Kwa hili la vita dhidi ya ukabila, jameni tuwaige Watanzania

Kaka andaa mada zinazuhusu nchi yako utaendeleza kitu ama kwenye jamii yako au nchi kiujumla.
Najua hutaelewa ushaur wangu ila think about it.
Achana na ya Tanzania kurafuta popularity mtandaoni.

Nakuona mwandishi mzuri jaribu kuandaa makala za ufugaji bora, ukulima wa tija, uvunaji wa maji ya mvua na kuyatumia katika uzalishaji, nk.
Kisha nenda kijijin ulipozaliwa wagawie hizo nakala bure.....Utaacha alama chanya duniani.

Umaarufu upi ninaoutafuta wakati hatufahamiani, huu ni mtandao wa kijamii ambapo kila mmoja anakua na uhuru wa kuwasilisha dukuduku lake ili wadau wajadili na kuwekana sawa, ilmradi usivunje sheria za kimtandao aidha za Kenya au Tanzania au usivunje kanuni za Jamii Forums.
 
Ndio maana nikakuomba usome hiyo blog yote, wacha kuwa mvivu wa kusoma. Kiswahili kimetajwa tu kama mojawapo wa issue hapo, lakini kama ukiacha uvivu usome yote, utaona sababu za mimi kukutuma huko nikiwa na nia ya kuipa uzito hoja yangu ya jinsi Tanzania haikua imegawanyika kikabila wakati Nyerere anachukua uongozi.

Mkoloni hakua na nia ya kuing'ang'ania Tanzania, hivyo hakua na sababu za kuwagawa au kuwapiganisha kama alivyofanya Kenya. Nyerere aliwakuta Watanganyika tayari wameungana na kuwa kitu kimoja, mzungu alikua tayari amewaunganisha, pia alikuta Kiswahili kimesambaa, lakini pia mchango wake unatambulika kwenye kudumisha huo umoja wa Watanganyika na kukuza Kiswahili na kuhakikisha kinatumika kote kote na mashuleni.
Germany east Afrika ilikuwa ni Tanganyika, Burundi na Rwanda, baada ya vita ya dunia ya pili mjerumani aliposhindwa, Tanganyika iliwekwa chini ya Uingereza, Rwanda na Burundi ziliwekwa chini ya Ubelgiji, sasa kwanini Rwanda na Burundi ukabila umekuwepo kama sababu yako unayoitoa kwamba mkoloni hakuwa na sababu ya kutugawanya?, kwa sababu hata Rwanda na Burundi pia mkoloni hakuwa na sababu ya kuwagawanya kwasababu walijua wataondoka wakati wowote kama ilivyokuwa Tanzania?. hakuna mkoloni yeyote yule aliyependezwa na umoja wa anaowatawala, ona jinsi Raila na Uhuru wanavyowagawanya japo sio wakoloni.
 
Harafu upinzani ukiwa na top leaders hata wa wili tu kutoka mkoa mmoja wanaita ukabila,hivi unajua Tanzania hata kihistoria kuna makabila yalishindwa kusonga mbele japo yalikuwa yanamilkki utajiri kisa tu ya tabia zao za kukataa mageuzi ya wakati huo,mfano wachaga,wanyakyusa,wahaya wao walikubali kupokea elimu ya mkoloni wakiwa na plan Blakini msukuma na mnyamwezi waligomea elimu hii wakiamini ni ujinga leo katokea mjinga mwingine anajaribu kuwarudishia ujinga ambao awali baada ya kuona wenzao wanasongo wabadilike na kuwa kama wao kulingana na wingi wao kuleta matokeo chanya sasa anawarudisha katika ujinga ulio watia umasikini ili hali mali na utajiri umewazunguka!!huu ubaguzi hautatuacha salama
 
Ndio maana nikakuomba usome hiyo blog yote, wacha kuwa mvivu wa kusoma. Kiswahili kimetajwa tu kama mojawapo wa issue hapo, lakini kama ukiacha uvivu usome yote, utaona sababu za mimi kukutuma huko nikiwa na nia ya kuipa uzito hoja yangu ya jinsi Tanzania haikua imegawanyika kikabila wakati Nyerere anachukua uongozi.

Mkoloni hakua na nia ya kuing'ang'ania Tanzania, hivyo hakua na sababu za kuwagawa au kuwapiganisha kama alivyofanya Kenya. Nyerere aliwakuta Watanganyika tayari wameungana na kuwa kitu kimoja, mzungu alikua tayari amewaunganisha, pia alikuta Kiswahili kimesambaa, lakini pia mchango wake unatambulika kwenye kudumisha huo umoja wa Watanganyika na kukuza Kiswahili na kuhakikisha kinatumika kote kote na mashuleni.
Unajua usipende kuchukulia mambo kirahisi sana hasa yale yaliyokushinda, ukimuona mwenzako ameyafanikisha, badala ya kutoa sababu nyepesi ili kuhalalisha kusindwa kwako badala ya kujifunza ni vipi mwenzako alifanikiwa,sio busara hata kidogo.

Utasemaje Nyerere alikikuta Kiswahili kilishaenea Tanzania, nani aliyekieneza huku Tanzania na kwanini kisienee Kenya, Somalia au Msumbiji wakati Kiswahili kilikuwa ni lugha ya pwani ya afrika mashariki?

Kama ukabila ulikuwepo hata kabla ya kuja kwa wakoloni katika hizi nchi zetu, na mjerumani alitutawala kwa kanuni ya divide and rule kabla ya kuja muingereza, maana yake ni kwamba, muingereza alitukuta na ukabila wetu uleule wa asili kama ilivyokuwa Kenya, kwa hiyo ni muingereza ndiye aliyefanya kazi ya kutuweka pamoja?,
 
Ndio maana nikakuomba usome hiyo blog yote, wacha kuwa mvivu wa kusoma. Kiswahili kimetajwa tu kama mojawapo wa issue hapo, lakini kama ukiacha uvivu usome yote, utaona sababu za mimi kukutuma huko nikiwa na nia ya kuipa uzito hoja yangu ya jinsi Tanzania haikua imegawanyika kikabila wakati Nyerere anachukua uongozi.

Mkoloni hakua na nia ya kuing'ang'ania Tanzania, hivyo hakua na sababu za kuwagawa au kuwapiganisha kama alivyofanya Kenya. Nyerere aliwakuta Watanganyika tayari wameungana na kuwa kitu kimoja, mzungu alikua tayari amewaunganisha, pia alikuta Kiswahili kimesambaa, lakini pia mchango wake unatambulika kwenye kudumisha huo umoja wa Watanganyika na kukuza Kiswahili na kuhakikisha kinatumika kote kote na mashuleni.
Language Reform: How Nyerere killed tribalism

Huu ndiyo ukweli, sasa wewe endelea kujiliwaza na kumtetea Jommo Kenyatta kwa kushindwa kupambana na ukabila hapo Kenya, yeye aliona kujenga uchumi katika taifa changa kama la Kenya ambalo lilihitaji kulijengea misingi ya umoja kwanza, yeye alienda moja kwa moja kuanza na uchumi, matokeo yake ndiyo hayo, it is too late now.
 
Tatizo kubwa huwa nakua nalo kwa Watanzania, hampendi kusoma, yaani unakurupuka kujibu hoja bila kusoma. Mimi nimekuletea hiyo blog nikitegemea utasoma hadi mwisho, wewe umesoma paragraph moja ukakimbilia kujibu.
Tumia muda wako uisome yote, baada ya hapo ujibu kwa hoja ili kupangua hoja za huyo mwandishi.
Tatizo la huyo mwandishi wa hiyo blog uliyoweka ni kijana mdogo aliyezaliwa miaka kadhaa baada ya uhuru kwa hiyo anachosema ni kile alichosoma vitabuni. Kwa sisi tuliokuwepo tangu enzi za ukoloni hadi leo hii tunatambua juhudi za Mwl. Nyerere sio tu katika kukuza Kiswahili, bali katika kuwafanya watanzania kujiona ni watu wa taifa moja..
 
Ukabila haumalizwi kisa umempa uongozi nchi mtu wa kabila ndogo, Kenya nimeona ukabila hata kwa kabila ndogo, na ikumbukwe ukabila ulianza Kenya hata kabla hatujapata uhuru wa nchi. Wazungu waliutumia kutugawa maana tayari walikua wamenyakua mashamba na raslimali nyingi, hivyo walijaribu kila mbinu za kugawa mababu zetu kwa misingi ya ukabila.

