Rais Magufuli Barabara ya Mafinga-Mgololo saidia ijengwe kwa lami

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,826
9,533
Mheshimiwa rais Barabara hii ni muhimu sana inaunganisha wilaya ya Mufindi ambayo imo katika top 5 za uzalishaji wa viwanda hapa Tanzania lakini barabara hiyo inayoanzia mji wa Mafinga kupitia Mtili ,Sawala hadi kiwanda kikubwa cha Karatasi Afrika Mashariki na Kati cha Mgololo ni mbovu sana na kila ikijengwa kwa changalawe inabomoka haraka kwani mvua ni nyingi na Malori mazito ya mizigo yanapita kila mara.

Mheshimiwa rais wabunge wa jimbo hili wamekuwa wakiahidi kusimamia ijengwe kwa lami tangu miaka ya 80 lakini ahadi hazitekelezwi.

Ikumbukwe barabara hiyo inahudumia viwanda vya chai vya Itona,Lugoda,Kiwele,Kilima hivyo viwanda vinne ni vya chai....Pia inahudumia kiwanda cha karatasi Mgololo...Kuna kiwanda cha nguzo za Umeme cha Mehrab...Kuna wafanyabiashara wa kati kwa Mamia wanaviwanda vidogo na vya kati vya mbao,nguzo nakadhalika.

Lakini pia wilaya hii inazalisha mazao mbalimbali ya chakula na matunda yanayolisha miji hususani ya juu kusini.

Aidha kuna kilimo cha Kahawa kutoka Lulanda nk...Kwa ufupi Mheshimiwa Rais wilaya hii imesahaulika sana kujengewa barabara hii kwa kiwango cha lami....tafadhali toa agizo hawa wasaidizi wako wakamilishe ujenzi wa barabara hiyo mapema kwani imekuwa kero ya muda mrefu....Na kama ukifanya ziara huko Iringa Mheshimiwa tembelea kipande hicho ujionee mwenyewe...Mufindi inazalisha sana ila barabara haina...LAMI LAMI KWA MAFINGA MGOLOLO ROAD.
 
Mmhhh hili kweli tatizo ila wahusika watasikia kilio chako mkuu naijua sana hiyo njia ,kiukweli ni njia nyeti sana
 
Naunga mkono hoja.
Mufindi ni ilijaaliwa rasilimali nyingi sana. Hakuna barabara ya lami isipokuwa tu barabara kuu kwenda Mbeya iliyojengwa mwaka 1970.
Mufindi kuna mvua za kutosha
mazao kama mahindi,viazi,kahawa,chai na misitu kwa ajilj ya mbao, nguzo za umeme na karatasi.
Sijui tatizo ni nn. wakati mikoa mingine barabara za lami za kuunganisha vijiji
WABUNGE WAWILI MLIOPO TENA MIAKA KIBAO MNAFANYA NN?
 
Back
Top Bottom