Kwa jinsi wabantu tunavyoamini uchawi, naamini kuwa Kinjekitile alijua dawa yake itafanya kazi

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,893
Vitabu shuleni tuliaminishww kuwa Kinjekitile alifanya vile ili kuwapa wanajeshi moyo wa kupigana. Mi natilia shaka hili jambo. Limepotoshwa tu kumfichia aibu yule mzee. Kwa jinsi tunavyoamini ushirikina naona kuwa Kinjekitile aliamini dawa yake itafanya kazi.

Hadi leo watu wanajikinga kwa uchawi. Wezi wakikamatwa hukutwa na hirizi kubwa eti wanajikinga na vipigo. Wabantu imani za kishirikina zina sehemu kubwa sana kwenye maisha yetu.
 
Kinjekitile aliwahi kuhojiwa na BBC na akakiri kuwa dawa ile ilibadilisha risasi kuwa maji. Yeye mwenyewe alikiri hilo.
 
Vitabu shuleni tuliaminishww kuwa Kinjekitile alifanya vile ili kuwapa wanajeshi moyo wa kupigana. Mi natilia shaka hili jambo. Limepotoshwa tu kumfichia aibu yule mzee. Kwa jinsi tunavyoamini ushirikina naona kuwa Kinjekitile aliamini dawa yake itafanya kazi.

Hadi leo watu wanajikinga kwa uchawi. Wezi wakikamatwa hukutwa na hirizi kubwa eti wanajikinga na vipigo. Wabantu imani za kishirikina zina sehemu kubwa sana kwenye maisha yetu.
Si wabantu tu hata waarab wanatumia sana uchawi uliopo ndani ya Qur'an kwa kinga, ulaghai, na vinginevyo
 
Hivi wapiganaji wale wangeambiwa ukweli na kutumia mbinu za ambush kama Mkwawa, uwezekano wa ushindi ungekuwaje?
 
Hivi wapiganaji wale wangeambiwa ukweli na kutumia mbinu za ambush kama Mkwawa, uwezekano wa ushindi ungekuwaje?
Yangekuwa afadhali kuliko kutegemea uchawi. Pengine nao wangekuwa na akili ya kupata bunduki. Wanafalsafa wa vita wanasema ni uchawi ni mwiko jeshini.
Wanasema unafanya mtu kutoumiza akili kutumia mbinu na zana bali atategemea uchawi. Pia uchawi humfanya awe muoga.

Huko Ufilipino kuna watu wanaamini kuwa kuna majini au niseme mazombi ambayo hunyonya watu damu. CIA wanasoma culture zote duniani , wanalijua hili. Hawa waamini wanyonya damu wakaasi, CIA walichofanya ilikuwa wakiwaua waasi wanawaning'iniza kichwa chini miguu juu kwenye miti. Waasi kuona hivyo wakajua wanyonya damu wameingia, hata nguvu ya kupambana ikaisha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom