[MENTION][JFMP3][/JFMP3][/MENTION]WanaJF!
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa na mbunge wa jimbo la Hai, bwana Mbowe, amethibitisha kuwa yeye ana upeo mdogo sana kuhusu mambo ya sheria.
Bwana Mbowe amethibitisha hilo baada ya kueleza kuwa CHADEMA kufutwa haiwezekani kabisa na hiyo sababu aliyoitumia ndio kichekesho na imemdhalilisha kweli.
Sababu aliyoitoa bwana Mbowe ya kukingia chama chake kifua kuwa hakitaweza kufutwa na msajili si nyingine bali ni idadi ya wabunge, madiwani na wenyeviti wa vijiji.
Bwana Mbowe alieleza kuwa, "kufuta CHADEMA ni sawa na kufuta wabunge 49, madiwani zaidi ya 600 na wenyeviti wa vijiji zaidi ya 1000".
Kama bwana Mbowe angekuwa na maarifa kidogo sana ya sheria (kwa kupitia tu ile sheria ya vyama vya siasa) asinge weza kuongea hayo maneno ya ovyo kabisa kuhusu kufutwa kwa CHADEMA.
Ieleweke kuwa, chama cha siasa hakifutwi kwa kuangalia idadi ya wabunge, madiwani na hata wenyeviti wa vijiji waliotokana na chama hicho, bali kinacho angaliwa ni kama vigezo ama masharti yaliyo kwenye sheria yamevunjwa.
Mheshimiwa D inaonyesha wewe na chadema, chadema na wewe, umenikumbusha mbali enzi hizo kulikuwa na mchezaji anaitwa rashidi idi chama, yeye uwanjani alipewa kazi moja tu, kuhakikisha zamoyoni mogela hashiki mpira na alikuwa na fungu pekee la kazi hiyo hebu tuambie na wewe umetengewa kiasi gani kwa kazi hiyo?