Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Status
Not open for further replies.
Acha kulalamika! Kata rufaa kama umeonewa! Kuna sehemu ya kupeleka malalamiko yako! Kama uzi umeunganishwa ujue contents zina fanana!

Alalamike kwa nani wakati tayari tumeshasema hili si jukwaa huru

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mfumo kristu
unawapa fedha makanisa badala ya kwuasomesha watoto, ebu nambie hizo billioni 90 zingewasomesha watoto wangapi kila mwaka! Sielewi kuhusu Wakristu ila nafahamu watoto wengi wa kiislaam wanaachwa nyuma kwa sababu wamenyang'anywa shule zao, wananyimwa fedha za kujiendeleza. Ukinyimwa ELIMU ni sawa na kurudishw aktk utumwa.. Haya pekee ni sawa na utawla wa mkoloni japokuwa nao walidai kwamba wametulea elimu lakini ukweli ulikuja umbuka mwaka 1061 tulikuwa na madaktari wawili tu tukizidiwa hata na Zanzibar ilokuwa na watu wasiozidi millioni. Huwezi kunambia kitu mkuu wangu kwa sababu nimesoma ktk mfumo huo na najua taabu nilizozipata..
Ni ushauri mzuri ukawapa watu wa chama chako especially kipindi hiki ambapo mnaelekea kama vile mtachukuwa nchi.Ni mambo ambayo mnatakiwa muyafanyie kazi kwa manufaa si tu ya chama chenu,bali taifa kwa ujumla.Lakini hilo halimzuii JK kuwa responsible na huu udini ulionea nchini na kusababisha ule mshikamano wetu na umoja wa kitaifa kuwa mashakani kwa mara ya kwanza toka tupate uhuru.
Kwasababu ebu fikiria jinsi ambavyo eti ufisadi wa JK hauonekani machoni pa wanachama wa chadema kama wewe kwasababu ni muislam mwenzao.Hilo ndo janga kuu haswa kwa baadhi yetu.Ukombozi hautapatikana kwa misingi hii mkuu wangu.

Hivi mkuu kwahiyo unataka kubadili "mfumo kristo" kwenda mfumo gani?maana kama unataka mabadiliko ili watanzania wote wanaufaike,then huwezi kuyapigania kwa mgongo wa uislam kwasababu once again utakuwa unahatarisha usalama wa taifa kwa kuuweka umoja wetu wa kitaifa "rehani",matatizo tuliyonayo kama wananchi ni the same kabisa bila kuangalia dini.Mafisadi wako both wakristu na waislam,tunaweza kuwaona kama tukitumia macho ya utanzania.

Ni hayo kwasasa.Nashukuru kwa mjadala wa kiustaraab.Stay blessed.
 
Alalamike kwa nani wakati tayari tumeshasema hili si jukwaa huru

Chama
Gongo la mboto DSM
sasa kama si jukwaa huru unafanya nini humu mkuu?ama na wewe unapenda utumwa?
 
Ni ushauri mzuri ukawapa watu wa chama chako especially kipindi hiki ambapo mnaelekea kama vile mtachukuwa nchi.Ni mambo ambayo mnatakiwa muyafanyie kazi kwa manufaa si tu ya chama chenu,bali taifa kwa ujumla.Lakini hilo halimzuii JK kuwa responsible na huu udini ulionea nchini na kusababisha ule mshikamano wetu na umoja wa kitaifa kuwa mashakani kwa mara ya kwanza toka tupate uhuru.
Kwasababu ebu fikiria jinsi ambavyo eti ufisadi wa JK hauonekani machoni pa wanachama wa chadema kama wewe kwasababu ni muislam mwenzao.Hilo ndo janga kuu haswa kwa baadhi yetu.Ukombozi hautapatikana kwa misingi hii mkuu wangu.

Hivi mkuu kwahiyo unataka kubadili "mfumo kristo" kwenda mfumo gani?maana kama unataka mabadiliko ili watanzania wote wanaufaike,then huwezi kuyapigania kwa mgongo wa uislam kwasababu once again utakuwa unahatarisha usalama wa taifa kwa kuuweka umoja wetu wa kitaifa "rehani",matatizo tuliyonayo kama wananchi ni the same kabisa bila kuangalia dini.Mafisadi wako both wakristu na waislam,tunaweza kuwaona kama tukitumia macho ya utanzania.

Ni hayo kwasasa.Nashukuru kwa mjadala wa kiustaraab.Stay blessed.
Chama changu hakina matatizo hata kidogo isipokuwa tuhuma zinazowafuata baadhi ya viongozi kutumiwa na cartel fulani ndizo nisizokubali zipite tu pasipo kulaaniwa. Iwe dr.Slaa, Mbowe au Zitto huwa mstari wa mbele kuanzisha mada hapa JF kutafuta ukweli ni upi..Ujumbe nimeshaufikisha kama hawatasoma hapa watakuja ambiwa Mkandara ana msimamo gani na sipo pekee maana nimefuatilia swala hili kwa muda mrefu sasa..

Na usidhani nina mawasilino ya karibu na viongozi wa Chadema - hapana sina, bali ni mwanachama kama wengineo waloweka imani kubwa juu ya chama hiki kuuondoa utawala huu madarakani pasipo kujali kuna Kikwete muislaam ama Lowassa Mkristu..

Hii habari na kumchafua JK kwa udini wakati yeye anawapa makanisa billioni 90 kila mwaka, nafuu ya kodi, serikali ikiwasomesha walimu wao bure halafu wanakuja toza wanafunzi mamilioni ili kulipa mishahara ya walimu wao, akitoa michango ya mamillioni ktk ujenzi wa makanisa, shule na zahanati na bado mshiriki mkubwa wa mfumo wa kikoloni uloasisiwa mwaka 1992 ambao waislaam wamekuwa wakiulalamika kwa miaka yote hawasikilizwi.. Huyu JK ni mdini kivipi haswa!..kwa sababu ya Sheikh Ponda!
- Ndipo napopingana na wewe kwa sababu hawakwazi wakristu wala hawasaidii lolote Waislaam...
 
Ni Kweli kabisa mamilioni ya MoU yanavyo pelekwa Chadema kupitia mgongo wa katoliki na zaidi ya hatari
 
Chama changu hakina matatizo hata kidogo isipokuwa tuhuma zinazowafuata baadhi ya viongozi kutumiwa na cartel fulani ndizo nisizokubali zipite tu pasipo kulaaniwa. Iwe dr.Slaa, Mbowe au Zitto huwa mstari wa mbele kuanzisha mada hapa JF kutafuta ukweli ni upi..Ujumbe nimeshaufikisha kama hawatasoma hapa watakuja ambiwa Mkandara ana msimamo gani na sipo pekee maana nimefuatilia swala hili kwa muda mrefu sasa..

Na usidhani nina mawasilino ya karibu na viongozi wa Chadema - hapana sina, bali ni mwanachama kama wengineo waloweka imani kubwa juu ya chama hiki kuuondoa utawala huu madarakani pasipo kujali kuna Kikwete muislaam ama Lowassa Mkristu..

Hii habari na kumchafua JK kwa udini wakati yeye anawapa makanisa billioni 90 kila mwaka, nafuu ya kodi, serikali ikiwasomesha walimu wao bure halafu wanakuja toza wanafunzi mamilioni ili kulipa mishahara ya walimu wao, akitoa michango ya mamillioni ktk ujenzi wa makanisa, shule na zahanati na bado mshiriki mkubwa wa mfumo wa kikoloni uloasisiwa mwaka 1992 ambao waislaam wamekuwa wakiulalamika kwa miaka yote hawasikilizwi.. Huyu JK ni mdini kivipi haswa!..kwa sababu ya Sheikh Ponda!
- Ndipo napopingana na wewe kwa sababu hawasaidii lolote Waislaam...
Mkuu nimekupata sana.Ushauri wangu ni kwamba inabidi uwe makini kama mwanachadema ili isije ikawa kama ule msemo wa "Crabs in a bucket..."

JK ni mdini kwasababu ndiye aliyeuchochea kwenye uchaguzi wa 2010 na madhara yake yako wazi kwasasa.Hii hali haikemei,na kwa mantiki hiyo,yeye ni mdini.

Under his watch,nchi inajadili kila jambo kwa misingi ya udini.Nadhani hapo ndo unampendea na ndiyo maana huoni huo kama ni udini.Unaona kwa anaonewa kwa uislam wake.

Kiasi cha kwamba hata viongozi wa chadema hususan Slaa unakuwa na wasiwasi naye kwani umelishwa chuki na kuamini.

Usipokuwa makini inawezekana msiweze kusolve hayo mambo na pengine ukajitoa chadema.Ila siamini kama waislam wote wa chadema wana msimamo wa kusema JK anaonewa kwa kuwa ni muislam.Huyo atakuwa si chadema.

Ukiyatizama matatizo ya watanzania kwa jicho la kitanzania,basi utayaona matatizo ya watanzania ni si ya waislam peke yake wala wakristu peke yake.

Tulipo kama Taifa,hizi za udini wala haikutakiwa iwe issue kabisa.Taifa linatuhitaji kama watanzania.Kama kuna matatizo,kuna namna ya kuyashughulikia kama watanzania,na tukasolve issue.

Kwa kumalizia,napenda uniambie ni mfumo gani unataka uwe mbadala wa mfumo kristo.Tuanzie hapo.Hila nisingependa thread hii ijadili hayo.Kwasababu ni somewhat out of its original purposes.
 
Mkuu nimekupata sana.Ushauri wangu ni kwamba inabidi uwe makini kama mwanachadema ili isije ikawa kama ule msemo wa "Crabs in a bucket"

JK ni mdini kwasababu ndiye aliyeuchochea kwenye uchaguzi wa 2010 na madhara yake yako wazi kwasasa.Hii hali haikemei,na kwa mantiki hiyo,yeye ni mdini.

Under his watch,nchi inajadili kila jambo kwa misingi ya udini.Nadhani hapo ndo unampendea na ndiyo maana huoni huo kama ni udini.Unaona kwa anaonewa kwa uislam wake.

Kiasi cha kwamba hata viongozi wa chadema hususa Slaa unakuwa na wasiwasi naye kwani umelishwa chuki na kuamini.

Usipokuwa makini inawezekana msiweze kusolve hayo mambo na pengine ukajitoa chadema.Ila siamini kama waislam wote wa chadema wana msimamo wa kusema JK anaonewa kwa kuwa ni muislam.Huyo atakuwa si chadema.

Ukiyatizama matatizo ya watanzania kwa jicho la kitanzania,basi utayaona matatizo ya watanzania ni si ya kwaislam peke yake wala wakristu peke yake.

Tulipo kama Taifa,hizi za udini wala haikutakiwa iwe issue kabisa.Taifa linatuhitaji kama watanzania.Kama kuna matatizo,kuna namna ya kuyashuhulikia kama watanzania,na tukasolve issue.

Kwa kumalizia,napenda uniambie ni mfumo gani unataka uwe mbadala wa mfumo kristo.Tuanzie hapo.Hila nisingependa thread hii ijadili hayo.Kwasababu ni somewhat out of its original purposes.
Nitarudia tena kusema JK hana Udini kwa maana ya kwamba udini ni pale anawakandamiza wakristu. JK alishinda uchaguzi wa mwaka 2010 kwa upumbavu wetu sisi wenyewe tulipokuwa tukishindana na CUF kuhusu imani za dini. Mapadre wote nchini walimpitisha JK kwutokana na misaada yake akiitwa chaguo la Mungu kwa mara ya pili.

Tatizo la Udini lilianzishwa makanisa na vijiweni pindi alipowaahidi waislaam mahakama ya kadhi. Mkamwita mdini na hata kuzungumziwa makanisa.. Ndipo waislaam nao wakaja juu wakifikiria msanii JK atawapa hiyo mahakama ya kadhi. JK asingeweza kabisa kushinda uchaguzi wa mwaka 2010 kama tungebakia ktk ktk siasa badala ya kuwasikiliza Mapadre, Masheikh na Maaskofu wakichochea Udini.

Ushindi wa JK umetoka kwetu sisi kutokuwa na beki wazuri na CCM waliweza kupenya ktk ngome zetu kwa kutumia fursa tulowapa sisi wenyewe kwa sababu badala ya kukishambiulia chama CCM na Ufisadi kama walivyofanya viongozi wetu sisi tukadakia Udini kumshambulia JK na mahakama ya kadhi. Mada zaidi ya 5 zilihusu Mahakama ya kadhi tu na waandishi ni wanaChadema na Mapadre, wengine wakienda hadi misikitini kusikiliza hotuba na kuzileta humu, hivyo tukawapa mwanya waislaam pia kumshambulia Dr.Slaa ambaye alikuwa Padre na hivyo kuweka wasiwasi juu ya uongozi wake. Nilitoa tahadhali nyingi sana hapa JF juu ya hilo, lakini kama kawaida yenu huwa hamuamini anayoyasema Mkandara lazima mpinge kwa sababu hayapo karibu na ukweli mnaoupenda.. Ikala kwetu..

Mkuu wangu imetosha kwa leo tuache hizi siasa za udini.. zipite siku hatuandiki uchochezi wa aina yoyote baina ya Waislaam na Wakristu kwa sababu haitusaidii na nakuhakikishia Chadema watakuwa na wakati mgumu sana uchaguzi wa mwaka 2015 ikiwa tutaendelea kuchochea moto huu..
 
Nitarudia tena kusewma JK hana Udini kwa manaa kwamba anawakandamiza wakristu. JK alishinda uchaguzi wa mwaka 2010 kwa upumbavu wetu sisi wenyewe tulipokuwa tukishindana na CUF kuhusu imani za dini. Mapadre wote nchini walimpitisha JK kwutokana na misaada yake akiitwa chaguo la Mungu kwa mara ya pili.

Tatizo la Udini lilianzishwa makanisa na vijiweni pindi alipowaahidi waislaam mahakama ya kadhi. Mkamwita mdini na hata kuzungumziwa makanisa.. Ndipo waislaam nao wakaja juu wakifikiria msanii JK atawapa hiyo mahakama ya kadhi. JK asingeweza kabisa kushinda uchaguzi wa mwaka 2010 kama tungebakia ktk ktk siasa badala ya kuwasikiliza Mapadre, Masheikh na Maaskofu wakichochea Udini.

Ushindi wa JK umetoka kwetu sisi kutokuwa na beki wazuri na CCM waliweza kupenya ktk ngome zetu kwa kutumia fursa tulowapa sisi wenyewe kwa sababu badala ya kukishambiulia chama CCM na Ufisadi kama walivyofanya viongozi wetu sisi tukadakia Udini kumshambulia JK na mahakama ya kadhi. Mada zaidi ya 5 zilihusu Mahakama ya kadhi tu na waandishi ni wanaChadema na Mapadre, wengine wakienda hadi misikitini kusikiliza hotuba na kuzileta humu, hivyo tukawapa mwanya waislaam pia kumshambulia Dr.Slaa ambaye alikuwa Padre na hivyo kuweka wasiwasi juu ya uongozi wake. Nilitoa tahadhali nyingi sana hapa JF juu ya hilo, lakini kama kawaida yenu huwa hamuamini anayoyasema Mkandara lazima mpinge kwa sababu hayapo karibu na ukweli mnaoupenda.. Ikala kwetu..

Mkuu wangu imetosha kwa leo tuache hizi siasa za udini.. zipite siku hatuandiki uchochezi wa aina yoyote baina ya Waislaam na Wakristu kwa sababu haitusaidii na nakuhakikishia Chadema watakuwa na wakati mgumu sana uchaguzi wa mwaka 2015 ikiwa tutaendelea kuchochea moto huu..
JK si mdini kwasababu anawakandamiza wakristo.

Ni kweli tuonane baadaye hata mimi natoka kidogo.Nina uhakika kabisa matatizo yetu kama watanzania tutayamaliza kama watanzania na si vinginevyo,hilo nina uhakika nalo kabisa.

Kwa kumalizia,patriotism has something to do with the love for your country,where as nationalism is about the nation.

Nitakaporudi hapa,nitakukumbusha kuhusu swali langu la msingi kwako kuwa ni mfumo upi tofauti na mfumo kristu ambao unapendelea tuwe nao.

Stay blessed.
 
Kwa hili wala sintosubiri urudi.. Mfumo pekee unaotufaa ni ule unaolenga kuondoa UJINGA kaa msingi wa maendeleo yetu na no one is left behind. Shule na Hospital zote za serikali zitaendeshwa na serikali na zile za makanisa, misikiti na watu binafsi zitajiendesha kama Private schools wakitoza wanafunzi ada za masomo, malazi na kadhalika. Let all Private schools be private..

Serikali yetu itashirikiana na shule binafsi kwa kulipa ada za watoto watakaochaguliwa kujiunga na shule hizo ama wagonjwa kutibiwa Hospitali hizo na zitapewa grades kutokana na facilities walizonazo. Shule za daraja la kwanza zitatakiwa kuwa na uwezo fulani, zenye maabala, walimu na hata viwanja vya michezo ktk kushiriki mashindano ya kitaifa. Si watoto wote wana vipaji vya kusoma wapo wengine wazuri ktk michezo na sanaa. Serikali itawawezesha watoto kusoma na sio shule kujiendesha.

Hospital vile vile kufikia daraja la kuitwa Hospital itatakiwa kuwa na vifaa kadhaa,ukubwa kadhaa ama madaktari bingwa kadhaa na wenye sifa kadhaa..Hivyo badala ya serikali kuwapa fedha CSSC kwa sababu ni wadau, fedha hizo ziende moja kwa moja kuwasomesha watoto walioshinda mitihani iwe hata shule za kanisa maadam mtoto amechagua shule hiyo na upande wa matibabu hivyo hivyo.

Inasikitisha sana kuona wapo watoto wameshinda mtihani kwa div 1 wanapelekwa form six au University lakini watakuja shindwa kulipia ada, malazi na kadhalika na kuondolewa masomoni wakati walofanya vibaya watachukua nafasi zao kwa sababu wazazi wao wana uwezo. Mfumo huu ndio maana tunajenga Taifa la wajinga. Uzalendo pasipo Natinalism huwezi kuusimamisha ni sawa na mtoto asiyemjua mzazi wake kalelewa uwanja wa fisi unategemea atakuwa sawa na yule mwenye wazazi. Malezi mema hutangulia tabia ya mtoto, waswahili wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo..
 
Joka kuu linaloulea udini Tanzania ni Jakaya Mrisho Kikwete .
 
Mpaka sasa udini ndo uliopo akili mwa watu wanaingiza udini hata shm ambayo siyo, ila serikali inawaogopa waislamu? Kama siyo kwanini hawa watu wanaohubiri kugomea sensa wasifikishwe ktk vyombo vya sheria maana viongozi wetu wamekuwa wakidai ukigomea sensa uvunja sheria ya nchi?
 
Mada hii inamhusu JK kwa sababu ni Muslaam hivyo amnapigwa vita kwa sababu hiyo tusianze kuingiza watu wengine ambao hawapo ktk mjadala. JK anatuhumiwa Udini kwa sababu yeye ni Muislaam na kashindwa kumchukulia Sheikh Ponda hatua lakini kama angekuwa Mkrisru pengine kuna uwezekano angefanya ipasavyo...

Haya ndio mawazo wa watu wanajiita GT wa JF ambao kwao Dr.Slaa ni mbora zaidi kwa sababu ni mkirstu na hakika pengine kwe;li angemchukulia hatua Sheikh Ponda japokuwa sheikh huyo anawakiliosha mawazo ya watu wengi sana wengine sio waislaam lakini hawakuona sababu kabisa ya kipengele cha dini uondolewa tena na rais Muislaam.. Huyu JK mdini kweli amefikia hata kuwakatalia waislaam wenzake! Dah ama kweli Miafrika ndivyo tulivyo..

Jenga chama mkuu kama wewe ni mkweli.

Kwa kuangalia mchango wa Mkandara hapo juu na kwa kuzingatia comment yako kutokana na huo mchango wa Mkandara ndipo ninapolazimika kusema wazi kwamba HAPO NDIPO ndipo hasaa UNAPOKOSEA!! Yaani kwavile Mkandara ni CHADEMA basi unataka asa-support madai yako kwamba JK ni MDINI.....this's rubbish bana. Ni mbaya sana kuchanganya siasa na dini. Hapa unachoonesha ni kwamba wapenzi wote wa CHADEMA basi waunge mkono hoja yako ya UDINI kwa manufaa ya CHADEMA na sio kwa maslahi ya nchi!! Kwa bahati mbaya sana, pamoja na kukuomba utaje jambo moja la msingi la kudhihirisha UDINI wa JK lakini bado hujafanya hivyo!! Narudia, JK ni mwislam; hivyo utaje jambo linaloonesha kwamba JK anawapendelea Waislamu au anawakandamiza Wakristo......huo ndio udini ninaokuomba uutaje. Na kama hakuna suala la kuupendelea Uislamu au kuukandamiza Ukristo basi toa hapa japo kipande cha hotuba yake moja kinachoonesha udini wa JK....!! Ukikosa kutaja lolote katika hayo, basi ukubali kwamba hapa mdini sio JK bali ni wewe!! Mdini ni wewe unayemtaka JK Rais wa nchi amkamate Ponda....mdini ni wewe unayemtaka JK Rais wa nchi afungie magazeti ya Kiislamu! Madai kwamba JK ni mdini kwa kuwa hakemei mambo yanayoashiria udini ni madai mfu yasiyo na mashiko yoyote.

NARUDIA ombi langu lile lile....toa hoja ya kuonesha UDINI wa JK ili nisikuone kwamba kinachokusumbua ni chuki yako dhidi ya kuona Mwislam anakuwa na madaraka ndani ya nchi hii! Kuna mwenzako mmoja humu, kwa chuki zile zile zenye kuonesha udini uliopitiliza nafsini mwake aliwahi kuleta upuuzi hapa ambao aliuita eti KIKWETE PROJECT inayolenga kuhakikisha nchi inatawaliwa na Waislamu!
 
Udini huu ndio matokeo ya kazi kubwa ya YUSUFU MAKAMBA, ABDULRAHMAN KINANA na JAKAYA KIKWETE 2010.
 
Matatizo ya waislamu au wakristu yatamalizwa wakiwa kama watanzania je mnalijua hilo?
 
serikali sio raisi peke yake,serikali ni neno pana so kwa mana hiyo udini hauletwi na raisi kwa sababu serikali sio raisi peke yake.Serikalini kuna wakristo,waislamu,wapagani na wengine wengi.WATU WENGI WAMEPOKEA DEMOKRASIA YA KUONGEA LAKINI WAMESAHAU DEMOKRASIA YA KUSIKILIZA KILE MTU MWINGINE ANACHOONGEA
 
Mleta mada wewe ndio mdini namba moja naona unataka tuamini kuwa tanzania imegubikwa na udini ili tuwachukie majirani zetu na tusiaminiane tena.
 
Matatizo ya waislamu au wakristu yatamalizwa wakiwa kama watanzania je mnalijua hilo?

Mkuu wangu umesema vema.
Wengi wa wanaochangia hoja hii hawalijui hilo la utanzania kwa faida ya watanzania wa leo na vizazi vijavyo.

Asilimia kubwa ya wachangiaji

- wanaongozwa na jazba

-Wanaongozwa na hulka za upenzi wa vyama vya siasa

-Wanaongozwa na upenzi wa imani za kidini

-Wanaongozwa na upinzani wa kishabiki ndani ya jf kihistoria.

........nk

Kwa mantiki hiyo wameweka pembeni kabisa dhana ya hoja ambayo inahusu mjadala iwapo kikwete ni mdini au sio mdini. Wachangiaji badala ya kujadili falsafa ya mtoa hoja ambayo imejikita kumhusisha au kutomhusisha kikwete na kashifa za udini wanaleta mijadala ya mbona nyerere alikuwa ....., mbona mkapa alikuwa .....

Kama suala ni udini wa nyerere au mkapa nivema hoja nyingine ikaibuliwa kumjadili huyo nyerere au mkapa kuchanganya na hoja ya kumjadili kikwete ni kukwepa hoja. Yeye ndiye mtawala, mwenye mamlaka, mwenye maamuzi ya mwisho je anatumiaje madaraka yake kujitenga na huo udini? je nyerere hayupo madarakani kumlinganisha na mtawala mwenye mamlaka kunauwiano gani?

Tunahitaji kujadili kwa uwazi bila upendeleo na tuweke ushabiki pembeni, bahati mbaya kwa wachangiaji walio wengi mambo ni tofauti, kwao utazania ni subsidiarity na udini unapewa sifa, kweli tumepotea njia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom