Kuzuiwa viroba: Konyagi waanza kufunga virago?

Kuzuiwa viroba: Konyagi waanza kufunga virago?

hii habari ni ya uchochezi mleta mada jiandae kushughulikiwa
Acha vitishonendavkonyagi kaangalie watu wangapi hawana kazi, kuna mashine imeletwa mpya imefanya kazi miezi miwili tu leo wanaipeleka wapi? Acha vitisho wewe.
 
Hiyo ni kutaka kulazimisha waendelee kuuza Viroba ili vijana na taifa la kesho liangamie...haiwezekani lazima watanzania Fujifunze kutofautisha biashara na afya za vijana wetu. Kwa hili waondoke tu!
Suala la afya ya vijana kuangamia linatoka wapi tena wakati Tanzania Distillers wana leseni ya uhakiki ya TFDA na TBS ktk viwango vya ubora wa products zao? Kama ni suala la hivyo viroba toka nje ya nchi serikali basi izuie "Import" zake lakini konyagi waendelee na biashara for the benefit of our Economy. Kama ni suala la vijana kunywa kupindikia hili linahitaji elimu toka kwa wadau mbalimbali kwani hata kahawa ina madhara ikitumiwa bila kiasi.
 
Nimekuta mahari konyagi kubwa inafunguliwa wanapima kipimo kinachoendana na hera yako halafu inafungwa kusubiri mteja mwingine
Sasa watapimia tot kwenye nyungo za wauza sigara mkuu?? Bado itakuwa ngumu watu kuinjoy,kiroba ulikuwa unanbeba unatia mfukoni mkuu![emoji12] [emoji39]
 
Viroba vilisaidia kukuza uchumi, kama tatizo ni vijana kuharibika kwanini vijana hawa wasipewe somo juu ya madhara ya pombe na kuhakikisha mnunuaji ana kitambulisho awe na umri Zaidi ya miaka 21 au zaidi?
Vijana wa sasa hawaeleweki,sisi zamani tulikuwa tukipewa pombe na wazazi lkn maisha yanaendelea kama kawaida,tatizo siyo viroba tatizo ni kizazi chenyewe hakijui kutofautisha muda wa kazi na muda wa starehe,ushauri wako ni mzuri sana ila vijana wa sasa si wa mchezo mchezo[emoji29] [emoji23]
 
Viroba vilisaidia kukuza uchumi, kama tatizo ni vijana kuharibika kwanini vijana hawa wasipewe somo juu ya madhara ya pombe na kuhakikisha mnunuaji ana kitambulisho awe na umri Zaidi ya miaka 21 au zaidi?
Haswaa,kama ambavyo wanatahadharishwa kuwa 'uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako'.
 
Viroba vilisaidia kukuza uchumi, kama tatizo ni vijana kuharibika kwanini vijana hawa wasipewe somo juu ya madhara ya pombe na kuhakikisha mnunuaji ana kitambulisho awe na umri Zaidi ya miaka 21 au zaidi?
Mama hata mtu zaidi ya miaka 21 anaathirika.Tatizo si umri.I wish kungekuwa na marufuku ya pombe zote na sigara!
 
Kutokana na agizo la serikali lililopiga marufuku uzwaji wa viroba hapa nchini Kiwanda cha TDL maarufu kama Kiwanda cha Konyagi kimeanza kufunga virago na kupunguza wafanyakazi, baada ya kuona wanapata hasara kubwa kwani wanazalisha lakini hawana Soko.

Wakizungumza baadhi ya viongozi wakubwa kiwanda hapo walisema kiwanda hicho kilikuwa kimesha uza mashine za kuzalisha Konyagi ya chupa na kuagiza mitambo ya kuzalisha viroba.

Jambo hilo limefanya waanze kupunguza wafanyakazi na kudai wataendelea kupunguza kwani mtambo mmoja wa kuzalishia Konyagi unaendesha na watu watatu tu kwahiyo wafanyakazi wengine wote waanze kutafuta sehemu ya kwenda.
Konyagi ni wahapahapa wewe!waende wapi?acha majungu.
 
Back
Top Bottom