Kwa nionavyo, Wakili huyu hatakuwa na mwisho mwema kiroho

Kamkunji

Member
Sep 14, 2023
92
272
1. Mara ya kwanza Kesi iliyosumbua sana, ya yule mmiliki wa mabasi maarufu ya J Four(J4) ya kuwaua wadeni wake kwa kuwapiga risasi, mpaka kuhukumiwa kufungwa maisha(kama sijasahau ilikuwa kunyongwa hadi kufa) ambayo kiuhalisia ni kweli jamaa aliwaua watu wale(alikiri kuhusika), Wakili huyu kwa kuwa anafahamu namna alivyo na mtandao mkubwa wa mahakimu akaingilia kesi ile na kesi kuanza upya, na kwa dalili zilizokuwepo ni kwamba yule jamaa(J4) alikuwa anaelekea kushinda kesi(sijui kama hukumu ilishatoka maana niliondoka Tz, nikaacha kufuatilia) hivyo roho za wale waliouawa zikawa zimedhulumiwa kwa kujuana na nguvu ya pesa.

2. Kesi ya mke wa marehemu Bilionea Msuya,
Baada ya mauaji ya dada wa marehemu bilionea Msuya, mama wa mtoto mmoja na aliyekuwa akifanya kazi Wizara ya Fedha, kuuawa kwa kuchinjwa kama kuku, Mke wa marehemu bilionea Msuya alikiri kuhusika na mauaji yale kwa kigezo kuwa marehemu(dada wa bilionea Msuya) alikuwa akimsumbua sana kwenye mirathi, hivyo akahukumiwa kifungo cha maisha kama sijasahau

Ni yule yule wakili kuingilia kesi hiyo ambayo awali mtuhumiwa alikiri kuhusika na mauaji hayo, baada ya muda na wakili huyo kuchezesha kama kawaida yake, February mwaka huu muuaji kaachiwa huru bila shaka yoyote kua hakuhusika

Ni kesi hii ndiyo inayoibua maswali na kejeli nyingi kwa mahakama zetu na vyombo vya ulinzi na usalama hasa jeshi la polisi upande wa upelelezi, na wengi kuona kua kesi ile haikumtendea haki marehemu dada wa bilionea Msuya ambayo kimsingi ni kweli

Sasa mimi nimekaa na kutafakari sana, kimwili na hasa kiroho, nikajiuliza huyu wakili mwenye koneksheni na majaji mbona ameifanya pesa, koneksheni na elimu yake kama fimbo ya kuwachapia wale wasiofika bei,
Roho za marehemu hao zinalia, familia za marehemu hao zinataabika, watoto wa marehemu hao wanateseka sababu ya kuuawa kwa wapendwa wao, ni nani atazifuta machozi familia hizi, Ee Mwenyezi Mungu ni nani atawafuta machozi watoto wa marehemu hao ambao wengine walikua wakisoma shule nzuri leo hii wanaenda kidumu na mfagio sababu ya kuuawa kwa wapendwa wao na mbaya zaidi ukweli kupindishwa na mhusika wa kupindisha ukweli ni huyu wakili, ninajua nayeye ana watoto ana ndugu na ipo siku hao waovu anaowatetea, roho za marehemu zitamrudia yeye na kizazi chake kwa kua anafanya hivyo si kwa sababu watu hao walionewa bali watu hao wamemlipa pesa ya kutosha ambayo anaweza kugawana na wenzake na kesi ikapindishwa , na kuwashuhudia uongo marehemu hao

Ukweli utabaki pale pale, dunia tunapita, vile unavyowatendea wenzako nawe siku moja utatendewa vivyo hivyo kama si wewe basi kizazi chako. Pesa haijawahi kutosha na haitotosha kamwe, unashuhudia vipi uongo ambao unajua kweli yake, kweli pesa mwanaharamu, Ee Mwenyezi Mungu nijaalie nipunguze tamaa hasa dhidi ya pesa, sijui huyo mtoto wa dada wa Bilionea Msuya atakua na umri gani lakini katika kufikiria kwangu hata akiwa mkubwa ataoneshwa watu wawili waliohusika na kifo cha mama yake, Muuaji(ambaye awali alikiri) na wakili aliyemsimamia na kumtetea kua hakuhusika ilihali anajua kuwa alihusika.

