Kwa hili la vita dhidi ya ukabila, jameni tuwaige Watanzania

MK254

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Messages
12,017
Likes
10,010
Points
280
MK254

MK254

JF-Expert Member
Joined May 11, 2013
12,017 10,010 280
Kawaida huwa sikubaliani na mambo mengi ya Watanzania, mojawapo huwa unafiki wao wa kujifanya wastaarabu huku wakielekeza vidole vya kila aina ya lawama dhdi ya Wakenya, ilhali wao nimeishi nao na kuona walivyo na maovu ya kila aina.

Lakini juzi kuna tukio moja limetendeka kwao na nikaona kwa hilo wametupiga bao sana na wapo vizuri. Kwa mara ya kwanza nilitamani sana Kenya iwe kama Tanzania kwa hili la kuishi bila ukabila japo kwao upo kwa hali ya chini.
Kuna zoezi la ubomoaji wa majengo yaliyojengwa kwenye hifadhi za barabara, zoezi hili limeendelezwa bila huruma wala kujali nani au nini. Nimepitia sehemu inaitwa Kimara na kuona jinsi Magufuli ameamua harudi nyuma na aki nani huyu mzee hajaribiwi aisei, mafisadi wanatamani kuihama nchi ya Tanzania.

Sasa tatizo au kama Waswahili wasemavyo, kitumbua kikaingia mchanga pale ambapo ubomoaji huu ulifikia kwa makazi ya kabila lake kule Mwanza maana yeye hujiita Msukuma, akatangaza kwamba wale wasibomoeshwe na kuwa wanaobomoa waonyeshe human face au ubinadamu wakiwa huko Mwanza na kwamba watu wa kule walimpa kura nyingi.

Kitu nilichokiona ambacho nimetamani Kenya kuiga ni pale Watanzania walijitokeza kwenye mitandao na kulaani huo upendeleo wa kikabila. Yaani wamelaani kwa nguvu nyingi sana na kumkatalia kwa hiyo kauli, japo kuna wale die hard wa CCM huku mitandaoni walimsifia na kukubaliana naye bila aibu, hao wanaeleweka maana wanalipwa, huwa tunawaona hata kwenye nyuzi za habari za Kenya, wanatumia nguvu nyingi kushinda mitandaoni wakiponda kila chochote cha Kenya, siku hizi huwa nawapuuza maana wapo kikazi zaidi.

Jameni kwenye vita dhidi ya ukabila tuwaige Watanzania, pale rais au hata kiongozi wa upinzani anaonyesha upendeleo wowote wa kikabila, tuwe tunajitokeza na kumkatalia kwa nguvu nyingi ili tudumishe utangamano. Nina uhakika tunweza na inawezekana, Wakenya wengi tunaishi kwa amani na bila ukabila, lakini wanasiasa hutumia huko kutugawa kama mtaji wao. Leo hii rais Uhuru na naibu wake Ruto wakimteua mtu fulani kwa kigezo cha ukabila, wengi hatukemei, tunaishia kukumbatia huo uteuzi, vile vile tuliona kipindi Raila akiwa waziri mkuu alivyojaza watu wa kabila lake na ndugu kwenye ofisi ya uwaziri mkuu.

Vita dhidi ya ukabila vianze kwetu sisi huku mashinani, nina uhakika viongozi wataishia kutuunga mikono, lakini kama tukiishi kuwasubiri hao waje na sera zozote, watakua wanatutumia kama mtaji.
 
Ndalama

Ndalama

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2011
Messages
8,435
Likes
5,374
Points
280
Ndalama

Ndalama

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2011
8,435 5,374 280
Tumekuelewa
 
wiseboy

wiseboy

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2011
Messages
2,909
Likes
2,227
Points
280
wiseboy

wiseboy

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2011
2,909 2,227 280
Kaka andaa mada zinazuhusu nchi yako utaendeleza kitu ama kwenye jamii yako au nchi kiujumla.
Najua hutaelewa ushaur wangu ila think about it.
Achana na ya Tanzania kurafuta popularity mtandaoni.

Nakuona mwandishi mzuri jaribu kuandaa makala za ufugaji bora, ukulima wa tija, uvunaji wa maji ya mvua na kuyatumia katika uzalishaji, nk.
Kisha nenda kijijin ulipozaliwa wagawie hizo nakala bure.....Utaacha alama chanya duniani.
 
joto la jiwe

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Messages
7,432
Likes
7,116
Points
280
joto la jiwe

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2017
7,432 7,116 280

Hivi kawaida mtu anachukua kabila la baba yake au mama yake?, Magufuli mama yake ndiyo msukuma, ila baba yake sio msukuma, japo alikufa akimuacha magufuli akilelewa na mama yake
 
tuusan

tuusan

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Messages
8,458
Likes
5,921
Points
280
Age
27
tuusan

tuusan

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2016
8,458 5,921 280
Umeongea vyema....Raisi wetu hufanya mambo kwa sababu zinazoeleweka japo Mara kadhaa pia mambo hufanyika na tusielewe kwanini...
Kimara walikua na mpango wa kupanua barabara hadi chalinze Ni jambo lililokuepo japo limechelewa kutokana n.a. kutokua na fedha...kwahyo ndio wamelifanya sasa japo limeleta vilio sana kwa walioathirika japo kuna baadhi walishalipwa fedha za fidia. ..

Kuna nyumba 17000 zilikua zivunjwe bonde la mto msimbazi na aliagiza zisivunjwe kwahyo ilo lililotokea uko kwao nadhani linafanana na la msimbazi...

Ukabila uku kwetu hauna nafasi japo yapo makabila ambayo hua ni kama yanaangaliwa sana kutokana na kujipenyeza katika kila idara Yaani yamekua chachu kwa makabila mengine...
 
3

3rd man

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2017
Messages
699
Likes
302
Points
80
3

3rd man

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2017
699 302 80
babake ni jaluo,aliitwa mzee awiti
Hivi kawaida mtu anachukua kabila la baba yake au mama yake?, Magufuli mama yake ndiyo msukuma, ila baba yake sio msukuma, japo alikufa akimuacha magufuli akilelewa na mama yake
 
Ndumbayeye

Ndumbayeye

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2009
Messages
5,878
Likes
1,835
Points
280
Ndumbayeye

Ndumbayeye

JF-Expert Member
Joined Jan 31, 2009
5,878 1,835 280
kwani huko kenya hakuna vikabila vidogo mkavipa urais? sisi huku Julius hakutaka makabila makubwa yatawale nchi hii, tumekeuka tunakoma sasa!
 
joto la jiwe

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Messages
7,432
Likes
7,116
Points
280
joto la jiwe

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2017
7,432 7,116 280
Kaka andaa mada zinazuhusu nchi yako utaendeleza kitu ama kwenye jamii yako au nchi kiujumla.
Najua hutaelewa ushaur wangu ila think about it.
Achana na ya Tanzania kurafuta popularity mtandaoni.

Nakuona mwandishi mzuri jaribu kuandaa makala za ufugaji bora, ukulima wa tija, uvunaji wa maji ya mvua na kuyatumia katika uzalishaji, nk.
Kisha nenda kijijin ulipozaliwa wagawie hizo nakala bure.....Utaacha alama chanya duniani.
Kwanini na wewe usifungue ofisi ya kutoa ushauri ili uwasaidie wengi wenye kuhitaji ushauri wa maendeleo kama huu?, pia utatengeneza pesa kuliko hivi unavyofanya, ni kama kulazimisha kumshauri mtu ambaye hana uhitaji wa ushauri wako, utapoteza nguvu zako bure, sisi tulioko huku karibu wengi kama sio wetu tunashughuli zetu, tupo hapa kama kijiweni kupiga story, na kupumzisha bongo zetu baada ya majukumu, usiturudishe kwenye fikra ngumu za uchumi, utatukimbiza wengi.
 
MK254

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Messages
12,017
Likes
10,010
Points
280
MK254

MK254

JF-Expert Member
Joined May 11, 2013
12,017 10,010 280
kwani huko kenya hakuna vikabila vidogo mkavipa urais? sisi huku Julius hakutaka makabila makubwa yatawale nchi hii, tumekeuka tunakoma sasa!
Ukabila haumalizwi kisa umempa uongozi nchi mtu wa kabila ndogo, Kenya nimeona ukabila hata kwa kabila ndogo, na ikumbukwe ukabila ulianza Kenya hata kabla hatujapata uhuru wa nchi. Wazungu waliutumia kutugawa maana tayari walikua wamenyakua mashamba na raslimali nyingi, hivyo walijaribu kila mbinu za kugawa mababu zetu kwa misingi ya ukabila.

