N'yadikwa
JF-Expert Member
- Aug 10, 2014
- 6,869
- 9,692
Naomba niwakosoe watoa maamuzi. Kwanini feeder roads za barabara kuu itokayo Mafinga-Mgololo zina lami lakini hii barabara kwa miongo kadhaa sasa lami inaombwa lakini haiwekwi!? SERIKALI TAFADHALI WAANGALIENI WANANCHI WA ENEO HILI LA MAFINGA MGOLOLO kuna uchumi sana huko lakini mabarabara hayako vizuri.
Kilichonistaajabisha ni kwamba 35 Kilometre kutoka Mafinga town barabara zinazoingia vijiji vya ndani kama Sawala-Kitiru tayari ina lami kwa sehemu na Sawala-Iyegeya lami inabandikwa sio muda kazi inaendelea!
Sasa najiuliza kwanini hili barabara muhimu linalopitisha bidhaa muhimu kama Karatasi kutoka Mgololo factory,Mbao kutoka Saohill na kwa wakulima binafsi wa miti,Chai,Pareto,parachichi,Cinchona(hii ni mitishamba inayovunwa kupelekwa viwanda vya dawa na sumu kama ilivyo pareto),Magogo ya nguzo za umeme nk, nguzo za uzio,mabanzi nk, pia Halmashauri ya Mufindi hili ndo barabara lake kuelekea huko makao makuu mapya yanayotarajiwa haliwekwi lami!?
Tafadhali fanyeni huu mradi uanze lami lipite huko tuharakishe maendeleo zaidi ya sasa kama inavyofanyika kuweka lami huko ndani zaidi lakini mtu akitokea huko anakuja kukutana na barabara la vumbi tena hadi afike Mafinga.
Ikumbukwe huko kuna viwanda zaidi ya Vitano vya chai tu. Tuyatendee haki maeneo yanayotuingizia mapesa ya kutosha ikiwemo Mufindi.
Nawapongeza maji yamefika ila mabarabara kwa kweli bado.
PICHA: Hilo barabara panapoonekana anga la rangi ya Orange ndilo nalolizungumzia hapa hilo linaenda Mgololo kiwanda pekee cha kuchakata magogo ili kutengeneza karatasi katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.
PICHA NYINGINE: Barabara la Sawala Village linalokwenda Luhunga ambalo linapachikwa lami lije kukutana na hilo la Mgololo.
Wananchi huko wanachakalika kweli ila barabara bado mtikhani!