Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Kwa mambo haya - JK ni Mdini!

Status
Not open for further replies.
Umeyaona ya shekh PONDA tu, ya maasikofu hujayaona kweli wewe huiwezi siasa!!Waislam wanahaki ya kudai kipengele cha dini ktk sensa.kwanini wadai tembelea web hizi upate reference
1) www.wikipedia.com/tanzania
2) www.arc.com/tanzania

web zote hzo zinatoa idadi ya watanzania kwa mujibu wa dini yao wakati tangu 1967 watanzania hatuja hesabiwa kwa mjibu,wa dini zetu.swali hawa WA RC Takwim hz wanazitoa wapi????
Wana UAMSHO rudini darasani,vinginevyo mtatumiwa saana na CCMizi,hamjajua tu kama mshatumiwa na sasa hamtakiwi kwa kuwa kwa sasa hamna kazi ya kuwafanyia?,we vuta subira mtatakiwa tena senso ikiisha baada ya kuwa mmeorodheshwa kwa lazima mbali na TANGAZO lenu kuwa msilm yeyote atakae he,,sa,,bi,,w.a ni ''KHAFIRI'' Ww vp? siku zinakwisha ushachukua ukhafiri wako?,
USHAURI:Achaneni na chama cha mabwepande,PANDE ndo ficho lao kunasiku watawaficha huko viongozi wenu bila huruma,hawana urafiki hao zaidi ya kuwatumia na kuwabwaga sasa mmebwagwa cha ajabu mtarudiana tena.JIUNGENI m4c buuuure(ila mvue uamsho huku ni m4c tu).
 
Jk ajaleta udini kama unavyotaka kulazimisha, wewe unasukumwa na chuki za udini bahati nzuri humu JF tunajuana kwa michango yetu wewe ni mdini mkubwa tena una chuki kubwa na Waislam na Uislam kwa ujumla, bora angekuja mtu mwingine kuanzisha hii thread labda tungemulewa lakini sio wewe Mushi, ndio maana unakwepa kumelezea Mtei kuhusu udini wake sababu ni kambi yako, unachofanya kwenye hii thread yako ni kiziba shimo la panya na mkate.


Mkuu Ritz hebu tuchambue hoja na si kumshambulia mtoa mada. Kama anachosema sio kweli si kanusha kwa hoja utaeleweka vizuri tu.

Nikirudi kwenye hoja kwa hiyo wewe unakataa hakuna udini?

Naomba kauli yako, maana mleta hoja anajaribu kwa kila namna kuutafuta na kuupigania utanzani mingon mwetu bahati mbaya haeleweki.
 
@jmushi1, sasa hapa ndipo unapokosea kuweka mada hii lakini hutaki kusahihishwa kwa sababu ya nimani yako wewe. Nakwambia tu mdini ni wewe na hilo la gazeti la sauti ni tuhuma ambazo nakitaka chama changu kikanushe kama ni uongo maana Chadema sio Dr. Slaa hata siku moja ameingia chama kakikuta kama sisi tulivyokikuta.

Yeye ni binadamu na anaweza kushawishika kwa lolote, hivyo siwezi kuweka dhamana yangu kwa mtu yeyote hata iwe mwanangu wa kumzaa anaweza kushawishika..Sipo Chadema kwa sababu ya Dr. Slaa, Mbowe wala Mnyika isipokuwa naamini ktk kupingana na sera za CCM na tuko mstari mmoja..Kama Chadema watazienzi baadhi ya sera za CCM zinazoendeleza ya mkoloni kwa madai ya Udini wakati elimu na Afya vinadorora nchini sintokubali kuendeshwa.Natanguliza fikra na mawazo yangu yanawakilishwa na chama gani ktk harakati hizi sio kuamini na kushabikia Uchadema..

Kama hilo kwenye RED lingefahamika na kuwa ndio base ya wana-CHADEMA walio wengi basi huo ukombozi unaohubiriwa ungefika pasipo na shaka yoyote na kwamba pasingekuwa na namna yoyote ambayo ya kuifanya CCM iendelee kuwapo madarakani after 2015! Lakini kwa bahati mbaya, kuna wana-CHADEMA wengi tu, tena wenye ushawishi na ambao wapo pale kwa ajili ya watu fulani!!
 
udini umelelewa sana na serikali hii maana kila mtu siku hizi kila mtu anaongelea dini yake. so serikali hii dhaifu ndo agenda yake.
 
Kiukweli thread kama hii ni hatari kwa taifa, hamna kitu hapa, ni fitna majungu, uchonganishi, ubaguzi na malengo ya kuwagawa watu. Kwa watu wanaochunga muda wao vizuri lazima atapita njia tu, hasa ukizingatia mtoa uzi amekosa hoja za kutuandikia. Mzee ondosha haraka hii.
 
Mwe! Ili CCM ishinde lazima watumie karata ya dini unakumbuka Igunga yule mama? Karata hii nirahis kuitumia kwa sasa kwasababu nirahis kuwadanganya waislam wengi kwa hesabu rahis. Upo tayar kutawaliwa na kafir aendeleze mfumo kristo au muislam mwenzio wengi wao watajib astakhafir bora muislam. Kwa stail hii utakua umepata mtaji mzur wakuanzia kupunguza kura za mgombea mwenye sifa kwasababu anajina linalosadikika kuwa si la kiislam. Kwasasa hii ndio karata rahis wanayotumia ccm bila kujal madhara yake kwa kizazi hiki na kijacho. Kuiondoa ccm madarakan inahitaj waislam walioelimika na wenye uzalendo na nchi kusimama kidete kupinga hoja hizo kuanzia masjid mpaka kwenye mikutano ya hadhara.
 
Mimi nasema, hakuna namna ya kufukia huu udini, tusubiri mapigano tu.
 
Udini uko nchini mwetu kuliko wakati wowote ule toka tupate uhuru.Kwani JK ana agenda ya kusilimisha taifa?Unadhani hata wasio na dini watakubali?hujui kuna wazalendo wa kweli watakaoyachanja makalio ya wadini?kama huamini,subiri tufike huko.Tuna muda na nafasi za kutizama kwa macho ya kizalendo,na kulipigania taifa hili na watu wake.Ninarudia tena,mafisadi wanajificha kwenye mwavuli wa udini,hilo hawataweza.Over our dead bodies,and I'm talking about nationalist and true patriots.
jmushi1,
Bado kabisa hujanishawishi kukuondoa kwenye tuhuma chafu za udini.....hapa unachofanya hivi sasa ni kujaribu kupigana kiume ili ufifishe hoja yako ya msingi toka kwenye main thread......kwa kutoa tafakuri ya kina kupitia Main Thread uliyoitoa; unakosa kabisa uhalali wa kujinasibisha na uzalendo; at least kwa sasa!! hebu angalia unapochanganya changanya mambo ili kuipotezea thread yako iliyokuvua nguo ya ndani! Hapa umeleta tena hoja ya mafisadi kujificha kwenye mwamvui wa dini.....unaona unavyojifanya mjanja wewe; unataka mtu aseme "Kwani Lowassa anayepita pita kanisani ni Mwislamu..." ili upate cha kusema kwamba wewe hapa unapinga aina yoyote ya udini...., thubutu, hupati mtu hapa; wewe hoja yako ni Udini wa JK; kwamba JK Mwislamu hivyo anauelea lea Uslamu simply because amemuacha Sheikh Ponda na vyombo vya habari vya kiislamu hataki kuvifungia!!!
 
Maneno ya kikwete kwenye uzinduzi wa bunge 2010: Hauhitaji hata kusoma sana katikati ya mistari kuelewa hoja ya jmushi1.

Hatari ya Uchaguzi 2010 kwa Umoja

Naomba nirudie kuelezea kusononeshwa na kusikitishwa kwangu na baadhi ya
viongozi wa dini na wanasiasa waliowataka Watanzania wawachague watu kwa dini zao. Jambo hili linapaswa kukemewa kwa nguvu zote na kila mmoja wetu. Nawaomba viongozi wa kisiasa ambao vitendo hivi vya kibaguzi vilifanywa na vinafanywa kwa niaba yao au kwa kuwanufaisha wao wasikae kimya. Watoe kauli kukemea uovu huu. Hapa nchini Watanzania wenye dini mbalimbali wanafanya kazi pamoja, wanasaidiana, wanashirikiana katika shughuli mbalimbali za kijamii bila kujali dini zao, wanaishi pamoja.

Tusikubali zipandikizwe mbegu za chuki baina ya Watanzania.

Nawapongeza na kuwashukuru Watanzania kwa kukataa kugawanywa kwa misingi ya dini katika uchaguzi huu. Narudia wito wangu kwamba sasa viongozi wote wa siasa, wa dini, wanahabari, viongozi wa kimila, kijamii na wengineo wanaoipenda nchi yetu, tuungane kuziba nyufa na kutibu majeraha yaliyoletwa na uchaguzi huu.
Kwenye uchaguzi wa ubunge kule Igunga, Mashehe waliwaita waandishi wa habari na kutangaza kuwa waislam wasiichague CHADEMA. Huu ni mfano hai wa UDINI.

NasDas, Ritz, Njiwa, Zomba... ni kiongozi gani wa serikali alikemea kile kitendo?
Kikwete kama kiongozi mkuu wa nchi hii. Kiongozi anayetakiwa kuonyesha njia kwa vitendo, ameshafanya nini zaidi baada ya kutoa ile kauli 2010 kukemea udini?

Sina hamu ya kudiscuss sana nilikuwa nataka majibu tu hapo...
 
Mjadala siyo jmushi1 hapa,kafungue thread hapa si pahala pake.Mkishindwa hoja ndo mnaleta personal attacks.Mjadala hapa ni mkuu wa nchi na udini wake.Unachotakiwa useme ni kwamba JK si mdini base on so and so...

sasa mkuu! tukijadili udini wa jk wakati mleta mada yeye mwenyewe ni mdini! ... obvious wakati unaandaa kurusha thread yako ushaweka conclusion kichwani mwako! ... wewe ni mdini umejaribu sana kujificha lakini ndio hivo hisia zako zakuzidi muda mwengine! ... allegations hizi angetoa mtu aliye neutral kungekuwa na cha kujadili
 
Umeyaona ya shekh PONDA tu, ya maasikofu hujayaona kweli wewe huiwezi siasa!!Waislam wanahaki ya kudai kipengele cha dini ktk sensa.kwanini wadai tembelea web hizi upate reference
1) www.wikipedia.com/tanzania
2) www.arc.com/tanzania

web zote hzo zinatoa idadi ya watanzania kwa mujibu wa dini yao wakati tangu 1967 watanzania hatuja hesabiwa kwa mjibu,wa dini zetu.swali hawa WA RC Takwim hz wanazitoa wapi????
Wanajihesabu WENYEWE makanisani.Basi na nyie muwaige kwa kujihesabu huko misikitini mtajua IDADI yenu ni ngapi?
 


Maneno ya kikwete kwenye uzinduzi wa bunge 2010: Hauhitaji hata kusoma sana katikati ya mistari kuelewa hoja ya jmushi1.


Kwenye uchaguzi wa ubunge kule Igunga, Mashehe waliwaita waandishi wa habari na kutangaza kuwa waislam wasiichague CHADEMA. Huu ni mfano hai wa UDINI.

NasDas, Ritz, Njiwa, Zomba... ni kiongozi gani wa serikali alikemea kile kitendo?
Kikwete kama kiongozi mkuu wa nchi hii. Kiongozi anayetakiwa kuonyesha njia kwa vitendo, ameshafanya nini zaidi baada ya kutoa ile kauli 2010 kukemea udini?

Sina hamu ya kudiscuss sana nilikuwa nataka majibu tu hapo...


kikwete kama Rais wa nchi ana viongozi wa ngazi za chini ambao wanauwezo wa ku handle issue kama hizo .. sio kila jambo aongee kikwete! sasa kazi ya wakuu wa mikoa .. mawaziri.. etcl itakuwa ni nini..?!

 
Kama muungwana udini upo kwa kiwango kikubwa sana kwa sasa hivi. Huwa sipendi kujiingiza kwenye thread like this. Lkn leo imenibidi. Mwasisi yupo na mwenye kulimaliza pia yupo. Tuache ushabiki ktk hili na litasumbua sana lisipochukuliwa hatua thabiti mapema. Nchi yetu itakuwashaked ndani(udini) na nje(Malawi)
 
Nchi ilipofikia,credits huwa anapewa rais na serikali yake,kwahili la udini,hakuna ubishi umeshaota mizizi.Na sijawahi kusikia kauli ama vitendo kutoka kwa JK vya kukemea haya mambo ya udini.

Kinachonifanya niamini ni JK,ni kwasababu hao wanaopinga kasi ya upinzani,wanapoijibia serikali ya ccm,basi wanaoonyesha chuki za wazi kabisa za kidini.Ule udugu tuliokuwa nao wakitanzania haupo tena,na sijui utarudi kwa njia gani.

Kuna habari kuwa hata mtu na mke wake wanataka kutoana roho kwasbabu hizo hizo.Sheick Ponda alipotoa kauli kinyume na yakwake kuhusu sensa,kaliachia na gazeti lenye kusambaza sumu hizo huku akilifungia lenye kusema ukweli(mwanahalisi)

Ninamini kabisa kuwa tulipofikia,uwezekano wa kuingia kwenye vurugu na mapigano ya kidini ni mkubwa kuliko wakati wowote ule kwenye historia ya Tz toka tupate uhuru.

Kama JK ni mdini,tufanyeje?Ni wazi anapenda haya yaendelee kuwepo kwasababu ni kama anauwa ndege wawili kwa jiwe moja,yani kwasababu yeye ni fisadi na mdini,basi issue za ufisadi wake anazifukia kwa kupenyeza sentiments za kidini kwasababu anajuwa the issue is extremely sensitive.

Je kama taifa tutapona dhidi ya udini huu wa JK?je kukitokea mapigano,nani atakuwa responsible?Je nini kifanyike kukomesha udin8I hu?ama tumeridhika?!....

Kaka yangu kwanza hongera kwa kuliona hilo na kulitilia hofu. Pili ni kwamba kaka umesahau kusema nini kifanyike. Labda mie niseme kwa ninavyoona.
1.kwanza kabisa serikali iache mara moja upendeleo kwa mujibu wa imani,iache kwa kuvunja mkataba wa kifisadi baina ya makanisa na serikali. Kaka mtoa mada kama kweli umeandika post hii ukiwa huru kifikra basi hili utaliona kama ni tatizo.
2.kanisa liache mara moja kuingilia siasa za nchi.
3.serikali ipige marufuku mara moja watu wa imani nyingine kuingilia maombi ya watu wa imani tofauti pindi waiombapo serikali yao jambo ambalo wao kwa mujibu wa imani yao litawasaidia,hapa mifamo iko wazi (a)mahakama ya kadhi wakristo inawahusu nini? (b)oic,ivi nchi kujiunga na oic kanisa litaathirika nini? Etc
4.serikali ishughulikie zile sehemu zenye kuleta migongano ya moja kwa moja mfano(a)baraza la mitihani NECTA hapo serikali inatakiwa ilivunje na liundwe upya kwa kuzingatia malalamiko yaliyopo. (b) mgawanyo wa madaraka serikalini unaupendeleo wa waziwazi hilo liondoshwe.
5.katika ngazi za kisiasa iwe marufuku kwa mtu yeyote ambaye ni kiongozi wa kiroho au aliyewahi kuwa basi asiruhusiwe kugombea nafasi yoyote ili kuzuwia mifano ya akina mchungaji msigwa bungeni aliposimama kuwatetea wakristo nawakati yeye si mbunge wa wakristo peke yao.
Naomba kwanza niishie hapo. Kama nawewe siyo muathirika wa huo udini naamini utaunga mkono ushauri wangu kwa serikali na watanzania kwa ujumla.
 