Najua hata watu hao wangefungwa isingewaongezea kitu familia zao lakini kitendo cha wao kufungwa kingeleta ahueni kwa wapendwa wao.

Sijui kwanini kesi ya huyu dada wa bilionea Msuya imeniumiza sana, nimeumia sana, japo nikiri kuwa mimi sikuwahi kuwafahamu watu hao ila nilikuwa interested tu kuona haki ikitendeka kwa kua wauaji walikiri,

Ndugu na rafiki yangu wakili najua unazipenda kesi hizi kwakua zinakupa pesa ndefu kwa wakati mmoja lakini kweli ya mauaji ya watu hao unazijua, ni kesi zenye nguvu za kiroho, naomba nikukumbushe "Karma is a bitch" kama si kwako hata kwa vizazi vyako.

Mungu azitie nguvu familia za marehemu. "Sisi ni wake na kwake tutarejea"
Amina
 
Kwa hiyo mara ya kwanza alikili kosa , ila mara ya pili ajakili kosa, Me nazani Haina haja ya kulaumu sana ila tuangalie ni mazingira Gani yalisababisha huyu mama mara ya kwanza kukili kosa na mara ya pili kukataa kosa , unaweza Kuta alipigwa sana. ni kweli mahakamani haki hamna wengi wa majaji wanapenda ela tu ila tuvumilie ivyo ivyo
 
Marungu unayajua?
 
1. Mara ya kwanza Kesi iliyosumbua sana, ya yule mmiliki wa mabasi maarufu ya J Four(J4) ya kuwaua wadeni wake kwa kuwapiga risasi, mpaka kuhukumiwa kufungwa maisha(kama sijasahau ilikua kunyongwa hadi kufa) ambayo kiuhalisia ni kweli jamaa aliwaua watu wale(alikiri kuhusika), Wakili huyu kwa kua anafahamu namna alivyo na mtandao mkubwa wa mahakimu alifika bei na inakadiriwa ilikua kiasi cha Tsh milioni mia mbili(200M) akaingilia kesi ile na kesi kuanza upya, na kwa dalili zilizokuwepo ni kwamba yule jamaa(J4) alikua anaelekea kushinda kesi(sijui kama hukumu ilishatoka maana niliondoka Tz, nikaacha kufuatilia) hivyo roho za wale waliouwawa zikawa zimedhulumiwa kwa kujuana na nguvu ya pesa.

2. Kesi ya mke wa marehemu bilionea Msuya,
Baada ya mauaji ya dada wa marehemu bilionea msuya, mama wa mtoto mmoja na aliyekua akifanya kazi wizara ya fedha, kuuawa kwa kuchinjwa kama kuku, Mke wa marehemu bilionea Msuya alikiri kuhusika na mauaji yale kwa kigezo kua marehemu(dada wa bilionea Msuya) alikua akimsumbua sana kwenye mirathi, hivyo akahukumiwa kifungo cha maisha kama sijasahau,
Ni yule yule wakili, ambaye alifika bei ambayo inakadiriwa kua zaidi ya milioni 300 na kuingilia kesi hiyo ambayo awali mtuhumiwa alikiri kuhusika na mauaji hayo, baada ya muda na wakili huyo kuchezesha kama kawaida yake, February mwaka huu muuaji kaachiwa huru bila shaka yoyote kua hakuhusika,
Ni kesi hii ndiyo inayoibua maswali na kejeli nyingi kwa mahakama zetu na vyombo vya ulinzi na usalama hasa jeshi la polisi upande wa upelelezi, na wengi kuona kua kesi ile haikumtendea haki marehemu dada wa bilionea Msuya ambayo kimsingi ni kweli

