Barabara ya Mafinga Mgololo, barabara muhimu Tanzania iliyotelekezwa

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
6,825
9,533
Barabara ya Mafinga Mgololo kwenye kiwanda cha karatasi imetelekezwa.

Barabara hii inazalisha sana kwa sababu huku inakoelekea kuna viwanda lukuki vikiwemo:-
1. Kiwanda cha Karatasi- Mgololo
2. Kiwanda cha Hardboard- Mgololo
3. Kiwanda cha Chai - Lugoda
4. Kiwanda cha Nguzo za Umeme- Mehrab
5. Mashamba ya Msitu wa Taifa wa kupandwa - Sao Hill
6. Kiwanda cha Chai- MTC Mufindi Tea Company
7. Mashamba ya Cinchona(miti ya kutengenezea dawa)
8. Hoteli ya Kitalii-Fox Tanzania
9. Kiwanda cha Chai - Kilima
10. Kiwanda cha Chai - Kibena
11. Uvunaji mkubwa wa mazao ya miti kv mbao, magogo ya nguzo za umeme na hardboard
12. Kilimo cha Parachichi
13. Kilimo cha Kahawa
14. Kiwanda cha Nguzo Mtili
15. Viwanda angalau viwili vya Hardboard vilivyopo Mtili
16. HQ ya Halmashauri ya Mufindi iliyopo Itulavanu
17. Kiwanda cha Chuma- Luganga
18. Taasisi mbalimbali za Elimu kv Igowole secondary, Madisi Secondary, Village Schools Sawala Chuo cha Ualimu Iyegeya nk

Nakadhalika

LAKINI ajabu ni kwamba kwa zaidi ya miaka 30 sasa ahadi ya kuiwekea LAMI hii barabara haitekelezwi.

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan SISI wakazi wa MUFINDI hatuelewi ni kwanini barabara hili linaloanzia MAFINGA haliwekwi lami!?. Tunaomba uingilie kati wasaidizi wako wanakuangusha tuwekewe lami ili uzalishaji uwe na tija. BARABARA HILI NI BOVU SANA.

Na tunaomba litakapojengwa LIJENGWE kwa viwango sababu malori ya mizigo yanapita sana kwenye barabara hili MUHIMU mno kwa uchumi wa nchi yetu.

20220309_092717.jpg
20220309_092704.jpg
 
Mkuu juzi nilikuwa msibani hapo sawala. Nilikaa kwa saa moja kuhesabia ni ndinga ngapi zinapita. Aisee gari kumi zenye nguzo za mbao zenye mzigo wastani wa millioni 30.hilo ni saa moja tu.
Hii barabara ubovu wake unawanufaisha wachache. Yaani fungu la kila mwaka la kuweka kifusi kuna wachache wanapiga hela kila mwaka. Ahhh ikiwekwa lami watakula wapi??

Anyway kuwepo kwa lami kijijini kwangu mkonge hadi iyegeya kunaweza kuwafanya wqone aibu waieke lami.
Nb. Mkuu hiyo picha ya 2 uliyopiga mahali uliposimama inaonekana palikuwa na tukio na hilo tukio lilitukutanisha week hii bila kujuana. Fanya kuni pm

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msibani kwa mzee mmoja maarufu hapo Sawala nilikuwa hapo pia...inatia aibu kwamba barabara uliyoisema inayoanzia Njiapanda ya Lupeme Sawala village imewekwa lami...lakini pia barabara ya Kitiru isiyo na matumizi mengi pia imewekwa lami...nahisi kuna watu wananufaika kama usemavyo kuweka molam kila mara hapa...
 
Kwenye picha number mbili sio kitasengwa hapo?
Nimesoma na kufanya maisha pande hizo.
 
Barabara ya Mafinga Mgololo kwenye kiwanda cha karatasi imetelekezwa.

Barabara hii inazalisha sana kwa sababu huku inakoelekea kuna viwanda lukuki vikiwemo:-
1. Kiwanda cha Karatasi- Mgololo
2. Kiwanda cha Hardboard- Mgololo
3. Kiwanda cha Chai - Lugoda
4. Kiwanda cha Nguzo za Umeme- Mehrab
5. Mashamba ya Msitu wa Taifa wa kupandwa - Sao Hill
6. Kiwanda cha Chai- MTC Mufindi Tea Company
7. Mashamba ya Cinchona(miti ya kutengenezea dawa)
8. Hoteli ya Kitalii-Fox Tanzania
9. Kiwanda cha Chai - Kilima
10. Kiwanda cha Chai - Kibena
11. Uvunaji mkubwa wa mazao ya miti kv mbao, magogo ya nguzo za umeme na hardboard
12. Kilimo cha Parachichi
13. Kilimo cha Kahawa
14. Kiwanda cha Nguzo Mtili
15. Viwanda angalau viwili vya Hardboard vilivyopo Mtili
16. HQ ya Halmashauri ya Mufindi iliyopo Itulavanu
17. Kiwanda cha Chuma- Luganga
18. Taasisi mbalimbali za Elimu kv Igowole secondary, Madisi Secondary, Village Schools Sawala Chuo cha Ualimu Iyegeya nk

Nakadhalika

LAKINI ajabu ni kwamba kwa zaidi ya miaka 30 sasa ahadi ya kuiwekea LAMI hii barabara haitekelezwi.

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan SISI wakazi wa MUFINDI hatuelewi ni kwanini barabara hili linaloanzia MAFINGA haliwekwi lami!?. Tunaomba uingilie kati wasaidizi wako wanakuangusha tuwekewe lami ili uzalishaji uwe na tija. BARABARA HILI NI BOVU SANA.

Na tunaomba litakapojengwa LIJENGWE kwa viwango sababu malori ya mizigo yanapita sana kwenye barabara hili MUHIMU mno kwa uchumi wa nchi yetu.

View attachment 2144140View attachment 2144141
Serikali ya Zanzibar haiwezi kuja kutupa pesa huko kwa sasa 😂😂😂
 
Msibani kwa mzee mmoja maarufu hapo Sawala nilikuwa hapo pia...inatia aibu kwamba barabara uliyoisema inayoanzia Njiapanda ya Lupeme Sawala village imewekwa lami...lakini pia barabara ya Kitiru isiyo na matumizi mengi pia imewekwa lami...nahisi kuna watu wananufaika kama usemavyo kuweka molam kila mara hapa...
Yaani inatia hasira. Mbunge mwnyewe kuja huku ni nadra sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikikwambia urudi shule utasema nakukosea.
Sema tu. Ujinga wako kila mwanajukwaa anauona kama hujui kazi ya kodi inayolipwa na manufacturing industry wewe unakuwa kubwa la mapopoma. Mi najielewa eti.
 
Naimani wenye maamuzi watakuwa wameona.Hiyo Barabara miaka mingi inaliliwa lakini haijengwi.Yawezekana Kuna watu wananufaika kweli na huo ubovu wa Barabara.

Wasaidizi wa Mhe.Rais mpeni mama hii taarifa angalau mambo yaende sawa.
 
Back
Top Bottom