Kuwekana kwenye profile picha ndo kipimo cha upendo?

Kuwekana kwenye profile picha ndo kipimo cha upendo?

Ni usanii huo anaweka ili uamini uko peke yako hata akichepuka............watu wanagonga wake za watu bila aibu hiyp dp ni geresha tu
 
Hata mantiki ya mimi kuipost sura yake kwenye profile yangu siioni sana

Mimi ilimradi nimembeba moyoni baasi hilo ndio la muhimu zaidi.
Ishu ni kwamba moyoni nani anaona??dp tunaona nwn
 
Kama unamshuku mpenzi wako na ghafla ukaona kakuweka DP, ujue hapo tayari kashawa block wenzako wote. Binafsi nilishafanya sana hii mambo🙂
 
Kama raha yako ya mapenzi ni kupendwa basi amini unapendwa no matter what. Ila mapenzi ni kitu moja ngumu sana hasa kwa kizazi hiki kinachowaza ujinga zaidi.

Kuna watu wana act wanapenda mpaka wanavaliana nguo na waume zao lakin bado wanagongwa vizuri tu. Mtu anadiriki kupokea simu ya mumewe huku anasex na mwanaume mwingine bila hata haya. Na anambembeleza mumewe huku anaugulia maumivu ya mashine ya mwingine live.

Leo uniambie kuna kipimo cha mapenzi, we kama unaamin mwenz anakupenda, amini kwisha habari but hakuna kipimo cha mapenzi.
Ebw eeh, nadhani wewe upo aged.
Majibu yako ya kikomavu mno na yamekwenda shule.
Kwenye tasnia ya mapenzi hasa ya ki-leo kuna uongo wa kila sampuri.
Lakini kumuelewa mtu anayekupenda kwa dhati ni jambo rahisi mno, kuliko hata hicho kiashiria cha kudanganyana kwa profile pictures, usanii mtupu.
Mtu, (sijatumia mpenzi) akupendae kwa dhati utamsoma kwa dalili kuu zifuatazo.
Kwanza yakupasa umuelewe tabia yake halisi nje ya mahusiano yenu, yupoyupoje.
Pili, angalia anavyokuhendo wewe.
Kama anakauli za kihuni maeneo mengine, kwako atakunyenyekea kwa kauli za kiungwana.
Kama katili katika maeneo mengine, kwako atakuwa mpole na mnyenyekevu.
Kama ni mchoyo, ataficha kwa wengine na kukuwekea wewe.
Kama atakuwa ni mwizi, kwako atakuwa mwaminifu na kuificha tabia yake hiyo ovu.
Kama ni mhunimhuni, kwako atajirudi nakujiweka katika mstari.
Umpigiapo simu, aionapo namba yako, moyo wake hujawa na furaha tele na kupelekea kuipokea kwa unyenyekevu, ki-panick bila kupoteza hata sekunde moja.
Yapo mengi sana yanayoashiria upendo wa dhati. Na hayo machache niliyoeleza, mtu haombwi wala kufundishwa kukutendea wewe, bali hujituma mwenyewe, kwa hiyari yake bila kulazimishwa.
Ukiona mtu anaendeleza yale matendo yake halisi ya hovyo katikati ya penzi, elewa haujapata akupendae kwa dhati.
 
Back
Top Bottom