Kinachonishangaza

serikali imekataa kuweka kipengele cha dini na kabila kwenye sensa, lakini ukienda offisi za serikali kwa huduma mfano police wanakuuliza dini yako na kabila.
je hii ni sawa??? binafsi inanikera sana
 
Maneno ya kikwete kwenye uzinduzi wa bunge 2010: Hauhitaji hata kusoma sana katikati ya mistari kuelewa hoja ya jmushi1.


Kwenye uchaguzi wa ubunge kule Igunga, Mashehe waliwaita waandishi wa habari na kutangaza kuwa waislam wasiichague CHADEMA. Huu ni mfano hai wa UDINI.

NasDas, Ritz, Njiwa, Zomba... ni kiongozi gani wa serikali alikemea kile kitendo?
Kikwete kama kiongozi mkuu wa nchi hii. Kiongozi anayetakiwa kuonyesha njia kwa vitendo, ameshafanya nini zaidi baada ya kutoa ile kauli 2010 kukemea udini?

Sina hamu ya kudiscuss sana nilikuwa nataka majibu tu hapo...

Binafsi najisikia kinyaa sana jinsi jinsi mnavyoendekeza udini.....nakumbuka kwenye uchaguzi mkuu 2010, JK kwenye mikutano ya kampeni karibu yote, alikuwa anakemea suala la udini....wakatokea wapumbavu wakasema ni hatari sana kwa kiongozi wa nchi kuzungumzia zungumzia udini wakati nchi haina udini....wakafikia hata kusema eti hali hii inaweza kuwafanya hata wale ambao hawakuwa na hisia za udini, wakaanza kuamka....leo, wale wale wanasema JK hakemei UDINI.....watu wa ajabu sana nyinyi!
 
Wanajihesabu makanisani.Basi na nyie muwaige kwa kujihesabu huko misikitini mtajua hesabu yenu ni ngapi?
Hayo ni majibu ya kitoto mkuu. Kama wanajihesabu kanisani inamaana na hizo takwimu za waislam walizipata hukohuko kanisani? Hayo ndiyo majibu huketa
 





kikwete kama Rais wa nchi ana viongozi wa ngazi za chini ambao wanauwezo wa ku handle issue kama hizo .. sio kila jambo aongee kikwete! sasa kazi ya wakuu wa mikoa .. mawaziri.. etcl itakuwa ni nini..?!

Ndiyo maana nikauliza, kiongozi gani wa serikali alikemea kile kitendo.
Kwenye issue ya madaktari/walimu baada ya mawaziri kushindwa , kikwete alifanya nini?
Je kiongozi gani wa serikali anakemea udini? Na kama viongozi wameshindwa , Kikwete anafayafanyia nini maneno yake aliyosema wakati wa kuzindua bunge?
Tafadhali rejea post yangu unipatie majibu...
 
JF sio mali yako hii thread ungeifungulia chumbani kwako kama unachaguwa watu wa kuchangia, JF ni jukwaa huru.

Sijadiliani na wadini,we huna mpango wala huna haja ya kujibu posti yangu,changanya masaburi najuwa unamtetea baba yako.Kuna thread nyingi tu,peleka masaburi kwenye ile ya Zomba.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom