Kwa mambo haya - JK ni Mdini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jmushi1, Aug 29, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,599
  Likes Received: 2,001
  Trophy Points: 280
  Nchi ilipofikia,credits huwa anapewa rais na serikali yake,kwahili la udini,hakuna ubishi umeshaota mizizi.Na sijawahi kusikia kauli ama vitendo kutoka kwa JK vya kukemea haya mambo ya udini.

  Kinachonifanya niamini ni JK,ni kwasababu hao wanaopinga kasi ya upinzani,wanapoijibia serikali ya ccm,basi wanaoonyesha chuki za wazi kabisa za kidini.Ule udugu tuliokuwa nao wakitanzania haupo tena,na sijui utarudi kwa njia gani.

  Kuna habari kuwa hata mtu na mke wake wanataka kutoana roho kwasbabu hizo hizo.Sheick Ponda alipotoa kauli kinyume na yakwake kuhusu sensa,kaliachia na gazeti lenye kusambaza sumu hizo huku akilifungia lenye kusema ukweli(mwanahalisi)

  Ninamini kabisa kuwa tulipofikia,uwezekano wa kuingia kwenye vurugu na mapigano ya kidini ni mkubwa kuliko wakati wowote ule kwenye historia ya Tz toka tupate uhuru.

  Kama JK ni mdini,tufanyeje?Ni wazi anapenda haya yaendelee kuwepo kwasababu ni kama anauwa ndege wawili kwa jiwe moja,yani kwasababu yeye ni fisadi na mdini,basi issue za ufisadi wake anazifukia kwa kupenyeza sentiments za kidini kwasababu anajuwa the issue is extremely sensitive.

  Je kama taifa tutapona dhidi ya udini huu wa JK?je kukitokea mapigano,nani atakuwa responsible?Je nini kifanyike kukomesha udin8I hu?ama tumeridhika?!....
   
 2. songoros

  songoros Senior Member

  #2
  Aug 29, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Umeyaona ya shekh PONDA tu, ya maasikofu hujayaona kweli wewe huiwezi siasa!!Waislam wanahaki ya kudai kipengele cha dini ktk sensa.kwanini wadai tembelea web hizi upate reference
  1) www.wikipedia.com/tanzania
  2) www.arc.com/tanzania

  web zote hzo zinatoa idadi ya watanzania kwa mujibu wa dini yao wakati tangu 1967 watanzania hatuja hesabiwa kwa mjibu,wa dini zetu.swali hawa WA RC Takwim hz wanazitoa wapi????
   
 3. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  JK= Janga la Kitaifa
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  hakuna hasara kwa taifa kama kuwa na kiongozi wa juu asiye na msimamo wala hajui kwa nini yupo pale.

  Wakati anajipanga kuingia madarakani alitumia sana mbinu ya udini, pamoja na nyingine na kufanikiwa kuingia.

  Kama kawaida yake hakujua kama itafikia hapa, na hakuwa na njia mbadala ya kunusuru hali pindi mambo yataharibika.

  Jukumu au wa kulaumiwa ni sisis watanzania tuliokubali kuingozwa na mtu asiye na uelewa na sisi kukubali kumpa nafasi ya kutugawa.

  Mjinga akiwachonganisha werevu wawili, wa kulaumiwa si mjinga, bali ni wale werevu walioshindwa kujua lililo bora kwao.

  Badala ya kutumia 'platform' kama hii kunyoosheana vidole, ingekuwa jambo la maana kama tukakubali tofauti zetu na kutafuta 'common ground' ambapo tunaweza kusonga mbele kama taifa moja lililowahi kuwa na wananchi wasiotambuana kwa dini kwa majina yao au kwa uwezo wao katika uongozi.
   
 5. songoros

  songoros Senior Member

  #5
  Aug 29, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 156
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  THE BEST PRESIDENT AMBAE HAJAWAHI TOKEA TANZANIA.Ukweli ndo huo.
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  tutajipamba hapa kwa maneno, lakini ikitokea vita, tutakaoathirika hasa ni sie tusokuwa na uwezo wa kugharimia familia zetu kwenda kuishi nje.

  Wao utakuta familia zote ziko nje.
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  He is the best, in his own weird way.

   
 8. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Uko sahihi
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,599
  Likes Received: 2,001
  Trophy Points: 280
  mjadala hapa ni udini wa JK,miye sina shida na ndugu zangu waislam.Sasa hii ni double standard kuwahusisha wasiokuwa serikali ama vyama vya upinzani kuhusiana na kauli ya JK kuwa nyie waislam wenzake muhesabiwe.Lakini tunaoufahamu unafiki wa JK,yeye ndo kawatuma kina Ponda waeneze udini.Ni mnafiki sijapata kuona.

  Nina amini akija huko misikitini anawambia yeye ni muislam mwenzenu mwenye kupigania haki zenu,alikuja kusema hayo wakati wa kampeni.