Sasa mimi nimekaa na kutafakari sana, kimwili na hasa kiroho, nikajiuliza huyu wakili mwenye koneksheni na majaji mbona ameifanya pesa, koneksheni na elimu yake kama fimbo ya kuwachapia wale wasiofika bei,
Roho za marehemu hao zinalia, familia za marehemu hao zinataabika, watoto wa marehemu hao wanateseka sababu ya kuuawa kwa wapendwa wao, ni nani atazifuta machozi familia hizi, Ee Mwenyezi Mungu ni nani atawafuta machozi watoto wa marehemu hao ambao wengine walikua wakisoma shule nzuri leo hii wanaenda kidumu na mfagio sababu ya kuuawa kwa wpendwa wao na mbaya zaidi ukweli kupindishwa na mhusika wa kupindisha ukweli ni huyu wakili, ninajua nayeye ana watoto ana ndugu na ipo siku hao waovu anaowatetea, roho za marehemu zitamrudia yeye na kizazi chake kwa kua anafanya hivyo si kwa sababu watu hao walionewa bali watu hao wamemlipa pesa ya kutosha ambayo anaweza kugawana na wenzake na kesi ikapindishwa , na kuwashuhudia uongo marehemu hao,
Ukweli utabaki pale pale, dunia tunapita, vile unavyowatendea wenzako nawe siku moja utatendewa vivyo hivyo kama si wewe basi kizazi chako. Pesa haijawahi kutosha na haitotosha kamwe, unashuhudia vipi uongo ambao unajua kweli yake, kweli pesa mwanaharamu, Ee Mwenyezi Mungu nijaalie nipunguze tamaa hasa dhidi ya pesa, sijui huyo mtoto wa dada wa Bilionea Msuya atakua na umri gani lakini katika kufikiria kwangu hata akiwa mkubwa ataoneshwa watu wawili waliohusika na kifo cha mama yake, Muuaji(ambaye awali alikiri) na wakili aliyemsimamia na kumtetea kua hakuhusika ilihali anajua kuwa alihusika.

Najua hata watu hao wangefungwa isingewaongezea kitu familia zao lakini kitendo cha wao kufungwa kingeleta ahueni kwa wapendwa wao,
sijui kwa nini kesi ya huyu dada wa bilionea Msuya imeniumiza sana, nimeumia sana, japo nikiri kua mimi sikuwahi kuwafahamu watu hao ila nilikua interested tu kuona haki ikitendeka kwa kua wauaji walikiri,
Ndugu na rafiki yangu wakili najua unazipenda kesi hizi kwakua zinakupa pesa ndefu kwa wakati mmoja lakini kweli ya mauaji ya watu hao unazijua, ni kesi zenye nguvu za kiroho, naomba nikukumbushe "Karma is a bitch" kama si kwako hata kwa vizazi vyako.

Mungu azitie nguvu familia za marehemu. "Sisi ni wake na kwake tutarejea"
Amina
Mahakama ilikwishapoteza legitimacy yake. Especially chini ya Prof Ibrahim Juma kama Chief Justice
 
Bongo hakuna haki ukiingalia maelezo yakukiri yote yanatokea polisi baada ya kula virungu, ndugu yangu unaweza kupigwa virungu na kubanwa makende mpaka ukakiri umemuua Mzee magu wakati mzee watu alijifia na Covid
wacha nikwambie kitu,polisi hawapigagi mtu mwenye tuhuma za mauaji au ubakaji,kesi kubwa ubazoweza kupigwa sana ni ugaidi,ujambazi,au utekaji.

vibaka na wadokozi ndio wahanga wakubwa sana wa vipigo,ukiona mtu ana tuhuma za mauaji na kakiri mwenyewe polisi ujue ni kwa hiyari yake,ingawa bado anaweza kukataa pia mahakamani kwa ushauri wa wakiri wake.
 
1. Mara ya kwanza Kesi iliyosumbua sana, ya yule mmiliki wa mabasi maarufu ya J Four(J4) ya kuwaua wadeni wake kwa kuwapiga risasi, mpaka kuhukumiwa kufungwa maisha(kama sijasahau ilikua kunyongwa hadi kufa) ambayo kiuhalisia ni kweli jamaa aliwaua watu wale(alikiri kuhusika), Wakili huyu kwa kua anafahamu namna alivyo na mtandao mkubwa wa mahakimu alifika bei na inakadiriwa ilikua kiasi cha Tsh milioni mia mbili(200M) akaingilia kesi ile na kesi kuanza upya, na kwa dalili zilizokuwepo ni kwamba yule jamaa(J4) alikua anaelekea kushinda kesi(sijui kama hukumu ilishatoka maana niliondoka Tz, nikaacha kufuatilia) hivyo roho za wale waliouwawa zikawa zimedhulumiwa kwa kujuana na nguvu ya pesa.

