Ukweli mchungu: Watanzania wengi wanaoishi / kusoma ulaya na Marekani hawapeani kampani, Wakenya ndio kimbilio la watanzania wengi ughaibuni

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Hali halisi ndivyo ilivyo, wala sijui ni nini kinachoendelea huko ulaya na Marekani lakini watanzania wengi wanakwepana, hata kama wanaishi mji moja ni nadra sana ku mingle, kutembeleana, kujuliana hali na kutengeneza long term relationships, kuwa pamoja labda itokee mtz kafariki ndio watachanga arudi azikwe.

Watanzania wengi hujikuta wapo karibu zaidi ya wakenya wawapo huko ughaibuni, ni fact kabisa hata kwa wanafunzi wanaoenda masomoni huko ulaya ukiwauliza watakwambia haya kuanzia kushare rooms, kuishi pamoja, watu wa karibu, n.k. huwa wanatafuta kampani za kikenya,

Na cha ajabu ni kwamba lile bifu letu vuguvugu la Tz vs Kenya nahisi wenzetu huwa wanalichukulia kama utani tu sio serious sana kama watz wanavyowashambulia wakenya kwenye jukwaaa la wakenya humuhumu jamiiforums, ingekuwa vinginevyo basi watanzania wangepata shida sana huko Ughaibuni, Watz kwa watz wanakwepana, nae mkenya angekuwa anawakataa watz huko ughaibuni pangekalika ?

Comments kutoka kwa wadau :

Watanzania tuna umoja ndani ya nchi ila nje tunakwepana kila mtu kimpango wake, Wakenya wana ukabila ndani ya nchi yao lakini wakiwa nje ni kabila moja.

Wakenya are proud of their nation nje ya mipaka, Watanzania wanauponda sana utanzania na wanaona kwenda nje ndo njia ya kujivua utanzania
 
Hii kitu inawezekana ni kweli. Maana hata huku ground tu kusaidiana ni ngumu kweli nawaza walioko huko ughaibuni wanaishije
 
Fanya tena uchunguzi wako halafu uje tena. Na safari hii njoo na sababu zinazopelekea hali kuwa hivyo.
Hii kitu inawezekana ni kweli. Maana hata huku ground tu kusaidiana ni ngumu kweli nawaza walioko huko ughaibuni wanaishije
Watanzania tuna umoja ndani ya nchi ila nje tunakwepana kila mtu kimpango wake

Wakenya wana ukabila ndani ya nchi yao lakini wakiwa nje ni kabila moja.
 
Wakenya wanautaifa sana and they are proud of their nation. Watanzania wanauponda sana utanzania na wanaona kwenda nje ndo njia ya kujivua utanzania kiaina. Na ndo maana hawataki kuskia mambo za umoja wao. Ila wa TZ walioko Australia naona wanajitahidi sana kwa umoja
 
Watanzania tuna umoja ndani ya nchi ila nje tunakwepana kila mtu kimpango wake

Wakenya wana ukabila ndani ya nchi yao lakini wakiwa nje ni kabila moja.

Binafsi mimi uzoefu wangu uko tofauti na wa kwako. Nimeshuhudia haomajirani wakisemana vibaya.
Ila Wamalawi ni wapole sana.
 
Ulipozungumzia wamalawi nahisi ni mazingira ya Bondeni sauzi maana huko wamejaa, wanasifika kwa upole ila sometimes inawa cost sana kuwa wanyonge kupambania haki zao.

Eneo kama sauzi mishe nyingi ni nyeusi wengi wanaoenda huko wameshindikana hata nchi zao, hata watz kibao wanauza unga na kukaba, wakenya walioshindikana huko kwao nao huwezi wakosa.
 
Nonsensical. Haya madai siku zote yanatolewa na wamatumbi waliopo bongo ambao hawajui hata airport ipo wapi.

Tumeishi nje na wabongo wenzetu kwa amani na upendo. Tumeshirikiana kwenye kila nyanja inayohitaji ushirikiano. Hizi habari huwa mnatoa wapi?

Ushirikiano ni jambo la hiari, kuna mtu hataki kushirikiana na wabongo wenzake utamlazimisha? Kama yeye ana prefer wakenya hiyo ni preference yake can't fault wabongo wengine for that. And there's nothing wrong with that.

Ushirikiano pia una mipaka yake, kama unakuja na mentality za kusaidiwa kila kitu yani kuwa mzigo tunakunawa mchana kweupe. Kila mtu ana majukumu yake. Kama unahitaji ushirikiano wakati unajitafuta utasaidiwa ile uwe unabebeka. Ukija na tabia zako toka kwenu Chitipa watu wanapita hivi.

Jisaidie usaidiwe. Msaada ni hisani sio lazima. Keep that in your mind.
 
Ulipozungumzia wamalawi nahisi ni mazingira ya Bondeni sauzi maana huko wamejaa, wanasifika kwa upole ila sometimes inawa cost sana kuwa wanyonge kupambania haki zao.

Eneo kama sauzi mishe nyingi ni nyeusi wengi wanaoenda huko wameshindikana hata nchi zao, hata watz kibao wanauza unga na kukaba, wakenya walioshindikana huko kwao nao huwezi wakosa.

Sijawahi kuishi sauz, zaidi ya kutembelea. Nazungumzia kwa maeneo ya ulaya na marekani.
 
Hali halisi ndivyo ilivyo, wala sijui ni nini kinachoendelea huko ulaya na Marekani lakini watanzania wengi wanakwepana, hata kama wanaishi mji moja ni nadra sana ku mingle, kutembeleana, kujuliana hali na kutengeneza long term relationships, kuwa pamoja labda itokee mtz kafariki ndio watachanga arudi azikwe.

Watanzania wengi hujikuta wapo karibu zaidi ya wakenya wawapo huko ughaibuni, ni fact kabisa hata kwa wanafunzi wanaoenda masomoni huko ulaya ukiwauliza watakwambia haya kuanzia kushare rooms, kuishi pamoja, watu wa karibu, n.k. huwa wanatafuta kampani za kikenya,

Na cha ajabu ni kwamba lile bifu letu vuguvugu la Tz vs Kenya nahisi wenzetu huwa wanalichukulia kama utani tu sio serious sana kama watz wanavyowashambulia wakenya kwenye jukwaaa la wakenya humuhumu jamiiforums, ingekuwa vinginevyo basi watanzania wangepata shida sana huko Ughaibuni, Watz kwa watz wanakwepana, nae mkenya angekuwa anawakataa watz huko ughaibuni pangekalika ?

Comments kutoka kwa wadau :

Watanzania tuna umoja ndani ya nchi ila nje tunakwepana kila mtu kimpango wake, Wakenya wana ukabila ndani ya nchi yao lakini wakiwa nje ni kabila moja.

Wakenya are proud of their nation nje ya mipaka, Watanzania wanauponda sana utanzania na wanaona kwenda nje ndo njia ya kujivua utanzania
Wewe umeishi Ulaya ipi au USA ipi ukapata hili hitimisho? Ulaya nilioishi mimi ni kinyume na usemacho.
Kama alivyosema Bufa mambo kama haya huwa wanasema wamatumbi ambao Ulaya au USA wanaisikia tu au waliokuja kwa seminar ya wiki moja.
 
Kabisa mkuu.
 
Lisemwalo lipo. Sijainteract na Tanzanian diaspora wengi, ila niliokutana nao wote walinidisappoint, wakenya wanasaidiana sana ila kuna namna watataka wakutumie to their advantage hasa ukiwa mgeni
 
You attract vile wewe ulivyo. Hata wewe unawadisappoint wao sababu wote mnaendana.
 
kuna stry flan watz pale london mazee ukishajitambulisha tu kwao tu mwezi hauiishii immigration mlangoni haoo
 
Back
Top Bottom