Binafsi namawazo tofauti sana na baadhi ya watu humu JF na hata mitaani!
Sikatai mh.Lowassa kachafuka na labda ni kweli hasafishiki na kashfa aliyonayo ya RICHMOND.
Sikatai mh.Lowassa ni mlafi wa.madaraka.
Sikatai mh.Lowassa akiingia madarakana wengi watalia hasa wabaya wake.
Sikatai mh.Lowassa labda kweli kajilimbikizia mali zisizo halali.
Sikatai mh.lowassa kweli haaminiki na watanzania wengi kwakuwa ya maneno mengi mabaya yasemwayo
Lakiniiiiiii pia sikatai Lowasa.ndio kiongozi anayetakiwa kuitoa nchi hapa ilipo kwenda mbele......
Pia sikatai Lowassa ndiyo mtu mwenye msimamo na mtoa maamuzi yenye tija kwa nchi hata kama ni magumu vipi.
Ni kweli pia tukimpima Lowassa na wagombea wengine wa ndani ya chama chake na nje...anawazidi kwa uwezo!mwenye kubisha na abishe kuhusu hilo!!
Ni kweli pia usiopingika kuwa endepo UKAWA watasimamisha sura mpya kwenye uraisi asiwe mbowe,mbatia,wala slaaa,wala proff. Na wakaanza kumnadi mapema mgombea huyo machoni pa watanzania nitakuwa wakwanza kupanga mstari wa kupiga kura saa 12 asubuhi...
All in all Lowassa is the best option we have right now!!!!(katiba inaniruhusu kutoa mawazo binafsi)