Kuweka lami barabara ya Iyegeya hadi Sawala ila Mgololo highway haina lami sio poa!

Naomba niwakosoe watoa maamuzi. Kwanini feeder roads za barabara kuu itokayo Mafinga-Mgololo zina lami lakini hii barabara kwa miongo kadhaa sasa lami inaombwa lakini haiwekwi!? SERIKALI TAFADHALI WAANGALIENI WANANCHI WA ENEO HILI LA MAFINGA MGOLOLO kuna uchumi sana huko lakini mabarabara hayako vizuri.

Kilichonistaajabisha ni kwamba 35 Kilometre kutoka Mafinga town barabara zinazoingia vijiji vya ndani kama Sawala-Kitiru tayari ina lami kwa sehemu na Sawala-Iyegeya lami inabandikwa sio muda kazi inaendelea!

Sasa najiuliza kwanini hili barabara muhimu linalopitisha bidhaa muhimu kama Karatasi kutoka Mgololo factory,Mbao kutoka Saohill na kwa wakulima binafsi wa miti,Chai,Pareto,parachichi,Cinchona(hii ni mitishamba inayovunwa kupelekwa viwanda vya dawa na sumu kama ilivyo pareto),Magogo ya nguzo za umeme nk, nguzo za uzio,mabanzi nk, pia Halmashauri ya Mufindi hili ndo barabara lake kuelekea huko makao makuu mapya yanayotarajiwa haliwekwi lami!?

Tafadhali fanyeni huu mradi uanze lami lipite huko tuharakishe maendeleo zaidi ya sasa kama inavyofanyika kuweka lami huko ndani zaidi lakini mtu akitokea huko anakuja kukutana na barabara la vumbi tena hadi afike Mafinga.

Ikumbukwe huko kuna viwanda zaidi ya Vitano vya chai tu. Tuyatendee haki maeneo yanayotuingizia mapesa ya kutosha ikiwemo Mufindi.

Nawapongeza maji yamefika ila mabarabara kwa kweli bado.

PICHA: Hilo barabara panapoonekana anga la rangi ya Orange ndilo nalolizungumzia hapa hilo linaenda Mgololo kiwanda pekee cha kuchakata magogo ili kutengeneza karatasi katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.

PICHA NYINGINE: Barabara la Sawala Village linalokwenda Luhunga ambalo linapachikwa lami lije kukutana na hilo la Mgololo.

Wananchi huko wanachakalika kweli ila barabara bado mtikhani!View attachment 1532034View attachment 1532037View attachment 1532038View attachment 1532040View attachment 1532042View attachment 1532047View attachment 1532050View attachment 1532051
Uko sahihi mkuu, niulize swali la kizushi, hizo karatasi toka mgololo huwa zinauzwa wapi?
 
Nicko Muzungu

Kuna jamaa ake mwaka jana alikamatwa na mashine za EFD feki kilichompata ni siri yao
Imewatoka zaidi ya 1billion kuchomoka
dah Niko mzungu hv bado yupo?! Sijamsikia kitambo magwiji wa mbao na akina kilamulya enzi hizo za 2000z mwanzoni
 
Kuna watu wanasema barabara sio muhimu sana kwa hujawasikia mkuu
 
Sijawahi kuziona sokoni, labda kama huwa wanauziwa wajumbe tu
Zinauzwa kwa factories as raw material viwanda vya tissue na paper related products kama vile Tanpack Tissues cha Mikocheni wanapata rollers za karatasi kutoka Mgololo.

Na soko lake kubwa liko nje. Currently hakizalishi karatasi nyeupe ingawa soon wataanza.

Product za Mgololo Factory ni 100 % virgin natural sack brown kraft papers destined kwa ajili ya exportation worldwide na domestically.

Viwanda vya maboksi wananunua Mgololo, kiwanda kile hakiundi karatasi kwa ajili ya retail market wanaunda karatasi kwa ajili ya industrial consumption ambapo hao wadogo ndio wanaunda finals kv bahasha nk nk.

Product nyingine inauzwa nje mainly abroad na soko la Africa likiwemo Sadc.

Vizuri ni kwamba umeshajifunza.

Lete swali.
 
Yes, zinaitwa brown kraft papers ambazo huwa kwenye rollers my primary school classmate anafanya kazi hapo...anasema Mgololo kinaaminika sana nje kupeleka brown papers.

Hata Mimi nilishangaa kuambiwa karatasi zao ni Bora Sana nje😀😀! Best nakuja pm ...
 
Zinauzwa kwa factories as raw material viwanda vya tissue na paper related products kama vile Tanpack Tissues cha Mikocheni wanapata rollers za karatasi kutoka Mgololo.

Na soko lake kubwa liko nje. Currently hakizalishi karatasi nyeupe ingawa soon wataanza.

Product za Mgololo Factory ni 100 % virgin natural sack brown kraft papers destined kwa ajili ya exportation worldwide na domestically.

Viwanda vya maboksi wananunua Mgololo, kiwanda kile hakiundi karatasi kwa ajili ya retail market wanaunda karatasi kwa ajili ya industrial consumption ambapo hao wadogo ndio wanaunda finals kv bahasha nk nk.

Product nyingine inauzwa nje mainly abroad na soko la Africa likiwemo Sadc.

Vizuri ni kwamba umeshajifunza.

Lete swali.
Nimekusoma mkuu,
 
Mkuu za leo
nahiataji brown papers kwa ajili ya bahasha na vifungashio hao mawakala ntawapata wapi? Je unacontact zao? saidia mimi.

Yes, zinaitwa brown kraft papers ambazo huwa kwenye rollers my primary school classmate anafanya kazi hapo...anasema Mgololo kinaaminika sana nje kupeleka brown papers.
 
Back
Top Bottom