kwa lipi la maana alilolifanya lowassa hadi apewe nchi?
Kuna sababu nyingi za kusema lowassa hafai kuwa rais wa nchi hii licha ya kuwa mgonjwa wa macho na mgongo pia ni mmoja wa watu 11 waliotajwa kuwa ni mafisadi.
Amefanya nini la maana hadi tumpe nchi? Unamkumbuka kwa lipi zaidi ya kujiuzulu?
Pesa zake sio tiketi kuwepo ulazima wa kuingia ikulu. Kama anatafuta umaarufu,umaarufu sio kwa mazuri tu hata ufisadi na kujiuzulu napo aljulikana ndani na nje ya nchi.
Anaitwa mtu wa maamuzi magumu,maamuzi yapi? Kujiuzulu ni uwajibikaji sio maamuzi magumu. Maamuzi magumu yapi? Alikuwa anafukuza watumishi wa serikali majukwaani bila hata kuwapa nafasi ya kijitetea(natural justice).
Kama sio kuwaonea ni nini? Yeye alikuwa analalamika ooh mh spika,nimeonewa sana,nimesikitika sana hata sijaulizwa juu ya richmond sijapewa hata nafasi ya kujitetea(natural justice),amesahau kuwa usihukumu usije ukahukumiwa(mathayo 7:1)
wanasema alijenga shule za kata,je,alitumia pesa yake badala ya kodi za watz? Walitaka afanye nn wakati ulikuwa wajibu wake kama mtendaji mkuu wa shughuli za serikali za kila kitu?
Sababu zipi za kunishawishi kumpigia kura lowassa awe rais wa awamu ya tano?