Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Status
Not open for further replies.
Mkuu,kuna watanzania wa tofauti,kuna wale wenye kuelewa kuwa kuna utofauti kati ya kusimamia issue za taifa vs zile za dini,kuna wale wasiojuwa utofauti huo.Na pia kuna wale wanaojuwa tofauti hizo,lakini wanachaguwa maslahi ya dini kabla ya yale ya taifa.Ndo maana kuna tawala zilizowahi kupinga mambo ya dini kwenye mataifa wanayoyaongoza,Burundi ilikuwa ni mfano mmojawapo.Ninavyofahamu,kuna wananchi ambao wanafuata taratibu ama sheria za kimila inapokuja kwenye ndoa na mambo ya mirathi,na hayo wala serikali haihusiani nayo.

Ninasema hivyo kwasababu wale wanaotambua taifa kwanza then dini baadaye,wanaweza wasielewe,na inabidi waeleweshwe baada ya kukubaliana na wale wanaoelewa kwamba wale wasioelewa,basi waeleweshwe.

Pia binafsi nina swali,je mahakama hizo zinaweza kufunguliwa na misikiti bila kuihusisha serikali?kwa mfano,hata wakristo wana taratibu na sheria zao,na huwa zinafuatwa bila kuihusisha serikali.Nafahamu kuna wale wanaosema kuwa sheria zetu tulizoziadapt,basi chimbuko lake ni ukristo,na ndiyo maana wakristo huwa hawana shida nazo.Lakini ukiangalia kwa makini sheria wanazozitaka,basi ni sharia law.

Halafu pia, kuna wale wasiojuwa utofauti,yani hawajui kama mambo ya mahakama ya kadhi yana tofauti na sheria za nchi husika,wale ambao wanaweza kuona kama vile serikali iko bias.Ambao wanahisi kwamba sheria za mahakama ya kadhi ziko derived from sharia law,hao pia wanahitaji kueleweshwa.Kwahiyo kama wewe naelewa hayo,si kila mwananchi nayaelewa.
jmushi1,
It's very unfortunately that u're dragging me to the discussion that had never been of my interest! Narudia, unanilazimisha kwenye mjadala ambao cjawahi hata mara moja kuupigia upatu hapa ingawaje si kwamba naona wale wanaoujadili hawana umuhimu wa kufanya hivyo. Nalazimika kuyajadili haya kwa shingo upande hususani pale ninapoona watu ama kwa kutofahamu au kwa makusudi kupotosha! I'd like to explain very short about this here; i'd appreciate kama utaridhika na yale machache na kama hutaridhika nayo basi, with due resect ningekuomba utafute thread inayoelezea masuala ya mahakama ya kadhi ukajifunze huko kama kweli una nia ya kujifunza! Nafahamu hiyo thread humu jamvini ipo ingawaje sizani kama nimeshawahi kuipitia au kuchangia chochote huko coz' it's not part of my interest. Na hata kama nimepata kuchangia, basi sizani kama nilipata kuwa active contributor kama ambavyo nimepata kuwa kwenye baadhi ya mada. Na kama ungependa kufahamu msimamo wangu kwenye suala la Mahakama ya Kadhi, then simple and clear kwamba itakuwa unfair kama mahakama hiyo itahitaji kutumia national resources; kodi za wananchi in particular ingawaje kwenye baadhi ya nchi za Africa ambako hata hao Muslims sio largest population, bado mahakama hizo ni sehemu ya mahaka zinazohudumiwa na serikali...... Hata hivyo, vile vile mahakama hizo hazitakuwa na maana endapo hazitapata legal approval frm the government....kama hazitakuwapo kwa mujibu wa sheria za nchi! Kenya na Uganda, mahakama hizi zipo kwa mujibu wa sheria (KATIBA)

Sasa, turudi kwenye suala la mahakama yenyewe!

Machache ambayo ningependa kuyasema hapa ni kwamba watu wanapotosha kwa makusudi kuhusu suala zima la mahakama ya kadhi. Watu wanapenda sana kuingiza suala la Sharia Law ili ionekane ni jinsi gani Mahakama ya Kadhi isivyofaa kwenye jamii yetu....!! Hii ni kwavile, tunapozungumzia Sharia Laws, watu akili zao wanazipeleka moja kwa moja kwenye watu kukatwa mikono, watu kupigwa mawe hadi kufa kama hukumu ya uzinzi na mambo mengine kama hayo! Huu ni upotoshaji wa makusudi coz' hilo sio lengo la mahakama ya kadhi na wala haitakuja kuwa lengo lake hususani kwa nchi kama Tanzania. Karibu nchi zote za Kiislamu zina Mahakama ya Kadhi lakini ni chache sana kati ya hizo zenye zina-apply Full Sharia kwenye mahakama hizo...hilo lazima ufahamu kama kweli ulikuwa hufahamu! Hata hapa East Africa, kuna Uganda na Kenya zote zina Mahakama za Kadhi ambazo zipo kwa mujibu wa katiba na zote hizo zina-deal only na muslims personal matters [ndoa, taraka na mirathi]!

Likewise, tujaribu kutofautisha kati ya Canon Laws na Mahakama ya Kadhi....hivi vitu ni tofauti kimfumo! Kwa lugha nyepesi, tunaweza kufananisha Canon Laws na sheria za kimila wakati Mahakama ya Kadhi tunaweza kufananisha na mahakama za kimila! Canon Laws, kama ilivyo kwa sheria za kimila, hazikupata kufutwa na serikali lakini Mahakama za Kadhi kama zilivyo mahakama za kimila; zilifutwa na serikali! Wanachohitaji waislamu ni kurudishiwa mahakama zao na sio sheria zao coz' sheria zipo pale pale na wala hakuna wa kuzifuta labda hadi pale Uislamu utakapotokemea duniani kama itakuja kutokea jambo hilo! Aidha, Mahakama za Kadhi si Misikiti bali ni Mahakama za Kisheria to deal ONLY to matters affecting personal status of muslims ambazo ni masuala ya ndoa, taraka na mirathi....PERIOD! Hii wala si mahakama ambayo mwizi atapelekwa kuhukumiwa ingawaje wapotoshaji wanapenda kusema huo utakuwa mwanzo tu lakini hapo baadae watataka zikate watu mikono!!

MAHAKAMA ZA KADHI NA CANON LAWS:
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali, kuna tofauti kati ya Mahakama za Kadhi na Canon Laws. Na sizani kama kwenye Biblia kuna sehemu yoyote ambayo inaeleza ni namna gani mirathi inapaswa kugawanywa au ni namna gani taraka inapaswa kutolewa na rights za wahusika. Katika Quran wameeleza ni namna gani mirathi inapaswa kugawanywa ni akina nani wana haki ya kurithi kulingana na status ya marehemu(deceased family set up) na vile vile imeeleza vizuri mchakato wa taraka! Katika Uislamu, taraka ni suala la mchakato na sio suala la kuamka na kuandika taraka na kumwambia mkeo "TAKE THIS AND GO!" Kwenye Uislamu, except kwa suala la mirathi; kama hamna kifo, basi suala la mali linategemea na actual contribution ya mali husika kwa wanandoa. Hapa kuna uwezekano kwamba mali yote ikawa ya mke peke yake au ya mume peke yake au yao kwa pamoja kulingana na actual contribution ya kila mmoja! Lakini wakati mali ikiwa ni ya mwanamke kwa 100% basi halazimiki kutoa hata senti kumi kwa mtalaka wake; kwa mwanaume hata kama mali ni yake kwa 100% basi analazimishwa na Utamaduni wa Kiislamu kukata sehemu na kumpa mtalaka wake!! Hata kama mke ni Gavana wa BOT na mume ni mwalimu wa shule za kata; kwa mujibu wa Uislamu mwanaume huyu ana wajibu wa kutunza familia na mwanamke wala habanwi na sheria.....na mke huyu pamoja na ukwasi(utajiri) wake wote alionao bado ana haki ya kumpeleka mumewe huyu masikini kwenye mahakama ya kadhi kwamba mumewe haudumii familia! Mwanaume huyu maskini wala hana haki ya kumpeleka mkewe tajiri kwenye mahakama ya kadhi na kusema kwamba ingawaje mkewe ana pesa za kutosha lakini hatoi hata senti moja kwa ajili ya familia....huo si wajibu wake na akifanya hivyo ni kwa upendeleo wake tu huyo mwanamke na pindi anapofanya hivyo(kuhudumia familia); mwenyezi mungu anageuza mchango huo moja kwa moja kuwa sadaka! Hata hivyo, hapo haimaanishi kwamba Mwanamke akiwa na uwezo asihudumie familia; la hasha....busara inasema ahudumie tu na atapata malipo yake ya sadaka lakini halazimi na wala hatapata dhambi asipofanya hayo! So, mambo complicated kama hayo hayawezi kuwa handled na circular courts! Na kuwepo na sheria za kiislamu pasipo na mahakama za kadhi ni sawa na kuwa na graduates wa sheria pasi na kuwa na taasisi za ku-enforce sheria hizo!

