joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Kwa jinsi watanzania karibu wote humu JF wanavyopinga hoja yako, ni dalili tosha kwamba yale yote niliyokueleza kuhusu ukabila Tanzania na jinsi Nyerere alivyoufutilia mbali ni sahihi, sasa kwa kukusaidia zaidi, ukitaka kuifahamu Tanzania vizuri sana, jaribu kujiuliza maswali yafuatayoMimi simtetei Jommo Kenyatta, tena ukinichunguza sana huwa napenda mambo yawekwe bayana ili kama taifa tujue wapi tulianza kunyeshewa na mvua, huwa ninadiriki kufuata historia nje ya mambo tuliyoaminishwa kwenye vitabu tangu enzi zile. Wewe hapo ndiye mwenye matatizo kwamba hutaki mawazo nje ya kile mwalimu wa shule alikufundisha, maana nimekupeleka kwenye blog ya Mtanzania ambaye ameandika kwa kina mambo mengi kuihusu nchi yako, wewe umeingia uvivu wa kusoma na kuona heri unin'gan'ganizie badala ya kupangua hoja za huyo Mtanzania.
1)Tanzania, kama zilivyo nchi zengine zote za ukanda huu, ukabila ulikuwepo hata kabla ya kuja kw wakoloni, je nani aliwaunganisha watanzania na kumaliza ukabila?, waarabu, mjerumani, waingereza, Nyerere, au wananchi wenyewe tu walijikuta wanakuwa kitu kimoja automatically?
2)Kiswahili kilizaliwa katika pwani ya Afrika mashariki, je ilikuwaje kiswahili kienee na kupenya kwa kasi huku Tanzania lakini kisiweze kupenya huko Kenya, ni nani hasa aliyekieneza Tanzania na asifanye hivyo huko Kenya, au Mungu anaipendelea zaidi Tanzania kuliko Kenya kwa kueneza kiswahili Tanzania ambayo ilikuwa ni silaha muhimu kufuta ukabila?
3)Kama hoja yako ya kwamba mkoloni hasa wa uingereza hakuona umuhimu wa kutugawa, lakini kumbuka alitukuta tumeshagawanyika kutokea enzi za mababu zetu, je nani alituunganisha kama muingereza hakuona umuhimu wa kutugawa zaidi?
4)Kwanini Rwanda na Burundi ambao pia waliwekwa chini ya uangalizi wa Belgium, ambaye hakuona sababu ya kuwagawa kama Tanzania, kwanini wanaendelea na ukabila wao uleule wa kabla ya kuja kwa wakoloni?