Wakati wanampokeaza rais wa kwanza, tayari kulikua na migawanyiko ya kikabila, ila tatizo naye hakutaka kutumia hiyo fursa kujenga utangamano, walianza kulumbana na makamu wake Jaramogi ambaye naye alikua kama mfalme wa kabila lake la Wajaluo. Sasa ili kujilinda dhidi ya Odinga, Kenyatta naye akakusanya Wakikuyu na kuwaweka mkao wa umoja wa kikabila. Nchi kuanzia hapo haijapona tena, makabila madogo yakaiga tena hayo madogo madogo yamekua balaa.

Wazungu walikua tayari kuachia Tanganyika na hawakua na sababu za kuwagawa, hivyo Nyerere alipokea uongozi kwenye nchi ambayo tayari watu wake walikua wamoja, na kuanzia hapo naye akaendeleza huo umoja hadi leo.
Aiseee kwa Tanganyika umekosea alipokea taifa likiwa na ukabila sana kumbuka visa vya machifu wa kichaga na yule mwingine wa kule mbozi . sema jambo alilofanikiwa Mzee wetu ni kufanya ishu ya wafanyakaz kufanya Kaz sehemu ambayo hujazaliwa like mchaga alipelekwa kwenda kufanya Kaz jamii za wahaya au mhehe kwenda kuishi na kufanya Kaz kigoma na n.k lakin hakuishia hapo aliamua kujenga misingi ya umoja kwa kupitia shulen ambapo wanafunzi walikwenda kusoma mbali na kwao mfano watu walitoka Mbeya kwenda tabora au wa mwanza kwenda kibaha hivyo mtindo huo uliwajengea wanafunzi tokea wakiwa form 1 had 4 na 6 hali ya kujiona ni wamoja kwa kuunganishwa na umoja wao wa kuitwa utanzania na hivyo itikadi za ukabila na udini ziliweze kupunguzwa pa kubwa na hata walipo maliza vyuo vikuu kazi unapelekwa mbali na kwenu hivyo unajikuta huko unaweza kuoa au kuolewa lakin unajikuta huko ugenin ndiyo maisha yako we na familia yako unazoea hivyo kujiona nawe ni sehemu ya ile jamii. Lakin mwisho nyerere alikuwa mkali sana kuhusu viongozi wanaozungumzia au kuendekeza siasa za ukabila/udini na alijitahid Ku hakikisha makabila makubwa hayawezi kumeza makabila madogo .

Lakin jambo la mwisho japo hili watu wengi huwa hawasemi au ni wachache wenye ufahamu na hili

Baba wa Taifa hata maamuzi Yake ya kuamua kufuata mfumo wa socialism ( ujamaa) mbali na sababu zingine lakin lengo kuu alichagua siasa za aina kwa lengo la kuunganisha Taifa ambalo alikuwa anajua fika matatizo Yake kwenye udini na ukabila , na ujamaa nilikuwa ni aina ya siasa zenye kushawishi na kuendeleza umoja na undugu na kusadiana kama wana familia ni siasa ambazo kiukw zilisadia sana kuunganisha wananchi . ila tofaut na wakenya nyie waasisi wenu walichagua ubepari na mifumo yenu huko ni umimi zaid na sio umoja hivyo ile dhana ya umoja kwenu haipo
 
Acha uongo Mareale hajawahi kupinga Uhuru wa Tanganyika kitu kilichotokea ni Mwingereza ku-support uongozi wa Kichagga kwa kuona Mareale anafaa zaidi kutokana na utendaji wake chini ya serikali ya Mkoloni!
 
Nayaheshimu maoni yako, lakini nimekutana na Watanzania wazee walioishi miaka hiyo ya Nyerere na ambao husema kwamba wakati anatokea Butiama, tayari Watanganyika walikua wamoja. Hawakatai kwamba hakuwa wa msaada kwenye kupigana na ukabila, na alichangia pakubwa, lakini alikuta tayari watu wanaishi kwa ushirikiano.

