Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Kuhusu Mnaouita Ufisadi wa Mh. Lowassa
Fikiri pamoja nami juu ya tukio lifuatalo baada ya usomwaji bungeni wa taarifa ya iliyokuwa tume ya Mh. Mwakyembe: Mh. Mwakyembe, kufuatia baadhi ya wabunge kuendelea kulijadiri suala la RICHMOND hata baada ya wiki kadha toka bunge lilipolifunga suala hilo, alipata kutamka hivi, "....Mh. Spika, bunge lako likubali kuvunja kanuni zake ili suala la RICHMOMD lijadiriwe upya na sisi tuyaseme hata mengine tuliyoyaficha ili kulinda hadhi ya serikali...." Sasa ndugu yangu, nachopenda ujiulize hapo ni kuwa ni serikali ipi iliyotunziwa hadhi yake wakati Baraza la Mawaziri lilikuwa limevunjika na Waziri Mkuu wake kuaibishwa kiasi kile mbele ya jamii iliyokuwa ikimuheshimu sana?????!!!!!! Matukio ni mengi sana ambayo ukiyatafakari, na kuweka kapuni ushabiki wa kipuuzi wa vyama, basi utajua tu kuwa Mh. Lowassa alionewa tu. Na, kwa kweli walidhamiria kumnyang'anya nafasi yake. Kwa sababu ya muda na majukumu mengine ya kikazi, naomba tukio hilo moja liwe chachu ya wewe kutafakari matukio mengine kuhusu suala la RICHMOND- hakika utaujua ukweli. Mungu Yupo na Mh. Lowassa, na huyu ndiye Rais ajaye: na, kwa kweli kwa namna nchi ilivyo sasa, huyu ndiye afaaye kuwa Rais wetu.

Gedeon acha uongo EL alikuwa analalamikalalamika kwamba kaonewa ndo Mwakyembe akasema kama analalamika kwamba kaonewa yeye Mwakyembe alete ushahidi wa kuonyesha kwamba EL alihusika na swala zima la Richmond na kama hautakuwa kweli Mwakyembe atajouzulu.
Tangia siku hiyo Lowassa hajawahi kulalamika kwamba kaonewa. Alitiwa adabu akakaa kimya.
 
Mwache tu achukue tu hapa watu tunaishi ishi tu ili mradi kunakucha hakuna mabomu kama ya gongolamboto ukula mchicha mwingine ale kuku poa tu wewe tu na ubunifu wako Wa kuiba Kila MTU nchi hiii mwiziii sema lowasa kawazidi ubunifu Wa kuiba mkipewa nyie waiziii wadogo wadogo mtaiba sana mtatuuza had I watu
 
Kumjua mwenye richmond sio inshu, hoja mezani yeye kama pm alishndwa vp kukataa au kuzuia kusaini mikataba wa kifisadi wa richmond? Kama alishnkizwa na Profesa inamana kwake rais ni muhimu kuliko watz milioni 40? Jibuni hiyo hoja misukule wote wa bwana mamvi.

Acheni utani Mamvi kwenye Richmond anahusika moja kwa moja sema tu labda kuna wenziwe waloohusika nao hawakuadhibiwa wakati ule.
Hana sifa hata moja ya kuwa Rais wa Taifa hili.
 
Mnazan nan atapewa urais akomeshe jeuri,magonjwa na kifo? JIBU TAFADHALI
 
binafsi EL anafaa kujiuzulu in hekima kubwa kama aliiba kwanini hawakumshitaki mpaka leo

Hapo ndipo 2anze kujiuliza na kuwauliza hao wanaomhusisha katika kashfa hyo.....kwann kashfa ile haikusimamiwa kidete kama zilivyo nyingine na wanaodaiwa kuwa ni wahusika kuchukuliwa hatua??
 
pia ukitaka kujua walimfanyia fitina angalia Escrow inavyopigwa chenga utajua kuwa kila mwenye maono tofauti lazima ile kwake hata Richimond kulikuwa na uwezo wa kupindisha lakini kwa kuwa walimtaka EL walifanya hivyo kujifanya wanatupenda wananchi kumbe bure tu .ila Kwa kuwa hakuna anayebeba hata shilingi viongozi wangetambua tambura hilo Tanzania tungepona

Target ilikuwa ni kwa Edward Lowassa pekee.....maana cku zote mchapa kazi hodari katika ofisi yoyote ya serikali huwa hapendwi.
 