2. Kesi ya mke wa marehemu bilionea Msuya,
Baada ya mauaji ya dada wa marehemu bilionea msuya, mama wa mtoto mmoja na aliyekua akifanya kazi wizara ya fedha, kuuawa kwa kuchinjwa kama kuku, Mke wa marehemu bilionea Msuya alikiri kuhusika na mauaji yale kwa kigezo kua marehemu(dada wa bilionea Msuya) alikua akimsumbua sana kwenye mirathi, hivyo akahukumiwa kifungo cha maisha kama sijasahau,
Ni yule yule wakili, ambaye alifika bei ambayo inakadiriwa kua zaidi ya milioni 300 na kuingilia kesi hiyo ambayo awali mtuhumiwa alikiri kuhusika na mauaji hayo, baada ya muda na wakili huyo kuchezesha kama kawaida yake, February mwaka huu muuaji kaachiwa huru bila shaka yoyote kua hakuhusika,
Ni kesi hii ndiyo inayoibua maswali na kejeli nyingi kwa mahakama zetu na vyombo vya ulinzi na usalama hasa jeshi la polisi upande wa upelelezi, na wengi kuona kua kesi ile haikumtendea haki marehemu dada wa bilionea Msuya ambayo kimsingi ni kweli

Sasa mimi nimekaa na kutafakari sana, kimwili na hasa kiroho, nikajiuliza huyu wakili mwenye koneksheni na majaji mbona ameifanya pesa, koneksheni na elimu yake kama fimbo ya kuwachapia wale wasiofika bei,
Roho za marehemu hao zinalia, familia za marehemu hao zinataabika, watoto wa marehemu hao wanateseka sababu ya kuuawa kwa wapendwa wao, ni nani atazifuta machozi familia hizi, Ee Mwenyezi Mungu ni nani atawafuta machozi watoto wa marehemu hao ambao wengine walikua wakisoma shule nzuri leo hii wanaenda kidumu na mfagio sababu ya kuuawa kwa wpendwa wao na mbaya zaidi ukweli kupindishwa na mhusika wa kupindisha ukweli ni huyu wakili, ninajua nayeye ana watoto ana ndugu na ipo siku hao waovu anaowatetea, roho za marehemu zitamrudia yeye na kizazi chake kwa kua anafanya hivyo si kwa sababu watu hao walionewa bali watu hao wamemlipa pesa ya kutosha ambayo anaweza kugawana na wenzake na kesi ikapindishwa , na kuwashuhudia uongo marehemu hao,
Ukweli utabaki pale pale, dunia tunapita, vile unavyowatendea wenzako nawe siku moja utatendewa vivyo hivyo kama si wewe basi kizazi chako. Pesa haijawahi kutosha na haitotosha kamwe, unashuhudia vipi uongo ambao unajua kweli yake, kweli pesa mwanaharamu, Ee Mwenyezi Mungu nijaalie nipunguze tamaa hasa dhidi ya pesa, sijui huyo mtoto wa dada wa Bilionea Msuya atakua na umri gani lakini katika kufikiria kwangu hata akiwa mkubwa ataoneshwa watu wawili waliohusika na kifo cha mama yake, Muuaji(ambaye awali alikiri) na wakili aliyemsimamia na kumtetea kua hakuhusika ilihali anajua kuwa alihusika.

Najua hata watu hao wangefungwa isingewaongezea kitu familia zao lakini kitendo cha wao kufungwa kingeleta ahueni kwa wapendwa wao,
sijui kwa nini kesi ya huyu dada wa bilionea Msuya imeniumiza sana, nimeumia sana, japo nikiri kua mimi sikuwahi kuwafahamu watu hao ila nilikua interested tu kuona haki ikitendeka kwa kua wauaji walikiri,
Ndugu na rafiki yangu wakili najua unazipenda kesi hizi kwakua zinakupa pesa ndefu kwa wakati mmoja lakini kweli ya mauaji ya watu hao unazijua, ni kesi zenye nguvu za kiroho, naomba nikukumbushe "Karma is a bitch" kama si kwako hata kwa vizazi vyako.

