The ghost writer
JF-Expert Member
- Apr 5, 2023
- 835
- 1,717
Huu ni mwendelezo wa kuendelea kufanya "diagnosis analysis" ya aina maarufu za Profile Pictures zinazotumiwa sana na watumiaji wa mitandao ya kijamii hasa GenZ. Jinsi zinavyoonekana, na uhalisia wa Maisha Yao Mtandaoni na kwenye maisha halisi. Nje ya mitandao ya kijamii.
1.The Filtered Face PFP.
Hizi ni zile picha ambazo zimepigwa na Kisha kuwekwa filter, mfano wa filters za Snapchat au Instagram. (Mfano; ni ile yenye masikio na pua ya mbwa, filter inayong'arisha uso mpaka ncha ya pua inapotea, au ile inayoweka vipepeo kichwani)
Hawa ni watu wanaotumia teknolojia kupitiliza ili kuondoa makasoro yao yote ya kibinadamu.😅
Huu hapa uchambuzi wao Ndani ya Mtandao.
Kwenye kila post au selfie anayoweka, captions zake ni za kujiamini sana: "Born to shine ", "Natural beauty ", au "I woke up like this." Kazi yake ni kupokea sifa tu kwenye comments: "Wow, mzuri wewe!" naye anajibu kwa upole: "Asante mwaya 🥰."
Nje ya Mtandao (Uhalisia wa Maisha)
Ile picha yake ya profile unavyoiona ilihitaji kazi kubwa sana. Mwenye hiyo profile, Alikaa chumbani kwake masaa mawili😅, akijipiga picha (selfies) zaidi ya 150 huku akigeuza kichwa kushoto na kulia, akijaribu filter 15 tofauti. Hatimaye alipopata moja ambayo ilificha kila kitu kinachomsumbua, ndipo akaiweka mtandaoni kwa furaha.😂
Wakati picha yake ya profile inamwonyesha kama mtu anayeishi maisha ya usafi wa hali ya juu, lakini uhalisia wake ni tofauti. Kwenye meza ndani ya chumba chake kuna mrundikano wa mafuta ya jeli ya shilingi mia tano, mikorongo ya siri, na kioo kidogo kilichopasuka ambacho anakitumia kila siku kujikagua kabla ya kuwasha filter za simu yake.😅
Ana uoga mkubwa sana wa kupigwa picha na simu ya mtu mwingine, hasa zile simu zenye kamera halisi zisizo na filter (kama iPhone au Samsung mpya). Utamsikia akisema: "Ah hapana, mimi sitaki leo, sipo vizuri." Anaogopa ukweli usijulikane! 😅
2.The joker or smiler PFP.
Hili ni lile kundi la watu wanaoweka picha za watu halisi (iwe ni wao wenyewe au za wahusika wengine maarufu). Zikionekana wakiwa wameachama midomo kwa kicheko cha nguvu au tabasamu pana la "maisha ni matamu.😅
Maisha Yao Ndani ya Mtandaoni;
Kila post yake anataka kutuaminisha kuwa maisha yake hayana stress. Utamkuta ameweka mfano was captions kama: "Live, Laugh, Love" au "Tabasamu lako ndio ngao yako 😊.
Kwenye kila comments Kazi yake ni kusambaza upendo tu. Haonyeshi Maumivu hata mambo yawe magumu vipi, utamkuta na "emoji za moto 🔥, mioyo ❤️, na mikono ya kusifu 🙌". Picture yake ya profile inakuambia, "Mimi hapa duniani nimekuja kutalii, siumizwi na kitu.
Nje ya Mtandao (Uhalisia wa Maisha)
Ndio yule mtu ambaye kila sekunde analalamika kuhusu hali ya maisha, jinsi viatu vinavyombana, au jinsi foleni ya daladala inavyomchosha. Yale maisha ya "Live, Laugh, Love" yanapotea akiliona jua la mchana.😅
Ile picha inayomuonyesha anacheka kwa furaha? Alipiga picha zaidi ya 80, na mpaka anafikia hilo tabasamu, mpiga picha alimwambia, "Kaka hebu cheka basi, mbona unatazama kama unataka kupigana?" Ni kicheko cha kulazimisha baada ya kuchoka kusimama!😅
3. The drama fun girl PFP.
Hao sasa ndio "Marais wa Mahakama ya Udaku" Mtandaoni.
Hizi Huwa ni picha za msichana, (zikiwa ni picha zao halisi/Picha za watu wengi wasio maarufu ) Msichana mrembo akiwa ndani ya gari, ndani ya restaurant ya gharama akiwa ameshika kikombe vya chai, au ndani ya ndege akichungulia pembeni dirishani, Mtandaoni huwa wanaishi kwa ajili ya mtafaruku tu.😅
Huu hapa mchambo wao wa kichekesho:
The Gossip Queen. Watafuta Udaku. Ndio wa kwanza kucomment chini ya post yoyote ya mjadala mzito au ugomvi wa wasanii. Utawakuta wameweka emoji za popcorn (🍿) au wameandika: "Nipo hapa nisijekupitwa🙌" " tafadhari msinipite!🙏😂" . N.k
Kwenye Kila posts wanakomenti maneno mengi ya kushtuka kama "OMG!", "Eeeh jamani!", au "Kuna nini tena?" Wanajua jinsi ya kufanya jambo dogo lionekane kama ndio dharura ya kitaifa.😅
Kama ni rafiki/shoga yake au staa wao wanayemkubali akihusika kwenye drama yoyote, watakesha usiku kucha Instagram na TikTok au hata Hapa Jamiiforums wakimtetea kwa kuandika aya ndefu kuliko katiba ya nchi.😅
Kwenye Maisha Halisi (The Reality Check)
Mtandaoni wanaonekana kama watu wenye makeke na wanaojua siri zote za mjini, lakini live wanaweza kuwa ni watu wapole mno wanaoshinda wamejifungia chumbani wakiangalia tamthilia kwenye simu huku wameshinda wakila viazi vya kuchemsha. 😅
Pamoja na kupenda drama za mtandaoni, ukijaribu kugombana nao live au kuwafokea, ndio wa kwanza kulia haraka sana kisa tu sauti yako imekuwa ya ukali.
