Kuzuiwa viroba: Konyagi waanza kufunga virago?

Kuzuiwa viroba: Konyagi waanza kufunga virago?

Hii ishu yote ya viroba ni muendelezo wa kutokua makini. Tatizo lilianza serikali ilipoamua kufumbia macho viroba kuuzwa kiholela.

Tulishauri sana vipigwe marufuku kungali mapema ila kwa kua labda walinufaika basi wakakaa kimya.

Sasa ni kuisoma namba kila mmoja. Atakaezidiwa atajua cha kufanya mbele ya safari. Maana hawa watu hawaeleweki.
 
Hiyo ni kutaka kulazimisha waendelee kuuza Viroba ili vijana na taifa la kesho liangamie...haiwezekani lazima watanzania Fujifunze kutofautisha biashara na afya za vijana wetu. Kwa hili waondoke tu!
Tatizo ni kifungashio au content
 
Bad News kwa Kweli,Ujue viongozi wa serikali wanajua wana uhakika wa kupata mishahara kupitia kodi zetu ndio maana wanadhani hii haiwahusu,bandu bandu inamaliza gogo,watapunguza wafanyakazi kodi itapungua,mzunguko utapungua,watakuja wengine hivyo hivyo mzunguko utapungua,wakija kukosa hata hela ya kujilipa mishahara ndio akili itatulia....Tuache Siasa kwenye maisha ya watu,chanzo cha kuharibika vijana ni viroba?
 
Nipelekeeni salamu sigara zimeniathiri sana nimekua teja nina uhakika mapafu yangu yameshakua na rangi ya tairi naomba muheshimiwa kama unanisikia ukataze sigara na vile viwanda vifungwe muheshimiwa siko peke yangu waathirika wa sigara tupo wengi muheshimiwa "inawezekana" tukawazidi waathirika wa viroba muheshimiwa
Kwan ulishikiwa fimbo au bomba utumie, kwenye packet kwenyewe wameandika "uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako" kwahiyo unatumia for your own risk hapa sijui unalilia nini kijana.
 
Ee Mungu, tulikokosea TUSAMEHE, haya mambo sio ya kukurupuka, hivi rais anaona Tanzania inakoelekea ama!!!! Amevaa miwani ya mbao?
 
Kutokana na agizo la serikali lililopiga marufuku uzwaji wa viroba hapa nchini Kiwanda cha TDL maarufu kama Kiwanda cha Konyagi kimeanza kufunga virago na kupunguza wafanyakazi, baada ya kuona wanapata hasara kubwa kwani wanazalisha lakini hawana Soko.

Wakizungumza baadhi ya viongozi wakubwa kiwanda hapo walisema kiwanda hicho kilikuwa kimesha uza mashine za kuzalisha Konyagi ya chupa na kuagiza mitambo ya kuzalisha viroba.

Jambo hilo limefanya waanze kupunguza wafanyakazi na kudai wataendelea kupunguza kwani mtambo mmoja wa kuzalishia Konyagi unaendesha na watu watatu tu kwahiyo wafanyakazi wengine wote waanze kutafuta sehemu ya kwenda.
Ndio maisha, sio wote tunazalisha viroba lakini wengi tunalazimika kupunguza wafanyakazi.

Ushauri wangu kwa waajiri wajitahidi kuwaeleza wafanyakazi ukweli na Kama watakubaliana basi mishahara ipunguzwe ili kila mmoja apate japo kidogo. Ukiwatoa kazini wataenda wapi?

Spending power ya mtanzania imeshashuka sana, wote sasa tunagombea wateja walioajiriwa serikali kuu, angalau hao ndio wenye hela
 
Issue sio viroba pekee

Iwe ni pamoja na kila aina ya pombe yenye % ya kilevi inayoathiri afya ikiwemo bapa na baadhi ya wine. Na pia sigala na mengineyo.

Kwa hayo nadhani wananchi tutakuwa vzr
Nadhani katika awamu hii tutashuhudia vifo vingi vinavyotokana na magonjwa yanayoathiri afya ya akili kama stroke, heart attack na hata suicides zinazotokana na depression, kusongwa songwa na authorities kunakopitiliza
 
Hili ndiyo tatzo la kuongozwa na watu wanaoshindwa kutumia akili ndogo tu kujua uchumi ukoje
 
Bora uchumi ufe lakini raia wabaki na afya salama ya mwili na akili tofauti na sasa ambapo vijana wamebadilishwa kuwa wagonjwa na vichaa sababu ya hayo maroba . Waende tutakunjwa bia
Kwani kilichokatazwa ni kinywaji chenyewe au kifungashio.ata ivyo mimi najua tabia ya watu wa jamii fulani kua namatumizi mabaya ya vilevi kama pombe kupindukia,bangi,madawa yakulevya na mengine kama ayo chanzo chake ni mmomonyoko wa maadili unaotokana na malezi mabovu.kama jamii haijitambui ayo ndo madhara yake.
 
Hiyo ni kutaka kulazimisha waendelee kuuza Viroba ili vijana na taifa la kesho liangamie...haiwezekani lazima watanzania Fujifunze kutofautisha biashara na afya za vijana wetu. Kwa hili waondoke tu!

Vijana Wa taifa LA kesho ndo walikuwa wanywa viroba?

Piwa imekuwa kama bia watu ata hawaogopi kuinywa Tena.
 
Hii ishu yote ya viroba ni muendelezo wa kutokua makini. Tatizo lilianza serikali ilipoamua kufumbia macho viroba kuuzwa kiholela.

Tulishauri sana vipigwe marufuku kungali mapema ila kwa kua labda walinufaika basi wakakaa kimya.

Sasa ni kuisoma namba kila mmoja. Atakaezidiwa atajua cha kufanya mbele ya safari. Maana hawa watu hawaeleweki.
the main issue here is why the young people are the major consumers of viroba?
 
Hiyo ni kutaka kulazimisha waendelee kuuza Viroba ili vijana na taifa la kesho liangamie...haiwezekani lazima watanzania Fujifunze kutofautisha biashara na afya za vijana wetu. Kwa hili waondoke tu!
Mkuu wangu tanzania si nchi ya kwanza kuuza liquor, spirits etc watu wanakusanya mapato nchi za wenzetu kwa hizi pombe ni aibu kuhurumia afya ya mnywaji alafu ukamthamini mvuta sigara eti vijana wanaangamia, alafu eti unataka kukusanya mapato kupitiliza malengo utakusanya kwa nani sasa au wanataka kutuua watu wa chini.
 
Nadhani katika awamu hii tutashuhudia vifo vingi vinavyotokana na magonjwa yanayoathiri afya ya akili kama stroke, heart attack na hata suicides zinazotokana na depression, kusongwa songwa na authorities kunakopitiliza
aisee ile habari ya mfanyaiashara aliojiua Dodoma sio poa kabisa imagine mtu anafuata taratibu zote anashehena za billion moja halafu anakuja ny'ang'anywa dah...SAD...tujiangalie aisee ...maana hizi biashara ndo zinaongeza kutoa kodi yaani
 
Back
Top Bottom