Mungu azitie nguvu familia za marehemu. "Sisi ni wake na kwake tutarejea"
Amina
Acheni chuki na roho mbaya.
Mimi nimesoma hukumu ya ile kesi, nimejionea UJUHA, uwendawazimu na ukichaa upande wa mashtaka.
Kama pesa basi wamekula mashahidi wa Jamhuri ambao wengi wao ni polisi. Hao hao ndio ambao wamefanya upelelezi.
Mimi sio hakimu, lakini hata mimi ningewaachia huru watuhumiwa.

It is the principle of the law that, the accused person shall not be convicted on the basis of weakness of their evidence/defence but rather on the strength of prosecution evidence or case.
Angalia madhaifu niliyoyaona mimi:-
1. Majina ya mshitakiwa wa pili yamekosewa vibaya sana. Mashtaka ni dhidi ya REVOCATUS EVARIST MUYELA, wakati mshitakiwa anaitwa REVOCATUS EVAREST PATRICK MUYELA
Hayo majina kayakana si yake na hamfahamu mtu huyo.
2. Katika ushahidi kuna afande 1 alisema alipewa namba za gari na shahidi housegirl.....housegirl akasema yeye namba za gari hazijui anajua rangi na aina (make).
3. Kuna ushahidi kuwa housegirl alikamatwa siku chache baada ya mauwaji. Mwingine akasema alikuja kukamatwa miezi kadhaa mbele.
4. Shahidi 1 alisema alimhoji mshitakiwa namba 1 ofisi ya polisi Temeke. Aliyerecord tukio la mahojiano akasema walifanya hivyo kituo cha polisi Aiport.
5. Kuna shahidi akasema alishiriki zoezi la utambuzi (identification parade) akiwa kituo cha polisi Kilwa Rd majira saa 5 asubuhi. Karatasi ya maelezo inasema zoezi lilifanyika saa 12:49 mchana.
6. Eti OC-CID wa Kigamboni hakumbuki ni muda gani alifika eneo la tukio baada ya kuarifiwa kuna mauwaji na OCS wa Kibada.
7. Daktari wa post morten anasema alipokea maiti trehe 25 May na akaifanyia vipimo.....wakati kifo kimetokea tarehe 26 May.
8. Gari inayosemwa imetumika kwenda Kibada ilikua gereji siku zote za matukio. Na Jamhuri wameshindwa kukanusha hili.
9. Housegirl katishiwa hadi na bastola, lakini akashindwa kumwambia bosi wake vitisho vyote hivyo, mpaka kuwekewa bastola shingoni. Inakuingia akilini?

Kiufupi, upande wa mshtaka umeshindwa kuthibitisha kuwa watuhumiwa ndio waliomuuwa Aneth. Na sheria inataka uthibitishe beyond reasonable doubt. Sasa ukichunguza sana unaona hawa watu ni kama hawakuuwa wao ila waliplot na inawezekana kuna waliotekeleza mauwaji. Yule mwanamke hakuuwa bali mimi kwa maoni yangu inawezekana alikula njama. Wapo waliotekeleza mauwaji lakin Jamhuri imeshindwa kuwapata.

Mtamlaumu bure Kibatala, kama upuuzi wanafanya polisi kwa kuharibu upelelezi na kushindwa kunyoosha maelezo mahakamani.
 
Kuna kesi moja tandahimba kuna dada mmoja msukuma anafanya kazi halmashauri kwahiyo alichukua pesa milion 20 akampa dogo mmoja amnunulie korosho kwa mfumo wa kangomba, yule dogo hakununua hata kilo moja pesa kazificha mwisho wa siku yule dada kamdai kwa njia ya kawaida dogo anakataa kuwa hawajawahi kupeana pesa wameenda mpaka mahakamani dogo kashinda
 
Back
Top Bottom