Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 59,009
- 103,394
Kuna watu wengi waliituhumu CHADEMA kwa kutokwenda mahakamani baada ya kuporwa uchaguzi Mkuu wa 2020. Cdm walisema baadhi ya taasisi za umma zilizoingiziwa uozo wa siasa chafu za ccm, ni pamoja na mahakama.
Kwa sasa kwenye kesi hii ya Mbowe ushahidi unazidi kukaa wazi, na bado kesi haijafika mwisho, lakini tayari majaji wawili wameshatoka, na huyu wa sasa amejaa maamuzi ya utata, na sidhani kama atafika mwisho wa kesi.
Kubwa kuliko yote ni mahakama kutumika kuvujisha nyaraka kwa mashahidi wa jamuhuri kinyume kabisa cha sheria, na utawala wa mahakama uko kimya kuhusu hilo! Iwapo mahakamani ndio sehemu tunaambiwa ni ya kupatia haki, na inatakiwa tuiamini kuwa itatenda haki, wanashirikiana na watu waliobambikizia kesi, ni taasisi ipi tena ya umma inaweza kuaminika?
Kwa hapa tulipofikia ni kwa jinsi gani tunaweza kukwepa katiba mpya, wakati hadi mahakama imekubali kutumikia siasa chafu za CCM?