Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Hakuna trick yoyote, hiyo ni bahati ya mtende tu ilimdondokea jiwe, njia zote zilikuwa zimechorwa kuelekea kwa jasusi wa Rondo. Wajumbe waliomuweka ENL moyoni ndio walioamua kama wenzao jikoni wamemwaga mboga basi wao bora wamwage ugali tu wote wakose walale njaa.
Ila lazima ukubali Lowasa mpaka umauti unamkuta hakuwa na bifu na CCM...Alisharudi na walimalizana japo maelewano madogo hakuna ila sip bifu na CCM.
 
Kwenye siasa mambo ya kusalitiana ni kawaida na wanasiasa wanalijua hilo, Kinachofanya watu wamkosoe JK sio usaliti ni unafiki anaouonyesha na sio JK tu viongozi wengi wanaonyesha unafiki ila JK amekuwa # 1 on trending kwa sababu ya tukio la 2015.
All in all ....WANASIASA PUNGUZENI UNAFIKI HAYA MNAYOFANYA KWA EL NA NYIE MTAFANYIWA SIKU MUNGU AKIWAPENDA ZAIDI.

Hotuba yake ni fupi and clear
JK kabeba msalaba tu
But taifa halikumtaka lowasaa
 
Madaraka makubwa, usipokuwa na hekima, hasa hekima ya Mungu, yanalevya. Na ukikosa hekima unaweza kudhania kuwa wewe ni kila kitu, kwa sababu hakuna wa kukuhoji wala kukuadhibu.

Mathalani madaraka ya Rais wa Tanzania, anaweza kuyatumia vyovyote apendavyo, hata kuua, akitaka, na asihojiwe wala kushtakiwa mahali popote Duniani.

Lakini hawa watawala, kwa kukosa hekima huwa wanaamini kuwa hawawezi kuhojiwa Duniani, ahera wala hata na nafsi zao.

Marehemu Lowasa, aliuishi uaminifu kwa urafiki wake na Kikwete, lakini Kikwete alimsaliti na kumdhulumu rafiki yake.

Lowasa alijitoa kwa nguvu na moyo wake wote katika kuhakikisha Kikwete anakuwa Rais. Hata ndege iliyompeleka Kikwete Dodoma wakati anautafuta Urais, naambiwa iligharamiwa na Lowasa.

Serikali ya Kikwete ipopata msukosuko kutokana na kashfa ya Richmond, huku Msabaha akitamka wazi kuwa zigo la Richmond halikuwa lake kama waziri, kwa sababu wakati wote aliwasiliana na Serikali kupitia Waziri Mkuu, na hivyo kama kuna makosa, basi ni makosa ya Serikali nzima, Lowasa alimwendea Kikwete kumweleza kuwa yeye ameamua kujiuzulu ili kuilinda Serikali. Kikwete alikataa ombi la Lowasa kujiuzulu, lakini marehemu alishikilia msimamo wake, akiamini ndiyo njia ya kuiokoa Serikali ya Kikwete isidondoke, na pengine ipate imani ya aina fulani toka kwaWabunge.

Katikati ya safari yao, tofauti na makubaliano yao ya awali kuwa yeye marehemu amsaidie Kikwete kuwa Rais 2005, halafu Kikwete amsaidie marehemu kuutafuta Urais mwaka 2015, Kikwete alimtosa rafiki yake na kutaka Urais uende kwa mdogo wake.

Kikwete akifahamu wazi kuwa hakukuwa na mgombea yeyote ndani ya CCM na hata nje, wa kumzidi marehemu, akatumia madaraka yake, kuliondoa jina la Lowasa, lisipelekwe kwenye mkutano mkuu wa CCM.

Huku zaidi ya wajumbe 2,000 wa mkutano mkuu wa CCM wakiwa wamejiandaa kumpigia kura Lowasa RIP, kwa mshangao mkubwa wakaambiwa jina la Lowasa halipo.

Wajumbe wa mkutano mkuu, baada ya kuujua ukweli namna Kikwete alivyodhulumu haki ya rafiki yake wa awali ili Urais uende kwa mdogo wake, wakaitana nje, wakaambizana kuwa wale wote waliokuwa wamejiandaa kumchagua Lowasa, kura zao wampe mgombea aliyeonekana dhaifu kuliko wote, na ambaye amewekwa na Kikwete kama chambo. Ndipo ushindi ulipomwangukia Magufuli RIP.

Lowasa hakukata tamaa, aliamua kugombea nafasi ile ile kupitia CHADEMA. Sote tunayakumbuka mafuriko ya Lowasa. Lakini Kikwete akiwa amefunga mkataba wa kudumu wa kumdhulumu marehemu, huku majumuisho ya kura kutoka vituoni yakionesha wazi kuwa Lowasa alikuwa anaongoza kwa kura nyingi, aliwatuma Polisi kwenda kuvamia kituo cha ujumlishaji kura za Lowasa, wakapora computers zote, na kuwaweka mahabusu wajumlishaji wa kura.

Watanzania, nyakati hizi, tunaombeleza msiba wa Edward Lowasa, ambaye kiuhalisia ndiye aliyechaguliwa na wananchi kuwa Rais wa JMT mwaka 2015.

Lakini ni Kikwete pia, ndiye aliyemdhulumu ushindi wa Urais wa Zanzibar, Maalim Seif RIP.