Wakati wanampokeaza rais wa kwanza, tayari kulikua na migawanyiko ya kikabila, ila tatizo naye hakutaka kutumia hiyo fursa kujenga utangamano, walianza kulumbana na makamu wake Jaramogi ambaye naye alikua kama mfalme wa kabila lake la Wajaluo. Sasa ili kujilinda dhidi ya Odinga, Kenyatta naye akakusanya Wakikuyu na kuwaweka mkao wa umoja wa kikabila. Nchi kuanzia hapo haijapona tena, makabila madogo yakaiga tena hayo madogo madogo yamekua balaa.

Wazungu walikua tayari kuachia Tanganyika na hawakua na sababu za kuwagawa, hivyo Nyerere alipokea uongozi kwenye nchi ambayo tayari watu wake walikua wamoja, na kuanzia hapo naye akaendeleza huo umoja hadi leo.
 
Sio kweli hata kidogo kuhusu Tanganyika, umesema vizuri sana kuhusu Kenya, ila kuhusu Tanganyika hujasema ukweli, hali ilivyokua Kenya kabla ya uhuru ndivyo ilivyokuwa Tanganyika, tulikuwa na ukabila wa hali ya juu sana kabla ya hata kuja kwa wakoloni, tulikua chini ya machifu mbalimbali na vita vya ukabila vilikuwa vingi sana, wahehe chini ya Mkwawa walipigana karibu na makabila mengi sana na akayashinda na kuyateka, chifu chabruma, huko Bukoba walikuwa na Rumanyika, wachaga walikua na machifu wengi tu, Tanga kulikuwa na Kimweri, wakoloni walipofika, kwa mfano waarabu, kwa sababu walikuwa wanataka watumwa, walimfanya Mkwawa kuwa rafiki yao na kwa sababu alikua na nguvu sana walimuogopa, wakamdanganya, wakamsilimisha na akawa anawasaidia kupiga makabila mengine na kukamata watu watumwa

Baada ya waarabu, wajerumani walipokuja, waliendeleza tabia hiyo ya divide and rule kwa misingi ya kikabila, baada ya vita kuu ya pili, muingereza aliichukua hii nchi ikiwa na ukabila kama Kenya, na yeye aliupalilia tena sana, kwa mfano, wachaga walikuwa na machifu wengi, yeye akasema hataki kuzungumza na machifu hao kwa sababu hawana elimu, akamteua chifu mkuu wa wachago wote, anayeitwa Mariale, na alimtumia sana huyu Mariale kupinga juhudi za Nyerere za kudai Uhuru wa Tanganyika, nyerere akienda UNO kudai uhuru, na yeyey anapelekwa na muingereza kwenda kupingana na yale anayosema Nyerere, akisema kwamba Tanganyika haijawa tayari kujitawala kutokana na kuwa na makabila mengi yanayotofautiana sana, pia haijawa na uwezo hata wa kutengeneza sindano.

Baada ya Nyerere kuishawishi UNO na kukubaliana na hoja zake na kumpa Uhuru, jambo la kwanza alilolifanya nyerere ni kufuta cheo cha machifu Tanganyika nzima, kwa sababu ndiyo kitu alichosumbuka nacho sana huko UNO kwa sababu mangi Marialle alitumia kama sababu kubwa ya kutaka Tanganyika isipewe Uhuru.

Pia Nyerere alijua bila kujenga utaifa kwanza, nchi haiweza kwenda mbele, alitumia muda, fedha na nguvu za ziada katika miaka yake yote ya uongozi kupambana na ukabila, ikiwemo kukifanya Kiswahili kieleweke nchi nzima, kilikuwa ni lugha ya pwani tu kama huko Kenya, hakuikuta Tanzania haina ukabila, ilikuwa sawa na Kenya, Rwanda, Uganda na nchi zingine za Afrika, ila alifanya kazi ya ziada kuiweka nchi hapa ilipo hivi sasa, usione nchi imetulia ukadhani ni kwa kudra za Mungu, hapana.
 
Nayaheshimu maoni yako, lakini nimekutana na Watanzania wazee walioishi miaka hiyo ya Nyerere na ambao husema kwamba wakati anatokea Butiama, tayari Watanganyika walikua wamoja. Hawakatai kwamba hakuwa wa msaada kwenye kupigana na ukabila, na alichangia pakubwa, lakini alikuta tayari watu wanaishi kwa ushirikiano.

Mgawanyiko na vurugu za baina ya makabila ni jambo la zamani sana kwenye Afrika yetu hii, lakini mimi naongea kuhusu mambo ya hapo kabla na baada ya uhuru. Inawezekana siijui sana historia ya Tanzania, lakini kuna baadhi ya Watanzania ambao hudiriki kuandika mambo mengi kinyume na jinsi wengi wenu huwa mumeamini au kutaka kuaminisha, hebu soma hapa Nyerere Hakuendeleza Kiswahili, Bali Magufuli Ndiye Anakiendeleza Kiswahili..!!!!
 
Toyota escudo

Toyota escudo

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
2,541
Likes
1,756
Points
280
Toyota escudo

Toyota escudo

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
2,541 1,756 280
Kawaida huwa sikubaliani na mambo mengi ya Watanzania, mojawapo huwa unafiki wao wa kujifanya wastaarabu huku wakielekeza vidole vya kila aina ya lawama dhdi ya Wakenya, ilhali wao nimeishi nao na kuona walivyo na maovu ya kila aina.

Lakini juzi kuna tukio moja limetendeka kwao na nikaona kwa hilo wametupiga bao sana na wapo vizuri. Kwa mara ya kwanza nilitamani sana Kenya iwe kama Tanzania kwa hili la kuishi bila ukabila japo kwao upo kwa hali ya chini.
Kuna zoezi la ubomoaji wa majengo yaliyojengwa kwenye hifadhi za barabara, zoezi hili limeendelezwa bila huruma wala kujali nani au nini. Nimepitia sehemu inaitwa Kimara na kuona jinsi Magufuli ameamua harudi nyuma na aki nani huyu mzee hajaribiwi aisei, mafisadi wanatamani kuihama nchi ya Tanzania.

Sasa tatizo au kama Waswahili wasemavyo, kitumbua kikaingia mchanga pale ambapo ubomoaji huu ulifikia kwa makazi ya kabila lake kule Mwanza maana yeye hujiita Msukuma, akatangaza kwamba wale wasibomoeshwe na kuwa wanaobomoa waonyeshe human face au ubinadamu wakiwa huko Mwanza na kwamba watu wa kule walimpa kura nyingi.

Kitu nilichokiona ambacho nimetamani Kenya kuiga ni pale Watanzania walijitokeza kwenye mitandao na kulaani huo upendeleo wa kikabila. Yaani wamelaani kwa nguvu nyingi sana na kumkatalia kwa hiyo kauli, japo kuna wale die hard wa CCM huku mitandaoni walimsifia na kukubaliana naye bila aibu, hao wanaeleweka maana wanalipwa, huwa tunawaona hata kwenye nyuzi za habari za Kenya, wanatumia nguvu nyingi kushinda mitandaoni wakiponda kila chochote cha Kenya, siku hizi huwa nawapuuza maana wapo kikazi zaidi.

Jameni kwenye vita dhidi ya ukabila tuwaige Watanzania, pale rais au hata kiongozi wa upinzani anaonyesha upendeleo wowote wa kikabila, tuwe tunajitokeza na kumkatalia kwa nguvu nyingi ili tudumishe utangamano. Nina uhakika tunweza na inawezekana, Wakenya wengi tunaishi kwa amani na bila ukabila, lakini wanasiasa hutumia huko kutugawa kama mtaji wao. Leo hii rais Uhuru na naibu wake Ruto wakimteua mtu fulani kwa kigezo cha ukabila, wengi hatukemei, tunaishia kukumbatia huo uteuzi, vile vile tuliona kipindi Raila akiwa waziri mkuu alivyojaza watu wa kabila lake na ndugu kwenye ofisi ya uwaziri mkuu.

Vita dhidi ya ukabila vianze kwetu sisi huku mashinani, nina uhakika viongozi wataishia kutuunga mikono, lakini kama tukiishi kuwasubiri hao waje na sera zozote, watakua wanatutumia kama mtaji.
Ndugu yangu, kwanza hongera kwa kuliona hili la ukabila ambalo limeonekana kuwagawa hapo Kenya kwa mambo mengi.

Ni kweli, kuhusu kauli ya rais wetu haikuwa nzuri hata kidogo na nilitegemea wasaidizi wake watakuja kutoa ufafanuzi kuhusu kauli ile lakini hawakufanya hivyo. Binafsi naendelea kuilaani kauli ile na tabia ya kuongea lugha za asili huku akijua kuwa kila anapoongea yeye anaongea na taifa na si watu wachache waliokusanyika alipo.

Kwa upande wa Kenya, bado kuna kazi kubwa ya kufanya kuondoa elements za ukabila. Mwanzoni nilifikiri kuwa labda wakikuyu na wajaluo wakiungana kisiasa ukabila unaweza kuisha maana makabila haya mawili ndo sumbufu (japo na mengine yako hivyo ila hawa ndo vinara na chanzo).

Lakini matazamio yangu haya hayakuzaa matunda baada ya kuona mwaka 2002 odinga akiungana na mwai kibaki kuiondoa KANU madarakani kupitia muungano wa NARC. Muungano huu haukudumu sana nadhani ni kwa sababu ya maslahi na hivyo dhana ya hii ya kuunganisha makabila pia ikakosa mashiko.

Lakini ukiangalia vizuri, pamoja na rough za mzee kenyata dhidi ya Oginga Oginga ambazo pia zilileta ukabila zaidi, Hapo Kenya mfumo wa KIBEPARI ambao mlienda nao baada ya uhuru (japo una faida nyingine kiuchumi) haukuwaacha salama.

Mfumo huu wa ubepari kwa sababu unamfundisha kufanya mambo yake yeye kama yeye, na pengine kwa kushirikiana na watu wake wa karibu, ulikuwa chachu kubwa sana kueneza ukabila.

Wakikuyu ambao ni wafanyabiashara walianza kuiona wao ni bora zaidi kuliko wengine, hivyo utengano ukaendelea!

Hapa Tanzania mfumo wa ujamaa pamoja na hasara zake lukuki, umetusaidia sana kuondoa ukabila maana kwenye ujamaa kila mtu ni ndugu. Plus kitendo cha nyerere kufuta rasmi habari za chiefdoms, kuzuia redio na tv zote kutangaza kwa lugha za asili, kuhamisha watu wa eneo moja kwenda kuishi eneo jingine lenye rutuba na kuhimiza kiswahili pekee kitumike kama lugha ya mawasiliano, kulisaidia kuondoa dhana hiyo.
 
joto la jiwe

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Messages
7,432
Likes
7,116
Points
280
joto la jiwe

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2017
7,432 7,116 280
Nayaheshimu maoni yako, lakini nimekutana na Watanzania wazee walioishi miaka hiyo ya Nyerere na ambao husema kwamba wakati anatokea Butiama, tayari Watanganyika walikua wamoja. Hawakatai kwamba hakuwa wa msaada kwenye kupigana na ukabila, na alichangia pakubwa, lakini alikuta tayari watu wanaishi kwa ushirikiano.

Mgawanyiko na vurugu za baina ya makabila ni jambo la zamani sana kwenye Afrika yetu hii, lakini mimi naongea kuhusu mambo ya hapo kabla na baada ya uhuru. Inawezekana siijui sana historia ya Tanzania, lakini kuna baadhi ya Watanzania ambao hudiriki kuandika mambo mengi kinyume na jinsi wengi wenu huwa mumeamini au kutaka kuaminisha, hebu soma hapa Nyerere Hakuendeleza Kiswahili, Bali Magufuli Ndiye Anakiendeleza Kiswahili..!!!!
Nyerere amechangia pakubwa ukuaji wa Kiswahili duniani:Balozi Macharia | Idhaa ya Redio ya UM

Huwa wakati mwengine ninashindwa kukuelewa kwa jinsi unavyojenga hoja zako, Magufuli anatumia zaidi Kiswahili katika dhifa mbalimbali za Taifa kuliko Nyerere alibyokua akifanya, lakini a
iyekikuza Kiswahili duniani kote, wala sio Tanzania tu au east Afrika, hakuna anayemzidi Nyerere, ushahidi ni huo hapo niliokuwekea, hiyo ni UN inasema hivyo.

Tanganyika wakati tunapata Uhuru, lugha rasmi ya serikali ilikuwa ni kiingereza kama ilivyokuwa Kenya, aliyekifanya Kiswahili kuwa Lugha ya taifa ni nyerere, na alienda mbali zaidi akaamua hata masomo yote ya shule za msingi yawe yanafundishwa kwa Kiswahili, ndiyo sababu hata huyo Magufuli, asingekijua Kiswahili kama Nyerere asingebadili mitaala ya shule za msingi kuwa ya kiswahili, sisi wote tulikuwa tunazungumza lugha za makabila yetu, kiswahili kilikua ni rasha rasha tu kama kilivyo huko Kenya, tulipoanza shule ndiko kulikotufanya tuanze kuchanganya kiswahili.

Nyerere alipata misukosuko sana tuka ndani ya nchi na toka kwa wafadhili, pale alipochukua uamuzi wa kukifuta kiingereza katika shule za msingi, nchi ya kwanza kuzuia misaada ktk nyanja ya elimu ni Uingereza, hawakupendezwa na hatua hiyo hata kidogo, lakini alisimamia maamuzi yake hadi leo hii utaona karibu watanzania wote wanazungumza kiswahili cha aina moja, tofauti ni lafudhi tu, hii ni kwasababu, kiswahili kilikuwa standardized na kikafundishwa nchi nzima, ndiyo sababu nilikuambia Nyerere alitumia resources, muda na nguvu nyingi sana kukiweka Kiswahili hapa kilipo leo

Ni juhudi za Nyerere kupigania Lugha ya Kiswahili iwe ni miongoni mwa Lugha rasmi ya OAU, alianzisha vuguvugu hilo kwa kumtumia Salum Ahmed Salum, ambaye alitumikia umoja huo kama katibu mkuu kwa miaka 12 wakati Nyerere ni rais, na akisaidiwa na Samora Machelle, aliyekuwa rais wa Msumbiji kwa sababu yeye alikulia Tanzania wakati wa vita vya kuikomboa Msumbiji kwa hiyo alikuwa akizungumza kiswahili vizuri sana

Nyerere alikuwa akikipenda sana kiswahili, kiasi kwamba aliomba serikali ya Uingereza imruhusu kutafsiri vitabu vya muandishi Nguli wa Uingereza ,Shake Speer na aliruhusiwa na akaitafsiri riwaya ya mwandishi huyo kwa Kiswahili huku akiwa madarakani, kazi za Nyerere katika kukikuza kiswahili hapa duniani, hakuna mtu yeyote unaweza kumlinganisha na Nyerere, wewe google utajionea mwenyewe
 
Aliyoyatetea Mwalimu Nyerere yako dhahiri hadi sasa: Jamaica | Idhaa ya Redio ya UM
 
CHARMILTON

CHARMILTON

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2015
Messages
6,319
Likes
8,939
Points
280
CHARMILTON

CHARMILTON

JF-Expert Member
Joined May 30, 2015
6,319 8,939 280
Huu uzi una maana mbili.
 
ArD67

ArD67

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2016
Messages
2,805
Likes
1,949
Points
280
Age
36
ArD67

ArD67

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2016
2,805 1,949 280
Nimeupitia karibu uzi wote na michango yote, mleta uzi ameleta uzi wa msingi sana tena si kwa nchi yake tu bali hata kwetu, Nyerere alisema ukabila ni moja ya nyufa zinazoweza kulibomoa taifa letu... Na bado hadi leo huu ni ufa.

Ukitazama wengi waliokosoa hili kwa Tz, si kwamba ni kweli limewagusa ktk mantiki yake bali labda ni kwakuwa aliyezungumza yuko kinyume nao tu,,,,, sijasema ndivyo ilivyo lakini linawezekana haswa kwakuwa wengine wameliunga mkono,, nao wapo upande wake wala si kwamba hawajui madhara ya ukabila.

Ukabila si kuongea lugha ya kabila lako, bali unalichukuliaje kabila ukiyalinganisha na mengine? Nadhani hata Kikwete na Nyerere wakiwa ktk maeneo ya kwao walichomekea maneno ya kilugha chao. Sio shida, ila ukabila lazima ukemewe bila kujali anayeuleta yuko upande gani nawe.

Ukabila kwa zama hizi za kimuungiliano was kiuchumi, kisiasa na kijamii hauna tija tena. Hakuna kabila la wafugaji wala wakulima wala wafanyabiashara, yeyote popote akiona hilo ni fursa atalifanya tu, kwahiyo Masai anaweza kushirikiana na mhehe ktk ufugaji hata zaidi na mmsai mwenzake.

Mleta mada ameona kitu, si vibaya kujifunza lililo bora toka kwa jirani wako. Kuhusu kuwapa nafasi Kabila dogo, hii si njia ya kuibeza hata kidogo. Kenya Ukabila hautafutika hadi pale kabila dogo litakapoungwa mkono na makabila makubwa kuchukua nchi, hii ni njia bora kabisa. Msitarajie kuuondoa Ukabila wakati kuna wengine wanahisi kutengwa ktk nyanja fulanifulani, hata wawe na uchumi mzuri kiasi gani, dhana ya kutegwa tu itawasumbua, eg Libya.

Hamjachelewa, anzisheni vuguvugu hilo na kizazi cha kesho kitakuwa bora zaidi ya hiki.
 
MK254

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Messages
12,017
Likes
10,010
Points
280
MK254

MK254

JF-Expert Member
Joined May 11, 2013
12,017 10,010 280
Nyerere amechangia pakubwa ukuaji wa Kiswahili duniani:Balozi Macharia | Idhaa ya Redio ya UM

Huwa wakati mwengine ninashindwa kukuelewa kwa jinsi unavyojenga hoja zako, Magufuli anatumia zaidi Kiswahili katika dhifa mbalimbali za Taifa kuliko Nyerere alibyokua akifanya, lakini a
iyekikuza Kiswahili duniani kote, wala sio Tanzania tu au east Afrika, hakuna anayemzidi Nyerere, ushahidi ni huo hapo niliokuwekea, hiyo ni UN inasema hivyo.

Tanganyika wakati tunapata Uhuru, lugha rasmi ya serikali ilikuwa ni kiingereza kama ilivyokuwa Kenya, aliyekifanya Kiswahili kuwa Lugha ya taifa ni nyerere, na alienda mbali zaidi akaamua hata masomo yote ya shule za msingi yawe yanafundishwa kwa Kiswahili, ndiyo sababu hata huyo Magufuli, asingekijua Kiswahili kama Nyerere asingebadili mitaala ya shule za msingi kuwa ya kiswahili, sisi wote tulikuwa tunazungumza lugha za makabila yetu, kiswahili kilikua ni rasha rasha tu kama kilivyo huko Kenya, tulipoanza shule ndiko kulikotufanya tuanze kuchanganya kiswahili.

Nyerere alipata misukosuko sana tuka ndani ya nchi na toka kwa wafadhili, pale alipochukua uamuzi wa kukifuta kiingereza katika shule za msingi, nchi ya kwanza kuzuia misaada ktk nyanja ya elimu ni Uingereza, hawakupendezwa na hatua hiyo hata kidogo, lakini alisimamia maamuzi yake hadi leo hii utaona karibu watanzania wote wanazungumza kiswahili cha aina moja, tofauti ni lafudhi tu, hii ni kwasababu, kiswahili kilikuwa standardized na kikafundishwa nchi nzima, ndiyo sababu nilikuambia Nyerere alitumia resources, muda na nguvu nyingi sana kukiweka Kiswahili hapa kilipo leo

Ni juhudi za Nyerere kupigania Lugha ya Kiswahili iwe ni miongoni mwa Lugha rasmi ya OAU, alianzisha vuguvugu hilo kwa kumtumia Salum Ahmed Salum, ambaye alitumikia umoja huo kama katibu mkuu kwa miaka 12 wakati Nyerere ni rais, na akisaidiwa na Samora Machelle, aliyekuwa rais wa Msumbiji kwa sababu yeye alikulia Tanzania wakati wa vita vya kuikomboa Msumbiji kwa hiyo alikuwa akizungumza kiswahili vizuri sana