Huyu amekuwepo kwenye serikali ya ccm kwa miaka mingi sana na bado hajafanya lolote, hata kukishauri chama chake kiwaletee Watanzania maisha bora.

Huyu huyu alijiuzulu kutokana na kutokuwajibika katika kashfa ya Richmond.

Ni huyu huyu anatembea nchi nzima akimwaga fedha kuwania uraisi.

Bado watu kama nyie mnampigia debe ili awe raisi kupitia chama ambacho kimeleta majonzi makubwa kwa Watanzania walio wengi.

Nataka kuuliza je mna hisia za kujiangamiza?

Mbona wengine pia wanamwaga pesa na mnaenda kununulia unga wa ugali majumbani kwenu....na hamji hapa kuwasema?? Au kisa ndio wanaowapa namna ya kuishi??
 
Mbona wengine pia wanamwaga pesa na mnaenda kununulia unga wa ugali majumbani kwenu....na hamji hapa kuwasema?? Au kisa ndio wanaowapa namna ya kuishi??

Huyu yupo katika kundi lote la mafisadi ndani ya ccm, hivyo moja kwa moja anakosa sifa za kuwa raisi ajaye.
 
Mkuu Sibonike, kwa CCM hakuna aliye msafi (ili kumaanisha, aliyemsafi na awe wakwanza kumpiga jiwe LOWASA)....pengine basi sasa ni wakati wakujaribu vyama vingine!

Kupata msafi CCM ni sawa ni kutafuta sindano iliyodondokea kwenye simo la choo
 
Mkuu, binafsi siamini kuwa Lowasa anafaa kuwa raisi wa Tanzania ajae. Hii ni kutokana na historia yake kiutendaji akiwa mwanachama wa ccm.

Nieleze kwenye kashfa ya Richmond alizushiwa vipi, na kama alizushiwa kwa nini ilibidi ajiuzulu?

Sina imani na Lowasa, zaidi ya hapo sina imani na ccm kuleta mabadiliko hasa tukizingatia wamekuwa katika madaraka kwa miaka yote hii, mpaka leo hivi ambapo Watanzania wako hoi.

Ubovu wa wa maisha ya Watanzania vikiwepo umaskini, afya duni, elimu duni na ukosefu wa amani kwa ujumla, vimetokea wakati ccm inatawala.

Naomba unishawishi kuwa Lowasa, huyu huyu ambaye ni kada wa ccm mpaka leo, ataleata mabadiliko gani ndani ya chama hicho hicho ambacho kimeangamiza maisha ya Watanzania wengi.

Ni jambo gani muhimu, alilolifanya akiwa ndani ya ccm, linalotuonyesha kwamba alijaribu kubadilisha mwenendo wa chama chake kuelekea katika maisha bora kwa Watanzania?



Adili yake inaonekana wazi popote pale
Jasiri na aliyethubutu kufanya maamuzi ya kuchukua maji ziwaa Victoria kwenda shinyanga .
Kuuvunja mkataba wa wakoloni uliokuwa ukitunyima Fursa ya kutumia maji hayo ya ziwaa Victoria.

Tembelea kesho monduli jimbo pekee mmbunge Wake aliyefikia asilimia 150% ya kutekeleza manifesto yake Kwa barabara ,maji ,shule na huduma nyingine Za kijamii...

Mwakyembe mwalimu wa sheria na mtaalam wa Natural justice aliyeamua kuipindisha sheria na kuugeuza unafiki Kuwa ukweli kutengeneza hila juu ya Edward lowassa lakini mmpaka Léo wananchi wameziona hila zote Hizo na kumpendekeza Edward lowassa
Karibuni Safari ya matumaini
 
Katika hali isiyo yakawaida katika nchi yetu na ni jambo la kushagaza sana, ni huyu waziri mkuu aliyejihudhuru kwa wizi wa mali ya watanzani lowassa
,
nafikiri hakuna mtanzania yeyote asiyefahamu wizi ambao unafanywa na lowassa katika nchi yetu, hata mtoto wa shule ya msingi anajua kwamba kuna waziri mkuu katika historia ya tanzania aliwahi kujihudhuru kwa sababu ya wizi.

pamoja na kwamba lowassa ni mwizi lakn hadi hii leo, bado yuko kwenye chati ya siasa hapa nchini, yaani inafikia hadi na wakati watu kufanya utafiti wa chumbani na kumfananinisha na watu safi na wakombozi wa taifa(dr.slaa)

Je! unahisi ni nini kinachomfanya awe hivyo.

Mimi nahisi

(i)Ameajiri watu wasiopungua mia mbili katika maeno mbali mbali hadi kwenye social network na hela anazowalipa ni za wizi.

(ii)Nahisi ana makampuni anamiliki lakini kupitia migogo ya watu ili asijulikane

(iii) Kama siyo waganga wa kienyeji wanamdanganya basi ni Freemason
 
Katika hali isiyo yakawaida katika nchi yetu na ni jambo la kushagaza sana, ni huyu waziri mkuu aliyejihudhuru kwa wizi wa mali ya watanzani lowassa
,
nafikiri hakuna mtanzania yeyote asiyefahamu wizi ambao unafanywa na lowassa katika nchi yetu, hata mtoto wa shule ya msingi anajua kwamba kuna waziri mkuu katika historia ya tanzania aliwahi kujihudhuru kwa sababu ya wizi.

pamoja na kwamba lowassa ni mwizi lakn hadi hii leo, bado yuko kwenye chati ya siasa hapa nchini, yaani inafikia hadi na wakati watu kufanya utafiti wa chumbani na kumfananinisha na watu safi na wakombozi wa taifa(dr.slaa)

je? unahisi ni nini kinachomfanya awe hivyo.

mimi nahisi

(i)ameajili watu wasiopungua mia mbili katika maeno mbali mbali hadi kwenye social network na hela anazowalipa ni za wizi.

(ii)nahisi ana makapuni anamiliki lakn kupitia migogo ya watu ili asijulikane

(iii) kama siyo waganga wa kienyeji wanamdanganya basi ni freemason

Ni Mambo mawili makuu tu yanayomfanya Lowassa kuendelea kubaki katika chati za siasa ya Tanzania

  1. PESA/UTAJIRI WAKE
Suala la pesa/utajiri wake umeupataje, hii iwe topic ya siku nyingine. Lakini kwa sasa tukubaliane kuwa Lowassa ana utajiri usiopimika. Kwakuwa Watanzania wengi ni masikini aidha wa FEDHA au AKILI, basi Lowassa anatumia utajiri wake huo kuwanunua Watanzania hao ili aweze kutimiza ndoto safari yake.

Ametumia utajiri wake huo kuwanunua baadhi ay viongozi wa chama chake, wasomi, wamiliki ya vyombo vya habari, Spin doctors na Watanzania wa kawaida. Hao ndio wanaoendelea kumuweka juu katika siasa za Tanzania pamoja na kashifa za ufisadi zinazomuandama, lakini pia pamoja na kukataliwa na Muasisi wa chama chao CCM JK Nyerere kwamba hafai kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Lowassa kwa kufahamu hayo amefuata maneno ya busara ya wahenga wetu kwamba PENYE UDHIA PENYEZA RUPIA!

Kwa haraka utaona kwamba kama vile anafanikiwa, kwani katika Chama chake amewapiku wataka urais wengine wote (rejea utafiti wa TWAWEZA). Lakini Lowassa ana vikwazo VIWILI VIKUU kufikia hiyo safari ya ndoto yake. Kwanza ni KAMATI KUU ya CCM, tetesi zilivyo sasa ni kwamba CC itakata JINA lake na huo ndiyo utakuwa mwisho wa safari ya ndoto yake. Lakini PILI KIKWANZO cha pili kitakuwa wananchi kama kweli Kamati kuu itaogopa KUKATA JINA LAKE, Lowassa is UNLECTABLE, sidhani kama utajiri wake UTAHIMIRI kuwahonga wapiga kura wote wa JMT. Maana nguzo yake kubwa ni utajiri wake. Hata kama utajiri wake utahimiri kuna makundi ya jamii hayahongeki linapokuja suala la kuchagua viongozi kama vile Wapemba.

