Kwa herini wana wa JF Tutaonana msimu wa kilimo ukiisha...

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Nimeamua kurudi kijijini kwa muda kwa ajili ya kushiriki msimu wa kilimo. Sina hakika huko kama mitandao ya simu inapatikana. Ikiwa inapatikana basi tutaendelea kuwa pamoja. Nawashauri wote ambao wanapata mishahara kila mwezi lakini bado haitoshi. Twendeni shamba tukachape jembe maana Mungu hamtupi mja wake!! Nimepata kusoma mahali kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa hili.
 
nina uhakika tunaposherehekea miaka 50 ya uhuru wa tanganyika/tanzania bara huko kijijini kuna mtandao wa simu
 
Kilimo chenyewe hiki, labda ukalime matikiti maji, naona ardhi zenye rutuba wanavutiwa wawekezaji, lhali wakulima wadogo wazawa wanahimizwa kutumia mbolea za chumvichumvi. Anyways twakutakia heri, matango yakikomaa, usisahau kututumia
 
Kilimo kwanza!
Tumethubutu tumeweza tunasonga mbele.
Kila la heri mkuu, mazao yakiwiva tuite kuvuna!
 
Nimeamua kurudi kijijini kwa muda kwa ajili ya kushiriki msimu wa kilimo. Sina hakika huko kama mitandao ya simu inapatikana. Ikiwa inapatikana basi tutaendelea kuwa pamoja. Nawashauri wote ambao wanapata mishahara kila mwezi lakini bado haitoshi. Twendeni shamba tukachape jembe maana Mungu hamtupi mja wake!! Nimepata kusoma mahali kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa hili.

karibu, wenzio tushapanda mahindi na mbaazi mwezi umepita sasa....
 
Ukichukua line ya Airtel na Vodacom hata ujifiche wapi ndani ya nchi hii; kati ya provider hawa wawili lazima utakuwa umeunganishwa na mtandao...(walau ki- bar kimoja cha signal!!) Nasema hivi maana hata mabonde ya milima ya Kitonga na ile ya Sekenke mtandao upo pamoja na uhafifu wake. Ila ukichukua Zantel, Tigo na mingineyo huko vijijini utakuwa umechemsha, tena vibaya sana!!!

Kingine, ziwahi mvua za kupandia mazao zinanyesha hivi sasa pahala pengi ukiachilia ile mikoa miwili yenye ukavu. i.e. Dodoma na Singida. Kilimo chema ndugu!
 
Nimeamua kurudi kijijini kwa muda kwa ajili ya kushiriki msimu wa kilimo. Sina hakika huko kama mitandao ya simu inapatikana. Ikiwa inapatikana basi tutaendelea kuwa pamoja. Nawashauri wote ambao wanapata mishahara kila mwezi lakini bado haitoshi. Twendeni shamba tukachape jembe maana Mungu hamtupi mja wake!! Nimepata kusoma mahali kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa hili.

Mkubwa! Kila la Kheri ktk yote na bila shaka kama siyo matatizo ndiyo nyingi bila shaka tungekuwa wote! Huu usemi upo "KAMA UNATAKA MALI UTAPA SHAMBANI"
 
mvua zisiponyesha huko kijijini usirudi tena mjini wewe endelea tu kukaa huko huko.
 
Back
Top Bottom