Narudia tena: Serikali wekeni lami barabara ya Mafinga-Mgololo

Narudia tena: Serikali wekeni lami barabara ya Mafinga-Mgololo

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,307
Reaction score
12,810
Ndugu mnaoongoza serikali wekeni lami barabara hii muhimu kule Mufindi.

Barabara hii inaunganisha maeneo muhimu ya uzalishaji yenye viwanda kv:-
1. Kiwanda cha Karatasi Mgololo
2. Kiwanda cha majani-chai Rift Valley
3. Kiwanda cha majani-chai Brooke Bond
4. Kiwanda cha majani-chai Kilima
5. Kiwanda cha majani-chai Lugoda
6. Kiwanda cha nguzo za umeme cha Mehrab
7. Mashamba ya miti ya kupanda ya serikali
8. Nakadhalika...

Tafadhali jengeni kwa kiwango cha lami barabara hii...kila siku magari yanapita kuelekea kwenye viwanda hivi kupeleka malighafi za uzalishaji na kurudi na bidhaa kwa soko la ndani na nje...ni kwanini miaka nenda Rudi barabara hii tunaipigia kelele haijengwi???.... tafadhali ijengeni ili tuwaelewe...bado hatuwaelewi mmeahidi sana...itoshe!!!!
 
Sijawahi kufika huko, lakini masuala hayo ya barabara yana bodi yake: Bodi ya Barabara ya Mkoa (Road Board) ambayo Mwwnyekiti ni RC wajumbe ni DCs, Directors- LGAs, Viongozi wa Tanroads nadhani na wenyeviti/meya wa LGA. Kikao kikitoa azimio huwa linafanyiwa kazi.

My point is, kwa vigezo hivyo ukiomba kuwasilisha mada juu ya barabara hiyo kwenye kikao chao linaweza kufanyiwa kazi.
NB: ili kuweka nguvu zaidi, wenye taasisi ulizoaisha wakutane na kumuona RC kumweleza ombi hilo.
 
Wako bize na jichupi la nandi atwezi kukusikiliza samahani sana
 
Back
Top Bottom