SoC01 Jinsi Kilimo kilivyobeba utajiri na umasikini

Stories of Change - 2021 Competition

Mwanafunzi mtoro

JF-Expert Member
Aug 3, 2021
223
797
1: UTANGULIZI
Nchi yetu imebahatika kuwa na ardhi nzuri yenye uwezo wa kustawisha mazao ya aina nyingi yakiwemo ya biashara na chakula. Mikoa kama Morogoro, Mbeya, Rukwa, Rumuma , Kilimanjaro ,Mwanza ,Iringa na Mbeya ikiwa kama mfano wa maeneo ambayo kilimo kimekuwa kikifanyika katika maeneo mengi ya sehemu hizo. Kilimo kimepewa hadhi ya kuwa uti wa mgongo katika uchumi wa mtanzania. Hata hivyo Bado kilimo hakioneshi tija na uhalisia wa kuwa uti wa mgongo katika uchumi. Maeneo mengi ambayo kilimo kimekuwa kikifanyika bado hali ya maisha ya wakulima yameendelea kuwa magumu sana. Japokuwa pia kuna watu wengi waliofanikiwa kupitia kilimo lakini bado maendeleo ya kilimo hayaridhishi. Ipo namna inaweza kufanyika kilimo kuwa na tija kwa kuzipunguza changamoto nyingi zinazoikumba sekta hii. Wapo watu waliofanikiwa sana na pia wapo watu waliopoteza mitaji na mwelekeo wa maisha kwa kujihusisha na kilimo kitu ambacho kinafanya tusiwe na jibu la moja kwa moja kuhusu kilimo kama ni kazi ya uhakika au nayo ni kama kamali. Ni wakati muafaka sasa wa kuangalia ni kwa namna gani kilimo kitamnufaisha kila mtu atakaye husika kianzia mkulima mdogo wa ekali moja hadi kumi pia na wale wa ekali kumi hadi mamia ya ekali.

2: NAMNA KILIMO KINAVYOWEZA KUKUPA UMASIKINI
Kwa asilimia kubwa mazao ya kilimo nchi yetu yanazalishwa na wakulima wadogowadogo. Pamoja na wakulima hawa kuwa na uwezo wa kuihudumia nchi yetu katika mazao ya chakula na malighafi za viwandani lakini bado hali ya kiuchumi ya wakulima huko vijijini ni mbaya sana. Bado wanakabiliwa na maisha magumu kama vile ukosefu wa pesa za matibabu ,makazi duni, kushindwa kutoa huduma za kielimu kwa watoto wao na njaa za kila msimu zinazotokana na kuuza mazao mengi kwa bei ya hasara kipindi cha mavuno. Zipo sababu nyingi zinazowafanya wakulima wazidi kuwa masikini zikiwemo hizi chache.

(a) Sababu za kiuchumi;watu wengi wanao jihusisha na kilimo huko kijijini ni kutoka familia zenye kipato kidogo cha fedha. Wanatumia nguvu zao kama mtaji katika kilimo. Hufanya kilimo kama sehemu ya kupata chakula na mahitaji ya kifedha,wanatumia zana za kizamani kama jembe la mkono kuendesha shughuli za kilimo. Hata wale wanaotumia zana za kisasa kama trekta na mashine nyingine za kilimo sio wengi. Sababu za kiuchumi huwafanya walime mashamba madogo,kilimo cha kutegemea mvua. Wanashindwa hata kutumia mbolea kukuza kipato. Kutokana na sababu hiyo wengi hujikuta wanalima kupambana na njaa huku wakiendelea kubaki katika umasikini.

(b) Ukosefu wa utaalamu; sababu za kiuchumi pia zinawafanya wasilime kwa kufuata utaalamu unaohitajika katika zao husika. Mfano kilimo cha umwagiliaji.

(c) Sababu za kisiasa;mabadiliko ya kisera yanaweza kuathiri sekta ya kilimo na kumpa umasikini mkulima. Mabadiliko ya sera yanaweza kusababisha kupanda kwa bei ya pembejeo za kilimo kama vile mbolea,dawa za mazao na mashine za kilimo kwa kuwa asilimia kubwa ya vitu hivi tunaingiza kutoka nje ya nchi. Lakini pia sababu za kisiasa zinaweza kuathiri soko la mazao kwakuwa asilimia kubwa ya soko la mazao yetu lipo nje ya nchi hasahasa nchi jirani kama vile Kenya ,Uganda ,Rwanda ,Malawi nk. Mfano rejea mahusiano mabaya ya kisiasa na diplomasia yalivyoathiri soko la mchele na kusababisha hasara kwa wakulima wa mpunga. Rejea kushuka kwa soko la korosho nje ya nchi na kuyumba kwa wakulima wa korosho kule Mtwara na Lindi. Rejea kushuka kwa soko la mbaazi na dengu nje ya nchi. Pia rejea kushuka na kuyumba kwa soko la kahawa na mahindi nje ya nchi hasa Kenya. Matatizo yanasababishwa na siasa lakini matokeo yake ni umasikini kwa wakulima kwa kushindwa kurudisha hata gharama za kulimia ili kurudi tena msimu mpya wa kilimo.

(d) Uhakika wa soko; kwa asilimia kubwa umasikini wa mkulima unatokana na kukosekana kwa soko la uhakika. Mkulima bado anaendelea kuzalisha mazao yake huku aikwa hamjui mteja wake na zaidi hajui hata ni bei gani ataiuza hayo mazao yake. Mfano katika hili rejea habari za kukosekana kwa soko la uhakika wa nyanya zinazolimwa kule Ilula Iringa ,au Dumila na Kilosa kule Morogoro. Au jiridhishe kwa kuwauliza wakulima wa mpunga kule Mbeya ,Rukwa au Ifakara na Mvomero kule Morogoro. Kuna watu walipeleka nyanya Dar es salaam wakauza kwa hasara wakalipa nauli ya gari la mzigo hadi wakaishiwa nauli ya kurudi makwao. Wakulima wa nyanya pale Mangae ,Doma na Melela kule Morogoro waliamua kuwaachia nyani wale nyanya. Kwanini mkulima asiwe masikini kwa soko la kubeti namna hii?

(e) Kukosekana kwa uhuru wa kupanga bei ya mazao kwa mkulima. Mkulima hana uhuru wa kupanga bei ya mazao yake kama ilivyo kwenye bidhaa zingine. Anaandaa shamba,anapanda ,anatumia dawa na kuvuna kwa gharama na yeye ndio anayejua gharama husika lakini anamsubiri mnunuzi amtajie bei ya mazao yake. Basi hiyo bei mkulima angetajiwa kabla ya kuanza kilimo ajabu bei anapangiwa wakati akishavuna. Mfumo huu ungetumika hata kwa bidhaa kama simenti,bati na sukari basi wazalishaji wangeshindwa kuendesha shughuli za uzalishaji kwa ukubwa wa hasara. Kupangiwa bei na mnunuzi ambaye hajui bei ya pembejeo wala maandalizi ya shamba huu ni mfumo wa kumpa umasikini mkulima.

3:KILIMO KINAVYOWEZA KUKUPA UTAJIRI
Kwa asilimia kubwa wanao nufaika na kilimo sio wakulima wenyewe,ndio sio wakulima wenyewe bali ni wakulima wachache na makundi mengine ya watu. Makundi yafuatayo ndio yananufaika na kilimo.
(a) Wakulima wakubwa; hawa ni wale wakulima wachache wenye uwezo wa kulima kianzia ekali mia moja na kuendelea. Wana mitaji mikubwa ya kukabiliana na kilimo. Wana uwezo wa kulitafuta soko ndani ya nchi na nje ya nchi.
(b) walanguzi wa mazao; kundi hili ni watu wanaoenda kijijini na kutafuta kununua mazao kwa wakulima kwa bei nafuu sana . Wengine huyasafirisha nje ya nchi na wengine kuweka stoku hadi pale bei itakapokuwa nzuri. Wanatumia vipimo tofauti vya kununua na kuuzia. Wanajipangia bei wafikapo kwa wakulima.
(c) wamiliki wa mashine za nafaka; hawa ni wale wanaomiliki mashine kubwa za nafaka kama vile kukoboa mpunga,kusaga mahindi na kukamua alizeti. Wana uhakika na soko la ndani na nje ya nchi wanapata mazao kwa bei rahisi sana kutoka kwa wakulima. Mfano hata bei ya mahindi au mchele ikiwa mbaya Sana wao wana soko la uhakika na faida ya uhakika tofauti na mkulima ambaye hana namna kwa bei yoyote anayokutana nayo lazima auze.
(d) wamiliki wa viwanda vidogo vidogo na vikubwa.Hawa ni wale wamiliki wa viwanda kama vile vya kusindika nyanya au viwanda vya ngano kutengeneza bidhaa mbalimbali mfano biskuti mikate na maandazi, viwanda vya mafuta ya kura ya alizeti na ufuta , viwanda vya chai, kahawa na viwanda vya sembe nk . Viwanda hivi vinatengezeza faida kuliko mkulima.

4: SABABU ZINAZOFANYA WACHACHE WANUFAIKE.
(a) ukosefu wa mitaji; kilimo kimeonesha kuwa na faida sana lakini kwa wale wenye mitaji mikubwa ,wenye uwezo wa kulima mashamba makubwa,zana za kisasa na kupambana na changamoto ya soko la mazao.
(b) kukosekana kwa soko la uhakika; kukosekana kwa soko la uhakika kumefanya wakulima wengi kudidimia kiuchumi . Hili limesababisha wachache wenye uwezo wa kulitafuta soko wafanikiwe zaidi kwa kuwa faida ya kilimo iliyopaswa kwenda kwa watu wengi inakwenda kwa watu wachache. Mfano rejea mafanikio waliyonayo wenye viwanda vya sembe , mchele ni tofauti na mafanikio waliyonayo wakulima wa mazao husika. Rejea mafanikio waliyonayo wafanya biashara wa viazi ni tofauti na wakulima wa viazi huko Mbeya,Njombe na Iringa. Rejea mafanikio waliyonayo wafanya biashara wakubwa wa dengu huko Mwanza na Shinyanga ni tofauti na wakulima wa zao husika ukilinganisha hali yao kiuchumi.

5:NINI KITATOKEA KAMA HALI ITAENDELEA KUWA HIVI
Mambo mengi yanaweza kutokea ikiwemo;
(a) baa la njaa; wakulima wanaotumia pesa watakata tamaa kutokana na hasara za mara kwa mara. Wakulima watakao endelea ni wale wanaotumia nguvu kama mtaji. Mwisho tutazidi kukubwa na baa la njaa la mara kwa mara.
(b) kilimo hakitaweza kuchangia kutatua tatizo la ajira; tatizo la jira linaonesha kishamiri na sio kuisha. Kama kilimo kingewekewa misingi bora kingeweza kuwakusanya vijana waliomaliza vyuo mbalimbali nchini wakajiajiri huko. Lakini kutokana na kuwa kazi ya kubahatisha wengi wanashindwa kuwa na pakuanzia.
(c)umasikini kwa mkulima; hali hii niionayo sasa kama itaendelea basi siioni dalili ya mkulima kuondoka kwenye umasikini angali yeye ndio mzalishaji mkubwa na tegemeo kwenye sekta zingine.

6: NINI KIFANYIKE ILI KILA ANAYEJIHUSISHA NA KILIMO ANUFAIKE
Yafuatayo yanaweza kufanyika ili kila anayeshiriki katika sekta ya kilimo apate faida;

(a) Kwa serikali
Kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya pembejeo na zana za kilimo. Mfano kwasasa asilimia kubwa ya mbolea inatoka nje ya nchi jambo lonaloongeza gharama za uzalishaji.
Kupunguza kodi katika pembejeo za kilimo kama vile mbolea,madawa na zana kama vile trekta na mashine nyingine za kilimo.
Kuboresha masoko nje ya nchi kwa kuwa na mahusiano mazuri ya kidiplomasia.
Kuondoa au kupunguza utitiri wa kodi mipakani kwa mazao ghafi au bidhaa za kilimo yanayoenda nje ya nchi
Kutoa mbolea kwa wakulima kwa mikopo isiyo na riba .
Kuboresha vyama vya msingi vinavyonunua mazao kama pamba ,korosho au kahawa ikiwemo kuwalipa kwa wakati na kwa being yenye faida kwa wakulima.
Kuzidisha ujenzi wa miundombinu kama vile reli na barabara ili ku hochea uhakika wa kusafirisha mazao toka kijijni hadi kulifikia soko la uhakika . Mfano reli ya kisasa itasaidia kwa kiasi kikuwa kukua kwa sekta ya kilimo. Barabara za uhakika hadi vijijini zikiongezeka zitachochea kukua kwa sekta ya kilimo
Kuchochea ujenzi wa viwanda vya kusindika mazao. Mazao kama nyanya na matunda yasiyoweza kuhifadhika kwa muda mrefu gharani yanaweza kuwa na soko la uhakika na kuinua kilimo.
Serikali iweke sera na kuzisimamia ,kusiwe na kilimo cha maonesho ya nane nane na kubaki kwenye makaratasi.
Kuongeza bajeti kwenye kilimo ili kuwezesha tafiti mbalimbali za kilimo katika vyuo vyetu nchini kama vile SUA, MATI , Ukiliguru na vinginevyo kufanyika ili kuongeza uzalishaji.

(b)kwa mtu binafsi
Mtu mmoja mmoja anaweza kufanya haya ili kunufaika na kilimo
Kulima kwa kufuata utaalamu ili kuongeza kipato na thamani ya mazao
Kufuatilia na kujua soko husika la mazao unayotaka kulima kabla kuanza kulima.
Kufuatilia taasisi zinazotoa mikopo ya zana za kilimo kama trekta na mashine nyingine kwa gharama ndogo za awali( down payment) na riba nafuu .
(c)kwa taasisi za mikopo
Taasisi za mikopo zina mchango mkubwa Sana katika kuinua sekta ya kilimo ikiwemo
Kutoa elimu juu ya mikopo kwenye kilimo.
Kupunguza malipo ya awali kwa mikopo ya zana za kilimo . Mfano kama taasisi inakopesha trekta kwa milioni 70 ,malipo ya awali ni 20% ambayo ni sawa na 14M basi ni vema wakapunguza hadi mfano labda 10% ambayo ni sawa na kama 10 M. Hi itachochea wakulima wengi kumiliki zana za kilimo na kuongeza uzalishaji.

HITIMISHO
Naamini kilimo kikiondolewa vikwazo basi itakuwa sekta nyeti zaidi na itakayoondoa tatizo la ajira kwa asilimia kubwa sana hapa nchini.
 
Mkuu umetisha Sana hongera

Next time NAOMBA ufanye analysis pia juu ya ufugaji wa wanyama wote wanaoliwa ili tujifunze Zaid Kama umeandika kwa ajili ya STORY OF CHANGE basi mkuu japo umechelewa lakini ushindi ni wako
 
Ingekuwa kula tunda kwa masihara hapa tungekimbiana big up bro
 
1: UTANGULIZI
Nchi yetu imebahatika kuwa na ardhi nzuri yenye uwezo wa kustawisha mazao ya aina nyingi yakiwemo ya biashara na chakula. Mikoa kama Morogoro, Mbeya, Rukwa, Rumuma , Kilimanjaro ,Mwanza ,Iringa na Mbeya ikiwa kama mfano wa maeneo ambayo kilimo kimekuwa kikifanyika katika maeneo mengi ya sehemu hizo. Kilimo kimepewa hadhi ya kuwa uti wa mgongo katika uchumi wa mtanzania. Hata hivyo Bado kilimo hakioneshi tija na uhalisia wa kuwa uti wa mgongo katika uchumi. Maeneo mengi ambayo kilimo kimekuwa kikifanyika bado hali ya maisha ya wakulima yameendelea kuwa magumu sana. Japokuwa pia kuna watu wengi waliofanikiwa kupitia kilimo lakini bado maendeleo ya kilimo hayaridhishi. Ipo namna inaweza kufanyika kilimo kuwa na tija kwa kuzipunguza changamoto nyingi zinazoikumba sekta hii. Wapo watu waliofanikiwa sana na pia wapo watu waliopoteza mitaji na mwelekeo wa maisha kwa kujihusisha na kilimo kitu ambacho kinafanya tusiwe na jibu la moja kwa moja kuhusu kilimo kama ni kazi ya uhakika au nayo ni kama kamali. Ni wakati muafaka sasa wa kuangalia ni kwa namna gani kilimo kitamnufaisha kila mtu atakaye husika kianzia mkulima mdogo wa ekali moja hadi kumi pia na wale wa ekali kumi hadi mamia ya ekali.

2: NAMNA KILIMO KINAVYOWEZA KUKUPA UMASIKINI
Kwa asilimia kubwa mazao ya kilimo nchi yetu yanazalishwa na wakulima wadogowadogo. Pamoja na wakulima hawa kuwa na uwezo wa kuihudumia nchi yetu katika mazao ya chakula na malighafi za viwandani lakini bado hali ya kiuchumi ya wakulima huko vijijini ni mbaya sana. Bado wanakabiliwa na maisha magumu kama vile ukosefu wa pesa za matibabu ,makazi duni, kushindwa kutoa huduma za kielimu kwa watoto wao na njaa za kila msimu zinazotokana na kuuza mazao mengi kwa bei ya hasara kipindi cha mavuno. Zipo sababu nyingi zinazowafanya wakulima wazidi kuwa masikini zikiwemo hizi chache.

(a) Sababu za kiuchumi;watu wengi wanao jihusisha na kilimo huko kijijini ni kutoka familia zenye kipato kidogo cha fedha. Wanatumia nguvu zao kama mtaji katika kilimo. Hufanya kilimo kama sehemu ya kupata chakula na mahitaji ya kifedha,wanatumia zana za kizamani kama jembe la mkono kuendesha shughuli za kilimo. Hata wale wanaotumia zana za kisasa kama trekta na mashine nyingine za kilimo sio wengi. Sababu za kiuchumi huwafanya walime mashamba madogo,kilimo cha kutegemea mvua. Wanashindwa hata kutumia mbolea kukuza kipato. Kutokana na sababu hiyo wengi hujikuta wanalima kupambana na njaa huku wakiendelea kubaki katika umasikini.

(b) Ukosefu wa utaalamu; sababu za kiuchumi pia zinawafanya wasilime kwa kufuata utaalamu unaohitajika katika zao husika. Mfano kilimo cha umwagiliaji.

(c) Sababu za kisiasa;mabadiliko ya kisera yanaweza kuathiri sekta ya kilimo na kumpa umasikini mkulima. Mabadiliko ya sera yanaweza kusababisha kupanda kwa bei ya pembejeo za kilimo kama vile mbolea,dawa za mazao na mashine za kilimo kwa kuwa asilimia kubwa ya vitu hivi tunaingiza kutoka nje ya nchi. Lakini pia sababu za kisiasa zinaweza kuathiri soko la mazao kwakuwa asilimia kubwa ya soko la mazao yetu lipo nje ya nchi hasahasa nchi jirani kama vile Kenya ,Uganda ,Rwanda ,Malawi nk. Mfano rejea mahusiano mabaya ya kisiasa na diplomasia yalivyoathiri soko la mchele na kusababisha hasara kwa wakulima wa mpunga. Rejea kushuka kwa soko la korosho nje ya nchi na kuyumba kwa wakulima wa korosho kule Mtwara na Lindi. Rejea kushuka kwa soko la mbaazi na dengu nje ya nchi. Pia rejea kushuka na kuyumba kwa soko la kahawa na mahindi nje ya nchi hasa Kenya. Matatizo yanasababishwa na siasa lakini matokeo yake ni umasikini kwa wakulima kwa kushindwa kurudisha hata gharama za kulimia ili kurudi tena msimu mpya wa kilimo.

(d) Uhakika wa soko; kwa asilimia kubwa umasikini wa mkulima unatokana na kukosekana kwa soko la uhakika. Mkulima bado anaendelea kuzalisha mazao yake huku aikwa hamjui mteja wake na zaidi hajui hata ni bei gani ataiuza hayo mazao yake. Mfano katika hili rejea habari za kukosekana kwa soko la uhakika wa nyanya zinazolimwa kule Ilula Iringa ,au Dumila na Kilosa kule Morogoro. Au jiridhishe kwa kuwauliza wakulima wa mpunga kule Mbeya ,Rukwa au Ifakara na Mvomero kule Morogoro. Kuna watu walipeleka nyanya Dar es salaam wakauza kwa hasara wakalipa nauli ya gari la mzigo hadi wakaishiwa nauli ya kurudi makwao. Wakulima wa nyanya pale Mangae ,Doma na Melela kule Morogoro waliamua kuwaachia nyani wale nyanya. Kwanini mkulima asiwe masikini kwa soko la kubeti namna hii?

(e) Kukosekana kwa uhuru wa kupanga bei ya mazao kwa mkulima. Mkulima hana uhuru wa kupanga bei ya mazao yake kama ilivyo kwenye bidhaa zingine. Anaandaa shamba,anapanda ,anatumia dawa na kuvuna kwa gharama na yeye ndio anayejua gharama husika lakini anamsubiri mnunuzi amtajie bei ya mazao yake. Basi hiyo bei mkulima angetajiwa kabla ya kuanza kilimo ajabu bei anapangiwa wakati akishavuna. Mfumo huu ungetumika hata kwa bidhaa kama simenti,bati na sukari basi wazalishaji wangeshindwa kuendesha shughuli za uzalishaji kwa ukubwa wa hasara. Kupangiwa bei na mnunuzi ambaye hajui bei ya pembejeo wala maandalizi ya shamba huu ni mfumo wa kumpa umasikini mkulima.

3:KILIMO KINAVYOWEZA KUKUPA UTAJIRI
Kwa asilimia kubwa wanao nufaika na kilimo sio wakulima wenyewe,ndio sio wakulima wenyewe bali ni wakulima wachache na makundi mengine ya watu. Makundi yafuatayo ndio yananufaika na kilimo.
(a) Wakulima wakubwa; hawa ni wale wakulima wachache wenye uwezo wa kulima kianzia ekali mia moja na kuendelea. Wana mitaji mikubwa ya kukabiliana na kilimo. Wana uwezo wa kulitafuta soko ndani ya nchi na nje ya nchi.
(b) walanguzi wa mazao; kundi hili ni watu wanaoenda kijijini na kutafuta kununua mazao kwa wakulima kwa bei nafuu sana . Wengine huyasafirisha nje ya nchi na wengine kuweka stoku hadi pale bei itakapokuwa nzuri. Wanatumia vipimo tofauti vya kununua na kuuzia. Wanajipangia bei wafikapo kwa wakulima.
(c) wamiliki wa mashine za nafaka; hawa ni wale wanaomiliki mashine kubwa za nafaka kama vile kukoboa mpunga,kusaga mahindi na kukamua alizeti. Wana uhakika na soko la ndani na nje ya nchi wanapata mazao kwa bei rahisi sana kutoka kwa wakulima. Mfano hata bei ya mahindi au mchele ikiwa mbaya Sana wao wana soko la uhakika na faida ya uhakika tofauti na mkulima ambaye hana namna kwa bei yoyote anayokutana nayo lazima auze.
(d) wamiliki wa viwanda vidogo vidogo na vikubwa.Hawa ni wale wamiliki wa viwanda kama vile vya kusindika nyanya au viwanda vya ngano kutengeneza bidhaa mbalimbali mfano biskuti mikate na maandazi, viwanda vya mafuta ya kura ya alizeti na ufuta , viwanda vya chai, kahawa na viwanda vya sembe nk . Viwanda hivi vinatengezeza faida kuliko mkulima.

4: SABABU ZINAZOFANYA WACHACHE WANUFAIKE.
(a) ukosefu wa mitaji; kilimo kimeonesha kuwa na faida sana lakini kwa wale wenye mitaji mikubwa ,wenye uwezo wa kulima mashamba makubwa,zana za kisasa na kupambana na changamoto ya soko la mazao.
(b) kukosekana kwa soko la uhakika; kukosekana kwa soko la uhakika kumefanya wakulima wengi kudidimia kiuchumi . Hili limesababisha wachache wenye uwezo wa kulitafuta soko wafanikiwe zaidi kwa kuwa faida ya kilimo iliyopaswa kwenda kwa watu wengi inakwenda kwa watu wachache. Mfano rejea mafanikio waliyonayo wenye viwanda vya sembe , mchele ni tofauti na mafanikio waliyonayo wakulima wa mazao husika. Rejea mafanikio waliyonayo wafanya biashara wa viazi ni tofauti na wakulima wa viazi huko Mbeya,Njombe na Iringa. Rejea mafanikio waliyonayo wafanya biashara wakubwa wa dengu huko Mwanza na Shinyanga ni tofauti na wakulima wa zao husika ukilinganisha hali yao kiuchumi.

5:NINI KITATOKEA KAMA HALI ITAENDELEA KUWA HIVI
Mambo mengi yanaweza kutokea ikiwemo;
(a) baa la njaa; wakulima wanaotumia pesa watakata tamaa kutokana na hasara za mara kwa mara. Wakulima watakao endelea ni wale wanaotumia nguvu kama mtaji. Mwisho tutazidi kukubwa na baa la njaa la mara kwa mara.
(b) kilimo hakitaweza kuchangia kutatua tatizo la ajira; tatizo la jira linaonesha kishamiri na sio kuisha. Kama kilimo kingewekewa misingi bora kingeweza kuwakusanya vijana waliomaliza vyuo mbalimbali nchini wakajiajiri huko. Lakini kutokana na kuwa kazi ya kubahatisha wengi wanashindwa kuwa na pakuanzia.
(c)umasikini kwa mkulima; hali hii niionayo sasa kama itaendelea basi siioni dalili ya mkulima kuondoka kwenye umasikini angali yeye ndio mzalishaji mkubwa na tegemeo kwenye sekta zingine.

6: NINI KIFANYIKE ILI KILA ANAYEJIHUSISHA NA KILIMO ANUFAIKE
Yafuatayo yanaweza kufanyika ili kila anayeshiriki katika sekta ya kilimo apate faida;

(a) Kwa serikali

(b)kwa mtu binafsi

Mtu mmoja mmoja anaweza kufanya haya ili kunufaika na kilimo

(c)kwa taasisi za mikopo
Taasisi za mikopo zina mchango mkubwa Sana katika kuinua sekta ya kilimo ikiwemo

HITIMISHO
Naamini kilimo kikiondolewa vikwazo basi itakuwa sekta nyeti zaidi na itakayoondoa tatizo la ajira kwa asilimia kubwa sana hapa nchini.
Umeandika vyema sana mkuu...ila ingependeza utupe mifano dhahiri ambayo umeifanya ww practical strory ingeleta chachu zaidi
 
Yaani ukope kwenye ka benki ka kienyeji unadhani utapata faida kweli? weye dogo unacheza weye! Kilimo kinataka usomi hasa ikiwemo kujua Lugha za kigeni!! ili upambanie kulijua soko vizuri! !! uwe na sauti bin akili ya kukopa kwenye Mabenki ya kimataifa!

lkn sera mbovu za sirikali zina wadidimiza wakulima pia!!... mfano sera ya ccm hakuna kuuza Mazao nje ya nchi!! sasa hapo utatokaje hapo?? nakupa Mfano Sumri msimu flani alilima tani million kumi za maharage! aliweza lisha nchi nzima lkn alibaniwa asiuze nje!

Kwa Tani zaidi ya hizo alilima nchini Zambia, akauza zote nje ya nchi na faida kubwa mara tatu kwa hiyo kilimo alicho kifanya nchini Zambia kwa mashamba ya kukodi kilimlipa zaidi kuliko mashamba yasiyo ya kukodi Bongo!

Ambayo pia mauzo yenye tija ya mazao ya tanzania yalikuwa yanaingiza fedha kidogo kidogo kwa muda mrefu zaidi, ..mpaka misimu inakutana, kwa mfano msimu hadi msimu hujauza hata kufikia Robo ya jumla za tani ulizo zalisha ,

hizi zote ni sera mbovu za wanasiasa mbumbu wasio soma!! km kina gwaji boy!! kilimo cha hivi kinarudisha maendeleo ya Mkulima/nchi nyuma sana! at least huyu ni msomi anajua trend ya biashara za kilimo Duniani! je mkulima mbumbu atajua haya?

Some times ni viroho vya Korosho na visununu vya kiswahili vinahusika, kutoka kwa wanasiasa!! yaani nimesha waona sana hawako - in broad sense! when it comes to agricultural sector, country wise beneficiaries'!

wako very narroweries mind gate! na hawajali kabisaaa!! tena hawajui kuwa hawajui! Labda uwe na connection ya moja kwa moja na Rais! km wa awamu ile!! huyu bana ni muelewa sana huyu jamaa! alipaswa kuzaliwa Ulaya ndo maana ni mweupe!

lkn sasa wenye wivu wa karibu yake walikuwa wanabana! maksudi tu!! tena kuliko hizo nchi nazpo kwambia kilimo kinafanyika wao kule wanakusadia na mahali pa kuuzia faster!!...na

una pewa na trend ya Makongamano ya Kilimo Duniani hapa Bongo lini limefanyika hili hata km lipo wataenda wasomi tuuu! waziri wa kilimo na jpo lake! wakirudi wanakalia taarifa, nchi za wenye akili ziko hivi.

Mkulima anapewa mikopo Nafuu ya pembe jeo!! akazalishe chakula bana wee! hata gonjwa likija ghafla dhidi ya mazao au mifugo ya Mkulima km kimeta serikali inanunua hiyo mifugo yako yote!! na unaongezewa na Mikopo juu ili ulime tena!

nchi km hii hawalii njaa kamwe!!.... Mkulima analindwa mno ajira yake yaani mtu anazalisha chakula umchezee weee!! watakuua! na km waziri wa kilimo na sera ukileta leta ujinga unapotezwa kirahisi mno! usilete mbwembwe na mlo!
 
1: UTANGULIZI
Nchi yetu imebahatika kuwa na ardhi nzuri yenye uwezo wa kustawisha mazao ya aina nyingi yakiwemo ya biashara na chakula. Mikoa kama Morogoro, Mbeya, Rukwa, Rumuma , Kilimanjaro ,Mwanza ,Iringa na Mbeya ikiwa kama mfano wa maeneo ambayo kilimo kimekuwa kikifanyika katika maeneo mengi ya sehemu hizo. Kilimo kimepewa hadhi ya kuwa uti wa mgongo katika uchumi wa mtanzania. Hata hivyo Bado kilimo hakioneshi tija na uhalisia wa kuwa uti wa mgongo katika uchumi. Maeneo mengi ambayo kilimo kimekuwa kikifanyika bado hali ya maisha ya wakulima yameendelea kuwa magumu sana. Japokuwa pia kuna watu wengi waliofanikiwa kupitia kilimo lakini bado maendeleo ya kilimo hayaridhishi. Ipo namna inaweza kufanyika kilimo kuwa na tija kwa kuzipunguza changamoto nyingi zinazoikumba sekta hii. Wapo watu waliofanikiwa sana na pia wapo watu waliopoteza mitaji na mwelekeo wa maisha kwa kujihusisha na kilimo kitu ambacho kinafanya tusiwe na jibu la moja kwa moja kuhusu kilimo kama ni kazi ya uhakika au nayo ni kama kamali. Ni wakati muafaka sasa wa kuangalia ni kwa namna gani kilimo kitamnufaisha kila mtu atakaye husika kianzia mkulima mdogo wa ekali moja hadi kumi pia na wale wa ekali kumi hadi mamia ya ekali.

2: NAMNA KILIMO KINAVYOWEZA KUKUPA UMASIKINI
Kwa asilimia kubwa mazao ya kilimo nchi yetu yanazalishwa na wakulima wadogowadogo. Pamoja na wakulima hawa kuwa na uwezo wa kuihudumia nchi yetu katika mazao ya chakula na malighafi za viwandani lakini bado hali ya kiuchumi ya wakulima huko vijijini ni mbaya sana. Bado wanakabiliwa na maisha magumu kama vile ukosefu wa pesa za matibabu ,makazi duni, kushindwa kutoa huduma za kielimu kwa watoto wao na njaa za kila msimu zinazotokana na kuuza mazao mengi kwa bei ya hasara kipindi cha mavuno. Zipo sababu nyingi zinazowafanya wakulima wazidi kuwa masikini zikiwemo hizi chache.

(a) Sababu za kiuchumi;watu wengi wanao jihusisha na kilimo huko kijijini ni kutoka familia zenye kipato kidogo cha fedha. Wanatumia nguvu zao kama mtaji katika kilimo. Hufanya kilimo kama sehemu ya kupata chakula na mahitaji ya kifedha,wanatumia zana za kizamani kama jembe la mkono kuendesha shughuli za kilimo. Hata wale wanaotumia zana za kisasa kama trekta na mashine nyingine za kilimo sio wengi. Sababu za kiuchumi huwafanya walime mashamba madogo,kilimo cha kutegemea mvua. Wanashindwa hata kutumia mbolea kukuza kipato. Kutokana na sababu hiyo wengi hujikuta wanalima kupambana na njaa huku wakiendelea kubaki katika umasikini.

(b) Ukosefu wa utaalamu; sababu za kiuchumi pia zinawafanya wasilime kwa kufuata utaalamu unaohitajika katika zao husika. Mfano kilimo cha umwagiliaji.

(c) Sababu za kisiasa;mabadiliko ya kisera yanaweza kuathiri sekta ya kilimo na kumpa umasikini mkulima. Mabadiliko ya sera yanaweza kusababisha kupanda kwa bei ya pembejeo za kilimo kama vile mbolea,dawa za mazao na mashine za kilimo kwa kuwa asilimia kubwa ya vitu hivi tunaingiza kutoka nje ya nchi. Lakini pia sababu za kisiasa zinaweza kuathiri soko la mazao kwakuwa asilimia kubwa ya soko la mazao yetu lipo nje ya nchi hasahasa nchi jirani kama vile Kenya ,Uganda ,Rwanda ,Malawi nk. Mfano rejea mahusiano mabaya ya kisiasa na diplomasia yalivyoathiri soko la mchele na kusababisha hasara kwa wakulima wa mpunga. Rejea kushuka kwa soko la korosho nje ya nchi na kuyumba kwa wakulima wa korosho kule Mtwara na Lindi. Rejea kushuka kwa soko la mbaazi na dengu nje ya nchi. Pia rejea kushuka na kuyumba kwa soko la kahawa na mahindi nje ya nchi hasa Kenya. Matatizo yanasababishwa na siasa lakini matokeo yake ni umasikini kwa wakulima kwa kushindwa kurudisha hata gharama za kulimia ili kurudi tena msimu mpya wa kilimo.

(d) Uhakika wa soko; kwa asilimia kubwa umasikini wa mkulima unatokana na kukosekana kwa soko la uhakika. Mkulima bado anaendelea kuzalisha mazao yake huku aikwa hamjui mteja wake na zaidi hajui hata ni bei gani ataiuza hayo mazao yake. Mfano katika hili rejea habari za kukosekana kwa soko la uhakika wa nyanya zinazolimwa kule Ilula Iringa ,au Dumila na Kilosa kule Morogoro. Au jiridhishe kwa kuwauliza wakulima wa mpunga kule Mbeya ,Rukwa au Ifakara na Mvomero kule Morogoro. Kuna watu walipeleka nyanya Dar es salaam wakauza kwa hasara wakalipa nauli ya gari la mzigo hadi wakaishiwa nauli ya kurudi makwao. Wakulima wa nyanya pale Mangae ,Doma na Melela kule Morogoro waliamua kuwaachia nyani wale nyanya. Kwanini mkulima asiwe masikini kwa soko la kubeti namna hii?

(e) Kukosekana kwa uhuru wa kupanga bei ya mazao kwa mkulima. Mkulima hana uhuru wa kupanga bei ya mazao yake kama ilivyo kwenye bidhaa zingine. Anaandaa shamba,anapanda ,anatumia dawa na kuvuna kwa gharama na yeye ndio anayejua gharama husika lakini anamsubiri mnunuzi amtajie bei ya mazao yake. Basi hiyo bei mkulima angetajiwa kabla ya kuanza kilimo ajabu bei anapangiwa wakati akishavuna. Mfumo huu ungetumika hata kwa bidhaa kama simenti,bati na sukari basi wazalishaji wangeshindwa kuendesha shughuli za uzalishaji kwa ukubwa wa hasara. Kupangiwa bei na mnunuzi ambaye hajui bei ya pembejeo wala maandalizi ya shamba huu ni mfumo wa kumpa umasikini mkulima.

3:KILIMO KINAVYOWEZA KUKUPA UTAJIRI
Kwa asilimia kubwa wanao nufaika na kilimo sio wakulima wenyewe,ndio sio wakulima wenyewe bali ni wakulima wachache na makundi mengine ya watu. Makundi yafuatayo ndio yananufaika na kilimo.
(a) Wakulima wakubwa; hawa ni wale wakulima wachache wenye uwezo wa kulima kianzia ekali mia moja na kuendelea. Wana mitaji mikubwa ya kukabiliana na kilimo. Wana uwezo wa kulitafuta soko ndani ya nchi na nje ya nchi.
(b) walanguzi wa mazao; kundi hili ni watu wanaoenda kijijini na kutafuta kununua mazao kwa wakulima kwa bei nafuu sana . Wengine huyasafirisha nje ya nchi na wengine kuweka stoku hadi pale bei itakapokuwa nzuri. Wanatumia vipimo tofauti vya kununua na kuuzia. Wanajipangia bei wafikapo kwa wakulima.
(c) wamiliki wa mashine za nafaka; hawa ni wale wanaomiliki mashine kubwa za nafaka kama vile kukoboa mpunga,kusaga mahindi na kukamua alizeti. Wana uhakika na soko la ndani na nje ya nchi wanapata mazao kwa bei rahisi sana kutoka kwa wakulima. Mfano hata bei ya mahindi au mchele ikiwa mbaya Sana wao wana soko la uhakika na faida ya uhakika tofauti na mkulima ambaye hana namna kwa bei yoyote anayokutana nayo lazima auze.
(d) wamiliki wa viwanda vidogo vidogo na vikubwa.Hawa ni wale wamiliki wa viwanda kama vile vya kusindika nyanya au viwanda vya ngano kutengeneza bidhaa mbalimbali mfano biskuti mikate na maandazi, viwanda vya mafuta ya kura ya alizeti na ufuta , viwanda vya chai, kahawa na viwanda vya sembe nk . Viwanda hivi vinatengezeza faida kuliko mkulima.

4: SABABU ZINAZOFANYA WACHACHE WANUFAIKE.
(a) ukosefu wa mitaji; kilimo kimeonesha kuwa na faida sana lakini kwa wale wenye mitaji mikubwa ,wenye uwezo wa kulima mashamba makubwa,zana za kisasa na kupambana na changamoto ya soko la mazao.
(b) kukosekana kwa soko la uhakika; kukosekana kwa soko la uhakika kumefanya wakulima wengi kudidimia kiuchumi . Hili limesababisha wachache wenye uwezo wa kulitafuta soko wafanikiwe zaidi kwa kuwa faida ya kilimo iliyopaswa kwenda kwa watu wengi inakwenda kwa watu wachache. Mfano rejea mafanikio waliyonayo wenye viwanda vya sembe , mchele ni tofauti na mafanikio waliyonayo wakulima wa mazao husika. Rejea mafanikio waliyonayo wafanya biashara wa viazi ni tofauti na wakulima wa viazi huko Mbeya,Njombe na Iringa. Rejea mafanikio waliyonayo wafanya biashara wakubwa wa dengu huko Mwanza na Shinyanga ni tofauti na wakulima wa zao husika ukilinganisha hali yao kiuchumi.

5:NINI KITATOKEA KAMA HALI ITAENDELEA KUWA HIVI
Mambo mengi yanaweza kutokea ikiwemo;
(a) baa la njaa; wakulima wanaotumia pesa watakata tamaa kutokana na hasara za mara kwa mara. Wakulima watakao endelea ni wale wanaotumia nguvu kama mtaji. Mwisho tutazidi kukubwa na baa la njaa la mara kwa mara.
(b) kilimo hakitaweza kuchangia kutatua tatizo la ajira; tatizo la jira linaonesha kishamiri na sio kuisha. Kama kilimo kingewekewa misingi bora kingeweza kuwakusanya vijana waliomaliza vyuo mbalimbali nchini wakajiajiri huko. Lakini kutokana na kuwa kazi ya kubahatisha wengi wanashindwa kuwa na pakuanzia.
(c)umasikini kwa mkulima; hali hii niionayo sasa kama itaendelea basi siioni dalili ya mkulima kuondoka kwenye umasikini angali yeye ndio mzalishaji mkubwa na tegemeo kwenye sekta zingine.

6: NINI KIFANYIKE ILI KILA ANAYEJIHUSISHA NA KILIMO ANUFAIKE
Yafuatayo yanaweza kufanyika ili kila anayeshiriki katika sekta ya kilimo apate faida;

(a) Kwa serikali

(b)kwa mtu binafsi

Mtu mmoja mmoja anaweza kufanya haya ili kunufaika na kilimo

(c)kwa taasisi za mikopo
Taasisi za mikopo zina mchango mkubwa Sana katika kuinua sekta ya kilimo ikiwemo

HITIMISHO
Naamini kilimo kikiondolewa vikwazo basi itakuwa sekta nyeti zaidi na itakayoondoa tatizo la ajira kwa asilimia kubwa sana hapa nchini.
Uzi mzuri
 
uzi mzuri sana, umezungumzia mengi mazuri kuhusu kilimo, njia pekee ya kumsaidia mkulima ni kuanzisha scheme za umwagiliaji nchi nzima kwa maeneo, kuondoa kodi kwenye pembejeo za kilimo ili kupunguza gharama za uzalishaji pia serikali ianzishe chombo kitakacho tafuta masoko ya uhakika nje ya nchi, hii ndio njia pekee ya kuleta tija kwenye kilimo, vinginevyo tutabakia kulaumiana na siasa zisizokuwa na mwisho.
 
Back
Top Bottom