Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Kwa lipi Lowassa apewe nchi?

Jamani tukiamua kumpa Lowassa tuvumilie Rais wetubkuwa anashinda ktk hospital huko Ujerumani na America kwa sababu Afya afya yake mgogoro (hujafa hujaumbika) na sidhani kama ana uwezo wa kumaliza kampeni nchi nzima akiwa salama.
 
Kwa lipi la maana alilolifanya Lowassa hadi apewe nchi?

Kuna sababu nyingi za kusema Lowassa hafai kuwa rais wa nchi hii licha ya kuwa mgonjwa wa macho na mgongo pia ni mmoja wa watu 11 waliotajwa kuwa ni mafisadi.

Amefanya nini la maana hadi tumpe nchi? Unamkumbuka kwa lipi zaidi ya kujiuzulu?

Pesa zake sio tiketi kuwepo ulazima wa kuingia ikulu. Kama anatafuta umaarufu,umaarufu sio kwa mazuri tu hata ufisadi na kujiuzulu napo aljulikana ndani na nje ya nchi.

Sababu zipi za kunishawishi kumpigia kura Lowassa awe Rais wa awamu ya tano?

Hivi Kikwete tulimpa nchi kwa jambo gani hasa alilolitenda kabla ya kupewa nchi?
Kwa kuwa tulianza kwa mizaha ngoja tuendelee na mizaha yetu, tumpe Lowasa nchi.
Hao watangaza nia wengine nao wana nini kipya ambacho EL anakikosa?
Yetu mizaha na tutapata raid kwa mizaha!!!
 
afadhali apewe, maana kwa miaka 9 sasa nchi ipo auto pilot! hakuna wa kuamua jambo! kila mtu analalamika! bora aje atuibie lakini awe na maamuzi endelevu!


Hivi hatuwezi kupata mwenye maamuzi endelevu asiyekuwa mwizi?
 
pia ukitaka kujua walimfanyia fitina angalia Escrow inavyopigwa chenga utajua kuwa kila mwenye maono tofauti lazima ile kwake hata Richimond kulikuwa na uwezo wa kupindisha lakini kwa kuwa walimtaka EL walifanya hivyo kujifanya wanatupenda wananchi kumbe bure tu .ila Kwa kuwa hakuna anayebeba hata shilingi viongozi wangetambua tambura hilo Tanzania tungepona
 
Mkuu Sibonike, kwa CCM hakuna aliye msafi (ili kumaanisha, aliyemsafi na awe wakwanza kumpiga jiwe LOWASA)....pengine basi sasa ni wakati wakujaribu vyama vingine!
 
Nchi hii kuendelea kukaa mikonono mwa magamba ni Janga la Taifa.
UKAWA ndo wanaweza kututoa kwenye tope wa Ufisadi tulilokwama katikati.
 
siwezi kutaja jina la mtu bali nataja sifa za mtu anayefaa kuwa rais wa nchi hii.
1. Awe mwadilifu na mzalendo
2. Awe na uwezo wa kutatua matatizo ya kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni
3. Awe ni mtu anayejali watu wake hususani wanyonge
4. Awe ni mtu anayeweza kulinda rasimali zetu kama madini,wanyama nk
4. Awe na uwezo wa kushughulikia wahujumu uchumi

5. Asiwe fisadi na awe na uwezo wa kuwashughulikia mafisadi wanauza nchi mchana kweupe
6. Asiwe mtu aliyewahi kujihusisha na ufisadi
 
Back
Top Bottom