  Na ndiyo maana aliposema muhesabiwe munalilaumu kanisa na chadema badala ya kumlaumu yeye aliyeitoa kauli hiyo,tayari mna udini!.

  Nina uhakika yeye ndo aliyewalisha sumu wana ccm wenzake kuhusu hayo mambo ya Mou.Kama yeye ndo mkuu wa serikali inayolalamikiwa udini,lakini lawama hizo zinapelekwa kwa upinzania ambao hawajawahi hata kuongoza nchi,unategemea nani mdini hapo?

  Amejificha kwenye kivuli cha unafiki,lakini mwanga wa JF ni mkali zaidi na kivuli hicho hakitamficha.

  Itafika mahali atafute walinzi na wasaidizi waislam,na jeshi afungue kitengo cha jeshi la waislam kwasababu hakuna sababu ya kumlinda rais mdini ambaye hajali kuhusu maisha ya wananchi wa dini zote!
   
 10. k

  kibodi Member

  #10
  Aug 29, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Familia yetu ni ya wakristo na waislamu na tupo imara pamoja kama zamani. Kijiji chetu kina waumini wa dini zote mbili na bado tunazikana kama zamani. Sijui umeandika haya baada ya kufanya utafiti wa kiasi gani?
  Mkuu tutajie hilo gazeti lenye kusambaza sumu hizo.
   
 11. Jaji

  Jaji Senior Member

  #11
  Aug 29, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anayebisha kuwa udini hakuna aendeleee kusibiri kwani atauona siku za karibuni sana.
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Dalili za udini zipo,tena zipo sana tu,ila sasa watanzania tunapaswa kuwa na akili za kuyachambua tuyaonayo na tuyasikiayo
   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa huwa hajui anacho kifanya kabisa!

   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,599
  Likes Received: 2,001
  Trophy Points: 280
  Kongosho,nimekupata sawia,umesema kuhusu finger pointing,je kama tumemgundua mtu mdini anayeharibu taifa letu unataka tufanyeje?kumbuka 2015 ni mbali sana kwa utaratibu huu sidhani kama tutafika salama.Kwasababu ni wazi uchu wa madaraka na kujikinga dhidi ya wananchi wanaopinga ufisadi.Kiongozi mkuu wa ccm na serikali anatumia dini ili apate supporters,kwasbabu hakna mtanzania bila kujali dini anayefurahishwa na ufisadi labda awe ananufaika nao.Wale wasionufaika,wamekamatwa kwa jina la uislam vs ukristo!tufanyeje kabla ya 2015 kama tuko serious? Ndo maana kwenye bandiko la kwanza nilimalizia kwa kusema "tufanyeje?ama ndo tumeridhika"?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,936
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  The best president in mal-administration and lazy affairs
   
 16. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  atakemea vp wakati yeye ndo muasisi wa Udini?
   
 17. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Nadhani hata wana CCM wana kushangaaa unacho kinena!

  Labda kama humjui rais anaye ongelewa!

  Maneno yako kama ya watu wa zama za mawe

   
 18. K

  Kaldinali JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2012
  Joined: May 25, 2012
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu

  Mimi mpaka sasa kuna kitu nashindwa kukielewa. Honestly speaking demages anazofanya Kikwete kiuchumi, kijamii na kisiasa ni kubwa kupindukia na zitakuwa na long term effects lakini inaoneka hakuna mtu hata mmoja (zaidi ya Mnyika na Ulimwengu) mwenye nguvu ya kumsema, kumkemea, au kumzuia.

  Japokuwa kila mtu anaongelea suala la udini kiushabiki (kama simba na yanga) lakini hili suala ni suala nyeti mno na inashangaza jinsi ndugu Kikwete anavyozidi kulilea na kulikuza. unfortunately watu wengi hawaelewi unyeti wa jambo hili na wanaendeleza ushabiki.

  kiuchumi na kisiasa ndi sijua hata niseme nini. I am speechless on the damages that this man has caused to our young Nation.

  Hakika huyu mzee ni janga kuu la kisiasa nchini Tanzania. Aligombea urais kwaa ajili ya personal reasons na ametawala for personal gains only. Watanzania na mambo yao ya msingi is at the bottom of his concerns.
   
 19. a

  alfazulu JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 735
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa jinsi hali ilivyo sasa huhtaji kushikwa mkono kuonyeshwa kinachoendelea, hukuwahi kusikia kuwa CUF kilikuwa chama cha waislamu, je hata sasa husikii kuwa CDM ni chama cha wakristo? hizo ni propaganda chafu sana zinazokusanya nguvu sasa mioyoni mwa watanzania, athari yake itakuwa kubwa sana, saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana, Tuombe Mungu atulinde. Wenye sera hzo za udini CCM. TAFAKARI.............chukua hatua...................vua gamba....
   
 20. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #20
  Aug 29, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Soma vizuri alicho kiandika!

   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...