Umegusia suala la mahakama za kadhi kuanzishwa na misikiti!!! This's very wrong mkuu wangu! Msikiti ni nyumba ya ibada na sio sehemu ya kutolea hukumu!! Msikiti utabaki msikiti na mahakama ya kadhi itabaki kuwa mahakama ya kadhi.....hivi vitu ni tofauti! Hata mimi naweza kusalisha msikitini; lakini sina weledi wa japo 10% wa kuwa hakimu wa mahakama ya kadhi!

Kwa kuchelea post hii kuwa ndefu na kuwa boring to read, niishie hapo tu!
 
NasDaz,nimekupata mkuu wangu,miye kamwe sijawahi kuipinga mahakama ya kadhi.Unakumbuka kwanza Mrema alipoileta hoja hiyo,basi ccm ndo nao wakaikurupukia,lakini binafsi sina shida na mahakama ya kadhi hata kidogo.

Ninachopinga mimi,ni watu kujenga hoja kwa misingi ya chuki.Kwa mfano mtu anayesema kuna mfumo kristo,halafu ndo huyo huyo anayedai mahakama ya kadhi,tayari unakuwa unahoji malengo yake.

Mfano haya mambo ya kuweka kipengele cha dini kwenye sensa.Kama tungekuwa tunaeleweshana kwa jinsi hii,basi labda tungeweza kuelewana,lakini wale wanaotaka mambo kama ya oic na hayo ya mahakama ya kadhi,wao wanasema kuwa mfumo mzima hauna maslahi na waislam na kwamba umewakandamiza.Na mifano inatolewa mingi kama hiyo ya elimu na hayo ya upotoshaji kuhusu Mou.

Mapro mahakama ya kadhi,wamekubali hoja yao ikatekwa na wale wenye misimamo mikali,ambao ukishawapatia kimoja,basi wanaona kwamba ni wakati wa kutaka kingine,na mwishowe itakuwa ni uadui miongoni mwa watanzania.

Kama unayo link ya huo mjadala,basi ningeshukuru unipatie ile niweze kuupitia.Binafsi kwasababu nilikuwa mshabiki wa Mrema enzi zile,basi hoja hiyo hata mimi nilishaisapoti.

Kwamba wakenya ama waganda etc wana sheria hizo zenye kuruhusu mahakama ya kadhi na oic,basi cha muhimu ni kuangalia nikivipi wao wamefanikiwa bila ya kuwa na matatizo.

Maana kama mkishaanza na hoja ya kwamba ninyi mko wangi zaidi ya dini nyinginezo,then ni lazima hoja zenu zitatiliwa mashaka na watanzania wengine either wenye dini za tofauti ama hata wasiokuwa na dini na wale wanaouweka utaifa wao mbele kabla ya hizi culture tulizoletewa.

Nashukuru kwa jitihada za kunielewesha.Ila ningependa kuisoma hiyo mada.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu NasDaz,kwa kuongezea,nadhani sisi tuna mfumo wa common laws,na si hizo "cannon law",nachelea kusema hizo ni propaganda kama unaamini mfumo wetu ni huo.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu NasDaz,kwa kuongezea,nadhani sisi tuna mfumo wa common laws,na si hizo "cannon law",nachelea kusema hizo ni propaganda kama unaamini mfumo wetu ni huo.

Mkuu wangu,
Binafsi sifahamu chochote kuhusu aina hizo mbili....jambo moja ambalo cna shaka nalo ni kwamba, mara kwa mara nimekuwa nikisikia kuhusu Canon Law na sio Common Law....na aidha, nimepata kusoma pahala kwamba hata Dr. Slaa miongoni mwa mambo aliyopata kusomea ni hizo Canon Law. So, kwavile sijapata kuwa na interest za kufahamu hizo sheria zinahusu nini hasa; basi ninavyosikia sheria za kanisa ndo nilizani ndo hizo hizo Canon Law! Haidhuru ukitoa darsa kuhusu hizo Canon na Common Law....ingawaje kwa sasa nitajaribu kuperuzi peruzi ili angalau niwe na mwanga.
 