Ni watu wenye hisia za haraka sana. Wanaweza kuangalia tamthilia ya uongo ya masaa mawili na kulia machozi ya kweli kabisa utadhani aliyefariki kwenye muvi ni ndugu yao wa damu!
4. The Flowers or Butterfly PFP.
Hawa ndio "Malaika wa Amani" mtandaoni.
Ni picha zinazopendwa sana na kina mama wa makamo, wadada wapole, hawa ni watu wanaotaka kuaminisha ulimwengu kuwa roho zao ni safi kama theluji.😅
Uchambuzi ndani ya Mitandao ya kijamii. (Social media check)
Ndani ya Mitandao ya kijamii, Kazi yake kubwa ni kusambaza jumbe za asubuhi njema, "Heri ya Jumapili", au "Mungu ni Mwema kila wakati 🙏
"Kwenye comments anajaza emoji za maua . Hawezi kuandika neno bila kuweka kuweka mikono ya kusali 🙏. Hawapendi Shari, Ukijaribu kubishana naye, anakujibu kwa upole mkubwa: "Barikiwa sana ndugu yangu," au anaweka tu emoji ya tabasamu na kuondoka. Utadhani hajawahi kukasirika tangu azaliwe.😅
Nje ya Mtandao (Uhalisia wa Maisha)
Simu yake inajaa masaa yote kwa sababu ya kudownload picha 500 za "Asubuhi Njema" alizotumiwa kwenye magrupu ya kifamilia.
Ndani ya mtandao anajifanya ni mtu wa amani na upendo, lakini maisha halisi nyumbani kwake? Yeye ndio simba wa familia! Ukisikia mtu anafokea watoto au wadogo zake asubuhi na mapema kwa sauti ya radi: "Nani ameacha vyombo havijaoshwa hapa?! Mna laana nyie!", basi ujue ni huyu mmiliki wa picha ya ua la waridi.
5. The Gym Selfie PFP.
Watu wenye hizi profile wanajiona tayari wao ni "Mawaziri wa Mazoezi na Protini (lishe)" mtandaoni. 😅
Hii ni ile picha ya mtu aliyesimama mbele ya kioo kikubwa cha gym, ameshikilia simu kwa mkono mmoja huku amekaza misuli ya mkono mwingine, au ni zile Picha zilizopigwa Wazee wa kazi wakiwa GYM.
Huu hapa uchambuzi wao Ndani ya Mtandao
Mtandaoni kazi yake ni kuweka picha za spika, vyuma, na unga wa protini (protein powder) mtandaoni, akiaminisha watu kuwa masaa 24 ya maisha yake anashinda akisukuma vyuma.😂
Mtandaoni ni Fitness coach Kwa Kila beginners anayeingia Gym, Anapost videos za dakika 15 akitoa lecture kuhusu splits, push ups, push pull legs... N.k utadhani ana PhD ya hypertrophy .😅
Ana playlist za Kila motivational videos, Mfano; "Discipline over everything.”, “Pain is temporary.”, “Built, not born.” ,Ukiangalia posts zake zote utadhani anaendesha mafunzo ya kijeshi, kumbe jana alifanya chest, biceps na akaenda kunywa juice.😂😂
Anaamini Kila Tatizo Lina Solution Ya Gym utamsikia akisema; Una stress?“Gym bro.” Umeachwa?“Gym bro.”Huna kazi?“Gym bro.”Una deni?“Gym bro.”Umekosana na familia?“Gym bro.” Hata kama moyoni unaweza kuwa unateketea lakini yeye: “Stay focused. Hit the gym.”😅
Kwenye comments anajaza emoji za ngumi 👊, misuli 💪, au moto 🔥. Hawezi kupongeza mtu bila kumwita "Mwamba" au "Bro."
Nje ya Mtandao (Uhalisia wa Maisha)
Hawa ndio wale utawakuta Gym wakishinda huku wanajitazama kwenye Kioo cha gym masaa 24.Kila akipita karibu na kioo anasimama akijiangalia misuli yake ilivyovimba Kisha anajipiga Picha .
Wakati mtandaoni anahubiri kuhusu milo maalum ya kujenga mwili (diet). Lakini uhalisia wa maisha ya nyumbani ni tofauti. Akishuka tu kwenye daladala akitoka gym, anapitia kwa mama ntilie na kuagiza: "Mama niletee ugali mkubwa wa buku, maharage, na mchuzi mwingi wa bure!" Maisha ya kula protein siku nzima ni bei ghali anashindwa kumudu.😅
Ana miguu ka Mishikaki. Kwenye picha ya profile anaonyesha tu kifua na mikono kwa sababu anajua siri yake kubwa hafanyagi mazoezi ya miguu (Leg Day). Utamuona huko mtaani, hapendi kuvaa jeans ya kubana bali anava jeans inayolegea(track) au bukta huku miguu yake ikiwa miembamba kama kiberiti, utadhani mwili wa juu umeazimwa kutoka kwa mtu mwingine.😂
Ana nguvu za kunyanyua vyuma vya kilo 80 gym kwa ajili ya sifa za mtandaoni, lakini mama yake akimwambia: "Sogeza hili kabati lisogee huku," anaanza kulalamika: "Ah mama, mgongo unaniuma sana leo, nimetoka kufanya mazoezi makali."
Part 4...is coming