Nyerere alikuwa akikipenda sana kiswahili, kiasi kwamba aliomba serikali ya Uingereza imruhusu kutafsiri vitabu vya muandishi Nguli wa Uingereza ,Shake Speer na aliruhusiwa na akaitafsiri riwaya ya mwandishi huyo kwa Kiswahili huku akiwa madarakani, kazi za Nyerere katika kukikuza kiswahili hapa duniani, hakuna mtu yeyote unaweza kumlinganisha na Nyerere, wewe google utajionea mwenyewe
Tatizo kubwa huwa nakua nalo kwa Watanzania, hampendi kusoma, yaani unakurupuka kujibu hoja bila kusoma. Mimi nimekuletea hiyo blog nikitegemea utasoma hadi mwisho, wewe umesoma paragraph moja ukakimbilia kujibu.
Tumia muda wako uisome yote, baada ya hapo ujibu kwa hoja ili kupangua hoja za huyo mwandishi.
 
joto la jiwe

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2017
Messages
7,432
Likes
7,116
Points
280
joto la jiwe

joto la jiwe

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2017
7,432 7,116 280
Tatizo kubwa huwa nakua nalo kwa Watanzania, hampendi kusoma, yaani unakurupuka kujibu hoja bila kusoma. Mimi nimekuletea hiyo blog nikitegemea utasoma hadi mwisho, wewe umesoma paragraph moja ukakimbilia kujibu.
Tumia muda wako uisome yote, baada ya hapo ujibu kwa hoja ili kupangua hoja za huyo mwandishi.
Wewe ulibadilisha mada juu kwa juu sasa unalalamika nini?, mada ilikuwa ukabila Tanzania ambapo ulisema mkoloni hakutugawa kikabila kama alivyowagawa Kenya, mimi nikakanusha na kukueleza kwamba Nyerere ndiye aliyefuta ukabila kwa kutumia muda na resources nyingi, lugha ya Kiswahili ikiwa ni moja wapo, sasa wewe unakurupuka kuonyesha kwamba Nyerere hajakiendeleza Kiswahili, kwani mada ilikuwa ni nani aliyekiendeleza kiswahili?
 
MK254

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Messages
12,017
Likes
10,010
Points
280
MK254

MK254

JF-Expert Member
Joined May 11, 2013
12,017 10,010 280
Wewe ulibadilisha mada juu kwa juu sasa unalalamika nini?, mada ilikuwa ukabila Tanzania ambapo ulisema mkoloni hakutugawa kikabila kama alivyowagawa Kenya, mimi nikakanusha na kukueleza kwamba Nyerere ndiye aliyefuta ukabila kwa kutumia muda na resources nyingi, lugha ya Kiswahili ikiwa ni moja wapo, sasa wewe unakurupuka kuonyesha kwamba Nyerere hajakiendeleza Kiswahili, kwani mada ilikuwa ni nani aliyekiendeleza kiswahili?
Ndio maana nikakuomba usome hiyo blog yote, wacha kuwa mvivu wa kusoma. Kiswahili kimetajwa tu kama mojawapo wa issue hapo, lakini kama ukiacha uvivu usome yote, utaona sababu za mimi kukutuma huko nikiwa na nia ya kuipa uzito hoja yangu ya jinsi Tanzania haikua imegawanyika kikabila wakati Nyerere anachukua uongozi.

Mkoloni hakua na nia ya kuing'ang'ania Tanzania, hivyo hakua na sababu za kuwagawa au kuwapiganisha kama alivyofanya Kenya. Nyerere aliwakuta Watanganyika tayari wameungana na kuwa kitu kimoja, mzungu alikua tayari amewaunganisha, pia alikuta Kiswahili kimesambaa, lakini pia mchango wake unatambulika kwenye kudumisha huo umoja wa Watanganyika na kukuza Kiswahili na kuhakikisha kinatumika kote kote na mashuleni.
 
Forum statistics

Threads 1,237,857
Members 475,675
Posts 29,303,701