Mgawanyiko na vurugu za baina ya makabila ni jambo la zamani sana kwenye Afrika yetu hii, lakini mimi naongea kuhusu mambo ya hapo kabla na baada ya uhuru. Inawezekana siijui sana historia ya Tanzania, lakini kuna baadhi ya Watanzania ambao hudiriki kuandika mambo mengi kinyume na jinsi wengi wenu huwa mumeamini au kutaka kuaminisha, hebu soma hapa Nyerere Hakuendeleza Kiswahili, Bali Magufuli Ndiye Anakiendeleza Kiswahili..!!!!
Mkuu sio kweli hii nchi ilikuwa na ukabila sana tunakwambia wazawa wa huku na kama alivyosema mdau hapo juu ni wengi wakimsumbua kisa huo ukabila hicho kisa cha mangi wa kichaga ni moja ya visa vingi vya ukabila walikuwepo machifu wengi waliosumbua .

Na kipind cha mkoloni yeye ndiyo ilikuwa fursa kuona sisi sio wamoja ili atutawale vizur
 
Tatizo la huyo mwandishi wa hiyo blog uliyoweka ni kijana mdogo aliyezaliwa miaka kadhaa baada ya uhuru kwa hiyo anachosema ni kile alichosoma vitabuni. Kwa sisi tuliokuwepo tangu enzi za ukoloni hadi leo hii tunatambua juhudi za Mwl. Nyerere sio tu katika kukuza Kiswahili, bali katika kuwafanya watanzania kujiona ni watu wa taifa moja..

Kama kweli ulizaliwa kabla ya uhuru na umeshuhudia hayo unayoyasema, maana kwenye mitandao kila mtu anaweza kujipa sifa zozote, haya basi shikamoo sina la kuongeza. Japo nazungumzia mambo ambayo niliyakuta yakijadiliwa na wazee, wakibishana kwa hoja kijiweni huko Dar.
Kuna wale walikua waking'ang'ania kwamba Nyerere aliwakuta Watanganyika wakiwa na umoja, walibishana kwa muda mrefu na kila mmoja kutiririka kuhusu historia ya Tanganyika ambayo haipo hata kwenye vitabu.
Hapo ndio nilijua taarifa za watu kama akina Oscar Kambona ambao hawatajwi kabisa kila mnapozungumza michango ya taifa lenu.

Japo kuna Watanzania huanzisha nyuzi kwajili yake lakini zinaishia malumbano, hebu fuata huu hapa Historia fupi ya marehemu Oscar Kambona
 
Germany east Afrika ilikuwa ni Tanganyika, Burundi na Rwanda, baada ya vita ya dunia ya pili mjerumani aliposhindwa, Tanganyika iliwekwa chini ya Uingereza, Rwanda na Burundi ziliwekwa chini ya Ubelgiji, sasa kwanini Rwanda na Burundi ukabila umekuwepo kama sababu yako unayoitoa kwamba mkoloni hakuwa na sababu ya kutugawanya?, kwa sababu hata Rwanda na Burundi pia mkoloni hakuwa na sababu ya kuwagawanya kwasababu walijua wataondoka wakati wowote kama ilivyokuwa Tanzania?. hakuna mkoloni yeyote yule aliyependezwa na umoja wa anaowatawala, ona jinsi Raila na Uhuru wanavyowagawanya japo sio wakoloni.
Safi mkuu nazan aje ajibu hili .

History ya umoja wetu nyerere huwez kumtenga
 
Kama kweli ulizaliwa kabla ya uhuru na umeshuhudia hayo unayoyasema, maana kwenye mitandao kila mtu anaweza kujipa sifa zozote,...
Sioni sababu zozote za kudanganya. Niko hapa kubanana na vijana tu (kula nao sahani moja).
 
Language Reform: How Nyerere killed tribalism

Huu ndiyo ukweli, sasa wewe endelea kujiliwaza na kumtetea Jommo Kenyatta kwa kushindwa kupambana na ukabila hapo Kenya, yeye aliona kujenga uchumi katika taifa changa kama la Kenya ambalo lilihitaji kulijengea misingi ya umoja kwanza, yeye alienda moja kwa moja kuanza na uchumi, matokeo yake ndiyo hayo, it is too late now.

Mimi simtetei Jommo Kenyatta, tena ukinichunguza sana huwa napenda mambo yawekwe bayana ili kama taifa tujue wapi tulianza kunyeshewa na mvua, huwa ninadiriki kufuata historia nje ya mambo tuliyoaminishwa kwenye vitabu tangu enzi zile. Wewe hapo ndiye mwenye matatizo kwamba hutaki mawazo nje ya kile mwalimu wa shule alikufundisha, maana nimekupeleka kwenye blog ya Mtanzania ambaye ameandika kwa kina mambo mengi kuihusu nchi yako, wewe umeingia uvivu wa kusoma na kuona heri unin'gan'ganizie badala ya kupangua hoja za huyo Mtanzania.
 
Acha uongo Mareale hajawahi kupinga Uhuru wa Tanganyika kitu kilichotokea ni Mwingereza ku-support uongozi wa Kichagga kwa kuona Mareale anafaa zaidi kutokana na utendaji wake chini ya serikali ya Mkoloni!
Rudi kasome vizuri history uje hapa na kama hakupinga kwanin alitaka kuanzisha taifa la jamii ya wachaga na wengine. najua wapo watu wa Moshi humu wenye kujua vyema historia watasema kuhusu hili
 
Sioni sababu zozote za kudanganya. Niko hapa kubanana na vijana tu (kula nao sahani moja).

Hehehe haya bana, subiri nitamshawishi mzee mmoja namfahamu mbishi kweli ajiunge JF halafu nimwelekeze hapa, nina uhakika huu uzi hapatatosha maana yule namfahamu jinsi huwa anan'gan'gania mpaka basi. Tena historia ya Tanganyika huwa anaiongea kama wimbo, labda umekutana naye Dar, hupenda sana kumsifia Kambona.
 
Kama kweli ulizaliwa kabla ya uhuru na umeshuhudia hayo unayoyasema, maana kwenye mitandao kila mtu anaweza kujipa sifa zozote, haya basi shikamoo sina la kuongeza. Japo nazungumzia mambo ambayo niliyakuta yakijadiliwa na wazee, wakibishana kwa hoja kijiweni huko Dar.
Kuna wale walikua waking'ang'ania kwamba Nyerere aliwakuta Watanganyika wakiwa na umoja, walibishana kwa muda mrefu na kila mmoja kutiririka kuhusu historia ya Tanganyika ambayo haipo hata kwenye vitabu.
Hapo ndio nilijua taarifa za watu kama akina Oscar Kambona ambao hawatajwi kabisa kila mnapozungumza michango ya taifa lenu.

Japo kuna Watanzania huanzisha nyuzi kwajili yake lakini zinaishia malumbano, hebu fuata huu hapa Historia fupi ya marehemu Oscar Kambona
Next time ni vyema kusikiliza jambo hasa kwa wahusika vijiwe tu vya kahawa haviwezi kukupa clear picture ya nin kilikuwa kinaendelea .nchi nzima tunayokwambia ni kwa sababu tulikuwa tunashuhudia hali ya ukabila maeneo yetu tuliyozaliwa na kusoma huko ila tulipopelekwa Shule za mbali na nyumban huko wengine tulijua kumbe msukuma ni ndugu yangu na sio adui yangu ( rejea nyuma visa vya mababu zetu bifu zao za kikabila na pia za jamii ya wafugaji na wakulima ) hivyo kujikuta tunakuwa wamoja na hata kipind cha likizo tukirudi nyumban tulikuwa mabalozi wazuri wa kuelezea mazuri ya makabila mengine , historia zao na vile wao wakivyoojifunza mazuri ya kabila langu.

Hata watz wengi tunajua kenya kuna ukabila ila hali halisi nyie ndiyo mnajua na sina haki ya kukupinga kwa story za vijiwen kuhusu ukabila wenu
 
Mimi simtetei Jommo Kenyatta, tena ukinichunguza sana huwa napenda mambo yawekwe bayana ili kama taifa tujue wapi tulianza kunyeshewa na mvua, huwa ninadiriki kufuata historia nje ya mambo tuliyoaminishwa kwenye vitabu tangu enzi zile. Wewe hapo ndiye mwenye matatizo kwamba hutaki mawazo nje ya kile mwalimu wa shule alikufundisha, maana nimekupeleka kwenye blog ya Mtanzania ambaye ameandika kwa kina mambo mengi kuihusu nchi yako, wewe umeingia uvivu wa kusoma na kuona heri unin'gan'ganizie badala ya kupangua hoja za huyo Mtanzania.
Unajua baada ya uhuru Mwl. Nyerere alifanya kitu kimoja cha maana sana na ambacho manufaa yake tunayaona hadi hivi leo. Aliweka mikakati mahsusi ya kuwachanganya watanzania, iwe mashuleni au makazini. Baada ya Azimio la Arusha 1967 alihakikisha anavunjilia mbali shule zilizotenganishwa kwa misingi ya dini na rangi. Kabla ya hapo kulikuwa na shule za watoto wa kizungu, kiasia na kadhalika. Pia kulikuwa na shule za madhehebu tofauti. Hii ilichangia kwa kiwango kikubwa kuwachanganya wanafunzi wajione wote ni kitu kimoja. Pia ni wakati huo tulianza kuitana ndugu (ingawa kwa sasa kuna wengine wanaitwa waheshimiwa n.k). Ukumbuke pia Mwl. Nyerere alikifanya Kiswahili kuwa lugha ya taifa mara baada ya uhuru. Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea wakati huo, licha ya mapungufu yake, ilichangia kwa kiasi kikubwa kuleta mshikamano baina ya matabaka tofauti katika jamii.
 
Ukabila haumalizwi kisa umempa uongozi nchi mtu wa kabila ndogo, Kenya nimeona ukabila hata kwa kabila ndogo, na ikumbukwe ukabila ulianza Kenya hata kabla hatujapata uhuru wa nchi. Wazungu waliutumia kutugawa maana tayari walikua wamenyakua mashamba na raslimali nyingi, hivyo walijaribu kila mbinu za kugawa mababu zetu kwa misingi ya ukabila.

Wakati wanampokeaza rais wa kwanza, tayari kulikua na migawanyiko ya kikabila, ila tatizo naye hakutaka kutumia hiyo fursa kujenga utangamano, walianza kulumbana na makamu wake Jaramogi ambaye naye alikua kama mfalme wa kabila lake la Wajaluo. Sasa ili kujilinda dhidi ya Odinga, Kenyatta naye akakusanya Wakikuyu na kuwaweka mkao wa umoja wa kikabila. Nchi kuanzia hapo haijapona tena, makabila madogo yakaiga tena hayo madogo madogo yamekua balaa.

Wazungu walikua tayari kuachia Tanganyika na hawakua na sababu za kuwagawa, hivyo Nyerere alipokea uongozi kwenye nchi ambayo tayari watu wake walikua wamoja, na kuanzia hapo naye akaendeleza huo umoja hadi leo.

Umekosea sana kuhusu historia ya Tanzania, muingereza alitumia Divide and rule katika makoloni yake yote hivyo Tanzania haikuwa exceptional kuhusu kipindi cha mjerumani n.a. yeye alipendelea baadhi ya makabila katika makoloni yake yote.. Jifunze ku give credit where it is deserved, Nyerere aliisaidia Tanzania sana hasa katika kuunganisha Taifa lenye makabila mengi mara tatu zaidi ya nchi yenu Kenya

Kwa upande wake Kenyatta hakujaliwa muono wa mbali yeye aliendekeza Ukabila kwa masilahi yake binafsi, njoo Tanzania utafute kabila la wazanaki (kabila la Nyerere) home nyadhifa zao.

I have met a lot of Kenyans(from different tribes) who hate Jommo Kenyatta to the fullest because yajinsi alivyolijenga taifa lenu but ukija Bongo wa2 wanaomchukia Nyerere ni wachache mno this just shows how different the fathers of these nations are perceived..
.
Nyerere huchukuliwa kama Nabii (kwa waAfrika wengi) Kenyatta huchukuliwa kama muasisi wa taifa aliyefeli na wananchi wake ..
 
Acha uongo Mareale hajawahi kupinga Uhuru wa Tanganyika kitu kilichotokea ni Mwingereza ku-support uongozi wa Kichagga kwa kuona Mareale anafaa zaidi kutokana na utendaji wake chini ya serikali ya Mkoloni!
Geza ama umesahau, au huijui historia vizuri, ninakuomba ulizia ikiwezekana wahadhiri wa chuo kikuu kuhusu historia ya mangi mkuu alichaguliwaje na wakoloni na jinsi gani alipinga Tanganyika kujitawala na sababu za kufanya hivyo, kumbuka wachaga hawakuwa na cheo cha mangi mkuu, ni cheo kilichobuniwa na mkoloni kwa ajili ya kufikia malengo yake, na mangi Marialle alipewa cheo hicho na mkoloni, sio wachagga wenyewe
 
Back
Top Bottom