Kwa kukutana na Maalim Seif: Kaimu Balozi wa Marekani amekiuka Mkataba wa Diplomasia?

View attachment 1352047

Bado haijafahamika walichoteta , lakini kuna dalili ya kishindo kikubwa kuikumba Tanzania .

Endeleeni kubaki hapa hapa Jf

This should serve as a wakeup call for Zanzibar leadership in particular - Balozi awezi kufunga safari kwenda visiwani kuonana specifically na maalimu Seif bila sababu za msingi,atakuwa ametumwa na Trump/Pompeo kudadisi kwa kina kinacho endelea visiwani - ni wazi viashilia vina onyesha USA imepania kuibana Tanzania zaidi on top kumzuia Makonda na family yake kutembelea USA things could become even worse if we don't take heed.

Ushauri wangu tusianze tena kujaribu kumuwekea mizengwe maalimu Seif au chama Chake ili hasiweze kugombea kiti cha Urais kupitia chama chake, tu tone down rhetoric za kumunanga Balozi wa Marekani kwa kufanya mazungumzo na maalimu Seif - tukifanya makosa ya kulazimisha mambo mwisho wa siku yatakuja ku-cost Taifa letu an arm and leg. Ni suala la kujitathimini kama Taifa,je, tunavyo vitendea vyama vya upinzani ni sawa au la? Je, wabunge wa vyama upinzani wanavyo kuwa treated Bungeni ni sawa? wakati mwingine wanazomewa kama watoto wadogo, kupigwa pigwa vijembe na mipasho ya taarabu - binafsi huwa na kereka na tabia hizi zisizo za kiungwana/staarabu.
 
Homeboy umeandika kama mlevi,hivi sisi kweli ni taifa ambalo Marekani au taifa lolote lililoendelea likitaka kutupandikizia ugonjwa watashindwa?

Ukumbuke unaishi katika nchi ambayo raia mpaka karne hii wanafundishwa umuhimu wa kunawa mikono kwa sabuni,wajenge vyoo,wasinye vichakani na watahiriwe na semina zinatolewa kwa msaada wa hao hao,dawa wanatusaidia hao hao hahahah
Kuna stage za kupandikiza ugonjwa hatua ya kwanza ni kuintroduce wagonjwa wachache let's say wanne au kumi mkijiroga mkatangaza kuwa nchini mwenu wamegundulika watu wenye ugonjwa husika kesho yake ndio wamafungulia kabisa bomba
 
Kinachowauma Lumumba FC walizani wao peke yao ndio wanaweza kuwa na mazungumzo ya faragha na balozi za nchi kubwa. Hicho ni kiwewe wanatamani kujua seif ameongea nao nini?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa huyo anaweza kufukuzwa nchini na mkabaki midomi wazi

God save us
Hebu mfukuzeni fasta fasta tuone kweli nyie mnamuweza beberu.
tapatalk_1580290163897.jpeg


dodge
 
CCM inapata uoga gani kama mpinzania atazungumza na balozi? Mbona wapinzani wamekuwa wanatoa maoni yao kwenye mitandao na hata kweye TV ambazo zinaonekana cuniani kote?

Mnyika si alizungumza wiki iliyopita tu akaelezea jinsi Chadema wanavyoona kwamba wanaonewa na mambo mengine mengi? Kwani mabalozi hawawaezi kuona hayo wakajua wapinzania wanavyosema? Kukutana na mpinzani kuna athari gani?

Na kama Maalim Seif ni rafiki na huyo kaimu balozi, hawaruhusiwi kuzungumza wawili wakiwa nyumbani kwa Maalim Seif? Mbona inaonekana kama kila atakachofanya mpinzani "kinatutiwa mbinu" ya kukigeuza kiwe ni kama jinai?

Nawaombeni sana nyie viongozi wa Chama Tawala hapa Tanzania, Kumbukeni kwamba hata panya akiona amezidiwa na mtu anayemwinda huwa huyo panya anamrukia huyo mtu amng'ate ili ashituke aachane naye.

Kumbukeni kwamba hata yaliyotokea kule Soweto Afrika Kusini yalihusisha watoto wadogi kabisa wa shule za msingi lakini kwa vile walivyokuwa wamechoka kuona wanaonewa walifika mahali wakasema afadhali wapigwe risasi wafe kuliko kukaa kimya wakiwa wanaonewa.

Nawaombeni Chama Tawala mtambue kwamba kama itafika mahali wapinzania waseme 'liwalo na liwe' hakuna atakayeweza kuzima huo moto. Na waathirika wakubwa watakuwa ni viongozi wenu.

Mnaweza kuwa mnadhani kwa vile Watanzania "wamezoea kuishi kwa amani" hawataweza kufanya jambo la kuvunja amani. Lakini, hali ya maisha hapa Tanzania ni ngumu sana kwa sasa. Watanzania wengi (asilimia sitini au zaidi) ni vijana, na vijana wana mihemuko.

Wengi hawana ajira hata wale ambao walisoma wakitegemea kupata ajira. Hawana mitaji ya kuanza ujasiriamali wala kufanya kilimo. Kwa hivyo, nawaomba sana, tena sana, viongozi wa CCM, mtambue kwamba you are sitting on a time bomb (mnakalia bomu ambalo linaweza kulipuka wakati wowote).

Nawaomba mbadilike katika namna yenu ya kufikiri. Pamoja na kujenga miradi mikubwa kama Stieglers, reli ya kisasa na kuwa na ndege nyingi, vijana hao watafurahi lakini kama wao hawafiadi na hiyo miradi bado mioyoni mwao hawatakuwa na furaha. Ni rahisi sana vijana kama hao kutumiwa kisiasa kusababisha amani ya nchi ipotee kabisa.

Tunamwomba Mungu hilo lisitokee. Lakini na nyie viongozi wa chama tawala, tafuteni mbinu za kuzalisha ajira nyingi kwa vijana na kuboresha uchumi wa mtu mmoja mmoja wakati uchumi wa taifa unapanda kama sasa.

Mungu ibariki Tanzania.
 
maramla,
Sikujua kuwa Balozi anayewakilisha nchi yake hapa Tanzania hawezi kutoka sehemu moja (DSM) na kwenda sehemu nyingine (Mikoani / Zanzibar) bila kibali cha Wizara ya Mambo ya Nje.
 
Back
Top Bottom