jmushi1,
labda nizungumze kidogo kuhusu swala hili kwa jinsi mnavyoliweka. Kwa wale wanaosema Nyerere alikuwa mdini binafsi yangu siwezi kuwapinga isipokuwa kwa kutoa ushahidi wangu dhidi ya madai yao maana Nyerere alikuwa Mkristu na wao (waislaam) wanaona hakuwapa haki yao stahiki kama Watanzania. nitawaonyesha kazi ya Nyerere kuwa haikulenga kuwakandamiza waislaam na alifanya kadhaa wa kadhaa badala ya kushindana kuhusu Ukiristu wake, Nyerere hakuongoza nchi yetu kwa kuliwakilisha kanisa au Vatican..
Kinachonishinda kuelewa ktk mada hii ni pale hoja nzima inaonyesha JK akiwakandamiza Waislaam kwa kukataa ombi lao la sensa halafu anatakiwa kuwamaliza kabisa.. Huyu JK aliyewaweza wakristu kupata mtaji na msahama wa kodi chini ya mfumo wa kikoloni bado anaitwa mdini kwa sababu hakumchukulia hatua Sheikh Ponda, muislaam mwenzake. Hii kitu kidogo haikukaa sawa kabisa na ndio maana nimesema JK sio mdini bali anawawezesha zaidi wakristu pia alipitishwa na viongozi wote wa makanisa kama chaguo la Mungu, hivyo udini wake uko wapi?. Huyu mtu kapata blessing za makanisa leo anatakiwa kummaliza kabisa Sheikh Ponda imekuwa mdini kwa kutochukua hatua kali.. Ama kweli waislaam hawatakiwi..
By the way, binafsi yangu sikubaliani kabisa na wale wanaomlaumu Nyerere na Udini, maana ni ktk utawla wake tulikuwa na baraza la waislaam la BALUKTA likipingana na BAKWATA na tukifanya hata mihadhara pasipo kutiwa shaka la Udini au Ugaidi, lakini alipoingia Mwinyi na baada ya muafaka wa MoU, Balukta ilipigwa vita vikali sana na hata kiongozi wake kukamatwa akateswa na kuuawa..Ni baada ya Nyerere tumeyaona ya Mwembechai, tumeona waislaam wakipangiwa hata siku ya kufunga na kufungua mwezi wa Ramadhan! haya maajabu sana ktk Uislaam.
Chini ya uongozi wa Nyerere alifuta mfumo kristu (mfumo wa kikoloni) alizuia kabisa asasi za kidini kujihusisha na shughuli za serikali na waifanye kazi yao ya kueneza neno la Mungu. Akataifisha shule na Hospital zote zilizokuwa chini la miliki ya dini na kuziweka mikononi mwa serikali na akatangaza Azimio la Arusha ambalo liliweka UMASKINI, UJINGA na MARADHI kama adui wetu wakubwa. Kwa hatua hiyo hakupendwa na waislaam na wakristu maana kilichofuata hakikuwa ktk fikra wala utamaduni wao.
Lakini leo baada ya kuacha vita hivi, tukavunja msisitizo wa kanuni za Ukristu - Separation between church and states kwa kuwapa kanisa mamlaka juu ya kuendesha elimu na Afya itakuwaje watu hawa Mwinyi, Mkapa na JK waitwe wadini kwa sababu ya imani zao badala ya kuitwa wadini kwa sababu wameliwezesha kanisa kuendesha shughuli za serikali?.
Pengine nambieni JK ni mdini kwa sababu anawateketeza Waislaam nitakubaliana na wewe maana Sheikh Ponda anapingana na msimamo wa JK.. Waislaam wawili wanaopingana, huwezi kuita mmoja ni mdini kwa kutomchukulia hatua mwenzake. Kifupi mada hii haina kichwa, ni bias imechukua mwelekeo ambao hauwezi kutetewa isipokuwa kudhangaza..