapi imesemwa kwamba lengo la mahakama ya Kadhi ni kutatua masuala ya kijamii yanayowahusu waislamu hususani masuala ya Taraka, Ndoa na Mirathi?! Sasa masuala hayo yanahatarisha U Tanzania wa nani?! Yaani mimi leo hii naacha mke, kisha namdhurumu mgawo wa mali na yeye anaamua kukimbilia kwenye mahakama ya kadhi ndo useme tunahatarisha u Tanzania?! u can't be serious broda! acheni kukuza mambo bana!
 
Mkuu,kuna watanzania wa tofauti,kuna wale wenye kuelewa kuwa kuna utofauti kati ya kusimamia issue za taifa vs zile za dini,kuna wale wasiojuwa utofauti huo.Na pia kuna wale wanaojuwa tofauti hizo,lakini wanachaguwa maslahi ya dini kabla ya yale ya taifa.Ndo maana kuna tawala zilizowahi kupinga mambo ya dini kwenye mataifa wanayoyaongoza,Burundi ilikuwa ni mfano mmojawapo.Ninavyofahamu,kuna wananchi ambao wanafuata taratibu ama sheria za kimila inapokuja kwenye ndoa na mambo ya mirathi,na hayo wala serikali haihusiani nayo.

Ninasema hivyo kwasababu wale wanaotambua taifa kwanza then dini baadaye,wanaweza wasielewe,na inabidi waeleweshwe baada ya kukubaliana na wale wanaoelewa kwamba wale wasioelewa,basi waeleweshwe.

Pia binafsi nina swali,je mahakama hizo zinaweza kufunguliwa na misikiti bila kuihusisha serikali?kwa mfano,hata wakristo wana taratibu na sheria zao,na huwa zinafuatwa bila kuihusisha serikali.Nafahamu kuna wale wanaosema kuwa sheria zetu tulizoziadapt,basi chimbuko lake ni ukristo,na ndiyo maana wakristo huwa hawana shida nazo.Lakini ukiangalia kwa makini sheria wanazozitaka,basi ni sharia law.

Halafu pia, kuna wale wasiojuwa utofauti,yani hawajui kama mambo ya mahakama ya kadhi yana tofauti na sheria za nchi husika,wale ambao wanaweza kuona kama vile serikali iko bias.Ambao wanahisi kwamba sheria za mahakama ya kadhi ziko derived from sharia law,hao pia wanahitaji kueleweshwa.Kwahiyo kama wewe naelewa hayo,si kila mwananchi nayaelewa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom