Kwa hapa Tanzania mwenye PhD ya ukweli aliyesomea akasota anatakiwa alipwe kiasi gani kama mshahara?

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Mimi napata tabu sana na wenye hizi shahada, Ninamaana ya kwamba Mtu ana PhD lakini anapambania kitu kidogo sana, hadi najiuliza huyu PhD yake kweli ni ya Ukweli na aliipambania kwenye tafiti na mengineyo ili aipate au ni feki, ni vile tu hawaja mkamata. Mara nyingi nimewaona wenye PhD wakihangaika na mishahara ya mil 2.5 kwenda chini hapo ni baada ya makato ya kodi ya serikali.

Kwa uelewa wangu mdogo mtu akiwa na PhD yeye mara zote huwa anatafutwa kutokana na field aliyoisomea na huwa ni ghali kidogo sio mtu rahisi kumlipa. Lakini nimeona mtu anapambana kuwa na cheo hata cha kati. Maeneo ambayo nimewaona wenye PhD wakilipwa vizuri ni Kenya, na wengine wanao lipwa Hapa Tanzania kwenye vyuo kama Arusha pale ESAMI na TRAPCA nilifurahi sana nikasema elimu ya hawa watu kweli wanaifaidi sana.

Nimalize tu kusema kwamba nina wasiwasi PhD nyingi sana sana ni za kuzawadiwa na zingine ni feki ndio maana watu wanajirahisisha kuangukia kazi ndogo na vyeo vidogo. Mpaka sasa waulize wametoa journal ngapi kwa mwaka ili wasomwe waliandika nn wanasema oh kazi za ofisi ni nyingi wakati kazi hizo za ofisin pia ni sehem ya tafiti, ya kujifunza na kuandikia makala na kushauri serikali, mashirika na jamii hata wanafunzi wa vyuoni.

Kifupi tu niseme kwamba rafiki zangu tunaoendelea kusoma tusome ili tupate vyeti tulivyo visomea kwa usahihi na iwe heshima na fedha tuzipate haswa.
 
Ndiyo Ukweli Wenyewe

Huo ndiyo ulio ukweli wenyewe.

Mengine haya ni jitihada za kuondoana kwenye reli tu mkuu.

Nani asiyejua kuwa kwa haki kabisa mtu hawezi kulipwa zaidi ya kile anachozalisha?

Kimsingi hakuwezi kuwapo exception yoyote, labda tu kwa mujibu wa katiba ya Tanzania iliyopo kuwahusu wabunge na vigogo serikalini.

Hiiiiii bagosha!
 
Huo ndiyo ulio ukweli wenyewe.

Mengine haya ni jitihada za kuondoana kwenye reli tu mkuu.

Nani asiyejua kuwa kwa haki kabisa mtu hawezi kulipwa zaidi ya kile anachozalisha?

Kimsingi hakuwezi kuwapo exception yoyote, labda tu kwa mujibu wa katiba ya Tanzania iliyopo kuwahusu wabunge na vigogo serikalini.

Hiiiiii bagosha!
Nawa~Zoom
 
Bongo kwenye elimu huwa tunajitesa sana.

Asilimia kubwa ya PhD holders wengi walisoma mpaka hizo level ili tu waitwe madokta.

Mfano mzuri Mwigulu na Magufuli.
 
Kwani kiongozi, mshahara mzuri unaanzia sh ngapi?

Lakin pia, Tanzania kwa ujumla hatujawekeza sana katika Research and Development! ndio mana wengi wa watu hawa wanategemea sana donor funded project.

Kuhusu misharaha, inategemea na mtu anafanyia wapi! upande wa taasis binafsi mara nyingi wanalipa mtu kutokana na output yake, ila serikalin wame Standardize mishahara kwa watumishi wa Umma kwa level zao za Elimu.

Sasa unaposema 2.5 ni kidogo, kulingana na Elimu, ungekuja na pendekezo iwe sh ngapi, lakini pia huwezi kumlipa mtu fedha nyingi wakati, nchi hatujawekeza katika tafiti.

Tukipunguza siasa na nchi ikawekeza katika wataalamu, naamin watu hawa watakuwa muhim na hakika itafaa walipwe pesa nyingi.
 
Baadhi ya wenye hizo PhD wanajipendekeza tu kwa mabosi kwenye hizo taasisi wanazofanyia kazi ila hamna cha maana.
Unakuta mtu ana PhD lakini mambo anayoongea na kumtetemekea bosi utafikiri ni darasa la saba.

Wengine ni kweli kuna mashaka kwenye hizo elimu zao.
 
well, nobody cares about your PhD au jinsi gani ulivyoipata.
kinachomatter ni ubora wa kazi zako unazozitoa.
au tegemea usipate kazi kabisa kama ubora wako ni hafifu kwenye field husika.

Yaani kisa una na phd ndio ulipwe mshahara mkubwa that's nonsene, who told you that?
 
PhD 2.5m? Ina maana mm na haka digilii kangu nawaacha mbaaali madokta kumbe on my takehome
 
hivi binadamu anaweza kutoa journal mkuu? 🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔. Hiyo journal anaitoaje, isije ikawa mtoa mada amekurupikia vitu asivyo vielewa.

Okay, ila kwa ninavyojua kila mtu husoma PhD kwa malengo yake. Mwingine anasoma ili apandiswe cheo, mwingine anasoma ili apate heshima ya kuitwa Dr. au Professor hapo baadaye.

Mwingine anasoma ili apate mwanya wa kufanya kazi za vyuoni. Kwa hiyo mtoa, mada usikariri waache watu na PhD zao.
 
Sasa huu si ni Mshahara wa degree holder anayeanza kazi ktk fani za Elimu na ualimu?!!!.
Umuhimu wa PhD kwa nchi kama Tanzania ni nini ? Hakuna investment yoyote kwenye research institutes sana sana tu wanaishia kuajiriwa kwenye academic institutions na penyewe hawatimizi majukumu yao wanaishia tu kufundisha (teaching) wakati Lecturer mwenye PhD anatakiwa afanye Teaching, Consultancy na Research....wanatakiwa walipe 700,000 kwa kutimizia jukumu moja la teaching !
 
Umuhimu wa PhD kwa nchi kama Tanzania ni nini ? Hakuna investment yoyote kwenye research institutes sana sana tu wanaishia kuajiriwa kwenye academic institutions na penyewe hawatimizi majukumu yao wanaishia tu kufundisha (teaching) wakati Lecturer mwenye PhD anatakiwa afanye Teaching, Consultancy na Research....wanatakiwa walipe 700,000 kwa kutimizia jukumu moja la teaching !
Sio wote mkuu, wengine Mchango wao unaonekana, wanafanya research ambazo zina tija kwa Taifa.
 
Back
Top Bottom