MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,760
- 48,407
Kawaida huwa sikubaliani na mambo mengi ya Watanzania, mojawapo huwa unafiki wao wa kujifanya wastaarabu huku wakielekeza vidole vya kila aina ya lawama dhdi ya Wakenya, ilhali wao nimeishi nao na kuona walivyo na maovu ya kila aina.
Lakini juzi kuna tukio moja limetendeka kwao na nikaona kwa hilo wametupiga bao sana na wapo vizuri. Kwa mara ya kwanza nilitamani sana Kenya iwe kama Tanzania kwa hili la kuishi bila ukabila japo kwao upo kwa hali ya chini.
Kuna zoezi la ubomoaji wa majengo yaliyojengwa kwenye hifadhi za barabara, zoezi hili limeendelezwa bila huruma wala kujali nani au nini. Nimepitia sehemu inaitwa Kimara na kuona jinsi Magufuli ameamua harudi nyuma na aki nani huyu mzee hajaribiwi aisei, mafisadi wanatamani kuihama nchi ya Tanzania.
Sasa tatizo au kama Waswahili wasemavyo, kitumbua kikaingia mchanga pale ambapo ubomoaji huu ulifikia kwa makazi ya kabila lake kule Mwanza maana yeye hujiita Msukuma, akatangaza kwamba wale wasibomoeshwe na kuwa wanaobomoa waonyeshe human face au ubinadamu wakiwa huko Mwanza na kwamba watu wa kule walimpa kura nyingi.
Kitu nilichokiona ambacho nimetamani Kenya kuiga ni pale Watanzania walijitokeza kwenye mitandao na kulaani huo upendeleo wa kikabila. Yaani wamelaani kwa nguvu nyingi sana na kumkatalia kwa hiyo kauli, japo kuna wale die hard wa CCM huku mitandaoni walimsifia na kukubaliana naye bila aibu, hao wanaeleweka maana wanalipwa, huwa tunawaona hata kwenye nyuzi za habari za Kenya, wanatumia nguvu nyingi kushinda mitandaoni wakiponda kila chochote cha Kenya, siku hizi huwa nawapuuza maana wapo kikazi zaidi.
Jameni kwenye vita dhidi ya ukabila tuwaige Watanzania, pale rais au hata kiongozi wa upinzani anaonyesha upendeleo wowote wa kikabila, tuwe tunajitokeza na kumkatalia kwa nguvu nyingi ili tudumishe utangamano. Nina uhakika tunweza na inawezekana, Wakenya wengi tunaishi kwa amani na bila ukabila, lakini wanasiasa hutumia huko kutugawa kama mtaji wao. Leo hii rais Uhuru na naibu wake Ruto wakimteua mtu fulani kwa kigezo cha ukabila, wengi hatukemei, tunaishia kukumbatia huo uteuzi, vile vile tuliona kipindi Raila akiwa waziri mkuu alivyojaza watu wa kabila lake na ndugu kwenye ofisi ya uwaziri mkuu.
Vita dhidi ya ukabila vianze kwetu sisi huku mashinani, nina uhakika viongozi wataishia kutuunga mikono, lakini kama tukiishi kuwasubiri hao waje na sera zozote, watakua wanatutumia kama mtaji.