Wanasheria wafungua Kesi ya kutaka Mbunge wa Ngorongoro afikishwe Mahakamani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,759
218,380
Mara zote tumeandika humu na kwingineko kwamba Shetani hajawahi kuwa na Rafiki , nadhani sasa mmeanza kuelewa tulichomaanisha .

Ukitetea Wananchi hata kama wewe ni Mwanaccm , ni lazima utashughulikiwa tu , hii ni kwa sababu ccm haipo kwa ajili ya Wananchi .

Screenshot_2023-08-23-18-52-41-1.jpg
---
Leo Jumatano Agosti 23, 2023 mawakili wa mbunge wa Ngorongoro, Emmanuel Ole Shangai anayeshikiliwa na polisi tangu juzi, wamefungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kuomba mteja wao afikishwe mahakamani pamoja na wananchi wengine 30.

Ole Shangai alikamatwa juzi wilayani Karatu akiwa njiani kwenda polisi baada ya kupata maelekezo kutoka kwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Arusha.

Wakizungumza na waandishi wa habari leo baada ya kupeleka maombi ya kufungua kesi hiyo, mawakili hao wamesema tangu mbunge huyo alipokamatwa, hawajui alipo.

Wakili Joseph Ole Shangai amesema wameamua kwenda mahakamani kusaka haki kwa maelezo kuwa makosa wanayotuhumiwa nayo yanadhamana kisheria.

Amesema juzi baada ya mbunge kukamatwa alikua naye polisi ambao walimuahidi wangempa dhamana mteja wake jambo ambalo limekuwa kinyume chake.

Wakili mwingine, Alayce Melau amesema, ‘’Tumepeleka maombi ya kesi kwa msajili tuna imani kesi itapangiwa hakimu wa kusikilizwa haraka uwezekavyo ili haki utendeke.
Baadhi ya wananchi wanaoshikiliwa hali zao ni mbaya maana baadhi ni wagonjwa kutokana na kipigo.’’

Hata hivyo, Polisi Mkoa wa Arusha hawajatoa taarifa yoyote ya kushikiliwa kwa mbunge huyo wa CCM. Jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justin Masejo kuzungumzia suala hilo zinaendelea.
 
Tanzania kiongozi pekee aliye kuwa kwa ajili ya kuona watu wanaondoka point A up to B,ni Nyerere pekee wengine wote sio viongozi wa CCM au CDM wote wapo after matumbo yao na familia zao.
Mwenyewe uchungu na Nchi kama Nyerere labda atapatikana miaka 100 ijayo.
 
hii ndo sisiem....sijui ni lini Mungu atatunusuru na hili Jini CCM..
Acha Matusi

nakukumbusha tu Chadema wanashiriki vikao vya TCD vinavyoshirikisha vyama vyote na Mwenyekiti wake ni Kinana

Mlitangaziwa kwa mbwembwe kuwa wamesusia lakini sasa hivi wanashiriki na hawajawatangazia Makamanda wao na hoja ni kubadili sheria ya uchaguzi ili iboreshwe kabla ya uchaguzi Mkuu, Rasimu ya Katiba mpya Mzee Kinana kishatangaza ni ya zamani sana na imepitwa na wakati.
 
Tanzania kiongozi pekee aliye kuwa kwa ajili ya kuona watu wanaondoka point A up to B,ni Nyerere pekee wengine wote sio viongozi wa CCM au CDM wote wapo after matumbo yao na familia zao.
Mwenyewe uchungu na Nchi kama Nyerere labda atapatikana miaka 100 ijayo.
Magufuli
 
Acha Matusi

nakukumbusha tu Chadema wanashiriki vikao vya TCD vinavyoshirikisha vyama vyote na Mwenyekiti wake ni Kinana

mlitangaziwa kwa mbwembwe kuwa wamesusia lakini sasa hivi wanashiriki na hawajawatangazia Makamanda wao na hoja ni kubadili sheria ya uchaguzi ili iboreshwe kabla ya uchaguzi Mkuu, Rasimu ya Katiba mpya Mzee Kinana kishatangaza ni ya zamani sana na imepitwa na wakati.
Mwenyekiti wa TCD siyo Kinana , halafu TCD siyo kamati ya Katiba ya akina Mukandara .
 
Tanzania kiongozi pekee aliye kuwa kwa ajili ya kuona watu wanaondoka point A up to B,ni Nyerere pekee wengine wote sio viongozi wa CCM au CDM wote wapo after matumbo yao na familia zao.
Mwenyewe uchungu na Nchi kama Nyerere labda atapatikana miaka 100 ijayo.
Kwa hiyo tufanyeje.
 
Hebu ulizia mapalala na kasanga tumbo huyu nyerere aliwafanyia kitu gani?
 
Back
Top Bottom