Natofautiana na nyie wote..Tanzania hakuna Udini ila Tz kuna U-njaa...ebu angalia hao wote wanaopigania udini ukiangalia wanaishia kwenye Ulaji tu,hakuna anaepigania kupata wafuasi ila kinachopiganiwa ni ulaji tu...ndio maana mifano yote umu imebase kwenye nani wanapata mlo zaidi...kwaio wote kina Ponda wanasumbuliwa na njaa zaidi sio kupenda dini zao.
 
Nashukuru kwa jitihada za kunielewesha.Ila ningependa kuisoma hiyo mada.

Post inayohusiana Mahakama ya Kadhi na OIC inapatikana Jukwaa la Jamii Intelligence. Ukifungua tu, unaanza kwanza kukutana na hiyo Thread toka kwa Mzee Mwanakijiji ambayo STICKY hapo since 2006!!! Binafsi, sina kumbukumbu kama nilishawahi kuipitia lakini leo nimeifungua na kukuta imeenda mbali sana....coz' ingawaje ni ya miaka sita iliyopita lakini bado inaendelea kuchangiwa. Link yenyewe ni hii: https://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/19947-juu-ya-oic-na-mahakama-ya-kadhi-188.html
 
Umeyaona ya shekh PONDA tu, ya maasikofu hujayaona kweli wewe huiwezi siasa!!Waislam wanahaki ya kudai kipengele cha dini ktk sensa.kwanini wadai tembelea web hizi upate reference
1) www.wikipedia.com/tanzania
2) www.arc.com/tanzania

web zote hzo zinatoa idadi ya watanzania kwa mujibu wa dini yao wakati tangu 1967 watanzania hatuja hesabiwa kwa mjibu,wa dini zetu.swali hawa WA RC Takwim hz wanazitoa wapi????

shida iko wapi wewe nawe tengeneza website yako weka link ujitajie idadi ya waislam unayoitaka bcoz it has nothing to do na strategic plans za serikali .na mkishajua wadini wenu basi ziwasaidie kufanya mambo yenu ya kidini.me sioni shida kwa rc kusema wakristo ni wangapi kwani nawe hujakatazwa kusema waislam ni wangapi......
 
Mbona hilo liko wazi kabisa
Rais Gani anakaa kimya hawezi kukemea vitendo viovu vinavyoendelea nchini kwake
Kazi yake kukata mitaa
 
jmushi1 -nadhani wewe ndo mdini na wengine kwenye orodha ya wanaofanana nawe. Ulitaka JK afanye ninui? Kama wewe sio mdini na mapadri kwa ujumla wenu kwa nini basi hamktaka kuinusuru nchi kwa kutaka muafaka ikiwa kweli kujua idadi ya watu kwa dini zao si tatizo? Nadhani tuelewe kuwa kuna ukweli unafichwa kuhusu nani mdini -Muislam au mkristu- kwa nin jmushi1 hakuona tatizo pale kanisa katoloki lilipotoa idadi ya watanzania wakiwemo waislamu na kwa nini ofisi ya waziri mkuu nayo ikatuia takwimu za kanisa? Mdini nani-mkatoliki aliyejipa mamlaka ya kuhesabu watu kwa namna alivyojua yeye au huyu anayetaka sasa kipengele cha dini kiwekwe ili ukweli wa wapi ni wengi utolewe na serikali? Changanua japo kidogo
 
unataka afanyeje? hao aliowaweka kumsaidia wamefanya nini? rais siyo msemaji wa kila siku na kila jambo linapojitokeza. Fistlady1 onesha kuwa wewe ni firstlady1 kwa kukomaa busara za upambanuzi si kubugizwa muono wa wengine
 
lkn kwa haki gani rc walikuwa na mamlaka ya kusema waisla wangapi na kwends kuitangaza tbc1? lau kama wangehesabu wakatoliki (wakiristu) hakuna ambaye angehoji
 
kinachotugharimu ni sheria zinazoshadadia kufanya uchaguzi wa raisi kila baada ya miaka mitano. Ingependeza kuboresha sheria hii ili kama kiongozi anayumba kimaamuzi basi ufanyike uchaguzi wakati wowote ili kuinusuru nchi,
 
Eti THE BEST PRESIDENT ambae hajawahi tokea Tanzania.....! Umetumwa nn wewe? kama huna cha kuandika chapa lapa
 