2. UPINZANI MADHUBUTI

Upinzani madhubuti pia umemusaidia Lowassa kuendelea kuwepo kati chati ya political landscape za Tanzania. Kama tunavyofahamu vigogo wa vigogo wa CCM hawataki kabisa Lowassa awe mgombea wa urais kwa CCM. Wote tunafahamu kampeini inayoneshwa wazi wazi na WAMA dhidi ya Lowassa, ambayo ni Taasisi ina MKONO WA IKULU. Kwasababu vigogo hao hawa uhakika nini atafanya Lowassa akiwa Rais, baada ya kutoswa na kutishwa ZIGO LA RICHMOND. Kama mnavyofahamu CCM ni chama cha MIZENGWE NA FITINA! Mambo yao hayafanyi kwa uwazi au kwa taratibu zinazofahimika. Mabo ya CCM yanaendeshwa kwa MIZENGWE NA FITINA. Rejea kisa cha Sitta alipoambiwa kwamba kama anataka kugombea tena uspika wa bunge la JMT, basi abadilishe jinsia na kuwa mwanamke, kwani zamu hii lazima speaker awe mwanamke.

Wakati CCM wanategemea kutumia MIZENGO NA FITINA kumuengua Lowassa au kumzuia kugombea nafasi Urais wa JMT kupitia CCM, CCM mara hii wanaokana kukwama kutumia mizengwe na fitina kuzima ndoto ya safari ya Lowassa, kwasababu ya upinzani madhubuti na imara.

CCM wanafahamu kwamba kama watatumia mizengwe na fitina kuzima ndoto ya safari ya Lowassa, Lowassa alishawaambia kabisa CCM, kuwa yuko tayari kukipasua chama vipande viwili. CCM wanafahamu kwamba Lowassa anao wanachama na wapenzi wengi sana nje na ndani ya CCM nchi nzima.

Kutokana na uimara ya ya vyama vya upinzani na hasa baada ya Muungano wa UKAWA. CCM wanafahamu fika kabisa kwamba kama Lowassa atatoka CCM na kuelekea huko atakapoamua, CCM asilani haitaweza kushinda UCHAGUZI MKUU. Wakati ambapo opposition parties zilikuwa weak CCM wasingejari kabisa. Kwani CCM wangefahamu fika kwamba hata akienda huko atakapokwenda CCM wana uhakika wa kushinda uchaguzi mkuu, japo wangeaathrika kidogo na percentage ya kura. Lakini nyakati hizi wanafahamu Lowassa akitoka nao CCM wamekwisha, political landscape ya Tanzania imebadilika. Ndiyo maana CCM waliweza kufanya hivyo kwa akina Mrema, Marehemu Prof Malima. Lakini kwa nyakati hizi CCM hawawezi kabisa kufanya hivyo, unless wamejibariki kwamba sasa CCM wanakuwa opposition party.

Kutokana na UIMARA wa opposition party, hivyo CCM wanataka kumu CONTAIN Lowassa. Yaanu KUMUDHIBITI Lowassa akiwa NDANI ya CCM, kwani akitoka NJE ya CCM itakuwa na sawa genie out of the bottle, hawataweza KUMDHIBITI tena Lowassa.

Hii strategy ya CONTAINMENT ya CCM dhidi ya Lowassa ndiyo pia inamuweka juu kwenye political landscape za Tanzania. Kwani Lowassa anaendelea kufanya vitu vyake kufikia ndoto ya safari yake. Ni vipi CONTAINMENT POLICY ya CCM itafanya kazi dhidi ya Lowassa that is remained to be seen, But once thing is CLEAR sio wote watakaoshinda vita hii yaani CCM on other hand and Lowassa on the other hand. LAZIMA mmojawapo kati ta CCM na Lowassa ATASHINDWA hiyo VITA?

Je kati ya CCM na Lowassa nani ATASHINDA hiyo VITA? BE THE JUROR YOURSELF.
 
LOWASSA mwizi sana, SLAA hana recodi yoyote ya kujivunia mpaka aitwe mkombozi wa taifa, tuache kupamabana kijinga mitandaoni
 
Back
Top Bottom