pengine Mtei aliuona udini wa Jk kabla yangu.Hakuna aliyejuwa JK ni mdini mwanzoni,rangi zake zimejionyesha na taifa linakwenda kombo.Kama miye ndo mdini nimesababisha hayo,then una hoja.Otherwise rudi kwenye hoja mkuu,mimi si rais wa nchi ati.Tafadhali jadili hoja si mimi.Unataka kufanya character assasination kwasababu umeudhika sana,hilo huwezi coz im nobody,hoja zinajisimamia zenyewe,pitia hii mada toka mwanzo,kuna waru wametoa maoni safi sana.
Una kazi kubwa ya kufanya kumtetea fisadi mdini,kwasababu matokeo yake ni wewe kuonekajna na nia moja,yani kutumia udini kulinda ama kuwakingia kifua mafisadi.Thats the truth.
Hakuna ambacho sijakujibu, labda kama hutaki kuelewa.....au unataka nikujibu kila kipengele peke yake?! Tuanze basi na wewe utoe hoja za ku-support madai yako!
1. Umesema: "Kinachonifanya niamini ni JK,ni kwasababu hao wanaopinga kasi ya upinzani,wanapoijibia serikali ya ccm,basi wanaoonyesha chuki za wazi kabisa za kidini.Ule udugu tuliokuwa nao wakitanzania haupo tena,na sijui utarudi kwa njia gani."
Sasa hapa unataka nijibu nini wakati hamna hoja ya kuijibu?! Labda nikuulize wewe: ni akina nani hao wanaoijibia serikali na waliijibia nini kinachoonesha chuki za wazi za udini?! NAOMBA UNIJIBU hapa otherwise hakuna hoja ya maana hapo uliyoieleza!
2. Aidha ukasema:"Kuna habari kuwa hata mtu na mke wake wanataka kutoana roho kwasbabu hizo hizo.Sheick Ponda alipotoa kauli kinyume na yakwake kuhusu sensa,kaliachia na gazeti lenye kusambaza sumu hizo huku akilifungia lenye kusema ukweli(mwanahalisi)"
Hapo pia nikakupa changamoto kwamba wenzako wanasema aliyelifungia Mwanahalisi ni Membe kwa ajili ya kumlinda mtuhumiwa namba moja kwenye makala ya Mwanahalisi ambae wanasema ni swahiba wa Membe hivyo nimeshangaa kusikia kumbe aliyelifungia Mwanahalisi kwa mujibu wako ni JK. But all in all, nikakuuliza, kwani kazi ya kufungia magazeti ni ya Rais hadi ulalamike ni kwanini hayafungii hayo magazeti yanayosambaza sumu...!!!! Nikakupa hadi mfano wa Mwakyembe na Kagasheki ambao wamechukua hatua bila kuingiliwa na Rais...sasa kwanini usimlaumu Waziri wa Habari kwa kutoyachukulia hatua hayo magazeti yanayomwaga sumu?! Nimekukumbusha kwamba Mwakyembe alitamka wazi, tena hadharani kwamba si kweli kwamba Mawaziri hawana mamlaka ya kuchukua hatua.....labda hapo ubadilishe mada kwamba Waziri wa habari alitaka kuyafungia magazeti yanayomwaga sumu lakini JK akakataza kwa sababu ni magazeti ya Kiislamu!! Kama huna hoja ya ku-support hayo basi nitaona hiyo nayo ni hoja isiyo na chembe ya mashiko!!!!
3. Vile vile ukachomekea hili: "Kama JK ni mdini,tufanyeje?Ni wazi anapenda haya yaendelee kuwepo kwasababu ni kama anauwa ndege wawili kwa jiwe moja,yani kwasababu yeye ni fisadi na mdini,basi issue za ufisadi wake anazifukia kwa kupenyeza sentiments za kidini kwasababu anajuwa the issue is extremely sensitive."
Hapa pia nimekuuliza.....hivi kashfa za ufisadi za nchi hii ni dhidi ya Waislamu pekee?! Ni kashfa ipi ya ufisadi ambayo hatimae JK akapenyeza UDINI ili kuficha tuhuma hizo dhidi yake na labda hao mafisadi wenzake?! Nitajie moja tu;hoja ya ufisadi ikafinyangwafinyangwa baada ya JK kuchomkea udini! Kama huna ya kuitaja basi nayo ni hoja nyingine nyepesi isiyo na mashiko yoyote kwa kuwa haiakisi unachokiubiri!!!
4. Hatimae ukamalizia: "Je kama taifa tutapona dhidi ya udini huu wa JK?je kukitokea mapigano,nani atakuwa responsible?Je nini kifanyike kukomesha udin8I hu?ama tumeridhika?!...."
Hebu hapa nipe jambo moja la msingi la udini wa JK!!! Wala usiniambie habari za akina Ponda na magazeti ya SAUTI simply because vipo vyombo husika vinavyotakiwa kuchukuwa hatua! Ipo Wizara Ya Mambo ya Ndani, Ipo Wizara ya Habari na mamlaka nyngine zenye meno ya kutosha kuchukua maamuzi dhidi ya hao akina Ponda! Kama hapo napo huna cha kuthibitisha, basi nitalazimika ku-conclude kwa mara nyingine kwamba wewe ndie mdini kwa kuwa umeshindwa kuthibitisha tuhuma za udini unazodai kuwapo!
Pamoja na yote, kwenye post zangu nimeshazungumza kwamba wakati wa kampeni JK alikuwa anakemea sana suala la udini, lakini watu wa ajabu ajabu wakadai nchi hii haina udini hivyo mdini ni huyo JK anayekemea kitu kisichokuwepo na hivyo anaweza kusababisha kupandikiza mbegu za udini!!!