Dhuluma ya Kikwete kwa marehemu hawa, itaitafuna nafsi yake mpaka siku yake ya mwisho. Madaraka yalimlevya, akaisahau haki. Akasahau kuwa madaraka ni kitu cha kuja na kupita, lakini haki huamua maisha yako ya leo na ya umilele.

Nina hakika, hata wakati huu wamsiba, watu watamtazama Kikwete kwa kujiuliza maswali mengi sana. Je, anaupenda sana na kuisikitikia mwili wa marehemu kuliko nafsi ya marehemu ilipokuwa hai?

Ndugu zangu, tutendeni haki ili tuwe na amani hadi siku za uwetu.

Kwa heri Lowasa, mtu uliyependwa na Watanzania walio wengi, ukadhulumiwa na wachache.

Mungu wa rehema, tunakuomba umtuze mja wako kwa raha ya milele kwani aliyathamini uhai wa wengine kuliko madaraka yake binafsi.
Kikweti hakumdhurumu lowasa, Bali aliwadhurumu watanzania haki ya kutawaliwa na raisi aliye mchaguwa wao. Kwa maneno kikwete ndiye aliye uwa watu wote walio uliwa na magufuli kwenye utawala wake. Mpaka Leo uonevu na wizi wa Mali, uuzwaji wa bandari na Mbuga za wanyama kwa warabu yote chanzo chake ni dhuruma ya Kikweti ya mwaka 2015.
 
Au ulikuja ku edit baada yangu kukujibu, basi mimi nilipoona tu yale makosa yako ya kiuandishi na kukujibu sikurudi tena kule juu kutazama maendeleo yako, nikaendelea na maisha mengine.

Hapa hoja wala sio tatizo, tatizo nilipokusoma kwa namna ulivyoandika nikaona huyu mtu kama ningekuwa karibu yake angenichapa makofi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Wewe ndiye umepanic. Mimi mara zote first post inakuwa na makosa halafu na edit.

Wewe ndiye umepanic.
 
Naona tunajichanganya tu, mkasa mzima wa Richmond ulishawekwa hapa JF kitambo nabulieleza mkasa mzima jinsi BT alivyousuka nanjumba bovu kumwangikia ENL. Sidhani kama aliomba nadhani mshambulizi yalimzidi ikabidi abwage manyanga. Akasema tatizo ni 'PM. PPP ENL
Tunajichanganya wapi?

Ukisema tunajichanganya bikanku point hapa ndipo yunapojichanganya, na kusema mambo generally tu ambayo yapo kwenye rekodi, na wewe unatuchanganya zaidi.
 
Hatari sana, kwahiyo mlitaka JK amsaidie EL kushinda Urais? Eti kwakuwa walikuwa marafiki? Kwahiyo tunaunga mkono Urais kugawiwa kwa minajili ya urafiki?.

EL alikuwa CCM na tabia hizi tunazomsema nazo JK ndio hizi hizi wana CCM wote wanazo, EL aliondoka CCM baada ya kukatwa pale Dodoma, kama alikuwa mwema alipaswa kuikacha CCM toka 1995 na sio kusubiri maslahi yalipokoma.

EL na JK wanajuana kuliko Mimi na wewe tunavyowajua, unapokwenda kumlaumu JK huku humjui EL kiundani nawewe itabidi tukuite mnafiki au mmbeya.

Mwenyezi Mungu ndiye anapanga kifo cha kila mtu na namna gani kitokee.
lowassa hakuhitaji sana msaada wa kikwete, kikwete analaumiwa kwa kupindisha mchakato ndani ya ccm ili kumfitini na kumdhibiti rafiki yake asipate uongozi
 
Nilichogundua
Kile alichosema ,mako da,kuwa EL alikuwa na kifua kipana!

Bora angeongeaga tu ,kukaa kwake kimya kumwacha balaa ,kunaumiza wasio husika,etc...
Japo Kwa muda ule ilikuwa sawa,ila duh,(km ni kweli)kusingiziwa kunauma unakaa na maumivu moyoni yanayoweza kudhohofisha afya .
 
Mbona ANC ilimchagua Jacob Zuma kuwa mgombea wake akiwa ananuka rushwa na ufisadi mtupu? Kwenye de facto monoparty kama hii yetu chama kinaweza kumpa mtu yeyote nafasi yoyote wanayotaka
.kuu,

Rwanda wameuana mauaji ya kimbari.

Na sisi tuuane mauaji ya kimbari kwa sababu Rwanda waliuana?

What kind of dilapidated logic is this?

Two wrongs do not make a right.
 
Ni siri iliyo wazi kwamba mfumo huo mzima unafuata maelekezo, muongozo na matamanio ya mwenyekiti
Badilisheni mfumo sasa, msimlaumu Kikwete.

Kwa sababu kama mfumo haujabadilika, hata Kikwete akifa, akibaki mwingine anaweza kuwachezea vile vile.

Tunaambiwa Nyerere alimkata Kikwete kwa kumbadilishia sheria wakati mchezo unaendelea. Tunaambiwa Kikwete alimkata Lowassa. Kama hayo ni kweli, Hili ni tatizo la kimfumo, si la mtu mmoja.

Tatizo la Watanzania wengi wanaangalia watu, badala ya kuangalia mfumo.
 
Back
Top Bottom