Ndugu Mkandara,Swala sio tuko wengi au laa isipokuwa sensa itatuwezesha kujua idadi ya Watanzania wote kwa ujumla wa makundi yao ya kijamii iwe watoto wanawake, makabila na hata dini zao tena inatakiwa tujue hata wageni wahamiaji na wale walioingia kinyemela. Wazanzibara wangapi wamehamia bara na Wabara kuhamia visiwani kisha tunatafuta reasons na kadhalika. Hii ndio maana kamili ya sensa ili kuiwezesha serikali yetu ya muungano kupanga mipango yake ya maendeleo kwa jamii nzima kwa kuzingatia tofauti zetu ambazo huzua kero ktk jamii kama zisipohusishwa.
Kinachonishinda kuelewa ni kwa nini mnakazania kuuliza kama waislaam ni wengi iweje?, hivi tunapo wahesabu wanawake na wanaume nchini (kipengele hicho) huwa tunataka kujua wingi wao au ni takwimu zinazoiwezesha serikali kupanga mipango yake ktk maendeleo kuwawezesha wanawake ktk sehemu za ujenzi wa taifa. Kila siku tumesikia wanawake wakillalamika kuhusu kutengwa ktk nafasi za kazi na masomo, utajuaje ukweli wa dhana hii pasipo kufanya sensa?.
Kwa nini serikali inataka kujua idadi ya watoto? Je, wakiwa wengi itafanya nini? na kwa nini serikali inataka kujua wingi wa wazee, Je wakiwa wachache itawafanya nini?. Hizi ndizo fikra zenu tu WINGI wakati swala sio wingi bali kujua hatua za kimaisha baina ya jamii zetu kwa miaka 10 iliyopita kunatokea mabadiliko gani na serikali itajiandaa vipi kuwaendeleza ama kuwalinda. Maswali haya mnashindwa kujiuliza isipokuwa la waislaam tu mbona husemi wakiwa wakristu wengi itakuwaje?
Hivi watu kuhamia sehemu kunaweza kujulikana tu watu wakiulizwa dini zao? Watoto wakiwa wengi serikali itapanga maendeleo kama huduma za afya na uzazi, mipango ya badae ya kujenga shule kulingana na idadi hiyo. Je, ikipata wapagani ni wengi zaidi itapanga mipango ya kuwapelekea misikiti na makanisa?
Ukweli ni kuwa popote walipo ndugu zetu waislamu watadai kufanyiwa vitu ambavo zinapaswa kufanywa na dini badala ya serikali hii ni kwa kuwa secularism kwa waislamu ni msamiati. Badala ya kutenga huduma au mambo yao na serikali watataka huduma nyingi zitoke serikalini au ziwe katika mfumo wa serikali. Huu mfumo unawezekana tu ambapo watu au waislamu ni wengi hivyo akili zao ziko sawa kidini na njia hiyo ya kuendesha serikali. Ni mfumo ambao ni wa ajabu kabisa lakini kwao uko sahihi. Nafikiri kwa idadi yoyote ambayo wangepata kwenye sensa wangeanza kudai haki za kuhudumiwa na serikali kwa huduma ambazo zinapaswa kuwa za kidini kama mahakama ya kadhi.
Mimi siamini waislamu ni wengi nchi hii hata nikichukua ramani ya Tanzania niiweke mkononi mwangu halafu nianze kuanisha maeneo ambako kuna waislamu. Ndio si kidogo lakini ni sehemu ndogo tu kulinganisha na maeneo walipotapakaa wakristo. Huko kwetu ukienda watu ambao hawajatembelea mjini hawajui kuna dini inaitwa uislamu labda kwa sasa kwa kuwa mawasiliano yapo kwa wingi. Nilitamani serikali ifanye hiyo sensa ili waislamu wajue ukweli kuwa ni wachache. Lakini najua hilo lisingeishia hapo. Swali; Wangekubali ni wachache? Wasingeanzisha malumbano mengine?
Na kwasababu Mkandara hujajibu swali la Jmushi1. Mimi naliuliza tena hilo swali; Serikali ikishajua waislamu, wakristo au wapagani ni wangepi inakuwaje? Inasaidia nini serikali? Inatusaidia nini watanzania katika kusukuma gurudumu la maendeleo?