Mkuu wangu,
Binafsi sifahamu chochote kuhusu aina hizo mbili....jambo moja ambalo cna shaka nalo ni kwamba, mara kwa mara nimekuwa nikisikia kuhusu Canon Law na sio Common Law....na aidha, nimepata kusoma pahala kwamba hata Dr. Slaa miongoni mwa mambo aliyopata kusomea ni hizo Canon Law. So, kwavile sijapata kuwa na interest za kufahamu hizo sheria zinahusu nini hasa; basi ninavyosikia sheria za kanisa ndo nilizani ndo hizo hizo Canon Law! Haidhuru ukitoa darsa kuhusu hizo Canon na Common Law....ingawaje kwa sasa nitajaribu kuperuzi peruzi ili angalau niwe na mwanga.
Madhali umeshasikia kuhusiana na canon law,basi wacha nikupe hints kuhusiana na common law.

Kwa kifupi,common law iko originated kutoka kwa waingereza.Nchi zote ambazo zilitawaliwa na waingereza,kwasababu ya colonial heritage,sheria zetu zimetokana na common law ambayo ni English legal sytem.

Common law imekuwa developed na majaji kutokana na maamuzi ya koti yaliyopita.Yani common law is based solely on precedent.

Hii ina maana kuwa,makosa yakitokea,halafu uamuzi ukafanyika,basi kosa likitokea tena,jaji ana refer hukumu kutokana na maamuzi ama hukumu zilizowahi kutolewa kwenye kosa kama hilo.

Sheria hizi zimeendelea ku "evolve" kutegemeana na jamii husika.

Kimsingi,hakuna crime mpya,na kwahiyo crime yoyote ikitokea,basi maamuzi yanayotolewa,huangalia ni kitu gani ama ni maamuzi gani yalitolewa huko nyuma wakati kosa hilo lilifanyika ama kutokea,hiyo ndo maana halisi ya kusema "it is a base on precedent"

Kwa misingi hiyo basi,common law kwa sasa,zina constitute broader decisions kutokana na jamii husika,bases zake ni uingereza,lakini maamuzi mengine yanatokana na culture za jamii husika.Hata nchi nyingi tu za waislam zina basis za common law.

Kama umepata mwanga kidogo kuhusiana na common law,basi nijulishe.Ama kama kuna pahala hujaelewa,basi nijulishe.
 
Si ukae kimya kama huna points,PUMBA HIZO!

Who are you talking to?maana dalili za ukichaa ni nyingi,hii ni mojawapo.Jifunze ku quote,maana hata haijulikani umemwelekezea nani bandiko lako hili.
 
Who are you talking to?maana dalili za ukichaa ni nyingi,hii ni mojawapo.Jifunze ku quote,maana hata haijulikani umemwelekezea nani bandiko lako hili.
Hilo ni stone thrown in the dark.
na wewe ndie umepiga kelele...
 
Wewe songoro unapata taabu bure kuuliza wakatoliki wanapata wapi hizo data. Wao wamehesabu waomini wao makanisani. Weather hizo data ni sawa au si sawa ni jambo lingine. Sasa waislamu wakipenda na wao wahesabu waomini wao misikitini sio kulazimisha serikali ikusanye data ambayo haina kazi zaidi ya kuleta tafrani. Kama jamii ya kitanzania inakubaliana dini zisitoe idadi ya waomini wao hadharani basi itungwe sheria.
 
Familia yetu ni ya wakristo na waislamu na tupo imara pamoja kama zamani. Kijiji chetu kina waumini wa dini zote mbili na bado tunazikana kama zamani. Sijui umeandika haya baada ya kufanya utafiti wa kiasi gani?
Mkuu tutajie hilo gazeti lenye kusambaza sumu hizo.


Samani kaka, nimekubali kweli upo kijijini, ipo Radio ya hawa watu inaitwa Radio Imani na lipo Gazeti lao linaitwa Ann Nur, ni full udini na kueneza chuki kati ya watu hawa wa dini tofauti, na ipo pia TV yao inaitwa TV Imani, ninacho kijua mimi kwa sheria za vyombo hivi vya ki Electronic, huwezi ruhusiwa kurusha matangazo yako kwa watu wengi kama bado upo kwenye majaribio, hii TV imeanza moja kwa moja na kuingia kwenye settelite, hapa sian shaka kwamba sheria zimepuuzwa, anyway, huyu ndo JK!
 
Hilo ni stone thrown in the dark.
na wewe ndie umepiga kelele...

Hakuna kilichopo gizani,yani thread yote na wewe ndo umekuja na hii?kweli uko gizani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom